Afisa Ustawi wa Jamii Mahabusu ya Watoto Mbeya, Gloria Kibira amekutwa amefariki nyumbani kwake ndani ya Mahabusu hiyo ,Jijini Mbeya!
Taarifa za awali zinaonyesha kuwa alikutwa amefariki mida ya saa tatu usiku tarehe3.2 baada ya marafiki zake kumtafuta Kwa simu na akawa hapokei.
Watoto wake walikuwa shuleni, na baada ya kurudi nyumbani walidhani mama yao hajarudi kazini na wakaamua kupika, kula na kulala! Baadaye wafanyakazi wenzake waligundua maiti chumbani kwake.
Pamoja na taarifa rasmi ya tukio Hilo haijatolewa, lakini inasemekana kuwa huenda Afisa huyo aliuawa
Marehemu ameacha watoto watatu.
Baadhi ya majirani wameeleza kuwaa ulinzi ktk eneo Hilo linaloendeshwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii sio madhubuti.
Mwili wa marehemu umesafirishwakwenda Bukoba kwa mazishi