JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Katika mazingira ya kawaida askari polisi haruhusiwi kutumia nguvu dhidi ya mtuhumiwa yeyote isipokuwa tu kama mtu huyo anakataa kukamatwa au anajaribu kutoroka
Ijapokuwa askari polisi anaweza kutumia nguvu, lakini hayuko juu ya sheria, na iwapo atatumia nguvu isivyohitajika atachukuliwa hatua za kinidhamu au kufunguliwa mashtaka kwa kosa la jinai.
Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002. Bila kufafanua "nguvu ya lazima", Kif. 29 (6) kinaeleza kwamba si ruhusa kwa afisa wa polisi kuhusika katika madai ya umma au mashtaka ya kosa la jinai ya kifo au majeraha yaliyosababishwa na matumizi ya nguvu chini ya sheria. Wakati huo huo pia, Kif. 33 (8) kinaeleza kwamba maafisa wa polisi wanalindwa dhidi ya mashtaka ya ukamataji wa aina yoyote uliofanywa kwa nia njema chini ya sheria
Upvote
2