SI KWELI Mauaji mapya Kibiti: Serikali iweke hadharani idadi ya askari na raia waliouawa mpaka sasa

SI KWELI Mauaji mapya Kibiti: Serikali iweke hadharani idadi ya askari na raia waliouawa mpaka sasa

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kwa taarifa za uhakika ni kuwa tangu January hadi sasa sio chini ya askari 20 walikwisha uwawa ila serkali Inafanya siri hata sisi hatukuruhusiwa kufika KIBITI kwa kuambiwa kuwa mkuu wa wilaya na kamati yake ya ulinzi na usalama hawaruhu Kwa kuwa eneo ni hatari sana.

IMG_8260.jpeg

Kwa taarifa za uhakika ni kuwa wale magaidi wa kipindi cha magufuli wamerudi Kwa kasi wana silaha nzito za moto huku idadi ya askari ikiwa ndogo baada ya eneo kuonekana shwali baada ya operation ya kipindi cha magufuli

Nitoe wito kwa serikali iweke wazi ili raia wajue nini kiaendelea rufiji kwa umma isifanye Siri huku hali ikizidi kuwa mbaya.

USSR
 
Tunachokijua
Jeshi la polisi nchini kupitia akaunti yake rasmi inayopatikana kwenye Mtandao wa X (zamani Twitter) limekanusha ujumbe unaosambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kusema kuwa hakuna matukio kama hayo, Kibiti ni shwari na salama.

Limewataka wananchi kupuuza ujumbe huu pamoja na wote wasioitakia mema nchi yetu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo mauaji yanayojumuisha eneo la Mkuranga, Kibiti na Rufiji (MKIRU) yalianza mapema Januari 2015 yakihusishwa na vikundi vya vijana wanaopata mafunzo kutoka kwenye kundi la al-Shabaab nchini Somalia.

Kwa mujibu wa Gazeti la Jamhuri, Kwa miaka minne hadi mitano hadi kuanza kwa mauaji haya, vijana kadhaa kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Rufiji, hasa Ikwiriri, wamekuwa wakisajiliwa na kundi hilo la kigaidi, huku wazazi wao wakiambulia ujira wa dola 3,000 za Marekani (zaidi ya Sh milioni 6).

Akizungumza na JAMHURI, mmoja wa wakazi wa Ikwiriri ambaye hakupenda kutajwa jina lake gazetini kwa sababu za kiusalama, alisema kumekuwa na wimbi la vijana wenye umri wa miaka 16-25 kupelekwa kwenye mafunzo huko Somalia.

“Hapa Ikwiriri katika kipindi cha miaka kama mitano iliyopita kumekuwa na wimbi la vijana wadogo kupelekwa Somalia. Inasemekana wanakwenda kujiunga na kikundi cha al-Shabaab, lakini vijana hao wamekuwa wanapatikana kupitia kwa mawakala kadhaa kwenye misikiti.

Si kweli kwamba polisi hapa Ikwiriri hawajui, maana hata ukifuatilia wale viongozi wa vijiji ambao wamekuwa wakitoa taarifa za vijana hao wamekuwa wakiuawa kwa staili inayofanana… sasa hapo unaweza kuona namna zoezi (kazi) linavyokuwa gumu,”
alisema.
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani wakati ule, Mwigulu Nchemba, yeye kwa upande wake aliwahi kunukuliwa akidai "mauaji hayo yana harufu ya kisiasa," na kuhoji "Ujambazi gani huo wa Wana CCM tu? Hako kamchezo tumeshakagundua. Dhahiri, huo ni ushamba wa vyama vingi.”

Waziri Mwigulu alikwenda mbali zaidi na kudai kuwa chanzo cha mauaji hayo ni chuki za vyama vya upinzani dhidi ya CCM.

Aidha, aliyekuwa Rais wa awamu ya 5 Hayati Magufuli aliwahi kuagiza Jeshi la Polisi kuhakikisha linakomesha mauaji haya ya raia wasio na hatia.

Mei 4, 2018, Zitto Kabwe akiwa Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo alitoa hotuba Bungeni akibainisha kuwa zaidi ya Watanzania 380 walikuwa wamepotea huko MKIRU.
Juzi tumetoka mbeya kuzika ndugu yetu (mwanajeshi) yeye mkewe na mtoto wa maika minne waliowawa na magaidi KIBITI Kwa kinachodaiwa kuwa ni wanajihadi wenye imani Kali sana .

