Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Maisha bora kwa kila mtanzania kweli??? kama tumefika kupigana bei???? duh!!!

...historia inajirudia,...si unakumbuka machifu walianza kuwauza mateka utumwani...

NDIVYO TULIVYO (?)
 
Hii ni aibu na kweli,

Pentekoste sii Walokole???

Vipi tena??

Tuamini dini/thehebu gani?

Amini imani yako inayokutuma, usifuate dini/dhehebu kwa kuwa fulani kafanya kitu fulani, balikwa kuwa dini/dhehebu inafundisha mafundisho fulani....

hivi ni PENTEKOSTE imekutwa na hayo mabaki au MCHUNGAJI?
 
Pengine hawa ni sawa na wanaovaa herizi waliolezwa kwenye thread moja hapa kabla haijafutwa
 
........mmmmmmmmmmmmh so terrible. This might call for religious regulation especially when it comes to granting leadership.
 
Jamani tuwe makini na kushambulia tu cheo cha uchungaji bila kuwa na uhakikia. Gazeti linasema Mchungaji wa Pentekoste kwasababu waliona joho jeusi. Kuwa na joho jeusi hakumaanishi kuwa huyo ni Mchungaji wa Pentekoste. Kwanza wachungaji wa Pentekoste hawavai majoho, wanaendesha ibada kwa kuvaa nguo zao za kawaida. Pili kwanini hawataji jina la kanisa? Tanzania hutuna madhehebu linaloitwa pentekoste. Neno hili linatumiwa collective kwa makanisa mengi kama vile Pentekoste holiness, Tanzania free pentekoste, Elimu Pentekoste, Assembles of God nk. Pia kwanini hawataji kanisa lake lipo eneo gani, usharika upi? hii imekaa kama kutia chumvi na kukashifu tu.

Endapo itadhihirika kuwa kweli huyo ni Mchungaji, tunatarajia kusikia Kanisa likiomba radhi kwa kosa lhilo la mtumishi wao.

Pia endapo inadhihirika huyo siyo Mchungaji, au si mchungaji wa pentekoste, gazeti liwe tayari kuiomba radhi jamii na kanisa kwa kutoa habari za uongo na kashfa.

Otherwise, ninafarijika kwamba vita inakwenda vizuri sasa, yaani polisi wameanza kuamka na kufanya kazi yao vizuri.
 
....mmmmhhh...........MaxShimba vipi hapo........mafundisho ya wapi haya
 
Hii ni aibu na kweli,

Pentekoste sii Walokole???

Vipi tena??

Tuamini dini/thehebu gani?



Ndugu yangu wala usishangazwe na Mchungaji kukutwa na viungo vya albino, ndi siku za mwisho ati! Usimwamini mtu kwa namna alivyo. Hata kama akiongea anatoa cheche za moto mdomoni!!! imani ni swala binafsi kati ya mtu na kile anachokiamini! Biblia inasema katika Jeremia kuwa wapo manabii ambao walikwenda kusema( kuhubiri) kwa jina la Bwana lakini Mungu hakuwatuma! Tena katika siku ya hukumu wapo watakaojitetea kwamba walikuwa watumishi wa Bwana, walitoa pepo na kufanya miujiza kwa jina la Yesu lakini U=Yesu mwenyewe atasema.Ondokeni kwangu,siwajui!
 
Makubwa haya jamani, kumbe kanisa ndio liko nyuma ya mauwaji ya Albino au ni mchungaji tu?
 
ndio wanacmamaga madhabahuni kutuombea/kutuonya tuache maaovu hawaaa, wao ndio kama hivi tena ya kina mchungaji kimaro ndio hivyo, loo kazi ipo.
 
Kweli dunia imefika ukingoni Mungu anisamehe itafika wakati hakuna imani tena katika dini zetu!
 
Tatizo tunasikia wanakamatwa tu lakini hakuna hukumu ya mfano ambayo ishatolewa ili waliobaki na biashara hiyo wajifunze
 
. Gazeti linasema Mchungaji wa Pentekoste kwasababu waliona joho jeusi. Kuwa na joho jeusi hakumaanishi kuwa huyo ni Mchungaji wa Pentekoste. Kwanza wachungaji wa Pentekoste hawavai majoho, wanaendesha ibada kwa kuvaa nguo zao za kawaida.

Mkuu Nziku,

Naomba nieleweshwe, hivi koti na joho ni kitu kilekile? Nauliza hivi kwa sababu kwenye habari tumeambiwa alikutwa na koti si JOHO....see below & clarify this!

“Baada ya kupekua katika nyumba ya Mwashilindi tulifanikiwa kupata dawa za binadamu, maji ya kuchanganya na dawa na koti jeusi mali ya Mchungaji Mwasenga,” alisema.
 
