Kwa kweli aibu ilipofikia nchi inatisha,
Nina rafiki yangu mmoja toka Pakistan kabla ya hili tukio kama wiki moja katika story tunapiga ananiuliza mambo kibao kuhusu Tz,
Nilimsifia sana nchi yangu ilivyo, mwisho alikuja kuniambia kuna nchi ya Africa hajui nchi gani wanauwa albino kwa sababu ya utajiri, dah nguvu ziliniisha kabisa, yeye akaniambia alisoma kwenye net kati ya Nigeria au nchi nyingine kasahau, ilibidi niunganishe yes Nigeria ile sio Tz, lakini moyoni roho sana iliuma sana hii ishakuwa aibu mno kwa nchi