SI KWELI Matumzi ya Wali mweupe yana hatari zaidi kuliko Soda kwenye kusababisha kisukari

SI KWELI Matumzi ya Wali mweupe yana hatari zaidi kuliko Soda kwenye kusababisha kisukari

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwepo na chapisho linalodai kuwa matumzi wa wali mweupe yana hatari zaidi kuliko soda kwenye maambukizi ya kisuakari
Je ? ni upi uhalisia wa chapisho hilo linalodai kusambzwa kwenye mitandao ya kijamii nchini Tanzania.
wali.jpg
 
Tunachokijua
Kisukari ni ugonjwa unaotokea wakati kiwango cha sukari kwenye damu (glukosi) kinapokuwa juu sana. Hali hii hutokea wakati kongosho lako halitengenezi insulini ya kutosha au halitengenezi kabisa, au mwili wako unaposhindwa kuitikia vizuri ufanyaji kazi wa insulini. Kisukari huathiri watu wa rika zote. Aina nyingi za kisukari ni za kudumu (kwa maisha yote), na aina zote zinaweza kudhibitiwa kwa dawa na/au kubadili mtindo wa maisha.

JamiiCheck imewasiliana na mtaalamu wa afya, Daktari Benard Kivuma kutoka Ifakara, Morogoro ambaye anafafanua uhalisia wa madai hayo.

Je, wali mweupe unasababisha kisukari?

Shahidi za kiutafiti zinaonesha kuwa ulaji mwingi wa wali mweupe, huu ambao tunatumia sana sana kila siku unahusishwa na ongezeko la hatari ya kupata kisukari ambao kwa jina la kitaalam tunaita type 2 diabetes. Vilevile matumizi ya mara kwa mara ya vinywaji vyenye sukari, kama hizi soda, pia nayo inahusishwa na ongezeko la hatari ya kupata kisukari.

Wali mweupe ni hatari zaidi kuliko soda?

Ila sio sahihi kusema ya kwamba wali mweupe ni hatari zaidi kuliko soda. Kwa sababu hivi vitu viwili havijatafitiwa katika kufanya ule ulinganisho wa moja kwa moja ambao unaweza kutuonyesha kusema kipi ni hatari kuliko kipi. Lakini pia hatari ya kisukari haiamuliwi na chakula kimoja pekee yake ambacho mtu anatumia.

Inahusishwa na vitu vingine ambavyo vinaunganishwa na hii, kama mlo ambao mtu anakula kwa ujumla kiasi anachokula, uzito wake wa mwili, shughuli anazofanya kila siku kama mazoezi na mambo mengine, historia pia ya familia ya ugonjwa huu. Kwa hiyo hivi vitu vyote vinajumuishwa katika kuongeza hatari ya kisukari.

Nini cha kufanya ili kupunguza athari ya wali mweupe na soda kwenye kuchochea uwezekano wa kupata kisukari?

Kwa hiyo cha muhimu kuzingatia ni kwamba taarifa kama hizi haziwezi zikatumika kwa ajili ya kufanya watu labda wawe na hofu ya kwamba wali ni, soda ipi ni bora na nini kwa sababu hazilinganishi. Lakini badala yake ni muhimu kuzingatia kiasi ambacho mtu anatumia.

Kwa hiyo kwenye chakula unatumia wali kiasi gani, unavyochanganya na mboga mboga nyingine za majani na vyakula vyenye nyuzi nyuzi, ambao tunaita fiber kwenye mlo, lakini pia kuongeza na protein pia na kupunguza unywaji wa vinywaji vyenye sukari.

Hii inasaidia katika kupunguza ile hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari. Lakini madai ya kwamba wali mweupe ni hatari zaidi kuliko soda katika kusababisha kisukari hayajathibitishwa kisayansi. Na vyote hivi vikiungana vinaweza kuongeza hiyo hatari lakini huwezi kusema ya kwamba moja ni hatari zaidi kuliko nyingine.
Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwepo na chapisho linalodai kuwa matumzi wa wali mweupe yana hatari zaidi kuliko soda kwenye maambukizi ya kisuakari
Je ? ni upi uhalisia wa chapisho hilo linalodai kusambzwa kwenye mitandao ya kijamii nchini Tanzania.View attachment 3675925
Maambukizi ya sukari huwa yapoje?

