Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Moderator Mhariri naomba muiangalie hii habari upya kwanza katika hili -----------forum haiwezi kuwa source ya habari nilitegemea mtoa mada atajikita kueleza maneno hayo Mbowe amesema wapi na amekaririwa na chombo kipi cha habari?Na ameongea akiwa wapi?

Kwanza kwenye hii habari hakuna sehemu hata moja ambayo kuna nukuu ya Mbowe akisema Jk ana husika na mauaji ya Albino!Au mtoa mada atwambie kuwa habari hiii hiyo forum imeitoa wapi?

Ukiangalia kichwa cha habari ni tofauti na yaliyo andikwa ndani!
tumia akili wewe Ruta
 
Last edited by a moderator:
Wewe unamuua Albino kwa kuongopewa na mganga kwa ajili ya tamaa zako za utajili wa haraka haraka harafu unamlaumu ki kwete wewe unaona hiyo imekaa sawa?
we kweli zero,hivi ni nani amiri jeshi nchi hii.ni nini majukumu yake kama amiri.soma katiba kila mtu ana haki ya kuishi
 
​sijui kwanni nguvu hii wanayoiagiza kupambana na maandamano ya upinzani isitumike kupambana na mauaji ya albino
 
huyu hata chadema wanajua uwezo wake ni mdogo kinachmsaidia ni ile helcopter na mwenye chama ni mkwe wake
 
we kweli zero,hivi ni nani amiri jeshi nchi hii.ni nini majukumu yake kama amiri.soma katiba kila mtu ana haki ya kuishi

Kwa hiyo na wewe una haki ya kuwaua ili jumba bovu limuangukie Amiri jeshi mkuu? Kumbuka mlinda nchii ni mwana nchii na kila raia ni askari kwa mwenzie tukishikamana kwa pamoja haya yote hayatatokea
 
Rais zaifu ever anashindwa kimpiga chini igp na mkurugenzi wa usalama wa taifa asije tokea rais mwingene wa hovyo hivi nchini.
 
Kuzama KWA mv bukoba serikali ilihusika , kushindwa kudhibiti madawa Ya kulevya serikali ilihusika , kuuwawa Kwa Tembo serikali ilihusika , matokeo Mabaya Ya shule Za kata serikali ilihusika ,Na Hata Haya mauaji Ya Albino wewe unganisha dots utaona wanavyohusika !!
 

Attachments

  • 1425195475430.jpg
    1425195475430.jpg
    53.9 KB · Views: 106
  • 1425195550033.jpg
    1425195550033.jpg
    65.1 KB · Views: 104
  • 1425195578115.jpg
    1425195578115.jpg
    60.1 KB · Views: 105
Kuna taarifa kuwa dr slaa alienda kwa mganga wake akaambiwa apeleke viungo vya albino ili mambo yake ya urais yamnyookee.uchunguzi unaendelea
 
Jeshi la police liko fit na ngangari kuzuia maandamano ya chadema tu!Albino tuwalinde wenyewe...kama wapinzani wanaweza kulazimisha bunge lijadili hoja ya kupigwa kwa lipumba basi sidhani kama wakiamua kulisimamia hili watashindwa,.
 
Hivi kama kweli viungo vya albino ni utajili mbona wenyewe si matajiri kivile wapo kawaida tu, jaman watanzania najua huo ni ujinga tu, lakini pia ninyi ni vipofu? hamuoni kwamba wao wenyewe yaan albino si matajiri? kama kuweka viungo vyao kwenye migodi unapata madini mengi je si zaidi ya wale wanaoishi nao maana wanaishina miili mizima si wangekua wakina Mr Mengi..... acheni ujinga jamani
 
Hunted down like animals and sold by their own families for £50,000: Tanzania's albinos hacked apart by witchdoctors who believe their body parts 'bring luck' in sick trade 'fuelled by the country's elite'


  • WARNING GRAPHIC CONTENT
  • Tanzania has the highest number of killings and attacks in Africa
  • Trade in body parts driven by belief albinos bring luck and wealth
  • Witchdoctors turning bodies worth thousands into charms and potions
  • Greed drives husbands to turn on wives, parents to turn on own children
  • Buyers thought to be some of Tanzania's richest and most powerful people
  • Fears killings will rise as the presidential election approaches in October

Tanzania's albinos are being 'hunted down like animals' as greed for money and influence drives families to turn on their own loved ones in a trade allegedly fuelled by some of the country's most powerful people.

