Wakati kesi za mauaji ya albino zikiendelea katika Mahakama Kuu maalum mjini Shinyanga na Kahama, watu wawili wasiojulikana wamemuua mtoto albino, Kulwa Gilibha (7) kwa kumkata kichwa na mkono wa kushoto, tukio ambalo lilitokea katika Kijiji cha Mombesi, Kata ya Loya, Tarafa ya Igalula, Wilaya ya Uyui, mkoani Tabora.
Imeelezwa kuwa baada ya kuuawa kwa mtoto huyo, wauaji hao walitokomea na viungo ya mtoto huyo kusikojulikana.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Emson Mmari, alisema jana kuwa mtoto huyo alikuwa pamoja na wenzake na bibi yao na ndipo wauaji hao walipoingia ghafla usiku, muda mfupi baada ya kula chakula.
Huku wakiwa na bunduki aina ya Shotgun, Kamanda Mmari alisema waliwasha tochi na kumbaini mtoto huyo ambapo walimkata na panga mbele ye bibi yake ambaye alishindwa kupiga kelele kwa kuhofia maisha yake.
Alisema polisi walibaini kuwa wauaji hao walitumia bunduki hiyo baada ya kuokota ganda la risasi katika eneo la tukio.
Kamanda Mmari alisema baada ya mauaji, wauaji hao walielekea njia ya Itigi ambapo kwa sasa wanasakwa.
Taarifa ya Katibu wa Chama cha Maalbino Mkoa wa Tabora, Mussa Kabinda, alisema kuwa hapo awali familia hiyo ilikuwa na mtoto mwingine albino aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha.
Kamanda Mmari amewataka wananchi wanaoishi na watoto albino kuwa karibu na wananchi ili kujihakikishia usalama wa watoto wao, kutokana na mtoto aliyeuawa familia yake kuwa mbali na wananchi wengine.
Wakati huohuo, kesi za mauaji ya albino na vikongwe zinazosikilizwa na Mahakama Kuu maalum mjini Shinyanga ambazo kwa mujibu wa ratiba zilikuwa zisimame kuanzia leo zimeongezewa muda.
Bila kutaja muda ulioongezwa na Jaji Kiongozi, Jaji Gadi Mjemas anayesikiliza kesi hizo jana Shinyanga aliahirisha shauri la mauaji ya vikongwe kwa karibu wiki mbili hivi.
Alisema kesi ya mauaji ya kikongwe Nhumbi Jiteleja wa kijiji cha Bunambiyu, wilayani Kishapu, mkoani hapa, imeahirishwa hadi Julai 15.
Wakati kesi hiyo ikiahirishwa, kesi ya mauaji ya albino Lyaku Willy inaendelea kusikilizwa leo.
Kesi hiyo ambayo ilikuwa itolewe maamuzi kuhusu kupokelewa ama kutopokelewa kwa maelezo ya mshitakiwa mmoja aliyoyatoa polisi, iliahirishwa kutokana na Jaji Mjemas kutomaliza kuandaa maamuzi yake hadi leo.
Katika pingamizi lao, upande wa utetezi unadaiwa kuwa mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Mboje Mawe alitoa maelezo ya kukiri kufanya mauaji wakati akiwa polisi baada ya kuteswa. Lakini upande wa mashitaka umedai kwamba hakuwahi kuteswa.
Wakati huohuo, mawakili wa upande wa utetezi wa washitakiwa wa kesi namba 24/2009 ya mauaji ya kukusudia ya albino Matatizo Dunia wa kijiji cha Bunyihuna wilayani Bukombe aliyekuwa na ulemavu wa ngozi wameiomba mahakama mjini Kahama kuanza kutoa utetezi wao Jumatatu ijayo kwa sababu ya mashahidi wao kutojipanga tayari kwa kutoa ushahidi.
Jamani kama mnakumbuka vyema miezi 2 tu iliyopita raia wa Marekani alikamatwa na ma-pirates wa kisomali eti USA iwape fedha ndipo imuachie,kilichotokea hasa nguvu za kijeshi zenye gharama kubwa walizoziingiza USA kumuokoa raia wao hamna asiyejua;maana wao wana amini kuwa serikali ina jukumu kubwa la kulinda usalama wa raia wake!
Lkn hii ni tofauti sana na nyumbani,hawa walemavu wa ngozi wanauawa kila siku na watu washirikina wanaotafuta ngozi zao eti zitawafanya kuwa matajiri.Na serikali hii zaidi ya PM Pinda kulia bungeni kutokana na kukerwa na vifo vya albinos hamna wanachofanya kumaliza mauji haya ya kutisha,juzi tu kwenye jimbo la waziri wa mambo ya ndani Masha pia albino mwingine kauawa!
Ingekuwa suala la Albino ni la nchi ingine nina imani JK angetuma askari wetu kusaidiana na nchi husika ili wakatokomeze mauaji hayo!uzoefu unaonyesha kuwa JK yupo tayari kusaidia nchi ingine kuliko kukomesha kwanza kadhia zinazoikumba nchi yake!alipeleka jeshi Comoro ambapo kanali mmoa mtukutu wa jeshi akachukua kwa nguvu kisiwa cha Anjoun bila ya kuua hata raia mmoja,lkn hajapeleka hata askari mmoja kule Tarime na Rorya ambapo hadi jana maiti za watu zaidi ya 31 walikuwa wamekwisha okotwa porini kutokana na mapigano ya kikabila,achilia mbali mali zilizozaharibiwa!
Sasa kama mmeshindwa kutulinda raia wa tz tuliowapa kura mna maana gani kuendelea kuwepo madarakani?kwa hili suala la mauaji ya kila siku ya albino nakuomba waziri Masha ujiuzuru,hauna faida na sisi kwani hufanyi kazi yako vyema ya kutulinda watz ambao ndio hasa tunaokulipa mshahara mnono!