Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Hilooo jinamizi la uongo Na fitina , Yerico huchoki na haya majungu yako na uwongo usio na mpaka.shame on you, na Safari utakipata unachokitafuta
 
Sasa ukiambiwa hata ushindi huu wa Kimbunga wa CHADEMA unatokana na viungo vya Albino na uchawi wa Rukwa utakataa? Usidhani wachawi wako CCM tu. Hili ni letu sote WATANZANIA. Dunia ingine ndivyo inavyotutazama.
Nilikuwa sijui kumbe uongozi unapatikana kwa uchafu kama huu!! Waliotawala muda mrefu watueleze vizuri!!
 
Mkuu...mimi ninayosema nina ushahidi mnadhani nadanganya?

Ni kweli tupu....Muda ukiwadia tutauweka wazi kila mtu ashuhudie

Msiwaone watu wengine wanaonekana kama watu...Ni wanyama jamani nyie acheni tu
Mkuu tunamuomba Mungu tuwe hai ili siku ya kumwagwa huo UKWELI tuwepo. Kumbe hata fisi hutumiwa kwenye mikutano aisee
 
Kauli yako yenyewe inachangia kuua Albino. Ni lini Watanzania tutajua kuongea? Kumbe basi inawezekana kupata huo Utajiri ama Urais kwa kuua wengine? Tangaza haiwezekani kwa namna yoyote ile kupata utajiri kwa mtindo huo. Kila mtu amekuwa mchawi ama mganga wa kienyeji kwa kuunga mkono aina ya uwongo na udanganyifu unaotumiwa na wachawi na waganga wa kienyeji. Msema uwongo ili ajithibitishe kwa waamini wake kwamba anayoyasema yanaleta maana, atatafuta kuyakamilisha kwa namna yoyote ile. Tumia lugha ya kubatilisha si kuunga mkono kwamba inawezekana.

nisaidieni hivi kwanini hakuna albino au kiwete masai. wao wako perfect kiasi gani? kwanini haya mauaji yasikike kanda ya ziwa tu? hapa kunakupakana matope siku zote watu wa kaskazini wanajenga taswira kanda ya ziwa haifai kwa kwani wanawasiwasi watalii watahamia mwanza kutoka arusha.
 
Mungu shusha neema yako uwalinde albino maana hawana ulinzi wala mtetezi
 
Tutaendelea kupiga kelele mpaka wakereke! Mbona akiuawa mtu wao watuhumiwa hukamatwa fasta?
Mkuu samahani kuna tajiri na masikini na kilio cha masikini huwa kiiza na cha tajiri huwa kinapaa mbengu saba ni sawa sawa na siku mmoja tuu huwa msako mkali lakini ni masikini na wakumlinda ni mungu tuu na siyo dola
 
Eee Mungu, ukatili huu hata lini!? Tunaamini kuwa si mapenzi yako yatokee haya.. Twaomba ufanye yaliyo mapenzi yako na mapenzi ya wa watu wako, Amen!!
 
Halafu ujue masopakyindi unakuwaga na busara wakati mwingine ukiamua..!
Mkuu katika maisha lazima tuishi na principles ambazo ni endelevu na zinazoheshimu UKWELI.
Sasa mtu anapotoa habari ambayo ni factually incorrect, anatakiwa aidha aombe radhi au aisahihishe.
Kuweka unazi wa kichama mbale ya facts ni kujidhalilisha na kujidharaulisha, kama mtoa mada anavyofanya.

Kwangu mimi hata kwa chama changu, kikikosea nakirarua tu, maana ukweli ni supreme.
 
Last edited by a moderator:
#untoldstory Nilipokiwa na umri wa miaka 7 nilianza kusikia "story" kuwa watu wenye albinism huwa hawafi ila wanapotea hichi kisa kilinikaa sana kwenye kumbukumbu zangu na mpaka leo nakikumbuka. Ilikuwa ni kawaida akipita mtu mwenye albinism tunatema mate kwenye vifua tukiamini kifanya hivyo kitazuia kuja kuzaa albinos tutakapokuwa wakubwa.

