SI KWELI Mauaji mapya Kibiti: Serikali iweke hadharani idadi ya askari na raia waliouawa mpaka sasa

SI KWELI Mauaji mapya Kibiti: Serikali iweke hadharani idadi ya askari na raia waliouawa mpaka sasa

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kwa taarifa za uhakika ni kuwa tangu January hadi sasa sio chini ya askari 20 walikwisha uwawa ila serkali Inafanya siri hata sisi hatukuruhusiwa kufika KIBITI kwa kuambiwa kuwa mkuu wa wilaya na kamati yake ya ulinzi na usalama hawaruhu Kwa kuwa eneo ni hatari sana.

IMG_8260.jpeg

Kwa taarifa za uhakika ni kuwa wale magaidi wa kipindi cha magufuli wamerudi Kwa kasi wana silaha nzito za moto huku idadi ya askari ikiwa ndogo baada ya eneo kuonekana shwali baada ya operation ya kipindi cha magufuli

Nitoe wito kwa serikali iweke wazi ili raia wajue nini kiaendelea rufiji kwa umma isifanye Siri huku hali ikizidi kuwa mbaya.

USSR
 
Tunachokijua
Jeshi la polisi nchini kupitia akaunti yake rasmi inayopatikana kwenye Mtandao wa X (zamani Twitter) limekanusha ujumbe unaosambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kusema kuwa hakuna matukio kama hayo, Kibiti ni shwari na salama.

Limewataka wananchi kupuuza ujumbe huu pamoja na wote wasioitakia mema nchi yetu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo mauaji yanayojumuisha eneo la Mkuranga, Kibiti na Rufiji (MKIRU) yalianza mapema Januari 2015 yakihusishwa na vikundi vya vijana wanaopata mafunzo kutoka kwenye kundi la al-Shabaab nchini Somalia.

Kwa mujibu wa Gazeti la Jamhuri, Kwa miaka minne hadi mitano hadi kuanza kwa mauaji haya, vijana kadhaa kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Rufiji, hasa Ikwiriri, wamekuwa wakisajiliwa na kundi hilo la kigaidi, huku wazazi wao wakiambulia ujira wa dola 3,000 za Marekani (zaidi ya Sh milioni 6).

Akizungumza na JAMHURI, mmoja wa wakazi wa Ikwiriri ambaye hakupenda kutajwa jina lake gazetini kwa sababu za kiusalama, alisema kumekuwa na wimbi la vijana wenye umri wa miaka 16-25 kupelekwa kwenye mafunzo huko Somalia.

“Hapa Ikwiriri katika kipindi cha miaka kama mitano iliyopita kumekuwa na wimbi la vijana wadogo kupelekwa Somalia. Inasemekana wanakwenda kujiunga na kikundi cha al-Shabaab, lakini vijana hao wamekuwa wanapatikana kupitia kwa mawakala kadhaa kwenye misikiti.

Si kweli kwamba polisi hapa Ikwiriri hawajui, maana hata ukifuatilia wale viongozi wa vijiji ambao wamekuwa wakitoa taarifa za vijana hao wamekuwa wakiuawa kwa staili inayofanana… sasa hapo unaweza kuona namna zoezi (kazi) linavyokuwa gumu,”
alisema.
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani wakati ule, Mwigulu Nchemba, yeye kwa upande wake aliwahi kunukuliwa akidai "mauaji hayo yana harufu ya kisiasa," na kuhoji "Ujambazi gani huo wa Wana CCM tu? Hako kamchezo tumeshakagundua. Dhahiri, huo ni ushamba wa vyama vingi.”

Waziri Mwigulu alikwenda mbali zaidi na kudai kuwa chanzo cha mauaji hayo ni chuki za vyama vya upinzani dhidi ya CCM.

Aidha, aliyekuwa Rais wa awamu ya 5 Hayati Magufuli aliwahi kuagiza Jeshi la Polisi kuhakikisha linakomesha mauaji haya ya raia wasio na hatia.

Mei 4, 2018, Zitto Kabwe akiwa Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo alitoa hotuba Bungeni akibainisha kuwa zaidi ya Watanzania 380 walikuwa wamepotea huko MKIRU.
Wanapoteza watu maboya,


Mimi ni Muislam na nnasema kama kuna Muislam anahusika basi auwawe hapo hapo. Huyo atakuwa ni Muislam jina, siyo Muislam imani.

