SI KWELI Matumzi ya Wali mweupe yana hatari zaidi kuliko Soda kwenye kusababisha kisukari

SI KWELI Matumzi ya Wali mweupe yana hatari zaidi kuliko Soda kwenye kusababisha kisukari

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwepo na chapisho linalodai kuwa matumzi wa wali mweupe yana hatari zaidi kuliko soda kwenye maambukizi ya kisuakari
Je ? ni upi uhalisia wa chapisho hilo linalodai kusambzwa kwenye mitandao ya kijamii nchini Tanzania.
wali.jpg
 
Tunachokijua
Kisukari ni ugonjwa unaotokea wakati kiwango cha sukari kwenye damu (glukosi) kinapokuwa juu sana. Hali hii hutokea wakati kongosho lako halitengenezi insulini ya kutosha au halitengenezi kabisa, au mwili wako unaposhindwa kuitikia vizuri ufanyaji kazi wa insulini. Kisukari huathiri watu wa rika zote. Aina nyingi za kisukari ni za kudumu (kwa maisha yote), na aina zote zinaweza kudhibitiwa kwa dawa na/au kubadili mtindo wa maisha.

JamiiCheck imewasiliana na mtaalamu wa afya, Daktari Benard Kivuma kutoka Ifakara, Morogoro ambaye anafafanua uhalisia wa madai hayo.

Je, wali mweupe unasababisha kisukari?

Shahidi za kiutafiti zinaonesha kuwa ulaji mwingi wa wali mweupe, huu ambao tunatumia sana sana kila siku unahusishwa na ongezeko la hatari ya kupata kisukari ambao kwa jina la kitaalam tunaita type 2 diabetes. Vilevile matumizi ya mara kwa mara ya vinywaji vyenye sukari, kama hizi soda, pia nayo inahusishwa na ongezeko la hatari ya kupata kisukari.

Wali mweupe ni hatari zaidi kuliko soda?

Ila sio sahihi kusema ya kwamba wali mweupe ni hatari zaidi kuliko soda. Kwa sababu hivi vitu viwili havijatafitiwa katika kufanya ule ulinganisho wa moja kwa moja ambao unaweza kutuonyesha kusema kipi ni hatari kuliko kipi. Lakini pia hatari ya kisukari haiamuliwi na chakula kimoja pekee yake ambacho mtu anatumia.

Inahusishwa na vitu vingine ambavyo vinaunganishwa na hii, kama mlo ambao mtu anakula kwa ujumla kiasi anachokula, uzito wake wa mwili, shughuli anazofanya kila siku kama mazoezi na mambo mengine, historia pia ya familia ya ugonjwa huu. Kwa hiyo hivi vitu vyote vinajumuishwa katika kuongeza hatari ya kisukari.

Nini cha kufanya ili kupunguza athari ya wali mweupe na soda kwenye kuchochea uwezekano wa kupata kisukari?

Kwa hiyo cha muhimu kuzingatia ni kwamba taarifa kama hizi haziwezi zikatumika kwa ajili ya kufanya watu labda wawe na hofu ya kwamba wali ni, soda ipi ni bora na nini kwa sababu hazilinganishi. Lakini badala yake ni muhimu kuzingatia kiasi ambacho mtu anatumia.

Kwa hiyo kwenye chakula unatumia wali kiasi gani, unavyochanganya na mboga mboga nyingine za majani na vyakula vyenye nyuzi nyuzi, ambao tunaita fiber kwenye mlo, lakini pia kuongeza na protein pia na kupunguza unywaji wa vinywaji vyenye sukari.

Hii inasaidia katika kupunguza ile hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari. Lakini madai ya kwamba wali mweupe ni hatari zaidi kuliko soda katika kusababisha kisukari hayajathibitishwa kisayansi. Na vyote hivi vikiungana vinaweza kuongeza hiyo hatari lakini huwezi kusema ya kwamba moja ni hatari zaidi kuliko nyingine.
Ugali hatari, wali hatari, sasa tule nini ambacho si hatari?
hakuna kitu ambacho sio hatar.
as long as kikiliwa kwa wastan na kikaenda kutumika kwa wastani. Sio hatari.

Ila kikiliwa kingi na kisiende kutumika kingi. Ndio hatar.

Hata wanaokula Mboga mboga na vitamins. Nazo Zikizidi wataumwa vile vile.

damu ikizidi utaumwa. Ikipungua utaumwa.

Kwahiyo ni kujua mwili wako. Na stage uliyofikia (umri).
Kama kitu haukihitaji kwa wingi. Basi Usikitumie kwa wingi.

Pia mwili unatofautiana.
Mfano. Kuna mtu by nature tu unakuta hapend kula mavyakula ya sukari na kuna mtu utakuta anapenda kula kula . Yaan ushakaa na mtu alafu akasema nina hamu na kitu kitamu. Na anakunywa soda hata 3 kwa siku. Bado wali. Bado maandazi.
Je? Unaona mwili wake ulivyo? L. Atakuwa bonge.
Na Huyu miaka 15 mbele. Mwili utagoma kupokea tena sukar . Na ataumwa kisukari.
 