Miaka ikakatika baada ya zaidi ya miaka 25 ya ile story "albino hawafi wanapotea" nikaanza kusikia matukio ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi. Medulla oblongata yangu ikakumbuka ile myth na kwa haraka sana nikahusisha mauwaji ya ndugu zetu na ile myth. Nathubutu kusema kwa kinywa kipana kuwa Serikali yetu ni Serikali ya kinafiki naamini tatizo hili lipo kwa muda mrefu sana miongo kwa miongo na linatambulika hii ni kutokana na myth ya "albino hawafi wanapotea " huu "utandawazi" uhuru wa habari na hizi social media ndio chachu kubwa kujulikana kwa uovu wanaofanyiwa ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi.

Tukienda kwenye maktaba ya magazeti ya enzi za "albino hawafi wanapotea " ambayo yalikuwa Uhuru, Mzalendo na daily news/Sunday newspaper hatuwezi kukuta habari za mauwaji ya albinos siamini kama hayakuwepo kwani kama yasingekuwepo basi hii myth "albino hawafi wanapotea " isingekuwepo wala nisingeisikia ndugu zetu hawa wamekuwa wahanga kwa miongo mingi kama si karne. Imenipelekea kuandika yote haya baada ya kisa alichonipatia rafiki yangu na class mate wangu mwenye mafanikio makubwa kwenye industry ya communication ya kuwa kuna mwana mama mmoja alimtania kwa kumuuliza ameua albinos wangapi kuweza kufika alipo leo hii! Huyu mwananama si Mtanzania na huyu rafiki yangu anafanya kazi nje ya Tanzania. Nimetafakari sana swali la yule mama jamaa yangu alisema alisikitishwa sana na swali lile na lilimuuza sana ila mimi kwa zaidi ya masaa 24 swali lile lineniumiza sana na ni swali lenye kudhalilisha nchi yetu.

Macho ya kimataifa hawatuchukulii poa kuhusu hii issue ya mauaji ya albinos. Tutegemee jamaa zetu waliopo nje watakuwa wakikejeliwa na ikibidi hata kushindwa kujitambulisha wao ni watanzania. Mwisho kabisa narudi kwa Serikali kwa niliyoyaandika na hasa mzizi wa story hii "albino hawafi wanapotea " Serikali inawajibika na hii kadhia na pengine kuna wenye mkono kwenye hili haiwezekani nafsi yenye uhai isife.


Anasema Allaah سبحانه وتعالى:



كُلُّ نَفْسٍ ذَآئِقَةُ الْمَوْتِ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ وَما الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلاَّ مَتَاعُ الْغُرُور

((Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kamili Siku ya Qiyaamah. Na atakayeepushwa na Moto na akatiwa Peponi basi huyo amefuzu. Na maisha ya dunia si kitu ila ni starehe ya udanganyifu)) [Al-'Imraan: 185]



Tusome Biblia.

Basi hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla hajamiliki mfalme awaye yote juu ya wana wa Israeli; Bela, mwana wa Beori; na jina la mji wake ni Dinhaba. Bela akafa, naye Yobabu, mwana wa Zera, wa Bosra, akamiliki badala yake. Yobabu akafa, naye Hushamu, wa nchi ya Watemani, akamiliki badala yake. Hushamu akafa, naye Hadadi, mwana wa Bedadi, akamiliki badala yake, ambaye aliwapiga Midiani katika uwanja wa Moabu; na jina la mji wake ni Avithi. Hadadi akafa, naye Samla, wa Masreka, akamiliki badala yake. Samla akafa, naye Shauli, wa Rehobothi karibu na Mto, akamiliki badala yake. Shauli akafa, naye Baal-Hanani, mwana wa Akbori, akamiliki badala yake. (1NYA 1:43-49)

Haya yalitokea miaka elfu tatu, au elfu nne iliyopita. Hapa tunaelezwa juu ya wafalme. Wao walizaliwa, walikua, na wakawa wafalme. Walitawala miaka kadhaa, baadaye walizeeka wakafa. Tena akaja mfalme mpya aliyetawala, akazeeka akafa.

