Matumizi ya Proforma Invoice ni nini?

Matumizi ya Proforma Invoice ni nini?

Michael Ngusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2014
Posts
1,637
Reaction score
463
Wakuu,

Proforma Invoice inatumika vipi? Pili, mimi ni freelancer na mteja anataka Proforma, nifanyeje? (niprint yangu? Je, vitu kama TIN na VRN ntatoa wapi au nibuni tu?

Au nitumie Proforma ya kampuni ambayo nimeajiriwa? (Ila services zangu ni tofauti.) Tatu, inamaanisha atanilipa kupitia Bank? Maana mimi nataka cash na je hatua inayofata baada ya mteja kupewa Proforma ni ipi, atoe advance sio?

Nisaidie tafadhali
 
Nelson Richard

sheria ya manunuzi iko hivi, mtu anapotaka kununua bidhaa yoyote kwa matumizi ya ofisi ni lazima aridhishe uongozi wa shirika ama kampuni kwamba amenunua bidhaa stahiki na hakukuwa na ujanja ujanja kama vile kununua kitu kwenye duka la ndugu jamaa ama rafiki..

.kwa hiyo ni lazima aende kwenye maduka matatu tofauti apewe bei .....kwa bidhaa ile ile moja kuna uwezekano utakuta bei zinatofautiana ndipo ukiwa kama afisa manunuzi unatakiwa uandae ripoti ya kushawishi ofisi inunue bidhaa kwa muuzaji huyu mwenye bei nafuu yenyee ubora ule ule.

kwa kawaida muhasibu hawezikutoa fedha bila ya profoma ushauru kwangu kwako kama unataka kuwa mfanyabiashara mkubwa ni vyema ukawa na kitu kama tin na vrn yaani uisajili biashara yako vinginevyo utawauzia watu binafsi wasio fuata taratibu za manunuzi
 
Last edited by a moderator:
Proforma Invoice Ni Hati Ya Awali Inayotumwa Kwa Mteja, Ikionyesha Bei Ya Bidhaa Ama Huduma. Inakuwa Na Jina La Muuzaji/Mtoa Huduma, TIN na VRN namba kama Amesajiriwa ngazi ya VAT.
Mtejaakiafikibeiiliyopoktk Proforma Invoice, Mauzo/Huduma Itafanyika, kisha itafuata hati ya madai, Tax Invoice.
Mfumo Wa Malipo na advance Ni Maelewano, Taslimu Ama Hundi, na vyovyote iwavyo, mlipwaji lazima atoe risiti kwa malipo aliyopokea, iwe ya kuandika ama ya EFD.
 
Ukiulizwa swali jibu swali si kutoa majibu marefu kama wanasiasa.

Proforma Invoice ni document kutoka kwa muuzaji kwenda kwa mnunuzi ikiwa na taarifa zifuatazo.

1. Aina ya bidhaa
2.Upatikanaji wa bidhaa
3.Idadi ya bidhaa
4.Bei ya bidhaa
Proforma Invoice ni tofauti na Invoice.Invoice ni kwaajili ya madai (demand or request for payment) while Proforma Invoice are commonly used as preminary invoice with QUOTATION.

sheria ya manunuzi iko hivi, mtu anapotaka kununua bidhaa yoyote kwa matumizi ya ofisi ni lazima aridhishe uongozi wa shirika ama kampuni kwamba amenunua bidhaa stahiki na hakukuwa na ujanja ujanja kama vile kununua kitu kwenye duka la ndugu jamaa ama rafiki...kwa hiyo ni lazima aende kwenye maduka matatu tofauti apewe bei .....kwa bidhaa ile ile moja kuna uwezekano utakuta bei zinatofautiana ndipo ukiwa kama afisa manunuzi unatakiwa uandae ripoti ya kushawishi ofisi inunue bidhaa kwa muuzaji huyu mwenye bei nafuu yenyee ubora ule ule. kwa kawaida muhasibu hawezikutoa fedha bila ya profoma ushauru kwangu kwako kama unataka kuwa mfanyabiashara mkubwa ni vyema ukawa na kitu kama tin na vrn yaani uisajili biashara yako vinginevyo utawauzia watu binafsi wasio fuata taratibu za manunuzi
 
Nipate mfano halisi wa profoma invoice na invoice
 
Ukiulizwa swali jibu swali si kutoa majibu marefu kama wanasiasa.

