Lole Gwakisa
JF-Expert Member
- Nov 5, 2008
- 4,768
- 2,361
AIBU! Aibu! aibu!huyu si mtumishi wa Mungu , katekwa na ibilisi!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Maisha bora kwa kila mtanzania kweli??? kama tumefika kupigana bei???? duh!!!
Hii ni aibu na kweli,
Pentekoste sii Walokole???
Vipi tena??
Tuamini dini/thehebu gani?
Hii ni aibu na kweli,
Pentekoste sii Walokole???
Vipi tena??
Tuamini dini/thehebu gani?
. Gazeti linasema Mchungaji wa Pentekoste kwasababu waliona joho jeusi. Kuwa na joho jeusi hakumaanishi kuwa huyo ni Mchungaji wa Pentekoste. Kwanza wachungaji wa Pentekoste hawavai majoho, wanaendesha ibada kwa kuvaa nguo zao za kawaida.
Kwa kweli kama khali imefikia huko hata viongozi wa dini nao wako kwenye mambo machafu kama haya hii ni hatari. Nafikiri kesi hii ni rahisi kwani jamaa wamekamatwa na vidhibiti. Wapewe adhabu kubwa iwe fundisho kwa wengine. Pia wale walio toa taarifa wapewe aksante yao kwa kufanikisha kukamatwa viungo japo maisha ya huyo hayakuokolewa au alipata ulemavu maana kama walikata mkono au kiungo chochote mwilini mwake, lakini pia through hizi habari tutafanikiwa kuwadefeat hawa jamaa. Kwani hao waliokamatwa nao wana mtandao ambao ni lazima wautaje. Hivyo kwa kiasi kikubwa itasaidia kutuma ujumbe kwa wengine wanaoendekeza tabia mbaya hizi kuwa nao siku zao zinahesabika watamulikkwa.Mchungaji ‘akutwa' na vipande vya albino
Merali Chawe, Mbeya
Daily News; Tuesday,February 17, 2009 @19:17
Mchungaji wa Kanisa la Pentecoste lililopo Idiwili Kata ya Iyula, wilayani Mbozi anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kukutwa na mabaki ya mwili wa binadamu yaliyokuwa yakiuzwa Sh milioni 30.
Cosmas Mwasenga (39) alikamatwa Februari 13 mwaka huu akiwa na Luseshelo Mwashilindi ambaye inadaiwa alikuwa ameyahifadhi nyumbani kwake mabaki hayo. Mabaki hayo ambayo Polisi inahisi kuwa ni ya albino, ni vipande vinne vinavyosadikiwa kuwa sehemu ya mikono.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Zelothe Stephen alisema leo kuwa watuhumiwa hao walikamatwa katika eneo la Mlowo, Mbozi. Akizungumzia tukio hilo, Kamanda Zelothe alisema Februari 12 mwaka huu, polisi walipata taarifa kuwa kuna kikundi cha watu Mlowo, wana vipande vya mabaki ya mwili wa mwanadamu vinavyosadikiwa kuwa ni mabaki ya mwili wa albino.
Alisema taarifa hizo zilidai kuwa kikundi hicho kilikuwa kinatafuta wateja ili kuwauzia vipande hivyo na kwamba watu waliokuwa wanatafuta wateja waligawanyika katika Wilaya ya Mbozi na baadhi ya mitaa ya Jiji la Mbeya.
"Tuliweka mtego na kukutana na watu hao ambao walisema wanauza viungo vya ‘kunguru mweupe' wakimaanisha albino, ambapo walikubaliana na kukutana na Mwashilindi ambaye alikuwa anahifadhi viungo na kufikia makubaliano ya kuvinunua kwa Sh milioni 30," alisema.
Alisema Februari 13, taratibu za kupata kiasi hicho cha fedha zilikamilika na walipofika kwa Mwashilindi alitoka akiwa na vipande vinne vya mabaki ya binadamu vikiwa vimefungwa katika karatasi, na Polisi wakamkamata. "Baada ya kupekua katika nyumba ya Mwashilindi tulifanikiwa kupata dawa za binadamu, maji ya kuchanganya na dawa na koti jeusi mali ya Mchungaji Mwasenga," alisema.
Aliongeza kuwa watuhumiwa wote wawili wanashikiliwa na watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika. Kamanda Zelothe alisisitiza umuhimu wa wananchi kutoa taarifa Polisi na kusema kwa kufanya hivyo, ndipo vitendo vya mauaji ya albino vitapungua. "Tunapenda kuwaomba wananchi waendelee kutoa taarifa za siri kwa viongozi wa juu, ili ziweze kufanyiwa kazi haraka," alisema.
Mkuu Nziku,
Naomba nieleweshwe, hivi koti na joho ni kitu kilekile? Nauliza hivi kwa sababu kwenye habari tumeambiwa alikutwa na koti si JOHO....see below & clarify this!
"Baada ya kupekua katika nyumba ya Mwashilindi tulifanikiwa kupata dawa za binadamu, maji ya kuchanganya na dawa na koti jeusi mali ya Mchungaji Mwasenga," alisema.
POLISI mkoani Mbeya inawashikilia watu wawili wakazi wa Kijiji cha Idweli, Kata ya Iyula, wilayani Mbozi, akiwemo mchungaji wa Kanisa la Pentekoste kwa tuhuma za kupatikana na viungo vya albino ambavyo vilikuwa vikiuzwa kwa Sh30milioni.
