Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Jaman tuwalinde albino kwa nguvu zote wanatesekaa saana wanaishi maisha ya kuogopa ndani ya nchi yao

Please comment kwa kuandika

NITAWALINDA DAIMA

kama unaguswa
 

Attachments

  • 1424448745741.jpg
    1424448745741.jpg
    32.1 KB · Views: 106
mbona watanzania tunapenda kulalamika sana?kwa nini hatupendi kufanya maamuzi magumu mpaka tusubiri watu wengine ndio waje wafanye maamuzi kwa niaba yetu wakati tunaelewa kabisa hao tuliowakabidhi ridha ya kutuongoza hawana nia ya kumaliza tatizo hili (na matatizo mengine mengi)?
wahusika naamini kabisa wanajulikana katika jumuiya zao,sasa itakuwa vyema tukiwaweka hadharani ili wenye nafasi ya kuwachukulia hatua wafanye hivyo.tukiendelea kuwaachia vyombo vya dola tujue kabisa kuwa tutakuwa tumeliwa.kwa nini tupige kelele tu wakati wanajulikana?kuna mzee mmoja wakati wa sakata la escrow aliwahi kusema kama angekuwa anaweza kumuwekea sumu Chenge au kuharibu mfumo wa gari la Chenge,angefanya hivyo siku nyingi.hawa watu hawaishi peke yao kwenye visiwa,kwa nini tusiwashughulikie kama kweli tuna nia ya dhati ya kumaliza haya matatizo?

Kwa hyo point hasa hasa hapo tufanyeje na tuanzie wapi kama viongozi wetu hawana nia kwa sasa....nani amfunge paka kengele....??
 
Ndugu wana jamii forum, Kwanza kabisa poleni na picha ya leo iliyomuonyesha mtoto akiwa amekatwa kinyama kisha kuzikwa!
Ndugu zangu leo nifadhaishwa sana na picha ile kiasi cha kutopata usingizi vizuri. Ni ukatili ukatili wa hali ya juu.
Naomba serikali kutumia DNA kuwatia nguvuni washukiwa hawa! Pili ni maono yangu kuwa serikali imeshindwa kudhibiti mauaji haya naomba wananchi waruhusiwe kuchukua sheria mkononi kumaliZa aibu hii.

nakerwa, nakeketeka, nararuliwa moyo na mahoka wafanyiwayo hawa ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi! Je elimu na dini haijastaarabisha wahuni?
 
Watanzania ni wanafiki sana tena sana, ni hatari watu hawa kuliko mchawi na mganga anayewatumia viongo vya ndugu zetu maalbino katika uganga wake

Leo kila mtu anajifanya kuimba nyimbo za kuzuia mauaji ya albino kanakwamba alikuwa uhamishoni hajui kuwa Tanzania ndipo kitovu cha haya na muasisi ni serikali ya Tanzania kwa miaka mingi.

Siafiki kampeni hizi za #stopkillingAlbinism kwasababu hazina uthabiti mioyoni mwa wahubirio, haina zuio halisi la uovu huu zaidi ya siasa.

Mimi siimbi nyimbo zenu zakinafiki juu ya mauaji ya Albino, Mda wa nyimbo za kipuuzi umepitwa na wakati, nyimo za mabembelezo mbele za uovu ni unafiki na siasa tu, Dhamira ikisimama ni lazima awajibike tuliyempa dhamana ya usalama wa maisha yetu ambaye ni SERIKALI

Mauaji ya albino hayatakoma kama hatutabadili mfumo wa siasa nchini, tunaaminishwa kwamba wafanyabiashara ndio wanahusika na mauaji hayo, ni kweli, lakini ni kwasababu ya mfumo mbovu wa utawala wenye mnyoko wa kifikra.

Vijana wenzangu Watanzania, tusimame wima taifa linaanguka, tuache siasa na na wanasiasa, tuokoe taifa hili lililotopea kwa wanyang'anyi wasio na soni kabisa.

Tuondoeni utawala huu dharimu kwa nyia yoyote na kwa silaha yoyo na wakati wowote kuanzia sasa, hatuna mjombo wa kutufunda haya, bali matatizo yetu yawe ndio umoja wetu, Tuunganishwe na magumu yetu, tuchukue hatua kwa mafaa ya vizazi vyetu, tusipumbazwe na siasa.

