#untoldstory Nilipokiwa na umri wa miaka 7 nilianza kusikia "story" kuwa watu wenye albinism huwa hawafi ila wanapotea hichi kisa kilinikaa sana kwenye kumbukumbu zangu na mpaka leo nakikumbuka. Ilikuwa ni kawaida akipita mtu mwenye albinism tunatema mate kwenye vifua tukiamini kifanya hivyo kitazuia kuja kuzaa albinos tutakapokuwa wakubwa.
Miaka ikakatika baada ya zaidi ya miaka 25 ya ile story "albino hawafi wanapotea" nikaanza kusikia matukio ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi. Medulla oblongata yangu ikakumbuka ile myth na kwa haraka sana nikahusisha mauwaji ya ndugu zetu na ile myth. Nathubutu kusema kwa kinywa kipana kuwa Serikali yetu ni Serikali ya kinafiki naamini tatizo hili lipo kwa muda mrefu sana miongo kwa miongo na linatambulika hii ni kutokana na myth ya "albino hawafi wanapotea " huu "utandawazi" uhuru wa habari na hizi social media ndio chachu kubwa kujulikana kwa uovu wanaofanyiwa ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi.
Tukienda kwenye maktaba ya magazeti ya enzi za "albino hawafi wanapotea " ambayo yalikuwa Uhuru, Mzalendo na daily news/Sunday newspaper hatuwezi kukuta habari za mauwaji ya albinos siamini kama hayakuwepo kwani kama yasingekuwepo basi hii myth "albino hawafi wanapotea " isingekuwepo wala nisingeisikia ndugu zetu hawa wamekuwa wahanga kwa miongo mingi kama si karne. Imenipelekea kuandika yote haya baada ya kisa alichonipatia rafiki yangu na class mate wangu mwenye mafanikio makubwa kwenye industry ya communication ya kuwa kuna mwana mama mmoja alimtania kwa kumuuliza ameua albinos wangapi kuweza kufika alipo leo hii! Huyu mwananama si Mtanzania na huyu rafiki yangu anafanya kazi nje ya Tanzania. Nimetafakari sana swali la yule mama jamaa yangu alisema alisikitishwa sana na swali lile na lilimuuza sana ila mimi kwa zaidi ya masaa 24 swali lile lineniumiza sana na ni swali lenye kudhalilisha nchi yetu.
Macho ya kimataifa hawatuchukulii poa kuhusu hii issue ya mauaji ya albinos. Tutegemee jamaa zetu waliopo nje watakuwa wakikejeliwa na ikibidi hata kushindwa kujitambulisha wao ni watanzania. Mwisho kabisa narudi kwa Serikali kwa niliyoyaandika na hasa mzizi wa story hii "albino hawafi wanapotea " Serikali inawajibika na hii kadhia na pengine kuna wenye mkono kwenye hili haiwezekani nafsi yenye uhai isife.
Anasema Allaah سبحانه وتعالى:
كُلُّ نَفْسٍ ذَآئِقَةُ الْمَوْتِ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ وَما الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلاَّ مَتَاعُ الْغُرُور
((Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kamili Siku ya Qiyaamah. Na atakayeepushwa na Moto na akatiwa Peponi basi huyo amefuzu. Na maisha ya dunia si kitu ila ni starehe ya udanganyifu)) [Al-'Imraan: 185]
Tusome Biblia.
Basi hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla hajamiliki mfalme awaye yote juu ya wana wa Israeli; Bela, mwana wa Beori; na jina la mji wake ni Dinhaba. Bela akafa, naye Yobabu, mwana wa Zera, wa Bosra, akamiliki badala yake. Yobabu akafa, naye Hushamu, wa nchi ya Watemani, akamiliki badala yake. Hushamu akafa, naye Hadadi, mwana wa Bedadi, akamiliki badala yake, ambaye aliwapiga Midiani katika uwanja wa Moabu; na jina la mji wake ni Avithi. Hadadi akafa, naye Samla, wa Masreka, akamiliki badala yake. Samla akafa, naye Shauli, wa Rehobothi karibu na Mto, akamiliki badala yake. Shauli akafa, naye Baal-Hanani, mwana wa Akbori, akamiliki badala yake. (1NYA 1:43-49)
Haya yalitokea miaka elfu tatu, au elfu nne iliyopita. Hapa tunaelezwa juu ya wafalme. Wao walizaliwa, walikua, na wakawa wafalme. Walitawala miaka kadhaa, baadaye walizeeka wakafa. Tena akaja mfalme mpya aliyetawala, akazeeka akafa.
Maisha ya mwanadamu ndivyo yalivyo. Mwanadamu anazaliwa, anaishi baadaye anafariki. Tena mtu mwingine anazaliwa, anaishi na hatimaye anakufa. Kizazi kingine kinatokea.
Hapa kulikuwa na mlolongo wa watu, au kama mnyororo wa watu. Walizaliwa na wakaanza kuishi kuelekea siku ile watakapokufa. Babu zetu walikuwa katika mlolongo huo. Hao nao walifariki na kizazi kingine kikazaliwa. Lakini kila mwanadamu aliyezaliwa ni lazima atakufa.
Swali iweje albinos wasife wapotee???