Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Wanasema uchungu wa mwana aujuae mzazi, kwa kitendo hiki cha juzi sisi kama wazazi hatupaswi kukikalia kimya, ni kitendo cha kikatili cha hali ya juu sana. Sasa hivi ubinadamu haupo kabisa, tunakwenda wapi? Tuache siasa katika mambo kama haya, tuunganishe nguvu zetu katika hili, ni sisi wenyewe tulaani kitendo hiki na kuwafichua binadamu hawa walikosa ubinadamu. Mungu ailaze pahala pema roho ya motto wetu mpendwa
 
Kuwatenga (isolation)kutakuwa ni tatizo kubwa la kibinadamu na dunia itatuangukia.Totally against basic huma rights!! Utasababisha madhara ya kisaikologia/ stress kwa watoto hawa kwamba wao sio binadamu wa kawaida.

Kutaja na kukandia viongozi sio jambo jema au suluhisho , lets look for the best way foward

Hapo ndipo mnapokosea kwanini lipingane na haki za kibinadamu? Mbona kuna watoto wengi tu yatima wanaishi kwenye kambi maalumu na nyingi zinafadhiliwa na kuendeshwa na hao hao Wazungu? Mbona kuna kambi ya Watoto yatima pale Mwenge/Sinza ya mama Mkapa S.O.S hamna kilio chochote ktk kwa hao unawasema?

Hakuna jinsi best way forward sasa hivi ndiyo hiyo kuchukuwa hawa watoto wote na kuwaweka mahali pamoja penye usalama mpaka hapo hali itakapotengemaa lkn hili ni gumu kwa maana wanaopaswa kutoa hiyo amri na kuhakikisha inafanya kazi yaani Pinda na Kikwete ndiyo wauwaji wakuu wa hawa watoto vinginevyo wangeshachukua hatua kwani huyu siyo mtoto wa kwanza kuuliwa na mpaka Dunia imeshapiga kelele sana sasa tatizo nini?
Mbona hakuna hata mtuhumiwa mmoja aliyenyongwa au kupewa adhabu kali kwa matukio ili iwe fundisho?
Hivyo maadamu hakuna linalofanyika mimi naamini kwamba wauwaji wakubwa wa hawa Watoto ni Pinda na Kiwete!
 
Kwa macho ya kitoto,aliwatazama,akajawa hofu. Alilia kitoto,kiganja cha mtu mzima, kikakibana kabisa kinywa cha mtoto Bahati.Sauti yake haikusikika kabisa.

Bahati hakujua kama yeye ni albino. Kwa akili za kitoto, saikolojia ya watoto, yeye alijiona salama mikononi mwa mama yake. joto la kifua cha mama, joto la manyonyo ya mama lilimburudisha na kujiona anapendwa tena yu salama.

Wanaume hawa wamemkaba...akiwa hai wanamnyofoa mikono mara miguu, maumivu makali ya visu na mapanga ya buchani yanasikika yakitenga ngozi, maumivu yanaingia ndani kwenye nyama na misuli,panga na kisu kinapogusa mfupa mchanga wa mtoto Bahati. Moyo mchanga wa Bahati unazimika. Hatimaye Bahati wa Geita kakata roho!!!

Bahati ameuawa hajui kama yeye ni albino.
Bahati ameishi mwaka mmoja na miezi miwili tu tangu aje duniani....
Kumbe Bahati hakujua kwamba yeye ni 'deal'.

Mwaka 2009 waliwauwa albino wengi tu...
Wanausaka utajili...
Wauaji na wanasaka vyeo vya kisiasa...

Vyeo na utajili uliojaa damu za albino....
Utajili na vyeo vyenye vilio na laana ya dunia yote.
Mabara matano ya dunia hii yamelaani mauaji haya. Visiwa vimelaani roho hii ya uroho wa madaraka na utajili ivumayo Tanzania.

Inasikitisha kwa kweli. serikali itoe tamko
 
Mkuu, albinism na sickle cell husababishwa na recessive gene, yaani hivi vinasaba huwa haviwezi kujionesha vinapokuwa vyenyewe, sasa basi katika tafiti siku hizi tatizo hili limeongezeka na kuacha maswali mengi, eti upande wa mke hakuna albinism na baba hamna albinism sasa je inakuwaje?

ukweli ni huu
katika vijiji vyetu siku hizi unapooa katika eneo hilohilo ulilozaliwa wewe na vizazi vyako vyote kunauwezekano Mkubwa wa inbreeding(yaani kuoana wenyewe kwa wenyewe) ikitokea hivyo inamaana kunachance kubwa ya kupata hizo recessive gene katika wawili nyie mlio ktk kijiji au eneo moja
ushauri
msioane mnaotoka Eno Moja
kama we wa Mwanza nenda oa kilimanjaro
 
Wakuu hii mambo ya albinism na sickle cell kwa sasa ni matokeo ya inbreeding yaani mnaoana wenyewe kwa wenyewe huko vijijini nawashauri ili kuondoa hizi recessive gene tutafute wake au waume mbali na mikoa yenu.
kwaufupi ni waambie tu kwamba kwa Africa sickle cell ipo west Africa na kwa Tanzania ni kanda ya Ziwa hivyo kisayansi tunasema hayo maeneo ni genepool au store ya gene za sickle cells, Albinism pia ipo sana maeneo hayo hayo
 
Mi nahisi kama ccm ndo wahusika basi ukawa ndiyo chanzo kinachopelekea hao ccm kufanya ivo ,,!!!!!kwasababu hizi katukio haya huwa yanatokea kipindi cha uchaguzi na watu ccm wanahofia kupoteza nafasi zao kwa ukawa..