It is believed albino body parts will bring a person wealth, or luck - and for that, people are willing to pay as much as $3,000 or $4,000 for a limb, or as much as $75,000 - about £50,000 - for the 'full set', a whole body.

People with albinism are regularly attacked by people who chop their limbs off - an act which either leaves them severely mutilated, or dead.

11.jpg
Tanzania's albino population is being hunted down by people who want to turn their body parts into potions and charms

Albinism, a hereditary genetic condition which causes a total absence of pigmentation in the skin, hair and eyes, affects one Tanzanian in 1,400, often as a result of inbreeding in remote and rural communities, experts say.

In the West, it affects just one person in 20,000.

Since people began collecting records of the attacks, there have been 74 killings and 59 survivors of attacks. Even the dead are not safe: 16 graves have been robbed.

And these are only the recorded cases.

The most recent case saw four-year-old Pendo Emmanuelle Nundi abducted from her home in December.

Her father and uncle were both arrested in connection with her disappearance, but - despite rewards offered of £1,130 and promises of swift action from the police - she has not been found.

Charities working in the area do not hold out much hope she will be returned safely, but - listening to survivors' stories - it is likely her end is, or will be brutal.

Mwigulu Matonange was just 10 when he was attacked by two men as he walked home from school with a friend.

They chopped off his left arm, before disappearing back into the jungle with their 'prize'.

'I was held down like a goat about to be slaughtered,' he told IPP Media after the February 2014 attack.

In Mwigulu's case, the two men were strangers: he had never seen them before.

But it is understood suspicion turned on Pendo's father after he took half-an-hour to report her abduction, despite there being neighbours who could have helped as soon as she was taken.


12.jpg
Who is my enemy? Josephat Torner, a campaigner for albino rights who works with charity Standing Voice, says family members have been involved in planning attacks against people with albinism.

It is not just parents. A 38-year-old woman with albinism was attacked with machetes by her husband and four other men while she was sleeping in February 2013, according to a UN report.

Her eight-year-old daughter watched her father leave the bedroom carrying her mother's arm.

Those living with albinism in Tanzania fear the lure of making a couple of hundred dollars - three times the minimum wage earned in the country - is placing them in danger, even from their own families.

'Now we can see the parents who are involved in planning the attacks. What kind of war are we fighting if parents and family do this? Who can we trust?' Josephat Torner, who campaigns for albino rights, asked.

'You do not know who is your enemy.'

Josephat, who himself is albino, added: 'People with the albinism are being hunted and killed for our body parts. It is because people want to become rich.

'We are still living in danger. It is because people, they have different ideas. Some people, they are thinking they should get our body parts and sell to different places.

'The question is, why? Why now? And who is behind the killings?'

Exactly who remains unknown.


"What kind of war are we fighting if parents and family do this? Who can we trust? You do not know who is your enemy" Josephat Torner, albino campaigner.

But Josephat - who has received death threats for his work, and was attacked in 2012 - said: 'The big fishes are behind the issue. It has been really a big discussion. If I say big fish, or big people, it is those who have enough resources, enough money.

'People sell the body parts for high prices. So it is not really small fish behind it.

'It could be politicians. It could be those people.'

24C75A5D00000578-2922243-Limbs_can_sell_for_as_much_as_4_000_about_2_667-a-5_1422286111632.jpg

Many albinos survive the attacks, but are left without arms or legs, which can sell for as much as $4,000. Pictures from Universal Initiative Foundation

albinoo.png

Josephat's theory is backed up by Peter Ash, a Canadian who set up the charity Under the Same Sun in 2009.