I used to know sukari is a NCD.
 
Mm sio Dokta. Ila Ngoja niandike kwa ufupi ninavyojua.

Wanga (carbohydrates ) kuna kiwango hubadilika na kuwa sukari (glucose) na kuingia kwenye damu.
Soda ina Sukari pia kwa kiwango kikubwa.

Mtu ambaye anasema hanywi soda kwa sababu ya Sukari nyingi. Lakini anakula wali usiku au kutwa mara 2. Bado yuko kwenye hatari ile ile au zaidi ya kuongeza Sukari mwilini.

Ingawa Sukari inahitajika kwenye mwili, ila inatakiwa iwe kwa kiwango.

Na namna mwili unavyochakata sukari /wanga ni tofauti baina ya mtu na mtu. Na hii pia ni kwasababu ya Genes /DNA.

Kuna Mtu Hata akila sukari nyingi, mwili unachukua kiwango kinachohitajika na kukitoa kingne kwa njia ya mkojo.
Kuna wengine Ukila sukari nyingi, mwili unachukua kidogo na kuhifadhi kiwango kinachozidi na sio kukitoa kama taka mwili.

Na hapa ndio kuna tofauti.
Utakuta mtu mnene kupita kiasi, jua kuna aina ya madini ambayo yalitakiwa yatoke kama taka mwili, ila hayajatolewa , yanahifadhiwa na kuwa Fat. Including na Sukari.

Kwahiyo hii ni namna miili inatofautiana.
Mwingne ata ale kiasi gan cha vyakula hivi. Mwili unavitoa nje na sio kuhifadhi. Na ndio maana kuna watu hawanenepi hata wale vipi na kuna watu wananenepa tu hata kama anakula mlo mmoja.

Je! Utajuaje sukari imezidi?.
 
Je utajuaje Sukari imezidi?.

Kwanza, mwili utakuwa unahifadhi sukari inayozidi kwa muda mrefu, ila baadae utachoka na itaamua kutoa excess ya Sukar kwa njia ya mkojo.

Mfano, unaweza ukala kipande cha Keki, alafu dk 2 mbele Ubongo ukatoa taarifa kuwa mwili unahitaji maji, kwahiyo gafla ukasikia kiu kikali. Na ukanywa maji mengi.
(Wakat dk chache nyuma hukuwa unasikia kiu).

Ni ishara kuwa ile Sukar ya keki iliyoingia haiitajiki kwa wingi namna ile. Kwahiyo yale maji yataenda mwilini na kuiondoa ile excess sugar kwa mkojo ndan ya nusu saa.

Kwahiyo dalili ya kwanza kujua sukari imezidi ni kusikia kiu kikali. na ya pili ni kukojoa mara kwa mara.

Mfano. Umekula wali usiku, ukalala. Ila gafla ukasikia kiu . Ukanywa maji na usiku huo ukaenda kukojoa mara 5 au 6. Jua kuwa kuna kiwango cha sukari kimezidi na hakihutajiki.

Kwahiyo kwa Lugha nyepesi.
Dalili ya kujua Kisukari kimepanda ni Kiu (ili mwili uiondoe ile sukari kwa njia ya mkojo) na kukojoa mara kwa mara hasa usiku . Kwa sababu tushazoea vyakula vingi vya usiku ni wali. Na wali una sukari.

Kuna kisukari aina mbili.
Hii ni ile kisukari iliyo common.
Diabetes 2.

Je kuna madhara gan Sukari ikizidi?.
 
Kwahiyo kabla mwili wako haujachoka na Sukari kupanda.

Unaweza ukajipima mwenyewe jinsi gan Ukila vitu vya Sukari/wanga kwa wingi mwili wako unavyoreact.