Waislam tunalaani vikali kitendo chochote kinachoashiria uvunjifu wa amani.
Asante Sana mkuu. Umeandika kwa busara.
 
Wameuwawa kwa kuwa ni askari pia mkristo

USSR

Sent from my TECNO B1c using JamiiForums mobile app
Huu ni ushetani wa hali ya juu. Mtu anafanya mambo ya kishetani halafu anajiita ana imani kali!! Imani kali ya shetani? Kuna watu imani zinawafanya wawe mashetani. Fikiria mtu kama Faizafoxy, bibi mzima alivyo na chuki na watu wasio waislam, unadhani mtu kama huyo akiambiwa akaue wasio waislam, ataacha kushangilia?

Kama kuna mtu anafanya mauaji kwa madai ya imani ya kidini, viongozi wakuu wa hiyo dini wakamatwe, wahojiwe, na ikiwezekana washtakiwe kwa mafundisho ya kishetani yanayosababisha mauaji dhidi ya binadamu.
 
Hii taarifa ifanyiwe kazi maana mdharau mwiba mguu utaota tende.
 
Hiyo njia siku hizi ina magari mengi ya kifahari yenye watu wenye ndevu mithili ya DW, siku moja nilitazama nikajiuliza hivi hawa wanakwenda wapi?
huyu kima wanamchekea, waache waendelee kumchekea.......
ame-overstay hapo, aondolewe kwa usalama wa wengi!
 
Hawa Magaidi wamerudije tena huko MKIRU wakati baada ya Oparesheni ile Kali iliyopelekea Wengi wao ( Magaidi ) Kuuwawa kuliundwa Kambi ya Kijeshi huko huku Makomandoo wakimwagwa kwa Wingi pamoja na Wanajeshi wa Kawaida na Watu wa Usalama wa Taifa ( TISS ) nao wamemwaga kwa Uwingi huko?
Jeshi linafanya kazi kwa amri toka kwa amiri jeshi, mengine unaweza kujiongeza, sio mpaka utafuniwe kilakitu
 
Hawa Magaidi wamerudije tena huko MKIRU wakati baada ya Oparesheni ile Kali iliyopelekea Wengi wao ( Magaidi ) Kuuwawa kuliundwa Kambi ya Kijeshi huko huku Makomandoo wakimwagwa kwa Wingi pamoja na Wanajeshi wa Kawaida na Watu wa Usalama wa Taifa ( TISS ) nao wamemwaga kwa Uwingi huko?
Mkuu, kwa taarifa za Al Jazeera za leo ni kwamba, Rais Zelensky wa Ukraine amewafuta kazi Military Recruiters wa mikoa yote nchi nzima kwa makosa ya rushwa na kupenyeza watu kinyemela maeneo ya mipakani.

Kwa hayo maelezo hapo juu kaa ukijua ya kwamba, njaa haina mwenyewe. Njaa haijui mwanajeshi, jasusi wala Polisi.

Kwani unafikiri wanajeshi au jasusi hapendi kuishi maisha mazuri (watoto kusoma English medium) au hana ndugu wanaomtegemea?

KGB na CIA wamekuwa wakihonga majausi wa kila upande pesa nono kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupewa nakala mbalimbali za siri.

Uzalendo huku tumbo lina njaa ni kazi ya bure kaka wakati wanasiasa wanachota millions of money na watoto wao.
 
Nina miaka sasa jf sijawahi kudanganya Wala kukutana na mpumbavu kama wewe

USSR

Sent from my TECNO B1c using JamiiForums mobile app
Hao wanaofanya mzaha na maisha ya binadamu wenzao ni uzao wa shetani. Unamwua mtu na mkewe na watoto, halafu unasema ni jihadi! Hiyo itakuwa ni jihadi ya shetani.
 
Dah chuki zingine buana sasa Mwamposa!? jamani kha!! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Huyo ni kichaa. Hivi huko kote wanakofanya huo ugaidi, wamepelekwa na Mwamposa? Hao ni wafuasi wa shetani, sawa na wale wanaowaua wasomali wenzao kwa madai eti wanataka nchi iongozwe kwa sharia law! Ni ushetani wa hali ya juu. Hivi Mungu anashindwa kumwondoa mtu yeyote kwenye uso wa Dunia mpaka akasaidiwe na punguani wanaojiita wana imani kali!!
 