'In a country like Tanzania, which is the 25th poorest in the world, the only people with that kind of cash are politicians or wealthy businessman,' he said.

But whoever they are, those buying the witch doctors' wares are clearly powerful.

Only 10 people have ever been brought to trial for their part in albino attacks or murders - but not one of them was a 'buyer'.

'The only people who have been convicted are the witch doctors and the hired killers,' said Peter.

'But they would never name the customer - even when the witch doctor is given the death sentence. Never has a customer been named.'


13.jpg
It is thought those buying the potions made by the witch doctors include some of the richest and most powerful people in the country

There are, campaigners know, times when more albino attacks take place. And they know, with the general election coming up in October, now is one of the most dangerous times to be an albino.

The UN warned political campaigners were turning to witch doctors to help them win election back in August.


"In a country like Tanzania, which is the 25th poorest in the world, the only people with that kind of cash are politicians or wealthy businessman Peter Ash, campaigner "


Josephat added: 'This year we are going to have an election. Since last year, we have been seeing attacks and killings.'

Already, there has been a noticeable increase.

Over the course of just 11 days last year, there were three attacks and two attempted attacks on people with albinism in Tanzania.

One man, thought to be in his early 20s, was found lying dead, his body mutilated, in the grass by some schoolchildren in a suburb of Dar Es Salaam.

The next day, a mother-of-seven was attacked in the Tabora region of Tanzania, losing her arm.


14.jpg
Pendo Sengerema, 15, pictured right with campaigner Vicky Ntetema, was one of three people attacked in 11 days last August

15.jpg
Children and adults are kept behind high walls in special centres, hidden away from the people who want to kill and maim them

A few days before, 15-year-old Pendo Sengerema was attacked as she ate dinner at home with her family.

They hacked off her right arm just below the elbow, before running off into the dark.

According to Under the Same Sun, a witch doctor had received an order from a wealthy client indicating that if Pendo's arm could be provided, it would garner a price of $600.

The attack left Pendo terrified, begging to be sent away from her village.

'I am asking the police to move me to a safer place and protect me because bad men might come back to kill me,' she pleaded.



"I am asking the police to move me to a safer place and protect me because bad men might come back to kill me
Pendo Sengerema, 15"


These 'safer places' are the centres set up around the country, where large number of people with albinism are living behind high walls for their own protection.

The camps were established after the first high profile waves of attacks, a knee-jerk response to a terrifying situation.

'It was supposed to be a short term solution,' Peter said. 'But there was no long term plan.'

Years later, they still exist - and now are not just for children: adults are kept behind the camps' high walls as well.

'Children who are there, they are living there maybe for seven years without going back to their families,' said Josephat.

'At the end of the day, families or communities do not want to allow them to go back. These children are growing up without any parental care.'

'If you ask the community why now are they forcing their children to the camps, they are saying it is where they belong. But we are not for the camps: we are for the community.'

16.jpg
Prejudice is such in Tanzania that children like Verdastus, pictured, are often unable to attend school

But the government now appears to be taking action: after widespread criticism of its reaction to Pendo's abduction, it moved to outlaw the witch doctors behind the killings.

They have not banned traditional healers who use herbs, however.

'These so-called witches bear responsibility for the attacks against albinos,' interior ministry spokesman Isaac Nantanga said.

But as to whether it will make a difference for those living in fear for their lives remains to be seen.

Harry Freeland, who spent seven years following Josephat and other Tanzanian albinos for his documentary In the Shadow of the Sun, was cautious.

albino.png

'Really, we can't jump to conclusions,' he said. 'It means nothing until we can see tangible results.

'There is hope for strong action. But we have heard statements like this before.'

Peter is less confident, pointing back to 2009, when President Jakaya Kikwete declared he was outlawing witch doctors.

But the sweeping statement sparked a backlash in a country where many people still rely on traditional medicines, and the new law was quietly ditched.

But this time, the government is also putting an emphasis on education.