Na jinsi gan hiyo sukari iliyozidi inavyotolewa mwilini.

Kunywa maji baada ya kula ni sawa, na kwenda kukojoa ni sawa. (Normal) . Ila ukiona unasikia kiu kali sana baada ya kula wanga au sukari, na baadae ukakojoa mara kwa mara ili sukari ile isiyohitajika itoke ndio kuna shida.

Kwahiyo Ukiona mwili wako unareact kwa hayo ya juu na ya post namba #9 jua huko miaka ya mbeleni una hatar ya sukari kupanda. Kwahiyo chukua hatua mapema. Kuupunguzia Mwili mzigo.

ina maana Punguza vyakula vyenye wanga na Sukari.
Mwili wako hauhitaj sukar ya namna hiyo uliyozoea kutumia.
 
Kwahiyo kabla mwili wako haujachoka na Sukari kupanda.

Unaweza ukajipima mwenyewe jinsi gan Ukila vitu vya Sukari/wanga kwa wingi mwili wako unavyoreact.

Na jinsi gan hiyo sukari iliyozidi inavyotolewa mwilini.

Ukiona mwili wako unareact kwa hayo ya juu post namba #9 jua huko miaka ya mbeleni una hatar ya sukari kupanda. Kwahiyo chukua hatua mapema. Kuupunguzia Mwili mzigo.
Asante kwa ilmu.

Ila mkuu mimi nilidhani kwa hiyo endless process ya kula sukari na kuhisi kiu, kunywa maji na kukojoa tayari inakuwa inasaidia so inakuwa haina hata ya kuchukua tahadhari yoyote unless mwili wako uwe haifanyi hizo processes
 
Mm sio Dokta. Ila Ngoja niandike kwa ufupi ninavyojua.

Wanga (carbohydrates ) kuna kiwango hubadilika na kuwa sukari (glucose) na kuingia kwenye damu.
Soda ina Sukari pia kwa kiwango kikubwa.

Mtu ambaye anasema hanywi soda kwa sababu ya Sukari nyingi. Lakini anakula wali usiku au kutwa mara 2. Bado yuko kwenye hatari ile ile au zaidi ya kuongeza Sukari mwilini.

Ingawa Sukari inahitajika kwenye mwili, ila inatakiwa iwe kwa kiwango.

Na namna mwili unavyochakata sukari /wanga ni tofauti baina ya mtu na mtu. Na hii pia ni kwasababu ya Genes /DNA.

Kuna Mtu Hata akila sukari nyingi, mwili unachukua kiwango kinachohitajika na kukitoa kingne kwa njia ya mkojo.
Kuna wengine Ukila sukari nyingi, mwili unachukua kidogo na kuhifadhi kiwango kinachozidi na sio kukitoa kama taka mwili.

Na hapa ndio kuna tofauti.
Utakuta mtu mnene kupita kiasi, jua kuna aina ya madini ambayo yalitakiwa yatoke kama taka mwili, ila hayajatolewa , yanahifadhiwa na kuwa Fat. Including na Sukari.

Kwahiyo hii ni namna miili inatofautiana.
Mwingne ata ale kiasi gan cha vyakula hivi. Mwili unavitoa nje na sio kuhifadhi. Na ndio maana kuna watu hawanenepi hata wale vipi na kuna watu wananenepa tu hata kama anakula mlo mmoja.

Je! Utajuaje sukari imezidi?.
Punguzeni ujuaji kwenye mambo msiyoyajua bora mbaki kuchambua Mpira na muzíki kwenye masuala ya mwili wa binadamu waachieni madokta na walimu basi.

Hivi sukari ukiitoa kwa njia ya mkojo hujui hiyo ni diabete mellitus tayari? Yani Figo lishindwe kunyonya sukari yote kurudisha mwilini half useme upo salama..... Hio ni ishara kubwa ya blood glucose ya juu kupindukia
 
Back
Top Bottom