Mauaji Mbeya: Afisa Ustawi wa Jamii adaiwa kunyongwa hadi kufa

Mauaji Mbeya: Afisa Ustawi wa Jamii adaiwa kunyongwa hadi kufa

Hii familia naifahamu,mama ya marehemu ni mtu poa sana mlokole wa watu,hata watoto wake wote including marehemu na wengine ni watu poa sana
 
Afisa Ustawi wa Jamii Mahabusu ya Watoto Mbeya, Gloria Kibira amekutwa amefariki nyumbani kwake ndani ya Mahabusu hiyo ,Jijini Mbeya!

Taarifa za awali zinaonyesha kuwa alikutwa amefariki mida ya saa tatu usiku tarehe3.2 baada ya marafiki zake kumtafuta Kwa simu na akawa hapokei.

Watoto wake walikuwa shuleni, na baada ya kurudi nyumbani walidhani mama yao hajarudi kazini na wakaamua kupika, kula na kulala! Baadaye wafanyakazi wenzake waligundua maiti chumbani kwake.

Pamoja na taarifa rasmi ya tukio Hilo haijatolewa, lakini inasemekana kuwa huenda Afisa huyo aliuawa
Marehemu ameacha watoto watatu.

Baadhi ya majirani wameeleza kuwaa ulinzi ktk eneo Hilo linaloendeshwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii sio madhubuti.

Mwili wa marehemu umesafirishwakwenda Bukoba kwa mazishi
Yale yaleeee! Inatisha sana.
 
vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifo vifoooooooooooooooooooooooo!
Madaraka yalianza kwa kutoa kafara lazima sadaka iendelee ili kusastain.
 
Tz nchi ya kijinga Sana yaan mtu akiuawa huwa inachukuliwa Kama kafa mbuzi na uchunguzi wake huwa na makengeza mengi
 
Kama alikua single mother,wachunguze vizuri,hasa wapenzi wake mbalimbali kama akikua nao.
 
Najiuliza maswali mengi sana ni technology imechukia advantage au nn kwenye hii nchi yangu ya maziwa na asali?

Kila kukicha na jambo jipya la ama mauaji ama kujinyonga.

Haya mambo huko siku za nyuma hatukuyasikia au kuyaona kwa sasa kulikoni?

Au wapi tunafeli Watanzania? Hatukuzoea kuona mambo kama haya so habari hizi sasa naona zishakuwa uniform kwa Tanzania nzima
Ni wakati sasa vyombo vya sheria na mamlaka za miji midogo kujitathimini!

Hayo ni mawazo yangu
Mimi nilikuwa nawaza kama wewe, nikafikiria sana mwisho nikaona hivi haya yote yanayotokea huenda ni kwa sababu ya huu uhuru wa vyombo vya habari na vyanzo mbali mbali kama mitandao ya kijamii vimechagiza haya yote tunayoyashuhudia leo na jana yaonekane na yafahamike?
Nikaenda mbali zaidi na kusema haya yalitokea hata hapo nyuma sema watu walishindwa kupeana taarifa kwa kuhofia usalama wao,kukamatwa na kushitakiwa na hii ni baada ya mitandao ya kijamii hapo awali kuminywa...
 
Ni mwendo wa kunyongana wadada wenye $$$ nunueni vibastora vitawasaidia
 
Watu wengine Ni wamevurugwa vibaya...

Hawajui lolote washakimbilia u-single mother... ..

Kwa maisha ya sasa ukaue kisa wivu Ni unyambi wa mwisho.. ..

Mapenzi yamewashinda kina Shakhrouq Khan ..mtaweza ..wakulungwa?!
 
Afisa Ustawi wa Jamii wa Kituo cha Mahabusu ya Watoto kilichopo Kabwe Kata ya Iyela Jijini Mbeya Groria Kibira(38) amekutwa ameuawa kwa kunyongwa na Watu wasiojulikana kwenye nyumba yake ambayo ipo ndani ya eneo la Kituo cha Mahabusu hiyo .

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema Watu wawili wanahojiwa ili kubaini chanzo cha mauaji "Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda Bukoba Kagera kwa ajili ya maziko.

Chanzo: Millard Ayo

My take: Simon Sirro unatafutwa, mfuate Ndugai tu.
Kwamba hapo sirro anahusika vipi? Au ndio siasa zenu!
 
Fuatilia basi tujue kilicho msibu mtoto mrembo
Hii familia naifahamu,mama ya marehemu ni mtu poa sana mlokole wa watu,hata watoto wake wote including marehemu na wengine ni watu poa sana
 
Hivi kweli unamnyonga single mother mwenye watoto3, daaa watu tuna tofautiana
 
Kwanini siku hizi mauaji yameongezeka sana Tanzania???
 
Back
Top Bottom