Kwa kweli kama khali imefikia huko hata viongozi wa dini nao wako kwenye mambo machafu kama haya hii ni hatari. Nafikiri kesi hii ni rahisi kwani jamaa wamekamatwa na vidhibiti. Wapewe adhabu kubwa iwe fundisho kwa wengine. Pia wale walio toa taarifa wapewe aksante yao kwa kufanikisha kukamatwa viungo japo maisha ya huyo hayakuokolewa au alipata ulemavu maana kama walikata mkono au kiungo chochote mwilini mwake, lakini pia through hizi habari tutafanikiwa kuwadefeat hawa jamaa. Kwani hao waliokamatwa nao wana mtandao ambao ni lazima wautaje. Hivyo kwa kiasi kikubwa itasaidia kutuma ujumbe kwa wengine wanaoendekeza tabia mbaya hizi kuwa nao siku zao zinahesabika watamulikkwa.
 

angalia taarifa yenyewe ndiyo hii hapa


Source: Mwananchi
 

We umekaa kupinga tuuu huyu ni mchungaji wa kanisa la kikristo huyu anatangaza dini kwa vitendo........hizi dini nyengine.


SAHIBA.
 
...Jamani tuwe makini na kushambulia tu cheo cha uchungaji bila kuwa na uhakikia. Gazeti linasema Mchungaji wa Pentekoste kwasababu waliona joho jeusi. Kuwa na joho jeusi hakumaanishi kuwa huyo ni Mchungaji wa Pentekoste...

crisp and cheese...! Huyu mchungaji yapaswa haombewe...!
in the name of father... the sun... and in the-hole-of hell he- goes... Amin
 
Huyu mchungaji hana Roho wa MUNGU ndo maana shetani amemtumia anavyotaka!jamani biblia inasema usiue!sasa yeye anakutwa na viungo vya albino!Ama kweli yametimia yaliyonenwa na Nabii Daniel!
 
Mlemavu wa ngozi mkazi wa Kijiji cha Butonga, Kata ya Sima, wilayani hapa, Yunis Bati (14) ameuawa kikatili na kukatwa miguu yake na kutoweka nayo. Kabla ya kukatwa miguu, Yunis alipigwa panga kisogoni na kufa papo hapo.

Tukio lilitokea saa 5.30 usiku wa kuamkia leo katika kitongoji cha Kahindaga B baada ya mlemavu huyo msichana kuvamiwa na watu wasiofahamika nyumbani kwao. Hili ni tukio la pili kutokea katika kata na wilaya hiyo katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja, kwani katikati ya Januari mwaka huu mlemavu mwingine wa Kijiji cha Sogoso katani humo aliuawa na kunyofolewa mguu mmoja.

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Elinasi Pallangyo, alithibitisha tukio hilo na kueleza kwamba serikali imesononeshwa kwa kuwa limetokea siku chache tu tangu yeye na viongozi wengine wa wilaya watoke katika kijiji hicho kuwaelimisha wananchi jinsi ya kupambana na mauaji hayo. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika eneo la tukio, Mkuu wa Wilaya alisema:

“Inakua vigumu sana kusimulia tukio hilo, lakini hali halisi ndiyo hiyo, ni mauaji ya kinyama sana sijawahi kuyaona, lakini kibaya zaidi ni kwamba mauaji haya yanakuja wakati tuko katika mchakato wa kuelimisha wananchi namna ya kupambana na matukio ya aina hii katika maeneo yao, imetusononesha na kutusikitisha sana,” alisema Mkuu wa Wilaya huku akijifuta machozi.

Akisimulia tukio hilo baba wa marehemu, Bahati Lugwisha (53), alidai kuwa usiku akiwa amelala ndani na mkewe na watoto wake wanne wa kike akiwamo marehemu, ghafla alisikia mlango ukivunjwa na watu asiowafahamu na kuingia ndani. Alisema baada ya kuingia, mmoja alipitiliza hadi chumbani mwake na kumbamiza na ubapa wa panga usoni na kumwekea panga shingoni huku akimtaka atulie; alitii amri huku wengine wakiwasimamia watoto wawili ambao nao ni albino waliokuwa wamelala chumbani.

“Wakati mmoja akiwadhibiti wale wawili chumbani ili wasipige kelele, mmoja aliendelea kumkata miguu marehemu huku mwingine akiwa nje, akimbana mke wangu ambaye alikuwa akifanya jitihada za kutoka nje kupitia dirishani,’’ alidai baba huyo. Aliongeza kuwa kabla ya kumkamata na kumnyofoa miguu mtoto huyo, kwanza alimwamuru kulala kifudifudi na kisha kumkata panga kisogoni kwenye mishipa ya fahamu, na kumkata miguu na kuinyofoa.

“Nadhani yule mtoto alikufa palepale, kwa sababu pamoja na kumkata miguu hiyo kwa tendo lililochukua karibu nusu saa, hatukusikia akipiga kelele za maumivu na baada ya watu hao kuondoka, tulipomwangalia alikuwa akitetemeka tu mwili wote,’’ alisimulia. Hadi mwandishi wa habari hizi anaondoka eneo la tukio jana mchana, zaidi ya wananchi 3,000 wa vijiji sita vya kata hiyo, waliofika katika eneo la tukio ili kuwasaka watuhumiwa hao, walikuwa wakiendelea kupiga kura za siri ili kuwabaini walihusika chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi. Source: Gazeti la Habari Leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…