Mauaji holela watuhumiwa wakiwa ni Polisi, tusisitize Uchunguzi

Mauaji holela watuhumiwa wakiwa ni Polisi, tusisitize Uchunguzi

Hili swala litaiondolea chadema umaarufu ujambazi uatesa watu kazanieni tozo ila sio ujambazi.
Hivi,wanakuja polisi nyumbani kwako na kuomba wakutane na mtoto wako(mjomba,mpwa au yeyote).Unamuita na wanamuhoiji/ongea naye.Baadaye wanaondoka naye wakidai ni kwa mahojiano zaidi kituoni kwani ni mtuhumiwa wa shauri fulani.Unafuatilia huko kituoni unaambiwa wameondoka naye hapo kituoni ameenda kuonesha vitu au silaha.Kesho yake unapewa taarifa kwamba nduguyo kapigwa risasi na kufa huko maporini.
Unapouliza kisa,unaambiwa nduguyo alikuwa anawakimbia askari huku anajibizana nao/kurushiana risasi kwa bunduki aina ya SMG.Sikupi maswali ya kukuongoza.Utapata picha gani hapo kwa hiyo hadithi?
 
Hatuwezi kutatua matatizo yetu wenyewe had uende ICC??? au umerukwa na akili unaelewa ICC inashughulika na mashauri ya aje?

Kwani wewe ni polisi ndugu? ICC husikiliza yakiwamo haya ambayo kesi hakimu nyani, watuhumiwa nyani na maofisa ushitaki nao ni nyani pia.

Hudhani kunawafaa sana huko ndugu Ili haki itendeke dhidi ya wanayoita "impunity?"
 
Nadhani kuna haja ya jeshi la polisi kufumiliwa kila eneo!
Mapolisi wameshakuwa na hulka kuwa wao wanaruhusiwa kuua wapendavyo na imezoeleka hivyo!
Wameshaona kuwa watawala huwa wanawapandisha vyeo kwa kuua, kutesa na kubambikizia watu kesi!
Nimesikia kile kitendo cha kishetani (nahisi hata shetani hawezi kufanya hili) cha kumlazimisha binti kulala na baba yake kabla ya kumuua baba yule!
Dhambi na laana hizi zitawagharimu ninyi, watoto na wajukuu zenu milele na milele!
 
Kwani wewe ni polisi ndugu? ICC husikiliza yakiwamo haya ambayo kesi hakimu nyani, watuhumiwa nyani na maofisa ushitaki nao ni nyani pia.

Hudhani kunawafaa sana huko ndugu Ili haki itendeke dhidi ya wanayoita "impunity?"
Hili shauri kila anaecomment tofauti unadhani ni polisi akili zako mbovu!!….
Iundwe kamati huru za kushughulikia makosa yanayofanywa na polisi!! na kuwajibisha
 
Hili shauri kila anaecomment tofauti unadhani ni polisi..
Huu ni unyonge wa kifikra na kutojiamini.
Hii hali inawakumba watanzania wengi sana, hata wale wanaoonekana ni wasomi nao wana shida hii.

Btw, kama anaye comment ni polisi ndiye haswa anahitajika ili ajibu hoja husika.
Huu woga sijui unasababishwa na nini!
 
Huu ni unyonge wa kifikra na kutojiamini.
Hii hali inawakumba watanzania wengi sana, hata wale wanaoonekana ni wasomi nao wana shida hii.

Btw, kama anaye comment ni polisi ndiye haswa anahitajika ili ajibu hoja husika.
Huu woga sijui unasababishwa na nini!
watu wamedumaa kiakili hawataki wazo tofauti na wanachokiwaza!! Mtu wa hivo kuona suluhu ya matatizo ni ngumu kwan ana mawazo mgando
 
Hatuwezi kutatua matatizo yetu wenyewe had uende ICC??? au umerukwa na akili unaelewa ICC inashughulika na mashauri ya aje?
Hatuwezi kama wote tu CHAWA kama wewe chawa mkubwa wetu! ICC naielewa kuliko wewe....... you need international attention, how do you get to the international community to know what is going on in Tanzania? Ukitaka kuwa msanii anayejulikana fanya kinyume cha kawaida, utajulikana and then you proceed in line with the reactions/responses you get!
 
Hili shauri kila anaecomment tofauti unadhani ni polisi akili zako mbovu!!….
Iundwe kamati huru za kushughulikia makosa yanayofanywa na polisi!! na kuwajibisha

Joined yesterday. Umeguswa? Au nawe ni mmoja wao?

Hiiiiiii bagosha!

Hivi polisi wawili tukiwatambua kwa comment zao tatizo liko wapi ndugu?
 