Tumalizapo kuivunja serikali hii ndipo tutarudi siasani, tusiruhusu ubwanyenye kututawala, tuondoe njaa kichwani, tuirudishe njaa mahali pake ambapo ni tumboni,

Lakini kumbukeni lazima tujikane wenyewe ndipo tulete ukombozi wa nchi, tuache ngono na pombe tufanye mageuzi ya mioyo yetu, tuwabadili vijana wenzetu na tujiwekee uhakika wa kuishe bila kuvunja sheria japo tuliowapa wasimamie sheria ni mabambucha wa taifa hili,

Ni aibu katika taifa lolote lenye vijana lakini binadamu wenzetu wanageuzwa biashara mhimu, niaibu kwa nchi yenye umri wa binadamu mwenye mkwe na wajukuu lakini hailini uhai wa binadamu na kinyume chake uhai wa serikali hii unategemea damu za ndugu zetu.

Vijana wakati ndio huu, wa miti kusema na mawe kujibu!
 
  • Thanks
Reactions: jme
True,kimya kingi,swala gumu hili ,serikali itumia nguvu kidogo,ina fahamika hizi ni imani za ushirikina ,kwanini waganga na watumaji hawakamatwi ,ila wanakamatwa watu walio tumwa,hii haiuwi mzizi wa jambo,siafiki pi
 
Haiwezekani kabisa kukaa kimya na kujifariji kwamba dhambi kama hii kwakuwa hukuifanya wewe basi utabaki salama.
Dhambi ya kunyamazia ukatili kama huu lazima itakuandama na kukuadhibu tu.Huwezi kubaki salama.
Lazima tushirikiane kwa nguvu zetu zote na akili zetu zote kuwasaka hao hayawani wanaofanya ukatili huu.
Tukiamua kutia nia wote nina imani uwezo wa kuwakamata hao hayawani tunao.
Tuamue kuacha shughuli zote na tufanye jambo moja tu kwa sasa.
Tutangazie rasmi nchi nzima "MSAKO WA HAYAWANI".


10968251_785502031536876_2007472755726052510_n.jpg
 
Wakuu viongozi wa kisiasa ndiyo wausika wakuu, wanakwenda kwa waganga wanatumwa viungo vya albino ili waweze kufanikiwa mambo yao, ndiyomana akuna wa kukemea au kufatilia ili swala. Inabidi sisi wananchi tuweze kuungana ili kuliangalia jambo ili kwa ukaribu.
Kunajamaa alisema alipewa deal na Kiongozi mkubwa la kufanya kazi iyo kwa ujira mnono akakataa but aliambiwa asiseme kitu akifanya mchezo atapotezwa. akuniambia ni nani alimtuma but ki ukweli ali ni tetesana. ukizingatia uchaguzi ndiyo umekaribia, tusipochukua atua Nduguzetu watakwisha au tutabaki na vilema wengi Albino.
 
Wanasiasa wakubwa ndiyo wafanya biashara wakuu, sasa hapa ni kuwaondoa hawa wafanyabiashara wakuu wanaokaa kwa mgongo wa siasa.
Eg: Nyoka mwenye makengeza
 
mwenye mbinu yoyote ya kipelelezi itakayowezesha kumgundua au kuwagundua hawa wauaji wa albino atusaidie sisi watz mfano wewe ni mtalaam wa it toa taarifa kwa uchunguzi wako kupitia elimu au udhoefu wako vilevile kama wewe ni mpelelezi wa nchi hii au wa kigeni tafadhali fichua uhalifu huu mkubwa maana leo wanasema albino dili ila kesho watesema wewe ndiyo dili sasa ili kudhibiti watu hawa lazima tupambane kwa taaluma zetu na udhoefu wetu wote maana tumechoka kabisa na huu uvunjaji wa haki za binadamu.

Kuna alternative kuu tatu:-

1.Wawekewe tracking kama micro chips au zinginezo kwenye miili yao viwe connected kwenye satellite au radar popote wawapo ndani ya Tanzania wawe ditected.