17.jpg
Josephat hopes Tanzania's albinos will one day be able to 'live like other people'

That's something Josephat has been doing for years: risking his life to go into remote villages to explain to people they are not ghosts, but human beings whose bodies will not bring luck.

He hopes to reach more people now, with the help of Harry's documentary.

And he hopes, eventually, that he will no longer have to leave his family behind in Dar es Salaam while he travels across the country.

In the meantime, he will continue to campaigning and trying to raise awareness.

'Why are we being threatened in our own country, because of our colour?' he asked.

'We are living like refugees in our own country because of our skin colour.

'We are being judged for our colour. We are being punished.

'What we are demanding is a right to life. This should be fundamental, but we are being denied it.'

'I want to live like other people, the way they live.'

Source: Tanzania's albinos hacked apart by witchdoctors | Daily Mail Online
 
HOTUBA YA MWISHO WA MWEZI FEBRUARI, 2015, YA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, ILIYOTOLEWA TAREHE 1 MACHI, 2015

Ndugu Wananchi;

Kama ilivyo ada tunamshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kuzungumza kupitia utaratibu wetu huu mzuri wa hotuba za kila mwisho wa mwezi. Kwa mwisho wa mwezi wa Februari nina mambo matano ninayopenda kuyazungumzia.

......................

Mauaji ya Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi

Ndugu wananchi;

Nimesikitishwa sana na taarifa kuwa mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) yameibuka upya baada ya hali kuwa tulivu mwaka 2011. Mwaka jana (2014) yalitokea matukio matatu katika mikoa ya Mwanza, Tabora na Simiyu na mwaka huu limetokea tukio moja mkoani Geita.

Lazima tulaani vikali mauaji ya ndugu zetu albino. Ni vitendo vya kinyama ambavyo havitegemewi kufanywa au kutokea katika jamii yeyote ya watu waliostaarabika, ya watu wanaomuabudu Mungu. Watu wenye ulemavu wa ngozi ni wanadamu wenzetu, wenye haki sawa ya kuishi na kupata hifadhi ya maisha yao kama walivyo wanadamu wengine. Hawastahili kufanyiwa wanayofanyiwa.

Hawapaswi kuishi kwa hofu katika kijiji chao, mtaa wao au katika nchi yao. Jamii nzima na sisi sote mmoja mmoja na katika umoja wetu, tunao wajibu wa kuhakikisha usalama wa maisha yao na mali zao kama ilivyo kwa watu wengine wote.

Kwa kweli, mauaji ya albino ni jambo linalofedhehesha na kulidhalilisha taifa letu. Ni vitendo visivyovumilika. Hatuna budi sote kushikamana na kuhakikisha kuwa tunapambana nao kisawasawa na kuwashinda. Tusikubali kamwe wakaturudisha kule kubaya tulikokuwa zamani.

Naungana na Chama cha Albino Tanzania kulaani ukatili huu na kutaka watu wote wanaojihusisha na ukatili huu wasakwe, wakamatwe, wafikishwe Mahakamani na kupewa adhabu kali inayowastahili wanapopatikana na hatia.

Ndugu Wananchi;

Napenda kuwahakikishia kuwa wakati wote Serikali imelipa uzito mkubwa suala la kudhibiti na kukomesha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi au kukatwa baadhi ya viungo vyao wenyewe wakiwa hai. Tumefanya hivyo bila ya kuchoka tangu tukio la kwanza baada ya mimi kuingia madarakani Aprili 17, 2006 na miezi mitatu tu kule Nyahunge, Geita alipouawa Alfa Amon ambapo watuhumiwa wawili waliuawa na raia.

Mwaka 2007 kulikuwa na matukio saba. Mwaka 2008 ndio ulikuwa mwaka mbaya sana walipouawa watu 18.

Kutokana na jitihada kubwa zilizofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wananchi mauaji yalipungua na kuwa tisa mwaka 2009. Mwaka 2010 kukawa na tukio moja na mwaka 2011 hapakuwepo na tukio lolote. Mwaka 2012 kukawa na tukio moja, mwaka 2013 aliuawa mtu mmoja na wawili kujeruhiwa.