Hakuna maendeleo kama Kuna uhalifu.
Nchi zote zilizoendelea walianza kuutokomeza uhalifu na wanaounga mkono Wahalifu. Afrika uhalifu ni mkubwa sana . Hata Tanzania. Watu wansjenga nyumba Kwa gharama kubwa sana. Mageti ,maukuta marefu mpaka Hewa inakosekana kisa Wahalifu. Hizo pesa za kujenga maukuta zingetumika hata kutoa sadaka Kwa maskini . Leo kila mtu ni ukuta na mageti ya chuma kwenye milango. Uhalifu ni mkubwa sana. Wahalifu wananyima watu usingizi. Wahalifu wanatamba na Wana mtandao mkubwa ndani na nje ya nchi.

Wahalifu ni adui mkubwa wa maendeleo ya mtu mmoja mmoja.
Kwa Sasa teknolojia ni kubwa sana haihitaji Tena uchunguzi mkubwa kuwabaini Wahalifu. Kwa Sasa Polisi wanatumia teknolojia kuwabaini Wahalifu.

Hivi Panya rodi unafikiri wanaowatuma ni watu unaoweza kuwabaini Kwa kutaka ushahidi wa kuwaona kwenye tukio. Wale wanaonekana kwa kutumia teknolojia. Polisi Kwa Sasa hawakamati mtu Kwa kimsingizia . Na dawa ya hao Wahalifu wanaotengene Vikundi vya kihalifu ni kuwapiga risasi TU hakuna namna ya kuwaacha. Ukiwapeleka mahakamani wanatoka asubuhi saa Tatu. Wanahonga na Wanapesa ,watahonga Wapelelezi,watahonga mahakimu ,watahonga waendesha mashitaka ,wataweka mawakili. Raia waliotoa Taarifa watadhiriwa na hao Wahalifu au hata kuuawa.

Hao wanaosema uchunguzi ufanyike ni wanufaika wa uhalifu.

Pesa za ugaidi zimeanza kupenyezwa nchini hili liko wazi.
Na mbinu za wale Magaidi wanazotumia ni kuhakikisha Polisi hawana nguvu ya kupambana nao. Na wakishafanikiwa kulifanya Jeshi la Polisi kuwa kama Chui wa Karatasi basi watakarisha mipango yao Kwa muda mfupi na baadae utaona shughuli za kigaidi zikishamiri.

Mapesa ya kigaidi yameshaanza kumwagwa hasa kwenye Chama Cha ACT Panya road. Hiki Chama kimulikwa sana. Ni ukweli kabisa ni chama hatari. Wamesikia Mwinyi anaimarisha Uchumi wa Zanzibar na hata mpango wa kuchimba mafuta. Wale Mabeberu hawapendi mafuta yachimbwe Zanzibar na hata Tanzania.

Wanawatumia wanaharakati na wanasiasa na waandishi wa habari uchwara.

Serikali iwe makini sana na Hawa mawakala wa ugaidi na uhalifu.

Kila mtu afanye kazi yake kihalali na sio wizi.
Wahalifu wa kutumia silaha wanatakiwa watokomezwe kwa risasi sio Kwa pingu.

Anayewatetea Magaidi na mbinu za ugaidi na mikakati ya kigaidi naye apigwe risasi mchana kweupe.
Hakuna maendeleo ya watu bila usalama.

Nchi zote zilimaliza uhalifu Kwa mtutu wa bunduki sio karatasi na kalamu.

Tukiwa na Majeshi legelege Kuna siku hata hakimu atapigwa makofi na watuhumiwa halafu tutasema ni haki yao kujitetetea. Hakimu na Jaji anashika kalamu na karatasi lakini usalama wake na ujasiri wake ni Kwa sababu Kuna Polisi aliyeshika bunduki yenye risasi ya moto inayoua binadamu asiyetii SHERIA . Hakuna kutii SHERIA kokote Duniani kama hakuna nguvu ya risasi.

Kuna mambo Mengi ya kupigania lakini sio kupigania Wahalifu . Hapana.
Kuna Mambo ya Bima ya Afya.
Kuna mambo ya Ada kubwa ya vyuo wakati wazazi ni wale wale walioshimdwa kulipa Elfu 20 ya ada shule ya sekondari. Chuoni wanatakiwa kutoa ada Mili mbili. Haya wanaharakati wapumbavu hawayasemei. Hawajui kuwa watu wanahitaji maisha yawe marahisi na sio kuona Wahalifu wakistawi.
Polisi wakiambiwa hata wasiwe na bunduki hasara sio kwao hasara ni Kwa jamii ambayo itawapa Wahalifu heshima.

Matumizi ya serikali ni makubwa sana wanaharakati na Chama Cha panyarodi na Magaidi Cha ACT hawasemi. Hii nchi Kwa mwaka inaagiza magari Mengi sana ya kifahari Kwa watawala wakati hawaagizi Ambulance kila kata. Wanasiasa uchwara hawasemi wanataka kudhibiti Polisi ili ugaidi uingie kirahisi.
.Amiri Jeshi mkuu inabidi awe makini na wanasiasa na wapambe wa ugaidi Wana mtandao mkubwa sana.
 
Back
Top Bottom