Mwlsamwel
Member
- Dec 13, 2017
- 76
- 75
Habari gani jamani. Mimi ni mmarekani aliyeishi Tanzania miaka miwili kuanzia 2014 mpaka 2016. Nimejiunganisha na jamii forums hivi karibuni tu lakini... Samahani nimechelewa. Basi...
Wakati nilikuwa kule, nilisikia sana kosa dogo moja la kiingereza. Niliona kwamba, kati ya kiingereza cha Marekani na kile cha Tanzania, matumizi ya "somehow" na "somewhat" kumbe yamegeuka. Kabla sijatoa mifano, nitafsiri hayo maneno kwa maana zao sahihi:
SOMEHOW: kwa jinsi fulani (tukumbuke kwamba "how" ndiyo "vipi" kwa kiswahili)
SOMEWHAT: kiasi fulani, kidogo
KIINGEREZA CHA TANZANIA (ambacho napendekeza si sahihi):
"It is somehow cold today" (Ni baridi kwa jinsi fulani leo) - lugha mbovu, hatueleweani
"It is somehow a problem" (Ni tatizo kwa jinsi fulani) - lugha mbaya sana, ina maana gani hiyo?
KILICHO SAHIHI ZAIDI (tutumie "somewhat" badala ya "somehow")
"It is somewhat cold today" (Ni baridi kiasi fulani leo) - lugha nzuri
"It is somewhat of a problem" (Ni tatizo dogo) - nzuri tu, tunaeleweana
"Somehow, I was able to get to work on time" (Kwa jinsi fulani, niliweza kufika kazini mapema) - matumizi mazuri ya "somehow"
Je, tumeelewa? Kama kuna maswali nitayajibu.