Maisha ya mwanadamu ndivyo yalivyo. Mwanadamu anazaliwa, anaishi baadaye anafariki. Tena mtu mwingine anazaliwa, anaishi na hatimaye anakufa. Kizazi kingine kinatokea.

Hapa kulikuwa na mlolongo wa watu, au kama mnyororo wa watu. Walizaliwa na wakaanza kuishi kuelekea siku ile watakapokufa. Babu zetu walikuwa katika mlolongo huo. Hao nao walifariki na kizazi kingine kikazaliwa. Lakini kila mwanadamu aliyezaliwa ni lazima atakufa.

Swali iweje albinos wasife wapotee???
 
Sasa ukiambiwa hata ushindi huu wa Kimbunga wa CHADEMA unatokana na viungo vya Albino na uchawi wa Rukwa utakataa? Usidhani wachawi wako CCM tu. Hili ni letu sote WATANZANIA. Dunia ingine ndivyo inavyotutazama.
Chadema hatuna imani hizo ccm asilimia kubwa jando meadisiwa tuu kutokana na kuadisiwa imani zakishenzi zimewaponza
 
Nikiwa katika safari yangu ya kwenda Mwanza,nilihitaji kupumzika kidogo katika mji wa Geita kwani ni mji kidogo aghalabu ukiwa na pesa utaona vituko vya ndugu zangu wakina Mwanamayu wanavyotumia zile ngawila za madini ya dhahabu.

Ndipo wazo likanijia niingie mtaa mmoja maarufu wa Shilabela.Pale niliwakuta kundi kundi kubwa la wakina Ngosha kwenye kijiwe kimoja maarufu pale Shilabela kwa unywaji wa kahawa' wakipiga vikombe vyao vya kahawa wakiwa wamejaza kwenye tuthemothi.

Ndipo jamaa mmoja aliyekuwa kakaa karibu yangu akatoa hoja akisema ''ICCM yaya ukuyinha kula bhalibhulaga bhigisu bha albino'' Akiwa na maana kwamba CCM hapana kuwapa kura kwa sababu wanawaua ndugu zetu akimaanisha ndugu zao wasukuma Albino... Mwisho wa kumnukuu.

Wengine waliokuwemo mle wakaonekana kumsapoti jamaa huyo aliyekuwa kavaa vibangili mikononi na miguuni,pia kiunoni mwake anajambia.

Pia zikasikika sauti za washirika wengine zikisema ''hana gete yaya ukuyinha kula ICCM bhangwicha u yohana'' Wakimanisha kwamba kweli kabisa CCM wasipewe kura wamemuua Yohana, yaani yule mtoto Yohana Bahati aliyeuawa kule Geita siku chache zilizopita.

Ndugu zangu wanajamvi, kiukweli maneno haya ya ndugu zangu wa Kanda ya Ziwa hususani hawa wa Geita yalinishtua sana na kuiona Tanzania yangu si kisiwa cha amani tena.
 
CCM haiwezi kukwepa lawama za adha zote wanazipata Watanzania kwa sasa. Kujitakasa kwao machoni pa dunia na mioyoni mwa wananchi ni kuhakikisha wanaongoza nchi kwa uzalendo, sheria na haki. Ninachelewa kusema it is too late kwa sasa.

CCM imeua Tanzania, tutunge nyimbo zitakazo tupa mshikamano na inspiration ya kufufua nchi yetu kwa umoja, upendo na uzalendo. Tunaweza kuinua taifa letu na kusahau yaliyopita, ingawa tutayatumia katika marekebisho na maboresho.
 
... ''hana gete yaya ukuyinha kula ICCM bhangwicha u Yohana'' ...

Sasa hapo CCM inahusishwa vipi moja kwa moja na mauaji ya maalbino? Sometimes watu wanaokaa kwenye vijiwe vya kahawa naona kama wana mtindio wa ubongo. Haiwezekani ukurupuke na useme kuwa CCM wanahusika na mauaji ya Albino bila kuthibitisha kauli yako.

