Watanzania ni wanafiki sana tena sana, ni hatari watu hawa kuliko mchawi na mganga anayewatumia viongo vya ndugu zetu maalbino katika uganga wake
Leo kila mtu anajifanya kuimba nyimbo za kuzuia mauaji ya albino kanakwamba alikuwa uhamishoni hajui kuwa Tanzania ndipo kitovu cha haya na muasisi ni serikali ya Tanzania kwa miaka mingi.
Siafiki kampeni hizi za
#stopkillingAlbinism kwasababu hazina uthabiti mioyoni mwa wahubirio, haina zuio halisi la uovu huu zaidi ya siasa.
Mimi siimbi nyimbo zenu zakinafiki juu ya mauaji ya Albino, Mda wa nyimbo za kipuuzi umepitwa na wakati, nyimo za mabembelezo mbele za uovu ni unafiki na siasa tu, Dhamira ikisimama ni lazima awajibike tuliyempa dhamana ya usalama wa maisha yetu ambaye ni SERIKALI
Mauaji ya albino hayatakoma kama hatutabadili mfumo wa siasa nchini, tunaaminishwa kwamba wafanyabiashara ndio wanahusika na mauaji hayo, ni kweli, lakini ni kwasababu ya mfumo mbovu wa utawala wenye mnyoko wa kifikra.
Vijana wenzangu Watanzania, tusimame wima taifa linaanguka, tuache siasa na na wanasiasa, tuokoe taifa hili lililotopea kwa wanyang'anyi wasio na soni kabisa.
Tuondoeni utawala huu dharimu kwa nyia yoyote na kwa silaha yoyo na wakati wowote kuanzia sasa, hatuna mjombo wa kutufunda haya, bali matatizo yetu yawe ndio umoja wetu, Tuunganishwe na magumu yetu, tuchukue hatua kwa mafaa ya vizazi vyetu, tusipumbazwe na siasa.
Tumalizapo kuivunja serikali hii ndipo tutarudi siasani, tusiruhusu ubwanyenye kututawala, tuondoe njaa kichwani, tuirudishe njaa mahali pake ambapo ni tumboni,
Lakini kumbukeni lazima tujikane wenyewe ndipo tulete ukombozi wa nchi, tuache ngono na pombe tufanye mageuzi ya mioyo yetu, tuwabadili vijana wenzetu na tujiwekee uhakika wa kuishe bila kuvunja sheria japo tuliowapa wasimamie sheria ni mabambucha wa taifa hili,
Ni aibu katika taifa lolote lenye vijana lakini binadamu wenzetu wanageuzwa biashara mhimu, niaibu kwa nchi yenye umri wa binadamu mwenye mkwe na wajukuu lakini hailini uhai wa binadamu na kinyume chake uhai wa serikali hii unategemea damu za ndugu zetu.
Vijana wakati ndio huu, wa miti kusema na mawe kujibu!