Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

..hii ni mara yako ya kwanza kuhusisha mauaji ya albino na jimbo la uchaguzi.

..hivi jimbo la Lau Masha ndiyo linaongoza kwa mauaji ya maalbino Tanzania?

..tulaani mauaji ya maalbino mahali popote siyo pale tu yanapotokea jimbo la Lau Masha
 
Sioni relevance ya mauaji kuhusishwa na uwaziri au ubunge. Uwaziri wa Masha kimaadili na kikatiba haumpi fursa ya kulipendelea jimbo lake.
Mauaji ya albino ni swala linalohitaji kupigwa vita ya kweli nasi sote, tusiruhusu mauaji haya yatumiwe na yeyote yule kisiasa.
 
I support this..... Pia wabakaji na walawiti watoto wauawe kabisa.

Ukatili wa hali ya juu jamani!

Nadhani njia sahihi ni kuwabana hawa ambao wameisha kamatwa, watajane hadi wale vigogo wahusika wakuu, wanao mwaga hayo mamilioni kwa ajili ya viungo vya hao wenzetu! Huu ni unyama kabisa.
 
Sioni relevance ya mauaji kuhusishwa na uwaziri au ubunge. Uwaziri wa Masha kimaadili na kikatiba haumpi fursa ya kulipendelea jimbo lake.
Mauaji ya albino ni swala linalohitaji kupigwa vita ya kweli nasi sote, tusiruhusu mauaji haya yatumiwe na yeyote yule kisiasa.

Nani anataka kusiasisha mauji ya albino? Cha muhimu kuangalia ni kama mti mkavu watendewa hivi, itakuwaje kwa mbichi? Masha lazima awe spoted kwa tukio hili kama waziri wa usalama wa raia. Polisi imefanya nn kutokomeza uovu huu sikitishi?
 
Nani anataka kusiasisha mauji ya albino? Cha muhimu kuangalia ni kama mti mkavu watendewa hivi, itakuwaje kwa mbichi? Masha lazima awe spoted kwa tukio hili kama waziri wa usalama wa raia. Polisi imefanya nn kutokomeza uovu huu sikitishi?

1.Masha kama waziri wa mambo ya ndani na si kama mbunge, kwahiyo ubunge wake hauhusiki na hili.
2.Nadhani tusiwe watu wa kulaumu tu, polisi wanajitahidi kuzuia uovu huu ingawa ni kweli kuwa utendaji wao sio perfect.
3. Kaniki, iwapo wewe sasa hivi tukikupa uwaziri wa mambo ya ndani utafanya nini tofauti na Masha juu ya swala la albino?
4.Iwapo utakuwa mbunge na waziri wa mambo ya ndani unaweza kuhakikisha jimboni kwako hakuna uovu unaotendeka? kwa njia gani?
 
......
Wilaya ya Nyamagana inahusisha pia jimbo la uchaguzi la Nyamagana ambalo linaongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Lawrence Masha. Jeshi la Polisi liko chini ya Waziri huyo. MM

Huu mtungo hautoshi kuchochea tuhuma dhidi ya Masha. Tunga uchochezi uliokaa kivingine!
 
1.Masha kama waziri wa mambo ya ndani na si kama mbunge, kwahiyo ubunge wake hauhusiki na hili.
2.Nadhani tusiwe watu wa kulaumu tu, polisi wanajitahidi kuzuia uovu huu ingawa ni kweli kuwa utendaji wao sio perfect.
3. Kaniki, iwapo wewe sasa hivi tukikupa uwaziri wa mambo ya ndani utafanya nini tofauti na Masha juu ya swala la albino?
4.Iwapo utakuwa mbunge na waziri wa mambo ya ndani unaweza kuhakikisha jimboni kwako hakuna uovu unaotendeka? kwa njia gani?

Nitaunda kikosi maalum cha kufuatilia mauaji ya albino. Itakuwa one of our top and serious agendae. Tutachunguza na kuzichukulia hatua madhubuti taarifa za uuaji huu. Kwa kifupi nitatangaza vita kali ya kuwasaka wauaji....kama walivyojaribu kupunguza ujambazi JK alipoanza kazi.