Jana nimeangalia kipindi cha "The Sporah Show" wageni wakiwa ni Albino mmoja hivi na mwanaharaki fulani wa Kizungu. Albino yule alisema kuwa wanauawa na kukatwa viungo maana eti ukitumia viungo vyao basi utaweza kufanikiwa kibiashara kama ni mfanyabiashara au kufanikiwa kisiasa kama ni mwanasiasa. Hapa huyu alizungumzia wafanyabiashara na wanasiasa.

Kwa mifano hiyo nashindwa kuunganisha dots mnaposema CCM wanaua albino wakati kila chama cha siasa kuna wanasiasa ambao ndio washukiwa wakubwa wa mauaji ya albino. Ina maana linapokuja suala la mauaji ya albino kwa matakwa ya kisiasa na vyeo CHADEMA waho hawausiki wakati wote wanasiasa!! Kwanini waseme CCM tu? Huo ni upotoshaji mkubwa sana.
 
CCM haiwezi kukwepa lawama za adha zote wanazipata Watanzania kwa sasa. Kujitakasa kwao machoni pa dunia na mioyoni mwa wananchi ni kuhakikisha wanaongoza nchi kwa uzalendo, sheria na haki. Ninachelewa kusema it is too late kwa sasa.

CCM imeua Tanzania, tutunge nyimbo zitakazo tupa mshikamano na inspiration ya kufufua nchi yetu kwa umoja, upendo na uzalendo. Tunaweza kuinua taifa letu na kusahau yaliyopita, ingawa tutayatumia katika marekebisho na maboresho.

hebu tuwe wakweli tatizo hili liko kanda ya ziwa tu? mbona sijaona albino mmasai au mchagga? mbona sijaona kiwete mmasai? wakizaliwa huwa wanaenda wapi?
 
Sasa hapo CCM inahusishwa vipi moja kwa moja na mauaji ya maalbino? Sometimes watu wanaokaa kwenye vijiwe vya kahawa naona kama wana mtindio wa ubongo. Haiwezekani ukurupuke na useme kuwa CCM wanahusika na mauaji ya Albino bila kuthibitisha kauli yako.

Jana nimeangalia kipindi cha "The Sporah Show" wageni wakiwa ni Albino mmoja hivi na mwanaharaki fulani wa Kizungu. Albino yule alisema kuwa wanauawa na kukatwa viungo maana eti ukitumia viungo vyao basi utaweza kufanikiwa kibiashara kama ni mfanyabiashara au kufanikiwa kisiasa kama ni mwanasiasa. Hapa huyu alizungumzia wafanyabiashara na wanasiasa.

Kwa mifano hiyo nashindwa kuunganisha dots mnaposema CCM wanaua albino wakati kila chama cha siasa kuna wanasiasa ambao ndio washukiwa wakubwa wa mauaji ya albino. Ina maana linapokuja suala la mauaji ya albino kwa matakwa ya kisiasa na vyeo CHADEMA waho hawausiki wakati wote wanasiasa!! Kwanini waseme CCM tu? Huo ni upotoshaji mkubwa sana.

Walioko kwenye maeneo husika ndio wanaoweza kututungia uongo wowote ila kinachakaribia na ukweli ni kuwa tunapokaribia uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu Albino wanahujumiwa sana. Hilo ni moja la pili ni kuwa idadi ya wanasiasa walio wengi ndio hao na kwa mwaka huu wako kama wana wasiwasi vile maana hata yaliyokuwa majembe yao wana hofu nayo.
 
tatizo albadiri za siku hizi hazina uzito....Masheikh wenyewe madhambi kibao......

Wapo wataalam bna....hujaongea na watu ukaambiwa.....kitu kama kweli ni haki yako ikisomwa hyo humalizi lisaa uone watakavyo puputika watu. Ni vile watu wanaogopa masharti yake magumu....
 
Back
Top Bottom