SI KWELI Mauaji mapya Kibiti: Serikali iweke hadharani idadi ya askari na raia waliouawa mpaka sasa

SI KWELI Mauaji mapya Kibiti: Serikali iweke hadharani idadi ya askari na raia waliouawa mpaka sasa

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kwa taarifa za uhakika ni kuwa tangu January hadi sasa sio chini ya askari 20 walikwisha uwawa ila serkali Inafanya siri hata sisi hatukuruhusiwa kufika KIBITI kwa kuambiwa kuwa mkuu wa wilaya na kamati yake ya ulinzi na usalama hawaruhu Kwa kuwa eneo ni hatari sana.

IMG_8260.jpeg

Kwa taarifa za uhakika ni kuwa wale magaidi wa kipindi cha magufuli wamerudi Kwa kasi wana silaha nzito za moto huku idadi ya askari ikiwa ndogo baada ya eneo kuonekana shwali baada ya operation ya kipindi cha magufuli

Nitoe wito kwa serikali iweke wazi ili raia wajue nini kiaendelea rufiji kwa umma isifanye Siri huku hali ikizidi kuwa mbaya.

USSR
 
Tunachokijua
Jeshi la polisi nchini kupitia akaunti yake rasmi inayopatikana kwenye Mtandao wa X (zamani Twitter) limekanusha ujumbe unaosambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kusema kuwa hakuna matukio kama hayo, Kibiti ni shwari na salama.

Limewataka wananchi kupuuza ujumbe huu pamoja na wote wasioitakia mema nchi yetu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo mauaji yanayojumuisha eneo la Mkuranga, Kibiti na Rufiji (MKIRU) yalianza mapema Januari 2015 yakihusishwa na vikundi vya vijana wanaopata mafunzo kutoka kwenye kundi la al-Shabaab nchini Somalia.

Kwa mujibu wa Gazeti la Jamhuri, Kwa miaka minne hadi mitano hadi kuanza kwa mauaji haya, vijana kadhaa kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Rufiji, hasa Ikwiriri, wamekuwa wakisajiliwa na kundi hilo la kigaidi, huku wazazi wao wakiambulia ujira wa dola 3,000 za Marekani (zaidi ya Sh milioni 6).

Akizungumza na JAMHURI, mmoja wa wakazi wa Ikwiriri ambaye hakupenda kutajwa jina lake gazetini kwa sababu za kiusalama, alisema kumekuwa na wimbi la vijana wenye umri wa miaka 16-25 kupelekwa kwenye mafunzo huko Somalia.

“Hapa Ikwiriri katika kipindi cha miaka kama mitano iliyopita kumekuwa na wimbi la vijana wadogo kupelekwa Somalia. Inasemekana wanakwenda kujiunga na kikundi cha al-Shabaab, lakini vijana hao wamekuwa wanapatikana kupitia kwa mawakala kadhaa kwenye misikiti.

Si kweli kwamba polisi hapa Ikwiriri hawajui, maana hata ukifuatilia wale viongozi wa vijiji ambao wamekuwa wakitoa taarifa za vijana hao wamekuwa wakiuawa kwa staili inayofanana… sasa hapo unaweza kuona namna zoezi (kazi) linavyokuwa gumu,”
alisema.
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani wakati ule, Mwigulu Nchemba, yeye kwa upande wake aliwahi kunukuliwa akidai "mauaji hayo yana harufu ya kisiasa," na kuhoji "Ujambazi gani huo wa Wana CCM tu? Hako kamchezo tumeshakagundua. Dhahiri, huo ni ushamba wa vyama vingi.”

Waziri Mwigulu alikwenda mbali zaidi na kudai kuwa chanzo cha mauaji hayo ni chuki za vyama vya upinzani dhidi ya CCM.

Aidha, aliyekuwa Rais wa awamu ya 5 Hayati Magufuli aliwahi kuagiza Jeshi la Polisi kuhakikisha linakomesha mauaji haya ya raia wasio na hatia.

Mei 4, 2018, Zitto Kabwe akiwa Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo alitoa hotuba Bungeni akibainisha kuwa zaidi ya Watanzania 380 walikuwa wamepotea huko MKIRU.
Mimi hii taarifa nashawika kuamini kwa kiasi fulani.Lakini nina mashaka na hiyo idadi ya mauaji.Mwananchi imeripoti kuvamiwa na kuuawa kwa Mwalimu wa kike Msemwa na Mtoto wake kujeruhiwa vibaya .Na Serikali ikiiamini hii taarifa itachukuwa hatua mapema.
Hawakusema kuhusu na askari pia

USSR

Sent from my TECNO B1c using JamiiForums mobile app
 
Juzi tumetoka mbeya kuzika ndugu yetu (mwanajeshi) yeye mkewe na mtoto wa maika minne waliowawa na magaidi KIBITI Kwa kinachodaiwa kuwa ni wanajihadi wenye imani Kali sana .

