Matumizi ya kiingereza: "Somehow" na "Somewhat"

Mwlsamwel

Member
Joined
Dec 13, 2017
Posts
76
Reaction score
75
Habari gani jamani. Mimi ni mmarekani aliyeishi Tanzania miaka miwili kuanzia 2014 mpaka 2016. Nimejiunganisha na jamii forums hivi karibuni tu lakini... Samahani nimechelewa. Basi...

Wakati nilikuwa kule, nilisikia sana kosa dogo moja la kiingereza. Niliona kwamba, kati ya kiingereza cha Marekani na kile cha Tanzania, matumizi ya "somehow" na "somewhat" kumbe yamegeuka. Kabla sijatoa mifano, nitafsiri hayo maneno kwa maana zao sahihi:

SOMEHOW: kwa jinsi fulani (tukumbuke kwamba "how" ndiyo "vipi" kwa kiswahili)
SOMEWHAT: kiasi fulani, kidogo

KIINGEREZA CHA TANZANIA (ambacho napendekeza si sahihi):

"It is somehow cold today" (Ni baridi kwa jinsi fulani leo) - lugha mbovu, hatueleweani
"It is somehow a problem" (Ni tatizo kwa jinsi fulani) - lugha mbaya sana, ina maana gani hiyo?

KILICHO SAHIHI ZAIDI (tutumie "somewhat" badala ya "somehow")

"It is somewhat cold today" (Ni baridi kiasi fulani leo) - lugha nzuri
"It is somewhat of a problem" (Ni tatizo dogo) - nzuri tu, tunaeleweana
"Somehow, I was able to get to work on time" (Kwa jinsi fulani, niliweza kufika kazini mapema) - matumizi mazuri ya "somehow"

Je, tumeelewa? Kama kuna maswali nitayajibu.
 
Wewe ndio mmarekani? Labda useme mpogoro wa malinyi ulanga na kiingereza chako cha kwa ras simba

Nilisahau kuomba msamaha kwa uwezo wangu mdogo wa kiswahili... Sielewi maneno yafuatayo:

mpogoro
malinyi
ulanga
ras

Tafadhali nielezee, nijifunze mimi mwenyewe!

Ndiyo, ni mmarekani, na kiingereza ni lugha yangu ya kwanza.
 
view Watakuwa wengi kuliko wachangiaji
pale mtu anapoleta hoja iliyonyooka, haina utata ni kawaida kuwa na wachangiaji wachache views nyingi zikiambatana na "likes".
Hapo hakuna cha kujadili labda angekuwa hayuko sahihi!
 
Upo sahihi. Watu wanapindisha lugha kwa kutokujua wasemacho.
 
Haya mmarekani !!
Asante kwa kujitambulisha hivyo kwa uzi wa kwanza kwenye hii acaunt mpya
 
Haya mmarekani !!
Asante kwa kujitambulisha hivyo kwa uzi wa kwanza kwenye hii acaunt mpya

Karibu uzi wangu wa kwanza... ni marufuku kujitambulishia nchi ya kuzaliwa? Sitaki kuvunja makanuni!
 
Nilisahau kuomba msamaha kwa uwezo wangu mdogo wa kiswahili... Sielewi maneno yafuatayo:

mpogoro
malinyi
ulanga
ras

Tafadhali nielezee, nijifunze mimi mwenyewe!

Ndiyo, ni mmarekani, na kiingereza ni lugha yangu ya kwanza.
Unatokea jimbo gani mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…