Asante mkuu... vp kuhusu kula wali usiku Ni sawa? nani aliyeweka ratiba ya kula usiku halafu tunalala na chakula hakifanyi kazi yoyote.....

Sijui nani alituchagulia wali.
Ila nadhani ni tamaduni.
Wali unaheshimika. Na ndio maana ukawekwa usiku ili Familia nzima ile.

Ila Usiku tunatakiwa kula chakula kilaini maana hakihitajiki.
Organ za mwili karibia zote zinafanya kaz nusu ya uwezo wake.

Hazihitaji nguvu/energy nyingi na hivyo hazihitaji chakula kingi.

Sasa kile chakula cha usiku kitahifadhiwa.
Kwahiyo ukifakamia mawali mengi. Yatahifadhiwa na kubadilishwa na kuwa Fat. Ili mwili uyatumie yakihitajika.

Sasa kama utaendelea tu kula mawali mengi. Na ambayo hayatumiki. Bas yataendelea kuhifadhiwa.
 
Halafu unakuta mtu tena saa 2 tu ameamkia supu na chapati.....

Unakuta ametuna ile mbaya...
 
Kwahiyo kabla mwili wako haujachoka na Sukari kupanda.

Unaweza ukajipima mwenyewe jinsi gan Ukila vitu vya Sukari/wanga kwa wingi mwili wako unavyoreact.

Na jinsi gan hiyo sukari iliyozidi inavyotolewa mwilini.

Kunywa maji baada ya kula ni sawa, na kwenda kukojoa ni sawa. (Normal) . Ila ukiona unasikia kiu kali sana baada ya kula wanga au sukari, na baadae ukakojoa mara kwa mara ili sukari ile isiyohitajika itoke ndio kuna shida.

Kwahiyo Ukiona mwili wako unareact kwa hayo ya juu na ya post namba #9 jua huko miaka ya mbeleni una hatar ya sukari kupanda. Kwahiyo chukua hatua mapema. Kuupunguzia Mwili mzigo.

ina maana Punguza vyakula vyenye wanga na Sukari.
Mwili wako hauhitaj sukar ya namna hiyo uliyozoea kutumia.

Heshima yako mkuu! Barikiwa.🤝🙏🙏
 
Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwepo na chapisho linalodai kuwa matumzi wa wali mweupe yana hatari zaidi kuliko soda kwenye maambukizi ya kisuakari
Je ? ni upi uhalisia wa chapisho hilo linalodai kusambzwa kwenye mitandao ya kijamii nchini Tanzania.View attachment 3675925
Sidhani kama Mitandao hiyo ya Kijamii imezingatia maelekezo ya Kisayansi au Ushauri wa Wataalam wa Afya.
Ninachoweza kusema 1. Kwa 100%; Kisukari sio Ugonjwa wa kuambukiza. Aliyesema hivyo arudi darasani au basi walau aGugo kupata undani wa kisukari (Diabetes).
2. Chapisho hilo halina Uhalisia.
Wali mweupe unahusiana na ugonjwa wa Beriberi
Soda inahusiana na Uchakavu wa Figo.
 
Sijui nani alituchagulia wali.
Ila nadhani ni tamaduni.
Hakuna aliyetuchagulia bali tumezaliwa na kujikuta tuko mazingira hayo.
Kila eneo lina chakula kikuu na pia kuna chakula kinachpendwa zaidi.
Ukienda Kagera, K'njaro utasikia sana habari za ndizi.
Ukija huku kwetu Umasaini utasikia sana habari za Ugali, maziwa, nyama
Ukienda kule nyanda zajuu kusini esp.Makete utasikia sana habari za viazi mviringo, Ugali n.k.
Lakini kote huko, Wali unapewa nafasi ya kipekee esp. kwenye sherehe, tafrija
na sikukuu.
Wali unaheshimika. Na ndio maana ukawekwa usiku ili Familia nzima ile.

Ila Usiku tunatakiwa kula chakula kilaini maana hakihitajiki.
Organ za mwili karibia zote zinafanya kaz nusu ya uwezo wake.

Hazihitaji nguvu/energy nyingi na hivyo hazihitaji chakula kingi.

Sasa kile chakula cha usiku kitahifadhiwa.
Kwahiyo ukifakamia mawali mengi. Yatahifadhiwa na kubadilishwa na kuwa Fat. Ili mwili uyatumie yakihitajika.

Sasa kama utaendelea tu kula mawali mengi. Na ambayo hayatumiki. Bas yataendelea kuhifadhiwa.
Utanenepa bure ilhali haupelekwi Mnadani/Buchani na matokeo yake ndo hayo Me wanakuwa na Viribatumbo na Ke Makebo
 
Halafu unakuta mtu tena saa 2 tu ameamkia supu na chapati.....