Kwa taarifa za uhakika ni kuwa tangu January hadi sasa sio chini ya askari 20 walikwisha uwawa ila serkali Inafanya siri hata sisi hatukuruhusiwa kufika KIBITI kwa kuambiwa kuwa mkuu wa wilaya na kamati yake ya ulinzi na usalama hawaruhu Kwa kuwa eneo ni hatari sana.

Kwa taarifa za uhakika ni kuwa wale magaidi wa kipindi cha magufuli wamerudi Kwa kasi wana siraha nzito za moto huku idadi ya askari ikiwa ndogo baada ya eneo kuonekana shwali baada ya operation ya kipindi cha magufuli

Nitoe wito kwa serkali iweke wazi ili raia wajue nini kiaendelea rufiji Kwa umma isifanye Siri huku hali ikizidi kuwa mbaya .

NOTE

story hii pia unaweza kuisoma kupitia gazeti la MWANANCHI Kwa nyongeza .

USSR

Sent from my TECNO B1c using JamiiForums mobile app
Tukushukuru kwa taarifa uliyoleta hapa.

Naona kila mtu anao mchango wake wenye manufaa katika jukwaa hili, bila kujali anasimamia wapi kisiasa.

Ninahofia, safari hii Tanzania inaweza kuchakazwa sana, pengine ndio mwanzo wa hali ile inayoonekana Somalia, au kule nchi za Sahel, Mali Niger, Burkina Faso na kwingineko.

Kidogo Kenya wao wamekwisha jizoelea na hali hiyo Kaskazini Mashariki ya nchi hiyo.
Pengine na sisi itatulazimu tuizoee tu, na maisha yaendelee, pale inapowezekana.

Hao jamaa watakuwa wamechagua wakati mzuri sana wa kulianzisha pya.

Sasa tutafanyeje, tukawaombe msaada Rwanda, maanake ndio pekee wanaoonekana kuwamudu wa aina hiyo.
 
Tubishane, tukosoane, tutofautiane, lakini siyo kuuana. Kuuana ni ushetani, ni unyama wa hali ya juu. Mtu kama anaona kifo cha binadamu mwenzake ni jambo la mzaha, huyo ina maana dhamira yake, kama mwanadamu, imekufa.

Wape pole waliopatawa na magumu haya. Kila aliyewahi kufiwa anajua machungu ya kufiwa. Lakini kifo cha kuuawa, kwa vyovyote kitakuwa kinaumiza zaidi kuliko kifo cha kawaida.
Kwani sababu ya kuuana ni nini mkuu 'Bams'?
Mi nadhani ni kuwafanya wote wanaopingana na kundi hilo la wauaji, wajisalimishe kwa matakwa ya.
Ikisha kuwa hivyo, mauaji yanakoma. Mfano mzuri ni Afghanistan, sasa hivi kwa vile kila mtu ali'submit' kwa matakwa ya mjahdin, nchi ipo shwari.

Hapa kwetu inawezekana hao watu wanatafuta eneo la kusimika himaya yao. Wakifanikiwa kuliteka eneo lote la mwambao, watakuwa wamefanikiwa sana, sidhani kuwa watakuwa na hamu ya kupeleka vita vyao mbali na eneo hilo.
 
Nimesoma muda si mrefu tweeter akaunti inavyoitwa Tanzania Abroad kuwa kuna miili 12 ya watu imegunduliwa Kibiti.
Taarifa hiyo inatoa wito kuwa kama kuna mtu ana Ndugu hajulikani alipo atoe taarifa.
 
Tukushukuru kwa taarifa uliyoleta hapa.

Naona kila mtu anao mchango wake wenye manufaa katika jukwaa hili, bila kujali anasimamia wapi kisiasa.

Ninahofia, safari hii Tanzania inaweza kuchakazwa sana, pengine ndio mwanzo wa hali ile inayoonekana Somalia, au kule nchi za Sahel, Mali Niger, Burkina Faso na kwingineko.

Kidogo Kenya wao wamekwisha jizoelea na hali hiyo Kaskazini Mashariki ya nchi hiyo.
Pengine na sisi itatulazimu tuizoee tu, na maisha yaendelee, pale inapowezekana.

Hao jamaa watakuwa wamechagua wakati mzuri sana wa kulianzisha pya.

