Watakuja wataalam,
Ila kibongobongo,hii inatagemea mambo mengi,kwanza foleni ya jiji yenyewe inakula mafuta,na pia uendeshaji wa mtu pia ni kigezo kingine.
Ila kitaalam zaidi watakuja wadau.
Altezza zenye injini ya 3S-FE (four cylinders) hutumia wastani wa lita moja kwa kila kilomita 9 au 10 kwa mizunguko ya mjini (stop and go) lakini kama ukikwama kwenye foleni na kuacha injini ikinguruma basi unaweza kwenda chini ya kilomita 9 kwa lita kutegemea na ubaya wa foleni (unaweza kumaliza lita moja bila kwenda kokote). Kwenye safari ndefu katika barabara nzuri Altezza zenye 3S-FE huenda kati ya kilomita 13 na 15 kwa kila lita moja kutegemea na uendeshaji. Lita 13 zinatosha kukutoa Dar mpaka Moro (umbali wa kilomita 190).