Kwa macho ya kitoto,aliwatazama,akajawa hofu. Alilia kitoto,kiganja cha mtu mzima, kikakibana kabisa kinywa cha mtoto Bahati.Sauti yake haikusikika kabisa.
Bahati hakujua kama yeye ni albino. Kwa akili za kitoto, saikolojia ya watoto, yeye alijiona salama mikononi mwa mama yake. joto la kifua cha mama, joto la manyonyo ya mama lilimburudisha na kujiona anapendwa tena yu salama.
Wanaume hawa wamemkaba...akiwa hai wanamnyofoa mikono mara miguu, maumivu makali ya visu na mapanga ya buchani yanasikika yakitenga ngozi, maumivu yanaingia ndani kwenye nyama na misuli,panga na kisu kinapogusa mfupa mchanga wa mtoto Bahati. Moyo mchanga wa Bahati unazimika. Hatimaye Bahati wa Geita kakata roho!!!
Bahati ameuawa hajui kama yeye ni albino.
Bahati ameishi mwaka mmoja na miezi miwili tu tangu aje duniani....
Kumbe Bahati hakujua kwamba yeye ni 'deal'.
Mwaka 2009 waliwauwa albino wengi tu...
Wanausaka utajili...
Wauaji na wanasaka vyeo vya kisiasa...
Vyeo na utajili uliojaa damu za albino....
Utajili na vyeo vyenye vilio na laana ya dunia yote.
Mabara matano ya dunia hii yamelaani mauaji haya. Visiwa vimelaani roho hii ya uroho wa madaraka na utajili ivumayo Tanzania.