Mwaka 2014 waliuawa watu watatu na wawili kujeruhiwa, na Januari, 2015 kumetokea tukio moja kule Geita.

Ndugu Wananchi;

Tangu mwaka 2006 mpaka 2015, watuhumiwa 139 wametiwa nguvuni, miongoni mwao wako watuhumiwa 16 wa matukio ya Desemba na Januari mwaka huu. Mashauri 35 yamefunguliwa mahakamani na kati ya hayo 10 bado yanaendelea na yapo katika hatua mbalimbali. Watuhumiwa 73 wameachiliwa na 15 wamepatikana na hatia.

Kati ya hao waliopatikana na hatia 13 wamehukumiwa kifo na wawili wamepata kifungo cha miezi 6. Watuhumiwa kwa matukio sita bado wanasakwa.

Matukio ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yametokea katika mikoa kumi kati ya mikoa 30 hapa nchini. Mikoa hiyo ni hii ifuatayo: Mwanza matukio 13, Kagera sita, Tabora matano, Geita manne, Mara manne, Kigoma manne, Simiyu matatu, Shinyanga mawili, Arusha moja na Mbeya moja.

Utaona matukio 41 kati ya 43 yametokea katika ukanda wa ziwa ambapo pia wanaongoza kwa mauaji ya vikongwe na wanawake kwa sababu za ushirikina.

Ndugu Wananchi;

Inawezekana kuwa matukio ya hivi karibuni yanaashiria kuwa uhalifu huu unataka kuibuka upya. Napenda kuwahakikishia ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi na Watanzania kwa jumla, kuwa hatutaacha hali iwe mbaya kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Tutatumia mbinu na maarifa tuliyoyatumia kukabili wimbi kubwa la mauaji lililokuwepo mwaka 2007 na 2008 na kwa sababu hiyo tukaweza kupunguza hadi kufikia kutokuwa na tukio lolote la mauaji mwaka 2011.

Tunachokiomba kutoka kwa wananchi ni ushirikiano na msaada wa kuwafichua watu wanaofanya vitendo vya mauaji na kukata viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi. Pia wasaidie kutoa taarifa kuhusu wanunuzi wa viungo hivyo na waganga wanaochochea mahitaji ya viungo vya albino. Ushirikiano wa wananchi wa wakati ule uliwezesha kupatikana kwa mafanikio niliyaeleza. Naamini safari hii tukifanya hivyo tutafanikiwa pia.

Ndugu Wananchi;

Kutokomeza kabisa matukio ya mauaji na ukataji wa viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi ni jambo linalowezekana. Hata hivyo, litategemea watu kuacha imani za ushirikina. Imani potofu, ati kuwa mtu akiwa na kiungo cha mtu mwenye ulemavu wa ngozi atafanikiwa katika shughuli zake za biashara, uvuvi na uchimbaji wa madini ndicho kichocheo cha uovu wote huu unaoendelea.

Ni ujinga ulioje kwa mtu kuamini kuwa mafanikio yake hayatategemea juhudi zake na maarifa yake bali kuwa na kiungo cha mwanadamu mwenzake mwenye ulemavu wa ngozi.

Nilisema katika hotuba yangu ya mwisho wa mwezi Machi, 2008 kwamba, kama kuwa na kiungo cha albino ndiko kutakakomfanya mtu kufanikiwa katika shughuli zake za kibiashara na kiuchumi basi ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi wangekuwa ndiyo matajiri wakubwa nchini na duniani. Maana wao sio tu wana viungo bali wana mwili mzima. Kwa sababu ya kuwepo imani hizi za hovyo, juhudi za kuelimisha jamii kuachana na imani hizi potofu ziongezwe. Naomba hili ndilo liwe jambo la msingi katika mapambano haya.

