Matumizi ya akili bandia (AI) yahofiwa kushusha ubora elimu

Matumizi ya akili bandia (AI) yahofiwa kushusha ubora elimu

Akili finyu wewe... Hiyo smartphone unatumia ya nini?
Hakuna namna ya kupingana na Teknolojia. Leo ni nani anaweza kupigana na matumizi ya simu ama komputa?
Kwa kuwa fikra zako zimebanwa huwezi kung'amua wala kufuatilia kujua hicho nilichokieleza, endelea na ushabiki wa teknolojia..
 
Chat GTP ni yakijinga sana, juzi kati nilikuwa semina Sasa mwisho wake kulikiwa na assignment ya kufanya online nikachekelea maana Ili niwe online nahitaji MB's na device yangu yaani hata Haina kujificha ni Mimi ku copy na ku_paste bas bana semina Zima nikawa hata sisikilizi kazi yangu ni kusaini tu nipo,

Kwenye hiyo assignment Kuna swali Moja hata sikulisoma nilifanya tu kulikopi halafu Nika paste kwa AI afanye chap kanipa jibu nikarudi kujibu bila hata kusoma swali, AI kanipeleka Chaka kumbe swali lenyewe rahisi kishenzi kama ningelisoma nigelipata bila hata iyo AI.

Maswali yote alifanya AI kazi yangu ilikuwa ni ku copy na ku paste, bila kujificha maana assignment yenyewe ya online, hakika Hilo dude linafanya tusitumie akili zetu.
Hiyo App unaipata wapi mkuu? hawa watoto wa chuo wa kizazi hiki tutawadhibiti vipi maana AI ndo atakuwa anafanya assignment zote. Kwenye test na mitihani ndo kutakuwa na shughuli pevu maana simu na laptop haziruhusiwi kwenye chumba cha mtihani.
 
Chat GTP ni yakijinga sana, juzi kati nilikuwa semina Sasa mwisho wake kulikiwa na assignment ya kufanya online nikachekelea maana Ili niwe online nahitaji MB's na device yangu yaani hata Haina kujificha ni Mimi ku copy na ku_paste bas bana semina Zima nikawa hata sisikilizi kazi yangu ni kusaini tu nipo,

Kwenye hiyo assignment Kuna swali Moja hata sikulisoma nilifanya tu kulikopi halafu Nika paste kwa AI afanye chap kanipa jibu nikarudi kujibu bila hata kusoma swali, AI kanipeleka Chaka kumbe swali lenyewe rahisi kishenzi kama ningelisoma nigelipata bila hata iyo AI.

Maswali yote alifanya AI kazi yangu ilikuwa ni ku copy na ku paste, bila kujificha maana assignment yenyewe ya online, hakika Hilo dude linafanya tusitumie akili zetu.
chatgtp mda mwingine anadanganya sana Asa maswali ya mahesabu anazunguka sana anajua maswali ya kujielezea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waambieni hao vilaza kuwa Technolojia ya sasa haizuiliki, Huko duniani waliko staharabika ambao ndio mliwacopy elimu wameamua kuukubali ukweli kuhusu technolojia.

Ukishindwa kupambana na jambo basi ungana nalo, hapo suluhisho ni serikali na hao vilaza wetu kuamua kutunga mifumo mipya ya kielimu tofauti na hii ya sasa ya kukalilishana upumbavu.

Kwa sasa tulitakiwa kuwekeza nguvu kwa wanafunzi waelewe masomo ya sayansi haswa mambo ya Computer na ubunifu wa technolojia zinazorahisisha maisha,

Sapoti kwa wabunifu huko mitaan+mashuleni, fanyeni research juu ya umuhimu wa mabadiriko ya kitechnolojia na athari kijamii, kiuchumi, kimaadili, maana haya mambo hayazuiliki ni lazima yatokee hata tupinge vipi,

kwa akili za wanadamu zilipofikia kwa kutaka kuutumia Uwezo wao wa akili kuvumbua mambo ambayo wanaona ni sahihi na yatareplace mbadala wa utegemezi+uwezo wa mwanadamu badala yake kuundwa kwa vifaa vitakavyofanya mambo ambayo mwanadamu angeyafanya au zaidi ya uwezo wa mwanadamu.

Tuelimike Technolojia ya AI ni nzuri kama tutaukubali ukweli, lkn tukiendelea kuona hili jambo ktk Muono negative basi lazima tupigike tu na hivi tunaongozwa na vilaza ambao wanajiamini na hizo akili za kukalili, basi tujiandae.
 