Hao wanaofanya mzaha na maisha ya binadamu wenzao ni uzao wa shetani. Unamwua mtu na mkewe na watoto, halafu unasema ni jihadi! Hiyo itakuwa ni jihadi ya shetani.
Hayo ni madhara ya indoctrination and brainwashing psychology. Mtu akiwa brainwashed vema, mbona Fanta atasema ni Coca na atabisha hilo mwaka mzima.
 
Juzi tumetoka mbeya kuzika ndugu yetu (mwanajeshi) yeye mkewe na mtoto wa maika minne waliowawa na magaidi KIBITI Kwa kinachodaiwa kuwa ni wanajihadi wenye imani Kali sana .

Kwa taarifa za uhakika ni kuwa tangu January hadi sasa sio chini ya askari 20 walikwisha uwawa ila serkali Inafanya siri hata sisi hatukuruhusiwa kufika KIBITI kwa kuambiwa kuwa mkuu wa wilaya na kamati yake ya ulinzi na usalama hawaruhu Kwa kuwa eneo ni hatari sana.

Kwa taarifa za uhakika ni kuwa wale magaidi wa kipindi cha magufuli wamerudi Kwa kasi wana siraha nzito za moto huku idadi ya askari ikiwa ndogo baada ya eneo kuonekana shwali baada ya operation ya kipindi cha magufuli

Nitoe wito kwa serkali iweke wazi ili raia wajue nini kiaendelea rufiji Kwa umma isifanye Siri huku hali ikizidi kuwa mbaya .

NOTE

story hii pia unaweza kuisoma kupitia gazeti la MWANANCHI Kwa nyongeza .

USSR

Sent from my TECNO B1c using JamiiForums mobile app
Kuzuia taarifa za kinachojiri mpakani mwa Msumbiji na Tanzania na Cabo Delgado ni bad timing.

Serikali iwaunganishe wananchi wake kupambana na huyu adui ugaidi. Vyombo vyetu vya ulinzi na isalama vinaelewa input ya raia hasa uzalendo ukiwekwa mbele.
 
Hao 100% hawana uhusiano na Uislam.
Hivi walioteka ndege na kuwaua watu mamia kule world trade centre, hawakuwa waislam?

Mohamed Atta (Egyptian),
Abdulaziz al-Omari (Saudi Arabian), Wail al-Shehri (Saudi Arabian),
Waleed al-Shehri (Saudi Arabian), Satam al-Suqami (Saudi Arabian).

Mehmet Ali Agca, aliyempiga risasi Papa John Paulo wa 2, hakuwa muislam?

Wanaojilipua kule Somalia, kuwaua binadamu wenzao, wakidai wanataka Somalia iongozwe kwa sharia law, siyo waislam?
 
Nikupe ushahidi upi sasa ?

USSR

Sent from my TECNO B1c using JamiiForums mobile app
Labda anataka umwingize kaburini mwa ndugu zako ili aamini kuwa magaidi wenye siasa kali kweli yamemwua ndugu yako. Ukimwonesha kaburi, bado atasema mmejenga tu, ndani hakuna mwili wa marehemu.
 
Tatizo hio taarifa kwenye gazeti la mwananchi siioni. Mtoa mada piga hata screenshot utuwekee hapa ilo gazeti.
 
Labda anataka umwingize kaburini mwa ndugu zako ili aamini kuwa magaidi wenye siasa kali kweli yamemwua ndugu yako. Ukimwonesha kaburi, bado atasema mmejenga tu, ndani hakuna mwili wa marehemu.
Mpuuzi huyu hapa tumeomba serkali itoe tamko la kuwa weka sawa raia yeye analeta ujinga

USSR

Sent from my TECNO B1c using JamiiForums mobile app
 
Mpuuzi huyu hapa tumeomba serkali itoe tamko la kuwa weka sawa raia yeye analeta ujinga

USSR

Sent from my TECNO B1c using JamiiForums mobile app
Tubishane, tukosoane, tutofautiane, lakini siyo kuuana. Kuuana ni ushetani, ni unyama wa hali ya juu. Mtu kama anaona kifo cha binadamu mwenzake ni jambo la mzaha, huyo ina maana dhamira yake, kama mwanadamu, imekufa.

Wape pole waliopatawa na magumu haya. Kila aliyewahi kufiwa anajua machungu ya kufiwa. Lakini kifo cha kuuawa, kwa vyovyote kitakuwa kinaumiza zaidi kuliko kifo cha kawaida.
 
Back
Top Bottom