Tukifanikiwa katika hili, matatizo yote haya yatakoma. Serikali na jamii haitalazimika kushughulikia mambo haya ambayo siyo tu ni fedheha hata kumsimulia mtu bali yanatisha na kusikitisha.

Ndugu Wananchi;

Wiki ijayo nitakutana na baadhi ya viongozi na wanachama wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi. Nimekubali maombi yao ya kukutana nao ili niweze kusikiliza maoni yao na tubadilishane mawazo juu ya namna bora ya kumaliza tatizo hili.

Mimi naamini kuwa ushirikiano wa karibu kati ya Serikali na jamii utatuwezesha kutokomeza mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi na kuliondolea taifa letu aibu hii.
 
.....
Ndugu Wananchi;

Wiki ijayo nitakutana na baadhi ya viongozi na wanachama wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi. Nimekubali maombi yao ya kukutana nao ili niweze kusikiliza maoni yao na tubadilishane mawazo juu ya namna bora ya kumaliza tatizo hili.

Mimi naamini kuwa ushirikiano wa karibu kati ya Serikali na jamii utatuwezesha kutokomeza mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi na kuliondolea taifa letu aibu hii.

RED: Wakati mwingine unaweza ukadhani miezi saba ni michache lakini kunawakati unaweza kuiona ni miaka saba...!

"TUDHIBITI,TUMALIZE KABISA VITENDO VYA AINA YOYOTE YA MAUAJI YA NDUGU ZETU KWA NIA YA DHATI KABISA" wito wangu kwa watanzania wote popote tulipo.
 
ALBINO:
Laiti kama watu wangeelewa maumivu na mateso wayapatayo
hawa ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi
basi ni dhahiri hivi vitendo vya kiukatili wasingefanyiwa
na
sheria iwepo 1 tu tena kali kuwa iwapo utakamatwa kwa kuhusika
na hivyo vitendo vya mauaji ya Albino
basi na wewe mtuhumiwa
unanyongwa pamoja na mtu mmoja wa familia yako hasa mtoto
wako coz watoto wako unahisi wana thamani kubwa sana hapa
duniani kuliko hata hao mnaowaua na kuwakata viungo vyao!
Kuwaua albino na kuwakata viuongo vyao ni kitendo cha kinyama
sana ambacho hakivumiliki kamwe!
na
waganga wa kienyeji na wapiga ramri nao waambiwe marufuku
fikiria
-jua linavyo wachoma ngozi zao!
- macho yao yanavyoathiriwa na mwanga!
-kisaikolojia walivyo na mzigo mzito wa kujiona kuwa ni tofauti na
wenzao
alafu
wachache tu wanaoendekeza tamaa zao za Mali wanawaua albino
na kuwakata viungo vyao!
kweli???
inauma sana tena mno
na wao ni binadamu kama sisi!
wana haki ya kuishi
tuwalinde kwa nguvu zote
tuwatetee kila hali
tuwapiganie kwa Mali zote
tukumbuke jambo moja tu kuwa wao kuwa hivyo sio Laana
na wala hawakupenda wazaliwe hivyo
na
sio makosa wao kuwa na hiyo hali!
binafsi nawapenda na nitawapenda daima
kwa sababu nyie ni sehemu ya maisha yangu!
na
nyie ni viumbe kama mimi ni vijana, wazee, baba, mama, Dada,
mjomba, shangazi na Binamu!
Albino ni ndugu zangu wa damu!
Albino ni watanzania wenzangu
Albino ni waafrika wenzangu!
Tuungane kuwalinda Albino!
 
Binafsi na nasema tena mimi binafsi kuafiki mategemeo ya wananchi juu kitu gani serikali yetu inatakiwa kukifanya hata katka mambo ambayo sisi wananchi wenyewe tunataka tuwe pamoja na serikali inayotuongoza. haya mauaji ya Albino yanafanywa na WANANCHI hayafanywi na serikali hivo kuitaka serikali ichukue jukumu hilo badala ya sisi wananchi wenyewe kuwa sehemu ya wawajibikaji. Kwa akili hii kila siku serikali yetu itajikuta inashughulikia matukio ya wahalifu badala ya kukomesha Uhalifu.