Tukio hilo linalomhusisha mchungaji, limekuja wakati nchi ikiwa katika kampeni ya kupambana na ukatili dhidi ya maalbino, ambayo hupewa msukumo pia na viongozi wa dini mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Zelothe Stephen alisema mtuhumiwa mwingine ni mkulima wilayani Mbozi.
Kamanda huyo alisema kukamatwa kwa watuhumiwa kulikuja wakati wakihaha kusaka wateja katika maeneo ya soko la Mwanjelwa jijini Mbeya.
Kwa mujibu wa Kamanda Stephen, watuhumiwa walipofika katika soko hilo Februari 16, walidai walikuwa wakiuza viungo vya kunguru mweupe.
Zelothe alisema kutokana na taarifa walizopata kutoka kwa raia wema, polisi waliweka mtego na kuwanasa baada ya kupatana kuuziana viungo hivyo katika mji wa Mlowo, wilayani Mbozi ambako kachero mmoja alifika Februari 16, kukamilisha mpango huo.
Alisema baada ya makubaliano ya kiasi cha Sh30 milioni kushindikana na kuahidiwa kukamilisha fedha hizo siku inayofuata (Februari 17), kachero huyo alifika na kiasi hicho cha fedha na kupeleka nyumbani kwa mmoja wa watuhumiwa na kukabidhiwa vipande vinne vya viungo hivyo, vikiwemo viganja vilivyohifadhiwa katika magazeti mawili tofauti.
Kamanda Stephen alisema baada ya kumkabidhi viungo hivyo, watuhumiwa walikamatwa na walipopekua nyumbani kwa mmoja wao, walikuta dawa aina mbalimbali na maji ya kuchanganyia dawa hizo.
Dawa hizo zinadaiwa kutumiwa kukamilishia matukio mbalimbali yanayotokea wilayani Mbozi, ikiwa ni pamoja na joho jeusi la mchungaji linalotumika kuendeshea ibada lililokuwa limetundikwa ukutani.
Kwa mujibu wa kamanda Stephen, watuhumiwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote mara baada ya uchunguzi kukamilika.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limetoa amri ya kukamatwa kwa watu wawili wa Kata ya Ivumwe, kwa uzembe waliofanya ambao ungesababisha mtoto mlemavu wa ngozi kuuawa na watu wasiojulikana.
Kamanda Stephen aliwataja watu hao kuwa ni balozi wa kata ya Ivumwe, Luda Mturo (44) na baba mzazi wa mlemavu wa ngozi, Daimon Masawe (42) ambaye pia ni mkazi wa Ivumwe mjini Mbeya.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda Stephen alisema Februari 5 mlemavu huyo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza, alivamiwa na watu wasiojulikana wakati akienda shuleni umbali wa mita 400 kutoka eneo analoishi.
Zelothe alisema siku ya tukio watu watatu wasiojulikana, akiwemo mwanamke mmoja, walimkamata mlemavu huyo na kumficha kwenye tanuli la kuchomea matofari.
Akisimulia mkasa huo, kijana huyo alisema mara baada ya kukamatwa na watu hao ambao anadai hawafahamu, alipita mwendesha baiskeli ambaye aliokoa uhai wake, baada ya watuhumiwa kumwona na kutimua mbio.
Alisema mara baada ya tukio hilo, mtoto huyo alirudi shuleni kuendelea na masomo na jioni alipofika nyumbani alimueleza mama yake aitwaye Upendo Masawe (40), ambaye alitoa taarifa kituo cha polisi kuhusiana na tukio hilo.
Kamanda Stephen alisema watuhumiwa hao wanashikiliwa na polisi kutokana na uzembe wa kushindwa kuimarisha ulinzi wa watu waliokuwa na ulemavu wa ngozi kwa kuunga mkono jitihada za serikali kupiga vita mauji hayo.
Jamani tuwe makini na kushambulia tu cheo cha uchungaji bila kuwa na uhakikia. Gazeti linasema Mchungaji wa Pentekoste kwasababu waliona joho jeusi. Kuwa na joho jeusi hakumaanishi kuwa huyo ni Mchungaji wa Pentekoste. Kwanza wachungaji wa Pentekoste hawavai majoho, wanaendesha ibada kwa kuvaa nguo zao za kawaida. Pili kwanini hawataji jina la kanisa? Tanzania hutuna madhehebu linaloitwa pentekoste. Neno hili linatumiwa collective kwa makanisa mengi kama vile Pentekoste holiness, Tanzania free pentekoste, Elimu Pentekoste, Assembles of God nk. Pia kwanini hawataji kanisa lake lipo eneo gani, usharika upi? hii imekaa kama kutia chumvi na kukashifu tu.
Endapo itadhihirika kuwa kweli huyo ni Mchungaji, tunatarajia kusikia Kanisa likiomba radhi kwa kosa lhilo la mtumishi wao.
Pia endapo inadhihirika huyo siyo Mchungaji, au si mchungaji wa pentekoste, gazeti liwe tayari kuiomba radhi jamii na kanisa kwa kutoa habari za uongo na kashfa.
Otherwise, ninafarijika kwamba vita inakwenda vizuri sasa, yaani polisi wameanza kuamka na kufanya kazi yao vizuri.
...Jamani tuwe makini na kushambulia tu cheo cha uchungaji bila kuwa na uhakikia. Gazeti linasema Mchungaji wa Pentekoste kwasababu waliona joho jeusi. Kuwa na joho jeusi hakumaanishi kuwa huyo ni Mchungaji wa Pentekoste...