Neural links inahusu nini?
Neuralink ni kampuni ya teknolojia iliyoundwa na Elon Musk ambayo inafanya kazi katika uwanja wa interfaces za ubongo-kompyuta. Lengo la Neuralink ni kukuza teknolojia inayowezesha ubongo wa binadamu kuunganishwa moja kwa moja na kompyuta au vifaa vingine vya elektroniki.

Wazo nyuma ya Neuralink ni kuunda njia ya kuunganisha akili za binadamu na kompyuta ili kuwezesha mwingiliano wa moja kwa moja kati ya mifumo ya dijiti na ubongo wetu. Hii inaweza kufanywa kupitia vifaa vya elektroniki vilivyowekwa ndani ya ubongo au karibu na ubongo, ambayo yanaweza kusoma shughuli za neva na kuhamisha data kati ya ubongo na vifaa vya nje.

Lengo kuu la Neuralink ni kutumia teknolojia hii kuboresha afya ya akili, kushughulikia shida za neva, na hata kuongeza uwezo wetu wa kufikiri na kushirikiana na teknolojia. Kwa mfano, inaweza kusaidia watu walio na ulemavu wa mwili kuweza kudhibiti vifaa vya elektroniki kwa kutumia mawazo yao pekee.

Yaani ubongo huu unaweza hata usiende shule tukakuwekea material tu via computer unakuwa unaelimu tyari maana ni upandikizaji wa microchip kwenye ubongo.

Walikuwa wanafanya majaribio kwa nyani. Nafkiri saiz wamepata go ahead ya kufanya test kwa binadamu kama nlivoona wiki ilopita.

Zaidi na zaidi ingia mtandaoni usome kdogo utajifunza mengi.
Ahsante
 
Hii fourth revolution ndo inaenda kuleta chapa ya mnyama ambapo unique ID zitatumika kuwatambua watu wote duniani ambazo zitakuwa connected na huduma mbalimbali. Kwa maana nyingine binadamu anaenda kufanywa mateka na waabudu shetani ili watimize malengo yao ya giza.​
Alama ya mnyama ni nini, na ipi?
 
Dah nilitaka kulifungulia uzi suala hili ratiba inanibana, afadhali wameshaliona, na hima walishughulikie haraka.

Chat GPT imevuruga kabisa elimu vyuoni, na imeibuka kwa kasi sana semester hii.

Kama haitopatikana namna bora ya kuishi na hili bomu Kuna wanafunzi watakuwa wanaingia vyuoni na wanatoka empty kama walivyoingia. Hasa ukizingatia vitoto vya siku hizi vipo empty sana vichwani, division I kali ila kichwani zero tupu!
Mkuu,
Hata internet wenzako walisema hivi kisa wao walikuwa wakitafuta material library.

Technology haizuiliki. Hiyo ni mitazamo tu ya hofu kupokea kitu kipya.
 
tukiuliza chanzo cha hizi teknolojia ni wapi?majibu hakuna ,inawezekanaje binadamu kuunda kifaa ambacho kinamuzidi akili? 100%? tuwe makini jamani ndo tushafanywa ndondocha ivo.teknolojia gani ambayo haina mechanism? mwalimu wao wa teknolojia ni nanii?
Umefuatilia ukaambiwa haina mechanism.

Unauelewa na programming?
Unaelewa vitu kama machine learning?
 
Kongamano la 8 la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu limeanza leo jijini Dar es Salaam ambapo wito ukitolewa kwa wanataaluma kuongeza umakini kukabiliana na changamoto za teknolojia mpya.

Kupitia kongamano hilo lililoandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), mada mbalimbali zimejadiliwa ikiwemo maandalizi ya taifa kuingia kwenye mapinduzi ya nne ya viwanda mojawapo ikiwa ujio wa teknolojia na athari zake chanya na hasi kwenye elimu.

Akichangia mada hiyo leo Juni 14, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Dodoma (Udom), Profesa Lughano Kusiluka ameeleza kuwa mapinduzi hayo yamekuja na changamoto ambazo zinaweza kuathiri mifumo mbalimbali ikiwemo elimu.

Amesema ili kuepuka athari hasi ni muhimu kwa wanataaluma kwenda na kasi ya teknolojia hizo ili kubaini udanganyifu unapojitokeza.

Akitolea mfano wa programu rununu ya Chat GPT amesema inatumika vibaya na wanafunzi hivyo ni muhimu kuwa walimu kuwa makini kufanya ufuatiliaji.

“Sasa hivi kuna hii Chat GPT ni teknolojia nzuri lakini matumizi yake yanaweza kuleta shida kwenye elimu yetu, huku vyuoni sasa hivi tuna shida mwanafunzi anaweza kukuletea tasnifu imeandikwa vizuri na akapata 'A' ukiifanyia tathmini utagundua wala hakustahili kupata hiyo alama.