Unakuta ametuna ile mbaya...
Saa saba kasoro unamsikia anaanza kujisemesha sijui nimpigie mama hawa aniletee ubwabwa na nini!!!

Yaani wewe uliyekunywa chai saa nne hujui hata kama kuna mpango wa kula tena but yeye anataka aendelee kujaza tumbo
 
Ande taratibu.
Na Nimesha declare mm sio Dokta.
Na nimesema ninayoyajua.

Labda nikuulize ww.
Je ni Dokta?.

Pili, Figo sio imeshindwa kunyonya Sukari, ila Figo inaitoa hiyo sukari iliyozidi. Ambayo Haihitajiki.

Kiungo kinachodhibiti sukari ni Kongosho. Ndio kinafanya Sukar iingie kwa damu.
Sukar itaingia. Ila ikizidi sasa hata Figo inashindw kudhibiti.

Na sukar itatoka kwa njia ya mkojo.
Na ndio maana mkojo wa mtu wa kisukari sisimizi wataufuata. Kwa sababu ina masalia ya sukari.

Au labda sijakuelewa ulimaanisha nn
Sasa kama sio dokta na una elimu haba basi uwe unaongea stori tu za vijiweni

Figo inachuja damu, na vitu vinavorud mwili baada ya huo uchujaji ni glucose yote maana ni muhimu hivo narudia uwepo wa sukari kwenye mkojo ni ishara ya moja kwa moja una diabete mellitus, Figo haina kazi ya kupunguza sukari kwa njia ya mkojo katika mazingira yoyote ya kawaida ispokua ukiwa na sukari tu

Homoni zinazo control katika regular basis ni insulin na glucagon lakini katika survival mode ni adrenaline hizo mbili haziwez Tena

Mwisho nyinyi ndo mnapenda kujifanya mnajua kila vijiweni na hamna mnalojua
 
Figo inachuja damu, na vitu vinavorud mwili baada ya huo uchujaji ni glucose yote maana ni muhimu hivo narudia uwepo wa sukari kwenye mkojo ni ishara ya moja kwa moja una diabete mellitus, Figo haina kazi ya kupunguza sukari kwa njia ya mkojo katika mazingira yoyote ya kawaida ispokua ukiwa na sukari

Labda hatujaelewana.

Je moja ya dalili ya mgonjwa wa kisukari ni kusikia kiu kali na kukojoa mara kwa mara?.

Je Sukari ikiwa nyingi kwenye damu, (figo inachuja damu) , figo itaruhusu ile sukar kutoka kwa njia ya mkojo?.
Kuna Mtu Hata akila sukari nyingi, mwili unachukua kiwango kinachohitajika na kukitoa kingne kwa njia ya mkojo.

Neno langu ni hili, labda ww ndio unahoji na kusema Ninadanganya.

Basi naomba tuambie ww. Sukar iliyozidi mwilini inatolewaje?.
 
Kwahiyo kabla mwili wako haujachoka na Sukari kupanda.

Unaweza ukajipima mwenyewe jinsi gan Ukila vitu vya Sukari/wanga kwa wingi mwili wako unavyoreact.

Na jinsi gan hiyo sukari iliyozidi inavyotolewa mwilini.

Kunywa maji baada ya kula ni sawa, na kwenda kukojoa ni sawa. (Normal) . Ila ukiona unasikia kiu kali sana baada ya kula wanga au sukari, na baadae ukakojoa mara kwa mara ili sukari ile isiyohitajika itoke ndio kuna shida.

Kwahiyo Ukiona mwili wako unareact kwa hayo ya juu na ya post namba #9 jua huko miaka ya mbeleni una hatar ya sukari kupanda. Kwahiyo chukua hatua mapema. Kuupunguzia Mwili mzigo.

ina maana Punguza vyakula vyenye wanga na Sukari.
Mwili wako hauhitaj sukar ya namna hiyo uliyozoea kutumia.
Umeniogopesha!🙆🏽‍♀️
 
Umeniogopesha!🙆🏽‍♀️
According na mwana anaeumwa kisukari. Yeye alikuwa anajisikia hivyo mwez mzima . Ndio akaenda hosp akaambiwa Sukar imezidi.

Anasema alikuwa anakojoa mara 5 hadi 6 usiku. Na anasikia kiu kali sana kila akimaliza kula.
 
Mimi naona ni kawaida kama unakunywa maji mengi jamani!🫢
 
Mimi naona ni kawaida kama unakunywa maji mengi jamani!🫢

Kusikia kiu kikali je?.
Usiku una kunywa maji meng?.

Yeye akimaliza kula anasema alikuwa anasikia kiu kikali sana na anakunywa maji lita 1.
 
Kusikia kiu kikali je?.
Usiku una kunywa maji meng?.

Yeye akimaliza kula anasema alikuwa anasikia kiu kikali sana na anakunywa maji lita 1.
Hmm hapana mimi maisha yangu yote nakunywa sana maji mwisho saa12-1
 
Back
Top Bottom