Sasa tutafanyeje, tukawaombe msaada Rwanda, maanake ndio pekee wanaoonekana kuwamudu wa aina hiyo.
Mkuu Rwanda? Serious.......
Unataka kumleta PakaShume Jikoni?
This Saga is Complicated, lakini amini kwamba Rwanda sio watu wema.
 
Kwani sababu ya kuuana ni nini mkuu 'Bams'?
Mi nadhani ni kuwafanya wote wanaopingana na kundi hilo la wauaji, wajisalimishe kwa matakwa ya.
Ikisha kuwa hivyo, mauaji yanakoma. Mfano mzuri ni Afghanistan, sasa hivi kwa vile kila mtu ali'submit' kwa matakwa ya mjahdin, nchi ipo shwari.

Hapa kwetu inawezekana hao watu wanatafuta eneo la kusimika himaya yao. Wakifanikiwa kuliteka eneo lote la mwambao, watakuwa wamefanikiwa sana, sidhani kuwa watakuwa na hamu ya kupeleka vita vyao mbali na eneo hilo.
Upo serious Mkuu?
Ni mchango wako ndio, na upo huru kuutoa lakini dah......
 
Pande hizi mambo hufanyika kimya kimya, sio kama huko mbele
 
Yaani JF nanyi mmefikia hatua ya kusema hii taarifa uzushi kwakuwa jeshi la polisi limekanusha? Mnakumbuka "SISITV" ya Kamanda "ZIRO"? Mimi nilitarajia nyinyi ndiyo mmeconfirm kwamba ni uzushi kwasababu ya kufanya uchunguzi kwa kumtuma mwanahabari wenu wa uchunguzi/Ukachero na kuja na taarifa.

Taarifa za polisi si za kuziamini kwa 100%.
 
Hi Jamii Check ni siasa tu yaani unapinga uzi kwa kutumia taarifa ya taasisi inayotuhumiwa kuficha ukweli...nilijua Mn communicate na watu waliopo ground tupate taarifa za uhakika kumbe another trash from government sources.
 
Hivi walioteka ndege na kuwaua watu mamia kule world trade centre, hawakuwa waislam?

Mohamed Atta (Egyptian),
Abdulaziz al-Omari (Saudi Arabian), Wail al-Shehri (Saudi Arabian),
Waleed al-Shehri (Saudi Arabian), Satam al-Suqami (Saudi Arabian).

Mehmet Ali Agca, aliyempiga risasi Papa John Paulo wa 2, hakuwa muislam?

Wanaojilipua kule Somalia, kuwaua binadamu wenzao, wakidai wanataka Somalia iongozwe kwa sharia law, siyo waislam?
Hivi yule adolf hitler aloua mamilioni ya watu hakuwa mkristo? Aliyemua JF Kennedy hakuwa mkristo? aliyemua John Lennon hakuwa mkristo? Aliyemua Malcom X je? Yule alieua vijana 80 katika kambi ya vijana kule oslo mwaka 2011 hakuwa mkristo? Hivi waliopandikiza bomu na kuua watu tele omagh hawakuwa wakristo? Infact mabomu yote yaliopandikizwa na kuua watu tele na IRA nchini uingereza hayakupandikizwa na wakristo? Hivi mauaji na chuki zinazoendele hadi leo nchini northern ireland si kati ya wakristo wa dhehebu moja dhidi ya dhehebu jengine? Hivi

Kuna mifano mimgi tu ambayo nikaa hapa kukutajia nitachukua zaidi ya mwezi kwa hivyo bora nikupe point yangu.Poiny yangu ni kuwa wauaji ni wauaji tu, pande zote wapo na wanatumia dini kwa sababu zao wenyewe, Usione mtu kaua na uka generalize faith nzima kuwa ndio tabia zao.
 
Hakuna pahala Mkristo ataua au atafanya jambo afu aseme anampigania Mungu.
Hakuna jihad kwenye Ukristo.
Hao wote uliowataja hawakufanya hivyo kwakuwa ni wakristo.
Walifanya hivyo kwa ideology zao.

Aina ya mafundisho wanayofundishwa waislam toka wakiwa watoto, kama mtu asipokuwa timamu ni rahisi kurubunika akidhani kwamba anampania Mungu.
Kumbe baadhi tu ya washenzi wanamtumia.
 
Back
Top Bottom