CCM inajitahidi kukatisha tamaa watanzania (discourage) juu ya matumizi ya mitandao kama njia sahihi na muhimu ya kuitoa CCM madarakani.
CCM wana msemo wao wa "watu wa mitandaoni" kuelezea au kubeza kinachoandikwa mitandaoni kuwa hakina taathira (effects) chanya ama hasi kwa watanzania.
CCM inajitahidi kujenga taswira kuwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ni watu wachache tena wasio na mahusiano na maisha halisi ya watanzania mitaani.
Lakini kwa takwimu za mwaka 2024, Kuna zaidi ya watanzania milioni 21 wanaotumia internet. Idaidi hiyo ya watumiaji internet ni sawa na asilimia 31 ya watanzania wote wanaokadriwa kuwa milioni 67.
Kama mitandao ya kijamii ikitumiwa ipasavyo kupeleka taarifa sahihi juu ya hali halisi ya nchi yetu, basi siyo muda CCM itapata inachostahili, yaani kutoka madarakani.