SI KWELI Matumzi ya Wali mweupe yana hatari zaidi kuliko Soda kwenye kusababisha kisukari

SI KWELI Matumzi ya Wali mweupe yana hatari zaidi kuliko Soda kwenye kusababisha kisukari

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwepo na chapisho linalodai kuwa matumzi wa wali mweupe yana hatari zaidi kuliko soda kwenye maambukizi ya kisuakari
Je ? ni upi uhalisia wa chapisho hilo linalodai kusambzwa kwenye mitandao ya kijamii nchini Tanzania.
wali.jpg
 
Tunachokijua
Kisukari ni ugonjwa unaotokea wakati kiwango cha sukari kwenye damu (glukosi) kinapokuwa juu sana. Hali hii hutokea wakati kongosho lako halitengenezi insulini ya kutosha au halitengenezi kabisa, au mwili wako unaposhindwa kuitikia vizuri ufanyaji kazi wa insulini. Kisukari huathiri watu wa rika zote. Aina nyingi za kisukari ni za kudumu (kwa maisha yote), na aina zote zinaweza kudhibitiwa kwa dawa na/au kubadili mtindo wa maisha.

JamiiCheck imewasiliana na mtaalamu wa afya, Daktari Benard Kivuma kutoka Ifakara, Morogoro ambaye anafafanua uhalisia wa madai hayo.

Je, wali mweupe unasababisha kisukari?

Shahidi za kiutafiti zinaonesha kuwa ulaji mwingi wa wali mweupe, huu ambao tunatumia sana sana kila siku unahusishwa na ongezeko la hatari ya kupata kisukari ambao kwa jina la kitaalam tunaita type 2 diabetes. Vilevile matumizi ya mara kwa mara ya vinywaji vyenye sukari, kama hizi soda, pia nayo inahusishwa na ongezeko la hatari ya kupata kisukari.

Wali mweupe ni hatari zaidi kuliko soda?

Ila sio sahihi kusema ya kwamba wali mweupe ni hatari zaidi kuliko soda. Kwa sababu hivi vitu viwili havijatafitiwa katika kufanya ule ulinganisho wa moja kwa moja ambao unaweza kutuonyesha kusema kipi ni hatari kuliko kipi. Lakini pia hatari ya kisukari haiamuliwi na chakula kimoja pekee yake ambacho mtu anatumia.

Inahusishwa na vitu vingine ambavyo vinaunganishwa na hii, kama mlo ambao mtu anakula kwa ujumla kiasi anachokula, uzito wake wa mwili, shughuli anazofanya kila siku kama mazoezi na mambo mengine, historia pia ya familia ya ugonjwa huu. Kwa hiyo hivi vitu vyote vinajumuishwa katika kuongeza hatari ya kisukari.

Nini cha kufanya ili kupunguza athari ya wali mweupe na soda kwenye kuchochea uwezekano wa kupata kisukari?

Kwa hiyo cha muhimu kuzingatia ni kwamba taarifa kama hizi haziwezi zikatumika kwa ajili ya kufanya watu labda wawe na hofu ya kwamba wali ni, soda ipi ni bora na nini kwa sababu hazilinganishi. Lakini badala yake ni muhimu kuzingatia kiasi ambacho mtu anatumia.

Kwa hiyo kwenye chakula unatumia wali kiasi gani, unavyochanganya na mboga mboga nyingine za majani na vyakula vyenye nyuzi nyuzi, ambao tunaita fiber kwenye mlo, lakini pia kuongeza na protein pia na kupunguza unywaji wa vinywaji vyenye sukari.

Hii inasaidia katika kupunguza ile hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari. Lakini madai ya kwamba wali mweupe ni hatari zaidi kuliko soda katika kusababisha kisukari hayajathibitishwa kisayansi. Na vyote hivi vikiungana vinaweza kuongeza hiyo hatari lakini huwezi kusema ya kwamba moja ni hatari zaidi kuliko nyingine.
Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwepo na chapisho linalodai kuwa matumzi wa wali mweupe yana hatari zaidi kuliko soda kwenye maambukizi ya kisuakari
Je ? ni upi uhalisia wa chapisho hilo linalodai kusambzwa kwenye mitandao ya kijamii nchini Tanzania.View attachment 3675925
Sasa huo mimi

Sasa huo mimi si nitautia mchuzi rosti halafu utabadilika rangi na kuwa wa njano? Hapo vipi?
 
Punguzeni ujuaji kwenye mambo msiyoyajua bora mbaki kuchambua Mpira na muzíki kwenye masuala ya mwili wa binadamu waachieni madokta na walimu basi.

