Matumizi ya Lugha ya Kiswahili: Hatimaye Mwakyembe ala matapishi yake

Tafautisha miaka hiyo na sasa, mambo yameadilika. Endeleb kuwa mtumwa wa lugha za watu
 
Miaka ya nyuma kidogo wakati wa Kugombea ubunge wa Africa Mashariki ndani ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mh Mwakyembe alitoa hoja kwa Spika Anna Makinda kwamba wagombea watumie lugha ya kiingereza kuomba kura ili kupima uwezo wao wa lugha wasije wakaifedhehesha nchi kwenye mijadala ya bunge la africa Mashariki , Spika Makinda akakubali mwongozo wa Mwakyembe hatimaye wagombea wakaanza kuomba kura kwa lugha ya kiingereza , huku Le Mutuz Super brand mmoja wa wagombea wa ccm akiangukia pua .

Hapa ndipo ulipoibuka msemo maarufu wa " IAM SORRY , IAM GLAD " msemo uliotokana na mmoja wagombea kuomba kujitoa kwenye kinyang'anyiro , lakini miaka michache tu siku ya leo Mwakyembe huyohuyo safari hii akiwa waziri wa michezo anawataka washiriki wa Miss Tanzania kutumia kiswahili kujibu maswali akidai ni lugha inayotumika dunia nzima !

Je ameusahau mwongozo wake wa Bungeni ?View attachment 860879

Kwetu Tandika Mwembeyanga kuna msemo maarufu kwamba UKIWA MUONGO USIWE MSAHAULIFU .

Naomba kuwasilisha .
Jamani ! Si umeshasema miaka kumi iliyopita ? Mambo yanabadilika.
 
Anatakiwa kuwa nicknamed Kigeugeu
Rejea andiko lake la PhD alilolikana kwenye BMK aliponukuliwa na Lissu kama sijakosea
Na hili la leo ni ushahidi tosha kuwa haaminiki
Mbona kuna wengine nao walisemaga kuwa watu fulani ni mafisadi papa na wanaushahidi mzito miaka ile baadaye tena wakasema watu wale wale ni wasafi mithili ya theruji kama zilivyo nywele zao tena mwenye ushahidi wa uchafu wao apeleke mahakamani ! Huyu wa lugha yeye akasimamia hoja ya uchafu wao mpaka wa leo. Muda unapoenda mambo hubadilika na sio ajabu.
 
Kuna wakati kuliibuka mjadala kuhusu lugha ya kiswahili iwe lugha ya kufundishia kuanzia sekondari mpaka Chuo kikuu, walioshupalia hivyo wao watoto wao wanasoma " English medium".
 
Miaka ya nyuma kidogo wakati wa Kugombea ubunge wa Africa Mashariki ndani ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mh Mwakyembe alitoa hoja kwa Spika Anna Makinda kwamba wagombea watumie lugha ya kiingereza kuomba kura ili kupima uwezo wao wa lugha wasije wakaifedhehesha nchi kwenye mijadala ya bunge la africa Mashariki , Spika Makinda akakubali mwongozo wa Mwakyembe hatimaye wagombea wakaanza kuomba kura kwa lugha ya kiingereza , huku Le Mutuz Super brand mmoja wa wagombea wa ccm akiangukia pua .

Hapa ndipo ulipoibuka msemo maarufu wa " IAM SORRY , IAM GLAD " msemo uliotokana na mmoja wagombea kuomba kujitoa kwenye kinyang'anyiro , lakini miaka michache tu siku ya leo Mwakyembe huyohuyo safari hii akiwa waziri wa michezo anawataka washiriki wa Miss Tanzania kutumia kiswahili kujibu maswali akidai ni lugha inayotumika dunia nzima !

Je ameusahau mwongozo wake wa Bungeni ?View attachment 860879

Kwetu Tandika Mwembeyanga kuna msemo maarufu kwamba UKIWA MUONGO USIWE MSAHAULIFU .

Naomba kuwasilisha .
Mwakyembe ndo katoa zawadi hii ya gari la Miss Tanzania?
IMG_20180909_091017.jpg
 
Kiingereza bado ni muhimu sana hasa kwa karne hii tuliyo nayo maana hata kuomba misaada kutoka kwa wazungu inabidi tutumie kiingereza ndio tunamuona poropesa kalamaganda karudi kila siku yupo nje ya nchi
Ohooo !!!
 
Nasikia mtambuka ni jitu zima, lakini it seems ni hopeless kichwani! It will be a breaking day if i happen to see him!
Hujui Kiingereza wala Kiswahili. Eti "it will be a breaking day", ha ha ha. Ndio maana umebaki kuchanganya lugha, huzijui zote. Utapata tabu sana.
 
Ni wazo zuri kukienzi Kiswahili. Hakuna haja ya kushobokea lugha za watu ndani ya nchi yetu. Huo ni ulimbukeni usio kifano.

Hao viongozi wanajifanya kushabikia kiswahili sasa ili kubeba udhaifu wa jamaa, lakini wao huona fahari sana watoto wao wakiongea kiingereza. Na hakuna hata mmoja anapeleka mtoto wake shule ya umma ambapo kiswahili ni lugha inayotumika.

Katika vitu sikubaliani navyo ni kusoma kwa kutumia kiswahili kisha ukienda kuomba ajira unatakiwa kuomba kazi kwa kiingereza. Na ni ukweli ulio wazi ukijua kiingereza hapa Tanzania hata kama huna elimu ya secondary unaweza kupata ajira tena ya mshahara mnono. Ni vyema kiingereza kitumike kufundishia masomo yote kuanzia chekechea kisha kiswahili kitumike nje ya masomo. Inapaswa watanzania tujue kiingereza na kiswahili kwa 100% kwani elimu kubwa hupatikana kwa kiingereza. Kisha tutumie kiswahili kwenye kuficha mambo yetu kama bungeni nk.
 
Mawazo ya kikoloni haya.
 
Kiingereza bado ni muhimu sana

Tena sio muhimu tu, bali ni lazima. Ukitaka kuijua dunia hii vyema ifahamu vizuri lugha ya kiingereza. Ukijua kiingereza unaweza kuishi popote hapa duniani na mambo yako ya kasonga. Kiswahili ni lugha ya kusengenyea tu.
 
Back
Top Bottom