Ombi langu ilikukomesha mauaji haya kati ya ccm na ukawa kuwepo na mapokezano ya uongozi eg miaka mitano ukawa mitano mingine ccm nafikiri haya yasingetokea,,,,ni mawazo tu kwa upande wangu sijui ww
 
Serikali hii ya CCM inawezaje kutuhakikishia maisha bora kwa kila mtanzania kabla haijatuhakikishia usalama wetu? Hizi slogan za kisiasa zilifaa sana wakati wa kudai uhuru, 1961. Karne hii tunataka matendo ndio yaandike historia, mfano ccm kwa matendo yake inaandika historia ya mauaji ya albino, vikongwe wa shinyanga, wakulima na afugaji; inaandika historia ya wizi wa mali za umma uliokithiri, escrow, epa, bomba la gesi, tenda za manunuzi ya serikali; ccm inaandika kwa matendo yake historia za kubaka haki za wananchi katika kuamua katiba yao, kudhulumu wananchi na kuwadidimiza katika umaskini wa kutupa, waalimu, wakulima, wanafunzi, wafanya biashara, na wafanyakazi kwa ujumla.

Let us change this ccm regime and allow our ears to listen to new songs, down ccm down with your fake dreams.
 
Hali imeonekana kuanza kushamiri tena, na ile dhana ya kuhusisha mauwaji ya albino na mambo ya kisiasa inaoneka kupata ukweli.
Ngoja tuone mwenendo utakuwaje.
 
Binafsi nimesikitishwa sana na mauaji ya ndugu zetu Albino

Inahuzunisha sana, ndugu zetu Albino wamefanywa kama wanyama.

Inauma sana sana binadamu wamekuwa na roho mbaya kuliko shetani

Kwa kweli haya matukio yananisikitisha sana mpaka natokwa na machozi,

Dah, yani nimelia. Its very sad.

Inahuzunisha sana

Malcolm X alishawahi kusema kuwa kwa kawaida watu wenye masikitiko hawafanyi chochote. Wanabaki kuhuzunika na kulia tuu kuficha hali zao. Lakini wakipatwa na hasira wanaleta mabadiliko.

Nyie ni baadhi ya sample ya watu ambao bado mnasikitika na kulialia tuu. Hamtawaletea mabadiliko albino kwa sababu bado hamjawa na hasira juu ya vitendo wanavyofanyiwa.

Mnamcheka Pinda kwa kusikitika na kulia hadharani wakati nyie mfanya hivyo hivyo humu.

Samahani kama nimekuwa too blunt, ila nadhani huo ndo ukweli kwa Watanzania wengi.
 
Unyama kama huu hauvumiliki. Watu waliopata elimu kutoka kanda ya ziwa wajitahidi kurudi vijijini kwao mara kwa mara kuibadilisha jamii yao iondokane na mawazo ya kijima!
 
....their guts are nothing but the roots of evils! The world is under the heavy dose of crime n violence!! It is crippled with murder n torture of innocent souls like this one!
 
Whoever did this their guts are nothing but roots of evils living under the heavy dose of crime n violence, they are crippled with murder n torture of innocent poor helpless souls like this one!!! They are the victims of their own bad blood!

But all in all n whatever the case GOD IS WATCHING...!!!
 
mshana jr, acha kabisa, hii picha leo imeniachia maswali ambayo sina majibu yake, kila nikitafakari mateso aliyoyapata huyu mtoto napata uchungu na hisia za huzuni vibaya mno. Wazazi wa huyo mtoto unafikiri wana hali gani, unafikiri bado wana imani na serikali kweli? So sad!
 
Last edited by a moderator:
mshana jr, acha kabisa, hii picha leo imeniachia maswali ambayo sina majibu yake, kila nikitafakari mateso aliyoyapata huyu mtoto napata uchungu na hisia za huzuni vibaya mno. Wazazi wa huyo mtoto unafikiri wana hali gani, unafikiri bado wana imani na serikali kweli? So sad!
Samaritan GOD IS WATCHING...!!!
 
Last edited by a moderator:
nadhani jamii inawavumilia wauaji, they should be known and be hanged.
 
nadhani jamii inawavumilia wauaji, they should be known and be hanged.
 
Wazo zuri lakini tatizo ni je nani wakumfunga paka kengere?
Upande mmoja kuna watu wa haki za dinadamu
Upande mwingine wanasiasa
wanatufanya tuamini kwamba labda ni kweli kwamba hao hao wasaka madaraka ndo wanaoua maalbino

who knows
 
Back
Top Bottom