Hawa watu wanafanya hivi kwa namna moja au nyingine kwa udhaifu wa jeshi letu la polisi na mikakati yake kwa sasa.

Appoint me Sir....;-)
 
Nitaunda kikosi maalum cha kufuatilia mauaji ya albino. Itakuwa one of our top and serious agendae. Tutachunguza na kuzichukulia hatua madhubuti taarifa za uuaji huu. Kwa kifupi nitatangaza vita kali ya kuwasaka wauaji....kama walivyojaribu kupunguza ujambazi JK alipoanza kazi.

Hawa watu wanafanya hivi kwa namna moja au nyingine kwa udhaifu wa jeshi letu la polisi na mikakati yake kwa sasa.

Appoint me Sir....;-)

Kwa hiyo hakuna utakachofanya tofauti kwa sababu kikosi hicho kipo na mauaji ya albino yako kwenye top agenda za wizara ya mambo ya ndani na serikali kwa ujumla.
 
All in all ZM, hii serikali ni zembe kama sio zoba.....tumechoshwa na mauaji ya aina hii..... sina hakika na hayo ulosema hapo juu....serikali hii, sidhani.
 
Pamoja na kwamba ni tatizo la kitaifa sasa hili inabidi limguse zaidi Masha kwa kuwa limetokea nyumbani kwake
 
Sioni relevance ya mauaji kuhusishwa na uwaziri au ubunge. Uwaziri wa Masha kimaadili na kikatiba haumpi fursa ya kulipendelea jimbo lake.
Mauaji ya albino ni swala linalohitaji kupigwa vita ya kweli nasi sote, tusiruhusu mauaji haya yatumiwe na yeyote yule kisiasa.

Mimi nafikiri kuhusishwa na jimbo lake ni kwa kuwa mtoa mada alitaka kutuonyehsa jinsi jitihada za kuwalinda hawa wenzetu zilivyo weak kiasi kwamba hata jimboni kwa mheshimiwa Bosi wa kina polisi ulinzi wa hawa ndugu zetu ni hafifu! Kama wameweza kuingia na kufanya ukatili wa aina hii 'nyumbani' kwa polisi je huko ambako ni kwa raia wa kawaida vijijini ambako ulinzi wa polisi ni mpaka usafiri hali ikoje?

Ni kama vile wauaji walikuwa wanajaribu kufikisha ujumbe wa ' hamtuwezi hata wewe vile vile hatukuogopi'

poleni wafiwa.


Polisi na ndugu zako tumechoka sasa tunachotaka ni kutiwa nguvuni hawa watu. HATUTAKI TENA HADITHI.
 
Katika hili lazima Masha alaumiwe kama yeye (waziri) binafsi. Hawa mawaziri wetu wanatumia muda mwingi wa kazi kujihusisha na siasa za kijungujiko kama walivyotumia muda na nguvu nyingi kule Busanda.
Busanda Masha alipata muda wa kutembelea kijiji hadi kijiji kutoa vitisho na ahadi hewa, mbona anashindwa kutumia muda wake kujikita katika maeneo yanayofahamika kwa kukithiri mauaji haya? Haoni kwenda kwake ktk maeneo hayo kama waziri wa mambo ya ndani kungeleta mabadiliko makubwa katika kutokomeza mauaji hayo?
Yanatokea sasa jimboni kwake,lakini kumbukeni alishasema mauaji ya Albino sio jambo kubwa sana, ni uhalifu wa kawaida na watu wakamtaka ajiuzulu.
 
Kukiwa na UWAJIBIKAJI wa KWELI kwenye suala hili na mengine yanayolitafuna TAIFA letu hili, mambo kama haya yatakwisha ndani ya muda mfupi sana. Kwa mfano watauwawa MAALBINO wangapi ili Waziri wa Mambo ya ndani, IGP, DCI, RPC, OCD na OCCID wajiuzulu au wang'olewe madarakani?
Kama waliopewa dhamana ya kutuhakikishia usalama wetu na mali zetu wataachwa waendelee kula NCHI mambo haya hayatakwisha.
 