Hivi sukari ukiitoa kwa njia ya mkojo hujui hiyo ni diabete mellitus tayari? Yani Figo lishindwe kunyonya sukari yote kurudisha mwilini half useme upo salama..... Hio ni ishara kubwa ya blood glucose ya juu kupindukia
Humu kila mtu anachangia anachokijua sasa ni wewe msomaji kutumia akili zako kuamua uchukue lipi uache lipi so usimpangie mtu kusema anachohisi then aliendelea kufafanua post zake zilizofuata hata akatoa ushauri cha kufanya.
 
Asante kwa ilmu.

Ila mkuu mimi nilidhani kwa hiyo endless process ya kula sukari na kuhisi kiu, kunywa maji na kukojoa tayari inakuwa inasaidia so inakuwa haina hata ya kuchukua tahadhari yoyote unless mwili wako uwe haifanyi hizo processes

Inatakiwa process iende taratibu.
Sasa ww ukiona unakula wali alafu unakojoa mara 6 jua imetolewa sukar yote.

Inatakiwa angalau mara 1 au ukizidi sana ukojoe mara 2 ukishakula sukari.
Ila ukiona mwili unatoa sukar yote. Ina maana sukar iliyohifadhiwa inatosheleza . Na unayokula yote inatolewa.
 
We jamaa ni muongo sana na unaconfidence ya ajabu
 
Punguzeni ujuaji kwenye mambo msiyoyajua bora mbaki kuchambua Mpira na muzíki kwenye masuala ya mwili wa binadamu waachieni madokta na walimu basi.

Hivi sukari ukiitoa kwa njia ya mkojo hujui hiyo ni diabete mellitus tayari? Yani Figo lishindwe kunyonya sukari yote kurudisha mwilini half useme upo salama..... Hio ni ishara kubwa ya blood glucose ya juu kupindukia
Twende taratibu.
Na Nimesha declare mm sio Dokta.
Na nimesema ninayoyajua.

Labda nikuulize ww.
Je ni Dokta?.

Pili, Figo sio imeshindwa kunyonya Sukari, ila Figo inaitoa hiyo sukari iliyozidi. Ambayo Haihitajiki.

Kiungo kinachodhibiti sukari ni Kongosho. Ndio kinafanya Sukar iingie kwa damu.
Sukar itaingia. Ila ikizidi sasa hata Figo inashindw kudhibiti.

Na sukar itatoka kwa njia ya mkojo.
Na ndio maana mkojo wa mtu wa kisukari sisimizi wataufuata. Kwa sababu ina masalia ya sukari.

Au labda sijakuelewa ulimaanisha nn
 
Shida ni unatumiaje sukari inayoingia mwilini mwako...

Mfumo wa maisha ( unintentional daily lifestyle activities ) kwenye kutumia sukari iliyo mwilini ni bora kuliko mazoezi.

Vile vile aina ya sukari iliyo kwenye soda ambayo ina Fructose nyingi ni hatari zaidi kwa Maini yako.
 
Humu kila mtu anachangia anachokijua sasa ni wewe msomaji kutumia akili zako kuamua uchukue lipi uache lipi so usimpangie mtu kusema anachohisi then aliendelea kufafanua post zake zilizofuata hata akatoa ushauri cha kufanya.
Aseme yeye anachokijua.

asipandishe kisukari bure.
Pia anavyosema ni uongo. Aseme yeye nn ni cha kweli.

Juzi nimekaa na mgonjwa wa kisukari. Amenielezea mambo mengi. Amenielezea jinsi ilivyoanza kuhisi. Hadi kuumwa na anavyojisikia kwa sasa pia kama ni ya kurithi au ni mtindo wa maisha.

Kuna post nyuma nilisema kuwa kuna mshkaj wangu amepungua kilo 15 ndani ya miez 3 na anaumwa kisukari. Ndio huyo nilimwita tukala nae Kitimoto na Bia sehemu. Ni j2 ya juzi.
 
Duh..... Nianze kufanya utaratibu niachane nao.... Japokuwa its my delicious food...
Unajua shida sio kuacha wali.
Ila shida ni kula wali mwing zaid ya jinsi mwili unavyohitaji.

Shida sio kuacha kunywa soda au sukari .
Shida ni kunywa soda au kutumia sukar nying zaid ya mwili unavyohitaji.

Ww una miaka 50.
Alafu unakula wanga na Sukar na haufanyi mazoezi ili ile sukar na wanga utoke mwilini.
Unategemea nini?.

Ipo siku mwili utasema . Stop. Hatuhitaji tena sukari. Iko nying.
Na ndio shida inaanza.

Ila kama una pilika pilika. Tutumie kila kitu. As long as kinahitajika na kinatumika vizuri.
 
Asante mkuu... vp kuhusu kula wali usiku Ni sawa? nani aliyeweka ratiba ya kula usiku halafu tunalala na chakula hakifanyi kazi yoyote.....
 
Back
Top Bottom