Matumizi ya "Dr" kwa wanasiasa wetu ni PhD au vumbi?

Matumizi ya "Dr" kwa wanasiasa wetu ni PhD au vumbi?

Profesa

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Posts
905
Reaction score
624
Nakerwa na viongozi na wanasiasa hasa hao wanaotumia initial za "Dr" kwenye majina yao wakati rules haziruhusu.

Nakumbuka TCU iliwahi pia kuweka sawa hili kuhusu matumizi ya hii initial na kusisitiza kama una Degree ya Heshima ya Udaktari basi hupaswi kutumia hii initial ya Dr.

Lakini cha kushangaza aidha wanaitwa na wafuasi wao au wanaojipendekeza au wao wenyewe, lakini wahusika wanakaa kimya tu na kuacha majina yao kutumika hata kwenye vymbo nyeti kama bunge.

Nakerwa na jambo hili linaonyesha dhahiri wanasiasa wetu wasivyo makini na kupenda kusifiwa na kukumbatiwa kwa msifa ya bandia.

Kakamueni PHD tujue kweli na nyinyi ni miamba na mmnazo za kihalali na za kweli sio za kununua kama tulivyoona kwa watu maarufu kama wafanya biashara na viongozi wa dini.
 
hivi Dr Jakaya Mrisho Kikwete atakwenda USA wakati wa kuapishwa kwa obama?
Dr Augustine Lyatonga Mrema ni mbunge wa Vunjo(TLP)
lakini pia nimemmisi DR DIDAS MASABULI
 
pia kuna hawa
.dakta milton makongoro mahanga,
.dakta nchimbi

Hiv yule mshkaji "MSEMAKWELI" yuko wapi siku hiz atukumbushe ile list?
inawezekana kuna wengine wa aina hiyo wameongezeka
 
The list is not exhaustive
Dr. Kikwete
Dr. Makongoro
Dr. Maji Marefu
Dr. Matunge
............ etc
 
obama ana phd lakini hatumii DK, raila odinga , kibaki wana phd za honoraria nyingi tu, hata museveni , lakini huwezi sikia dr, museveni, dr,raila huu uzumbukuku ni wa hapa TZ,hata mkapa, nyerere walikuwa nazo lakini hawakupenda huu uzumbukuku wa jk na vilaza wengine.

kuna haja pia ya kufanya vetting ya hivyo vyuo vinavyotoa hizo phd za wansiasa huenda kuna hongo fulani
 
Hili la Obama kuwa na PHD hata mimi nimeshangaa sana,maana angekuwa Mwanasiasa wa BOngo angeforce atambuliwe hivyo! Kweli Obama yupo humble sana
 
Uswahili tu. Kuna mmoja nafanya nae kazi anajiita 'dr dr' manake ni medical dr afu ana phd. Performance zero!
 
Dr. Nyerere, Dr. Salim, Dr. Kikwete. Nyerere alikuwa anajiita Dr. wakati alikuwa hana PhD wala hakuwahi kupata Doctorate ya Heshima. Hiyo Doctorate ya Heshima amepewa miaka michache baada ya "kung'atuka". Salim na Kikwete wamepewa Doctorate za Heshima kutoka vyuo vikuu vinavyotambulika. Tafuteni lingine la maana, siyo hili.
 
The list is not exhaustive
Dr. Kikwete
Dr. Makongoro
Dr. Maji Marefu
Dr. Matunge
............ etc
hapo kwenye red, huyo kaenda mbele zaidi, ni professa.
mi namwona km mjanja fulan, katoka kivingine
 
obama ana phd lakini hatumii DK, raila odinga , kibaki wana phd za honoraria nyingi tu, hata museveni , lakini huwezi sikia dr, museveni, dr,raila huu uzumbukuku ni wa hapa TZ,hata mkapa, nyerere walikuwa nazo lakini hawakupenda huu uzumbukuku wa jk na vilaza wengine.

kuna haja pia ya kufanya vetting ya hivyo vyuo vinavyotoa hizo phd za wansiasa huenda kuna hongo fulani

Nimeshawahi kusikia Dr. Museveni kwenye media za Uganda.
 
Dr. Nyerere, Dr. Salim, Dr. Kikwete. Nyerere alikuwa anajiita Dr. wakati alikuwa hana PhD wala hakuwahi kupata Doctorate ya Heshima. Hiyo Doctorate ya Heshima amepewa miaka michache baada ya "kung'atuka". Salim na Kikwete wamepewa Doctorate za Heshima kutoka vyuo vikuu vinavyotambulika. Tafuteni lingine la maana, siyo hili.

Mwanangu kwa Dr. Nyerere umechemka.
Hizo Honorias Causa anazo kama ishirini hivi, kabla na baada ya kustaafu urais, na hajawahi kudai popote aitwe Dr., alipenda zaidi title yake ya 'mwalimu'
 
Wakati nasomea PhD yangu nilikwenda nyumbani kusalimu. Baba yangu akaniambia kuwa kuna mama mmoja anataka kuniona siku nyingi. Alipokuja huyo mama akaanza kunieleza matatizo yake mengi ya kiafya. Ikabidi nimueleze kuwa mimi sio daktari wa kutibu magonjwa bali nasomea udaktari wa filosofia. Nilivyomuona alionekana kuwa hakunielewa vizuri. Vivo hivyo na hao wanaopenda kutumia Dr. kila mahali hawaelewi vizuri maana ya PhD.
 
Back
Top Bottom