“Hii inatufanya vyuo vikuu na sisi tuone haja ya kuwekeza ili kuzibaini tasnifu zinazofanywa kwa njia hii, tuongeze umakini kwenye tathmini. Teknolojia hizi zipo na hatuna namna ya kuzikwepa lakini tuhakikishe hazitumiki kushusha kiwango cha elimu yetu,” amesema Profesa Kusiluka.

Akizungumzia hilo Mkurugenzi wa zamani wa Costech Dk Hassan Mshinda amesema teknolojia hiyo ni tatizo kwenye elimu kwani inawawezesha wanafunzi kufanya udanganyifu.

“Mtu anaweza kuandika tasnifu nzuri kabisa ya kurasa tano ndani ya dakika tano. Hata hivyo hatuwezi kupingana na maendeleo haya lazima tuendane na kasi hiyo. Changamoto ni kwamba kama tutaenda taratibu kila siku tutakuwa nyuma lazima kazi kubwa ifanyike kuendana na mabadiliko na maendeleo haya teknolojia,” amesema.
Wanalazimisha watu waendelee kutumia telefax na kuandikiana barua zama hizi?
 
Inabidi sasa wewe na wenzio mnao muabudu Mungu mje na teknolojia ya kuwatoa watu kwenye uzezeta huo wa kiushetani!!!
Hawa watu wako tyar wale mikate na samaki.

Yaani wanataka ukale, hawataki technology, ila ajabu wako Jf wanatumia simu
 
Hii fourth revolution ndo inaenda kuleta chapa ya mnyama ambapo unique ID zitatumika kuwatambua watu wote duniani ambazo zitakuwa connected na huduma mbalimbali. Kwa maana nyingine binadamu anaenda kufanywa mateka na waabudu shetani ili watimize malengo yao ya giza.​
Wewe haya umeambiwa na nani kama siyo mawazo yako tu.

Nieleze umejuaje
 
Hawa watu wako tyar wale mikate na samaki.

Yaani wanataka ukale, hawataki technology, ila ajabu wako Jf wanatumia simu
Pumbavu kabisa. Yaani watu wanavumbua vitu vya maanabwao wanakuja ku discourage visitumike. Wanadhani kukariri mambo ni sifa? Kama wameshindwa kuwa challenged na kubadili mfumo wa elimu ili uendelee juwa na maana kipindi hiki cha ChatGPT basi ni bure na walisoma pasipo kuelimika. Sababu tu walisoma kwenye umande vijijni na chini ya mti, basi ushauri wao ni kwamba wanafunzi kusoma darasani wakiwa wamekalia madawati ni anasa, wote wanatakiwa kusoma kama walivyosoma wao enzi zile, no madawati, no madarasa, hakuna kuvaa viatu n.k
 
Hii fourth revolution ndo inaenda kuleta chapa ya mnyama ambapo unique ID zitatumika kuwatambua watu wote duniani ambazo zitakuwa connected na huduma mbalimbali. Kwa maana nyingine binadamu anaenda kufanywa mateka na waabudu shetani ili watimize malengo yao ya giza.​
Acheni akili za kipuuzi. Binaadam walienza kupeana IDs miaka zaidi ya maelfu kwa maelfu yaliyopita. Walipoanza tu kutambuana na kutofautishana, baadaye wakaanza kutambuana kwa majina, baadaye wakaanza kuyambuana kwabnamba.
Mbona wewe mpaka sasa una IDs kibao tu.
Una ID ya shule, chuo, kazini, hospital, namba za simu, account number n.k. Hata humu JF umejipa ID unayotaka tukutambue nayo.
Mnajazana maujinga ujinga tu mwishowe dunia iwaache. Kuliko kusubiri iwaache si ni bora muiage dunia tu?
 
Acheni akili za kipuuzi. Binaadam walienza kupeana IDs miaka zaidi ya maelfu kwa maelfu yaliyopita. Walipoanza tu kutambuana na kutofautishana, baadaye wakaanza kutambuana kwa majina, baadaye wakaanza kuyambuana kwabnamba.
Mbona wewe mpaka sasa una IDs kibao tu.
Una ID ya shule, chuo, kazini, hosoital, namba za simu, account number n.k. Hata humu JF umejipa ID unayotaka tukutambue nayo.
Mnajazana maujinga ujinga tu mwishowe dunia iwaache. Kuliko kusubiri iwaache si ni bora muiage tu?
Alfu dunia huwezi kushindana nayo badala yake lazima uende nayo
 
Back
Top Bottom