2. Yafanyike maandamano (yenye lengo la kutoa matamko ya kupinga na kulaani mauaji ya albino) nchi nzima yatakayohusisha viongozi wa kiroho, mashekh, watoto wadogo, wanaharakati, albino na waumini wa kiislam na kikristo wa rika zote wafanye maombi ya kufunga siku tatu (yenye lengo la kumlilia Mungu na kuwalaani wanaoua albino) Mungu atasikia kilio na kuomba kwetu hakuna albino atakayeuwawa tena.

3.Serikali itangaze siku ya kupinga mauaji ya albino kitaifa. Siku hiyo yatolewe matamko mazito dhidi ya wauwaji wa albino ikiwa ni pamoja na dau nono kwa mtu atakayetoa taarifa za kusudio la mauji ya albino. Kama watatoa dau kubwa mtu atalinganisha dau la serikali na dau la mtu anayeutaka utajiri kwa viungo vya binadamu ataona bora afichue siri. Pia wakiwepo watuhumiwa wa mauaji ya albino ambao imeshathibitika wamehusika, wanyongwe hadharani mbele ya halaiki na vyombo vyote vya habari.

Mauaji yatakoma.......
 
MAUAJI YA ALIBINO

Taswira ya Taifa letu iko wapi,
utu wetu uko wapi?
Dunia inatushangaa ,
walimwengu wamepigwa duwazo.
Wapi tunasimama, AIBU KUU.

Wako wapi wanaharakati,
Wanaopiga kelele juu ya katiba,
Wako wapi wale wajuvi wa Escrow,
Wako wapi wanasiasa, wanaodhani wanadai haki,
Wako wapi wana jamii, WAKO WAPI?

Escrow ilipamba kila kurasa,
Katiba ilichakaza zetu fikra,
Richmond ilitikisa taifa,
Matokeo yamekuwa gumzo,
Albino wamepotezwa, HA HA HA HA.

Mitandao ya jamii kimya,
Jamii foramu wameziba mdomo,
Fasibooku wamebukiwa,
Twita wanayao mengi,
Instagramu mikono inaganzi,
Ngoja waishe watangule. ACHA NICHEKE.

Viongozi wadini nao!!
Midomo ina supagruu,
Wanashindwa kusema jambo,
Wanasubiri uchaguzi,
Wamekuwa wanamatukio, MMMH

Mdogo wangu kule nyumbani,
Jilinde mwenyewe,
Hata mimi kakako usiniamini,
Kwani ndugu pia twashiriki
Jilinde mwenye, jilinde dogo, JILINDEEEEEE

Tuko wapi, tuko wapi?
Mko wa wapi, mko wapi?
Wako wapi, wako wapi?
Tuko, wako, mko, wapi?
Haya, sawa, ngoja waishe, WALINDE EWE MOLA
 

Tukio hilo lilitokea jana saa saba mchana katika kijiji cha Bulyaheke, kata Bulyaheke, baada ya wananchi kumkamata mtuhumiwa huyo katika kijiji cha Kazunzu na kuwaongoza hadi kijiji cha Bulyaheke kwa mganga huyo.

Wananchi wa vitongoji vya Kazunzu, kijiji cha Nyambemba, kata ya Kazunzu, wakishirikiana na wa kitongoji cha Lueseselo, kata ya Bulyaheke, wamempiga kwa marungu, mawe na mapanga na kisha kumchoma moto mtu ambaye bado hajafahamika, wakimtuhumu kuwa wakala wa kuteka watoto wakiwamo walemavu wa ngozi (albino), akishirikiana na waganga wa kienyeji wapiga ramli kwa imani za kishirikina za kupata utajiri

Mbali ya kumuua, wananchi hao pia wamevunja na kuchoma moto nyumba 13 zilizoezekwa kwa bati mali ya mganga wa kienyeji mwanamke mpiga ramli mwenye umri wa miaka 40 (jina linahifadhiwa).

Hata hivyo, mganga huyo na familia yake walifanikiwa kuwatoroka wananchi hao.

Tukio hilo lilitokea jana saa saba mchana katika kijiji cha Bulyaheke, kata Bulyaheke, baada ya wananchi kumkamata mtuhumiwa huyo katika kijiji cha Kazunzu na kuwaongoza hadi kijiji cha Bulyaheke kwa mganga huyo.

