Matuta yote barabara kuu za mikoa yaondolewe; vivuko viwekwe vya chini ya barabara watu wakimbize magari wawezavyo bila vikwazo. Itapunguza rushwa pia

Matuta yote barabara kuu za mikoa yaondolewe; vivuko viwekwe vya chini ya barabara watu wakimbize magari wawezavyo bila vikwazo. Itapunguza rushwa pia

India ina watu wengi mno duniani lakini barabara za mikoa ukiwasha gari unatimua mbio bila shida huoni tuta popote. Vijijini hata kuwe na wafugaji vipi barabara huwa na kivuko chini kipana tu cha kupitisha hadi mifugo kwa hiyo juu yanakuwa yanapita magari tu kwa spidi bila hofu ya kugonga kiumbe aitwaye binadamu au mfugo.

Hii itasaidia pia kupunguza rushwa za barabarani za "ohhh ume overspidi!"

Na wale askari wa tochi si vibaya wakatafutiwa majukumu mengine. Miendo ya taratibu inaharibu magari na kuchelewesha uchumi. Gari imetengezwa na spidi ili zifikiwe, sio urembo.
Haya mambo ya kila kitu kujilinganisha na nchi zingine kwa kila jambo kwa vigezo visivyo halisi sijui mtaacha lini. Unalinganisha kwa kigezo cha wingi wa watu?

Hapa suala ni uchumi.
Gharama ya kujenga tuta na kujenga handaki au njia ya chini kupitisha watu ipi kubwa?
Je, kwa barabara zetu nchi nzima na kila kijiji zilipopita barabara kuu tutajenga vivuko vingapi vya chini au juu?
Je, uchumi wetu unaruhusu kubeba gharama za huo uchumi kama India?

Sio Magufuli aanze kuwakamua kodi zaidi ili ajenge hizo vivuko mnaanza kumtukana na kubeza kuwa anabana
 
Naunga mkono hoja matuta katika Highway ni makosa ila kuweka speed limit tuseme 120Kmph nakubali na kama issue kuna watu wanasema wanakusanya kodi toza alfu 30 per trip acha watu wakimbize gari kwa speed itakawekwa kama max 120 sasa kama wewe haki ukitaka kutembea 50 au 80 shauri yako. kuna sehemu wanaweka 30KPH unabaki unakanyaga break tu. Ila 50 zimezidi kwa kweli hata kijiji nyumba 3 tu 50.
 
Tanzania katika vitu vinakufa haraka ni Breki
Yaani ni break driving njia nzima mtu unaenda long safari muda wote mguu uko kwenye Breki loool
 
Back
Top Bottom