Proforma Invoice ni document kutoka kwa muuzaji kwenda kwa mnunuzi ikiwa na taarifa zifuatazo.

1. Aina ya bidhaa
2.Upatikanaji wa bidhaa
3.Idadi ya bidhaa
4.Bei ya bidhaa
Proforma Invoice ni tofauti na Invoice.Invoice ni kwaajili ya madai (demand or request for payment) while Proforma Invoice are commonly used as preminary invoice with QUOTATION.
Apa umemaliza nlitaka nicomment ila naona umeeleza vzuri sana

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ukiulizwa swali jibu swali si kutoa majibu marefu kama wanasiasa.

Proforma Invoice ni document kutoka kwa muuzaji kwenda kwa mnunuzi ikiwa na taarifa zifuatazo.

1. Aina ya bidhaa
2.Upatikanaji wa bidhaa
3.Idadi ya bidhaa
4.Bei ya bidhaa
Proforma Invoice ni tofauti na Invoice.Invoice ni kwaajili ya madai (demand or request for payment) while Proforma Invoice are commonly used as preminary invoice with QUOTATION.
Kwahio hili ndio jibu fupi. Ok
 
U go too personal.
Haya mambo mwenyewe nilikuja yajulia kazin ..
Hata mie sikuyajua mapema kama wewe ndio maana nimecomment kuhusu tatizo la elimu yetu haswa kwenye basics za business management and financial literacy. Hivi unajua zamani walikuwa wanasoma Bookkeeping na ilikuwa compulsory ila akatokea mpuuzi mmoja akafuta. Hii nchi kuna wapumbavu wameiharibu mnoo.
 
Nakala ya utoaji au "delivery order" ni hati inayotoa maagizo kwa mdhibiti wa ghala au kampuni ya usafirishaji kutoa bidhaa au vifaa kwa mpokeaji. Hutumiwa sana katika biashara ya kimataifa au shughuli za ndani kuhakikisha kuwa bidhaa sahihi zinapelekwa kwa chama kinachostahili na wakati uliokubaliwa. Nakala ya utoaji kawaida ina maelezo kama vile jina na anwani ya mpokeaji, tarehe na mahali pa utoaji, maelezo ya bidhaa au vifaa, wingi, habari ya mdhibiti wa ghala au kampuni ya usafirishaji, na maagizo au hali zingine muhimu. Hutumika kama uthibitisho wa umiliki na kupokea bidhaa na mpokeaji
 
Hata mie sikuyajua mapema kama wewe ndio maana nimecomment kuhusu tatizo la elimu yetu haswa kwenye basics za business management and financial literacy. Hivi unajua zamani walikuwa wanasoma Bookkeeping na ilikuwa compulsory ila akatokea mpuuzi mmoja akafuta. Hii nchi kuna wapumbavu wameiharibu mnoo.
Hapa sasa nimekuelewa na 100% uko sahihi sana.
Hiv ni vitu basic ambavyo ikiwezekana toka primary watoto wanatakiwa wavijue
 
"delivery note" ni hati inayotumiwa kuthibitisha kuwa bidhaa au vifaa vilitolewa kwa mpokeaji. Mara nyingi hutolewa na muuzaji au mtengenezaji wa bidhaa na huambatana na bidhaa zilizopelekwa kwa mpokeaji. Delivery note inaweza kujumuisha habari kama vile jina na anwani ya mpokeaji, tarehe na mahali pa utoaji, maelezo ya bidhaa au vifaa, kiasi, na habari nyingine muhimu kama vile masharti ya malipo. Inatumika kama uthibitisho wa utoaji wa bidhaa na kama hati ya kumbukumbu kwa kampuni
 
Mkuu hebu haya maelezo uliyoelezea hapa yaweke kwenye clearing and forwarding kama hutojali
 
Sijakuelewa

Yani namaanisha kwenye
Clearing and forwarding kuna ishu kama iyo ya kuchukua delivery order kama unataka kuclear gari kutoka bandarini iyo delivery order kwenye clearing and forwarding inakuwaje au ni kitu gani??
 
Back
Top Bottom