KIJANA2013
JF-Expert Member
- Jan 21, 2013
- 466
- 201
Kuwatenga (isolation)kutakuwa ni tatizo kubwa la kibinadamu na dunia itatuangukia.Totally against basic huma rights!! Utasababisha madhara ya kisaikologia/ stress kwa watoto hawa kwamba wao sio binadamu wa kawaida.
Kutaja na kukandia viongozi sio jambo jema au suluhisho , lets look for the best way foward
Hapo ndipo mnapokosea kwanini lipingane na haki za kibinadamu? Mbona kuna watoto wengi tu yatima wanaishi kwenye kambi maalumu na nyingi zinafadhiliwa na kuendeshwa na hao hao Wazungu? Mbona kuna kambi ya Watoto yatima pale Mwenge/Sinza ya mama Mkapa S.O.S hamna kilio chochote ktk kwa hao unawasema?
Hakuna jinsi best way forward sasa hivi ndiyo hiyo kuchukuwa hawa watoto wote na kuwaweka mahali pamoja penye usalama mpaka hapo hali itakapotengemaa lkn hili ni gumu kwa maana wanaopaswa kutoa hiyo amri na kuhakikisha inafanya kazi yaani Pinda na Kikwete ndiyo wauwaji wakuu wa hawa watoto vinginevyo wangeshachukua hatua kwani huyu siyo mtoto wa kwanza kuuliwa na mpaka Dunia imeshapiga kelele sana sasa tatizo nini?
Mbona hakuna hata mtuhumiwa mmoja aliyenyongwa au kupewa adhabu kali kwa matukio ili iwe fundisho?
Hivyo maadamu hakuna linalofanyika mimi naamini kwamba wauwaji wakubwa wa hawa Watoto ni Pinda na Kiwete!
Kwa macho ya kitoto,aliwatazama,akajawa hofu. Alilia kitoto,kiganja cha mtu mzima, kikakibana kabisa kinywa cha mtoto Bahati.Sauti yake haikusikika kabisa.
Bahati hakujua kama yeye ni albino. Kwa akili za kitoto, saikolojia ya watoto, yeye alijiona salama mikononi mwa mama yake. joto la kifua cha mama, joto la manyonyo ya mama lilimburudisha na kujiona anapendwa tena yu salama.
Wanaume hawa wamemkaba...akiwa hai wanamnyofoa mikono mara miguu, maumivu makali ya visu na mapanga ya buchani yanasikika yakitenga ngozi, maumivu yanaingia ndani kwenye nyama na misuli,panga na kisu kinapogusa mfupa mchanga wa mtoto Bahati. Moyo mchanga wa Bahati unazimika. Hatimaye Bahati wa Geita kakata roho!!!
Bahati ameuawa hajui kama yeye ni albino.
Bahati ameishi mwaka mmoja na miezi miwili tu tangu aje duniani....
Kumbe Bahati hakujua kwamba yeye ni 'deal'.
Mwaka 2009 waliwauwa albino wengi tu...
Wanausaka utajili...
Wauaji na wanasaka vyeo vya kisiasa...
Vyeo na utajili uliojaa damu za albino....
Utajili na vyeo vyenye vilio na laana ya dunia yote.
Mabara matano ya dunia hii yamelaani mauaji haya. Visiwa vimelaani roho hii ya uroho wa madaraka na utajili ivumayo Tanzania.
Binafsi nimesikitishwa sana na mauaji ya ndugu zetu Albino
Inahuzunisha sana, ndugu zetu Albino wamefanywa kama wanyama.
Inauma sana sana binadamu wamekuwa na roho mbaya kuliko shetani
Kwa kweli haya matukio yananisikitisha sana mpaka natokwa na machozi,
Dah, yani nimelia. Its very sad.
Inahuzunisha sana
Samaritan GOD IS WATCHING...!!!mshana jr, acha kabisa, hii picha leo imeniachia maswali ambayo sina majibu yake, kila nikitafakari mateso aliyoyapata huyu mtoto napata uchungu na hisia za huzuni vibaya mno. Wazazi wa huyo mtoto unafikiri wana hali gani, unafikiri bado wana imani na serikali kweli? So sad!