Kwa taarifa za uhakika ni kuwa tangu January hadi sasa sio chini ya askari 20 walikwisha uwawa ila serkali Inafanya siri hata sisi hatukuruhusiwa kufika KIBITI kwa kuambiwa kuwa mkuu wa wilaya na kamati yake ya ulinzi na usalama hawaruhu Kwa kuwa eneo ni hatari sana.

Kwa taarifa za uhakika ni kuwa wale magaidi wa kipindi cha magufuli wamerudi Kwa kasi wana siraha nzito za moto huku idadi ya askari ikiwa ndogo baada ya eneo kuonekana shwali baada ya operation ya kipindi cha magufuli

Nitoe wito kwa serkali iweke wazi ili raia wajue nini kiaendelea rufiji Kwa umma isifanye Siri huku hali ikizidi kuwa mbaya .

NOTE

story hii pia unaweza kuisoma kupitia gazeti la MWANANCHI Kwa nyongeza .

USSR

Sent from my TECNO B1c using JamiiForums mobile app
Pole sana kwa kufiwa na ndugu zako. Swala lolote la usalama wa wote, ni paramount, tunaomba uweke taarifa ya kina. Kama ni kweli, hao wanaoficha wanatakiwa kuwekwa kwenye kundi la wauaji, kwa maana hawataki watu wachukue tahadhari.
 
Hiyo njia siku hizi ina magari mengi ya kifahari yenye watu wenye ndevu mithili ya DW, siku moja nilitazama nikajiuliza hivi hawa wanakwenda wapi?
Na kupitia DP, wataingia wengi.
 
Kiti kakalia ndugu yao...bandari zimepewa ndugu zao hiyo jihadi wanamfanyia nani?
Wakati mwingine ugaidi huwa unafanywa na upande mwingine au watu ambao wana malengo mabaya na au kutaka kufanikisha kitu
Haya mambo ni mapana sana katika Dunia hii

Wanaweza wakasontea kidole huko kumbe ni huku, tafakari sana hata Oclahoma bombing USA walitangaza ni waislam magaidi kumbe alikuwa ndugu yao muzungu
 
Huwa kuna jambo linaandaliwa,huenda kuna watu wanaviziwa kukamatwa na kupewa kesi za ugaidi ama sirikali inatafuta sababu ya kupiga marufuku mikutano ya kisiasa kwa kisingizio cha usalama!!

Masheikh kabla ya kukamatwa enzi za Kikwete yalimea mambo ya ugaidi.

Jana IGP karindima kuna watu wanataka kupindua Samia!!
Hao hawawezi kumpindua muislam mwenzao. Umeona pale walipofanya mauaji ya kutisha kule Kenya. Walikuwa wanauliza dini yako, ukisema ni muislam, unaulizwa maswali ya dini ya kiislam, ukishindwa kujibu kwa usahihi, au ukasema ni mkristo, unauawa mara moja.
 
Pia katika awamu hii kuna ongezeko la vijana Watanzania wanaoenda kujiunga na vikundi vya kigaidi nje ya nchi.
Kila anapoingia rais muislam ,vijana wengi sana hupelekwa Somalia kujifunza ugaidi
 
Juzi tumetoka mbeya kuzika ndugu yetu (mwanajeshi) yeye mkewe na mtoto wa maika minne waliowawa na magaidi KIBITI Kwa kinachodaiwa kuwa ni wanajihadi wenye imani Kali sana .

Kwa taarifa za uhakika ni kuwa tangu January hadi sasa sio chini ya askari 20 walikwisha uwawa ila serkali Inafanya siri hata sisi hatukuruhusiwa kufika KIBITI kwa kuambiwa kuwa mkuu wa wilaya na kamati yake ya ulinzi na usalama hawaruhu Kwa kuwa eneo ni hatari sana.

Kwa taarifa za uhakika ni kuwa wale magaidi wa kipindi cha magufuli wamerudi Kwa kasi wana siraha nzito za moto huku idadi ya askari ikiwa ndogo baada ya eneo kuonekana shwali baada ya operation ya kipindi cha magufuli

Nitoe wito kwa serkali iweke wazi ili raia wajue nini kiaendelea rufiji Kwa umma isifanye Siri huku hali ikizidi kuwa mbaya .

NOTE

story hii pia unaweza kuisoma kupitia gazeti la MWANANCHI Kwa nyongeza .

USSR

Sent from my TECNO B1c using JamiiForums mobile app
Hawa Magaidi wamerudije tena huko MKIRU wakati baada ya Oparesheni ile Kali iliyopelekea Wengi wao ( Magaidi ) Kuuwawa kuliundwa Kambi ya Kijeshi huko huku Makomandoo wakimwagwa kwa Wingi pamoja na Wanajeshi wa Kawaida na Watu wa Usalama wa Taifa ( TISS ) nao wamemwaga kwa Uwingi huko?
 
Back
Top Bottom