Wakati kesi za mauaji ya albino zikiendelea katika Mahakama Kuu maalum mjini Shinyanga na Kahama, watu wawili wasiojulikana wamemuua mtoto albino, Kulwa Gilibha (7) kwa kumkata kichwa na mkono wa kushoto, tukio ambalo lilitokea katika Kijiji cha Mombesi, Kata ya Loya, Tarafa ya Igalula, Wilaya ya Uyui, mkoani Tabora.

Imeelezwa kuwa baada ya kuuawa kwa mtoto huyo, wauaji hao walitokomea na viungo ya mtoto huyo kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Emson Mmari, alisema jana kuwa mtoto huyo alikuwa pamoja na wenzake na bibi yao na ndipo wauaji hao walipoingia ghafla usiku, muda mfupi baada ya kula chakula.



Huku wakiwa na bunduki aina ya Shotgun, Kamanda Mmari alisema waliwasha tochi na kumbaini mtoto huyo ambapo walimkata na panga mbele ye bibi yake ambaye alishindwa kupiga kelele kwa kuhofia maisha yake.



Alisema polisi walibaini kuwa wauaji hao walitumia bunduki hiyo baada ya kuokota ganda la risasi katika eneo la tukio.



Kamanda Mmari alisema baada ya mauaji, wauaji hao walielekea njia ya Itigi ambapo kwa sasa wanasakwa.



Taarifa ya Katibu wa Chama cha Maalbino Mkoa wa Tabora, Mussa Kabinda, alisema kuwa hapo awali familia hiyo ilikuwa na mtoto mwingine albino aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha.



Kamanda Mmari amewataka wananchi wanaoishi na watoto albino kuwa karibu na wananchi ili kujihakikishia usalama wa watoto wao, kutokana na mtoto aliyeuawa familia yake kuwa mbali na wananchi wengine.



Wakati huohuo, kesi za mauaji ya albino na vikongwe zinazosikilizwa na Mahakama Kuu maalum mjini Shinyanga ambazo kwa mujibu wa ratiba zilikuwa zisimame kuanzia leo zimeongezewa muda.



Bila kutaja muda ulioongezwa na Jaji Kiongozi, Jaji Gadi Mjemas anayesikiliza kesi hizo jana Shinyanga aliahirisha shauri la mauaji ya vikongwe kwa karibu wiki mbili hivi.



Alisema kesi ya mauaji ya kikongwe Nhumbi Jiteleja wa kijiji cha Bunambiyu, wilayani Kishapu, mkoani hapa, imeahirishwa hadi Julai 15.



Wakati kesi hiyo ikiahirishwa, kesi ya mauaji ya albino Lyaku Willy inaendelea kusikilizwa leo.



Kesi hiyo ambayo ilikuwa itolewe maamuzi kuhusu kupokelewa ama kutopokelewa kwa maelezo ya mshitakiwa mmoja aliyoyatoa polisi, iliahirishwa kutokana na Jaji Mjemas kutomaliza kuandaa maamuzi yake hadi leo.



Katika pingamizi lao, upande wa utetezi unadaiwa kuwa mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Mboje Mawe alitoa maelezo ya kukiri kufanya mauaji wakati akiwa polisi baada ya kuteswa. Lakini upande wa mashitaka umedai kwamba hakuwahi kuteswa.



Wakati huohuo, mawakili wa upande wa utetezi wa washitakiwa wa kesi namba 24/2009 ya mauaji ya kukusudia ya albino Matatizo Dunia wa kijiji cha Bunyihuna wilayani Bukombe aliyekuwa na ulemavu wa ngozi wameiomba mahakama mjini Kahama kuanza kutoa utetezi wao Jumatatu ijayo kwa sababu ya mashahidi wao kutojipanga tayari kwa kutoa ushahidi.



