Nimejiuliza sana inawezekana vipi gari ishambuliwe kwa risasi zaidi ya 20 dereva asijeruhiwe hata kidogo na TL ajeruhiwe na risasi chache?
Baada ya kufikiria sana nimegundua haya kwa hisia zangu
1.vioo tinted vimesaidia sana(utaelewa ukisoma namba mbili)
2.dereva kama ana uzoefu na ulinzi alimwambia TL alaze kiti na asishuke kwenye gari. Baada ya kulaza kiti kichwa chake kilikuwa usawa wa mlango wa nyuma. Ndio maana kuna risasi zilipigwa kwenye kioo usawa wa kichwa hazikumpata,zilizompata ni miguuni ambapo ukilaza kiti miguu bado inabaki mbele, na za tumboni kwasababu hata ukilaza na kurudisha kiti nyuma kama una kitambi tumbo linabaki mbele
3.dereva alishuka na kuinama au kusimama usawa wa mlango wa nyuma,hapa tena tinted ilisaidia kumficha.
Nawaza hapa lile agizo la kuondoa tinted lingetekelezwa sijui ingekuwaje!
Hizi ni hisia tu waliokuwepo ndio wanajua nini hasa kilitokea na bado sijapata jibu kwanini dereva aliamua kwenda nyumbani wakati amehisi anafuatiliwa.