Altezza zenye injini ya 3S-FE (four cylinders) hutumia wastani wa lita moja kwa kila kilomita 9 au 10 kwa mizunguko ya mjini (stop and go) lakini kama ukikwama kwenye foleni na kuacha injini ikinguruma basi unaweza kwenda chini ya kilomita 9 kwa lita kutegemea na ubaya wa foleni (unaweza kumaliza lita moja bila kwenda kokote). Kwenye safari ndefu katika barabara nzuri Altezza zenye 3S-FE huenda kati ya kilomita 13 na 15 kwa kila lita moja kutegemea na uendeshaji. Lita 13 zinatosha kukutoa Dar mpaka Moro (umbali wa kilomita 190).
haupo serious wewe.