Ikumbukwe maneno ya rais wa Marekani J. F. Kennedy akisema:- "Ndugu zangu waamerika , usiulize ni kitu gani nchi yako itakutendea, jiulize utaifanyia nini nchi yako." na hii ndio msingi wa uthubutu kwa kila mwananchi katika kuijenga nchi yake badala ya kila siku kutegemea serikali wakati yapo mambo mambayo yanatulazimu sisi wenyewe kuhakikisha tunaishi kwa amani na usalama.

Hivi kweli imechukua hadi rais wa nchi kukutana na wanye ulemavu wa ngozi kujua yanayowasibu, sisi tukiongea katika mitandao na kulaani vitendo vya mauaji? Hivi sii vita vya serikali pekee ni vita yetu sote na tunaze sisi wenyewe kuweka ulinzi kwa wenye ulemavu wa ngozi, mbona kwa majambazi na wezi tuna doria za kila kata kulinda usiku? wengine nyumba zao wamejengea mageti makubwa na kuta kama jela kujilinda na wezi lakini inapofika swala la walemavu wa ngozi ni swala la serikali na utawala wa JK.

Labda nimalizie kwa kusema hivi, mimi nina hakika kabisa kwamba wenye kuvitaka viungo vya hawa watoto wetu wenye Ulemavu ni baadhi ya viongozi wetu na matajiri ambao wameaminishwa ushindi ktk mapambano ya Fitna za kisiasa kwani haiwezekani maskini anaweza kutoa fedha sawa na dollar za Kimarekani elfu 75 (Usd 75,000) kwa manunuzi tu ya viungo ukiacha tozo za mchawi aliyeitisha viungo hivyo.

sasa ikiwa mateja wa viungo hivi ni viongozi wetu halafu sisi tunawataka wao washughulikie mauaji ya Albino kweli hii inawezekana? Yaani kwa mlevi wa gongo, umtake yeye apige vita wauzaji Gongo! Hi hata katika elimu ya uchumi haiwezekani maana kuwepo kwa wateja ndiko husababisha kupatikana ili kuwatosheleza wateja iwe haramu ama halali ndio mfumo wa biashara. Unga unapigwa vita dunia nzima lakini kama sisi wananchi wenyewe hatutakuwa sehemu ya vita hiyo, tutashindwa tu maana hakuna kitu kibaya na chenye kuchukua umaarufu haraka kama haramu. Na hakuna utajiri wa nchi nyingi duniani ambao haupitii haramu hizi iwe riba, ulaghai, unga kuuza silaha na kadhalika. Ukiwa maskini yapo mengi hatuyafahamu ambayo ndio shehena ya matajiri - HARAMU.

Nawaomba wananchi wenzangu, tuache kuitegemea serikali kwani toka lini wamekuwa msitari wa mbele kupambana na uhalifu?. Tunaibiwa benki zetu ni lini mlisikia fedha imerudi? na mara nyingi wizi mdogo huwa sababu ya kufuta wizi mkubwa ndani ya bhizi hizo benki zetu. wameipa banki kuu fedha ya EPA, wauza unga, Escrow, wengine hata kodi hawalipi wameficha fedha Uswiss na serikali imeridhia kwa kutaka wananchi watoe ushahidi.. Sasa hili la mauaji nalo sijui tulitolee ushahidi maana walemavu wanauawa, lakini hatuna ushahidi wanaoutaka.

Binafsi, nimesha kata tamaa na serikali hii toka wakati wa Mkapa na sidhani kamamaobi yetu yatapokelewa zaidi ya kufunika chungu mwana haramu apite. Sisi ni wepesi wa kusahau na itafika mahala tutasahau tutaanza kutazama uchaguzi mpya kamna kwamba kutakuwepo na UWAZI ama uchaguzi tofauti na ulokwisha tangulia.

- Miafrika bana hakika tumelemazwa na Ukoloni...
 
Back
Top Bottom