Jamani kama mnakumbuka vyema miezi 2 tu iliyopita raia wa Marekani alikamatwa na ma-pirates wa kisomali eti USA iwape fedha ndipo imuachie,kilichotokea hasa nguvu za kijeshi zenye gharama kubwa walizoziingiza USA kumuokoa raia wao hamna asiyejua;maana wao wana amini kuwa serikali ina jukumu kubwa la kulinda usalama wa raia wake!

Lkn hii ni tofauti sana na nyumbani,hawa walemavu wa ngozi wanauawa kila siku na watu washirikina wanaotafuta ngozi zao eti zitawafanya kuwa matajiri.Na serikali hii zaidi ya PM Pinda kulia bungeni kutokana na kukerwa na vifo vya albinos hamna wanachofanya kumaliza mauji haya ya kutisha,juzi tu kwenye jimbo la waziri wa mambo ya ndani Masha pia albino mwingine kauawa!

Ingekuwa suala la Albino ni la nchi ingine nina imani JK angetuma askari wetu kusaidiana na nchi husika ili wakatokomeze mauaji hayo!uzoefu unaonyesha kuwa JK yupo tayari kusaidia nchi ingine kuliko kukomesha kwanza kadhia zinazoikumba nchi yake!alipeleka jeshi Comoro ambapo kanali mmoa mtukutu wa jeshi akachukua kwa nguvu kisiwa cha Anjoun bila ya kuua hata raia mmoja,lkn hajapeleka hata askari mmoja kule Tarime na Rorya ambapo hadi jana maiti za watu zaidi ya 31 walikuwa wamekwisha okotwa porini kutokana na mapigano ya kikabila,achilia mbali mali zilizozaharibiwa!

Sasa kama mmeshindwa kutulinda raia wa tz tuliowapa kura mna maana gani kuendelea kuwepo madarakani?kwa hili suala la mauaji ya kila siku ya albino nakuomba waziri Masha ujiuzuru,hauna faida na sisi kwani hufanyi kazi yako vyema ya kutulinda watz ambao ndio hasa tunaokulipa mshahara mnono!
 
Last edited by a moderator:
Duu, pumzika kwa amani mtoto Kulwa! Hivi Mungu wetu tunaye kuabudu na kukutumikia mbona unatuacha hivi? mbona unaacha viumbe wako ulio waumba wateswe namna hii? Ee maulana wanusuru viumbe wako! Myaka saba jamani?
 
Malafyale; Jamani kama mnakumbuka vyema miezi 2 tu iliyopita raia wa Marekani alikamatwa na ma-pirates wa kisomali eti USA iwape fedha ndipo imuachie said:
Hizi habari za kuuawa ma-albino kwa imani za kichawi na bila serikali kuchukua hatua zozote za kuwalinda huwa zinanikera sana na huwa najiuliza hivi kazi ya akina Masha na seriali nzima kuhusu kuwalinda raia wake ni kuchukua tu posho au?
 
Tangu serikali kutangaza rasmi kupambana na mauaji ya mazeruzeru (albino ni kizungu), bado mauaji mengine tena yameshatokea katikati ya harakati hizo. this is strange! kuna jambo linaloendelea hapo na si bure. ze utamu ilifungwa na kusambaratishwa kwa madakika machache tu baada ya mkubwa kukashifiwa. kabla ya hapo ilikuwa inaoperate bila mikwaruzo. ni wale wa chini waliokosa pa kusemea ndio habari zao zilitamalaki humo. sasanasema hivi, hadi hapo albino mwenye jina atakapokatwa kiungo ndipo serikali itaamka na kufanya kazi yake. kujibainisha maana yake ni kuchukua nafasi ya mtu mwingine na kuivaa kuona hali yake (empathy). sasa tunaomba hii empathy itimie pale mkubwa atakapochomolewa kiungo ili haya mauaji yakome maana kila kitu lazima kianzie na wakubwa. naomba kutoa hoja.
 
nakuhakikishia na hii 2010 lazima mauaji yaongezeke......
 
Back
Top Bottom