Richard Mangalamu baba wa mwanafunzi aliyetekwa, Winfrida (11) anayesoma darasa la nne Shule ya Msingi Kazunzu, alisema mtuhumiwa alimwachia mwanafunzi huyo kutokana na kumkuta ana chale mgongoni na kifuani akidai amepoteza ubora.

Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Wilaya ya Sengerema, Babu Sanare na Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Enock Mabula, kwa nyakati tofauti walithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Naye Diwani wa Bulyaheke, Bagadi Nyuki, akiwa eneo la tukio, alisema chanzo cha mauaji hayo ni marehemu kudaiwa kuwa juzi alimteka mwanafunzi wa kike anayesoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Kazunzu na kumvutia vichakani na kisha kumvua nguo na kumpapasa.

Inadaiwa kuwa alimuachia huru baada ya kugundua kuwa hakuwa na sifa zinazohitajika na mganga na mwanafunzi huyo alipofika nyumbani aliwaeleza wazazi wake na ndipo wakishirikiana na wanakijiji wenzao walianza kumsaka mtuhumiwa na kufanikiwa kumtambua.

Inadaiwa baada ya kubanwa mtuhumiwa huyo alikiri na kujitambulisha alikuwa ametoka kijiji cha Katoro, mkoani Geita na alikwenda Sengerema kwa kazi ya uwakala wa kuteka watoto.

Diwani huyo alisema marehemu aliomba apelekwe kijiji jirani cha Bulyaheke umbali wa kilometa sita kutoka Kazunzu kwa mwenyeji wake na mdau mwenzake, Sato, lakini wapofika walikuta amekwisha kutoroka.

Wakati huohuo, mwili wa mtoto Yohana Bahati aliyeuawa kwa kukatwa miguu na mikono, mwili wake utazikwa kesho katika kijiji cha Kataro, mkoani Geita.

CHANZO: NIPASHE
 
Wana JF,
Inaweza kuonekana kuwa swala la mauaji ya albino si la kisiasa lakini ukweli ni la kisiasa kwani mbali na kwamba jambo hili linahitaji maamuzi ya kisiasa kulikabili, jina la Tanzania linachafuliwa sana duniani. Naomba Mod uliache lijadiliwe katika forum hii.

Mauaji ya albino si tu kwamba ni ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu lakini ni jambo la kinyama na kishetani. Ni jambo ambalo labda lingefanywa wakati wa zama za mawe tungeelewa lakini zama hizi za sayansi na technologia huwezi kuamini watu wanafikiria mambo ya hovyo kiasi hiki. Kama jamii lazima tuchukue hatua maana tuna jukumu la kuwalinda ndugu zetu lakini pia taswira ya Tanzania kimataifa inafifishwa na swala hili. Ukweli serikali imeonyesha udhaifu mkubwa sana katika kushughulikia swala hili maana kila siku tunaambiwa kuna intelligensia ya polisi imegundua maandamano ya CUF, Chadema nk yatakuwa ya fujo lakini intelligensia hiyo inashindwa kufanya kazi katika mambo magumu ya usalama wa Taifa kama hili la mauaji ya albino.

Mimi napendekeza sheria ya ugaidi irekebishwe ili wauaji hawa washtakiwe kwa sheria hii. Pia kama jamii tuwe wakali kwa mambo ya kipuuzi ya waganga kwamba sheria ya ugaidi itamke kuwa kupatikana na vitu vya uganga kama viungo vya binadamu nk ni sawa na kupatikana na vifaa vya kutengenezea bomu. Inapaswa kutumia nguvu zote za dola kupambana na jambo hili la kipuuzi ambalo linaturudisha kwenye zama za mawe. Wakati wenzetu Korea Kusini wapo maabara wanatafiti namna ya kutengeneza smart phone bora zaidi sisi tupo kwenye tunguli. Hii lazima ifike mwisho.

Naomba kuwasilisha
 
Ipo Witchcraft ordinance ya 19....(?) inakataza ku-posess vita kama hivyo
 
safi sana. dawa ya muuaji ni kuuwawa tu...

ukiwapeleka polisi wanaachiwa na kurudi mitaaani.. dawa yao ni kuwaua tu tena kwa kuwakata viungo kimoja kimoja mpaka wafe
 
Back
Top Bottom