Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Thats right... nilitegemea mtaalamu wa mambo ya Unyani kama wewe ungekuja na expert opinion kuhusu hili wazo, badala yake unakenua meno kaa nyani. You could get hired on the spot to lead this kind of one-of-a-kind, life-saving project never before seen in the whole World...

a.ss is grass...........
 
Atengwa na wazazi kwa kuoa albino

]

Na Rehema Lippu, Dodoma

MKAZI wa Dodoma mjini, Bw. Peter Msangi, amejikuta katika wakati mgumu baada ya familia yake kumtenga kutokana na kuoa mwanamke albino, Bi. Mariam Simon.

Ndugu wa Bw. Harusi huyo walisusia sherehe ya kijana wao baada ya kumtaka amwache albino huyo, lakini bila mafanikio.

Kutokana na hali hiyo, wazazi walimfukuza kwa madai kuwa amewapelekea nuksi katika familia, kwani tangu ukoo huo umekuwapo duniani haujawahi kuzaa mtoto albino wala kuozesha mtu wa jinsi hiyo.

Katika utaratibu mzima wa kuhakikisha anapata jiko, aliwapa taarifa wazazi wake, lakini ilikuwa vigumu kueleweka kwa wazazi wake jambo ambalo lilimfanya ajishughulikie katika suala zima la mahari.

Pamoja na kuendelea na hatua hizo zote, wazazi wake waliendelea kumchukia na kumwona kama amechanganyikiwa lakini msimamo wake ulizidi kuwa madhubuti na kutaka kumaliza mahari, ili aweze kupata fursa ya kupangiwa muda wa kuoa.

Hata hivyo, juhudi za kuhakikisha anakamilisha hatua zote zilizidi kuwapa hasira wazazi wake ambao waliamua kutotaka kumwona hata kwa sura, kwa madai amewafanyia kitu kibaya.

Baada ya wazazi kususia harusi hiyo na kuamua kumfuta katika ukoo, Kanisa liliamua kumtafuta mzazi wa bandia ili kuweza kuondoa maswali mengi kwa watu walioalikwa kufika katika sherehe ambayo ilikuwa ya kufa mtu.

Majira ilizungumza na Bwana Harusi juu ya uamuzi wake na wa wazazi, alisema amempenda binti huyo ambaye ni albino kwani ana sifa zote za kuitwa mke mwema.

Bw. Msangi alisema kuwa anachotambua ni kila mtu ana kasoro zake na kila mtu ni mlemavu, hivyo suala la ngozi haliwezi kuwa kigezo cha kumfanya asimwoe binti huyo ambaye anajua wazi kuwa hakuna binti mzuri kama yeye.

“Albino ni mwanadamu kama mwanadamu mwingine na rangi yake imenivutia zaidi kwani hana tofauti na Wazungu," alisema Bw. Msangi ambaye sherehe yake ilikuwa kubwa kuliko kawaida.

Juu ya uamuzi wa wazazi kumtenga, alisema anachoshukuru wazazi wake ni kumlea vizuri na kumfundisha mema na mabaya, hivyo kwa kuwa ameishakua amechagua kumwoa mke huyo ambaye ni chaguo la moyo wake.

Alisema anachosubiri sasa ni kuona kama wazazi wake watamchukia yeye pekee au watawachukia pia wajukuu kama Mungu atawajalia kupata watoto hapo baadaye.

Kwa upande wake, Bibi Harusi, Mariam Saimoni alisema mpango wake na wa Mungu, ni kuona kila mwanamke anaolewa na yeye ameolewa kama walivyo wanawake wengine na kuhusu suala la yeye kuzaliwa albino si lake ni mpango wa Mungu.

Alisema kuwa albino si tiketi ya kukosa haki zake, bali anastahili kupata haki zake kama watu wengine na anawashukuru wazazi waliomsomesha na kumfanya aishi maisha mazuri kama watu wengine.

Pia alimsifu mumewe kwa ujasiri wa kumchumbia na kufuata taratibu zote kwa uaminifu, mpaka kufikia hatua ya kufunga pingu za maisha ingawa wamekuwa na mapito mengi, kwani alionekana kama anaoa mtu ambaye hastahili kuwa katika jamii.

Naye Theonestina Juma, anaripoti kutoka Bukoba, kwamba
mkazi wa kijiji cha Runazi Rusabya, wilayani Biharamulo, Bibi Magdalena Andrea (30), ambaye ni albino, ameuawa kwa mapanga na watu wasiojulikana waliomteka nyara wakati akitoka sokoni kuhemea mboga.

Aidha, katika tukio hilo, Jeshi la Polisi mkoani hapa linamshikilia mganga wa jadi, Bw. Lameck Laizariiyo (38) wa Tarime mkoani Mara, akidaiwa kuhusika katika tukio hilo.

Inadaiwa kuwa mganga huyo alikutwa na begi lililosheheni zana za uganga.

Habari zilizopatikana kutoka wilayani humo na kuthibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Bw. Arthur Magoti, zilisema tukio hilo lilitokea Septemba 21 mwaka huu saa 1.30 usiku umbali wa meta 10 kutoka nyumbani kwake.

Kamanda Magoti alisema katika tukio hilo, wauaji hao walimcharanga mapanga mabegani, kichwani na kumkata kiganja cha mkono kilichodondoka chini.

Hata hivyo, alibainisha kuwa watu hao hawakufanikiwa kuondoka na kiungo hicho ambacho hakikubainishwa kuwa kilikuwa cha mkono gani, licha ya habari zaidi kueleza kuwa kilikuwa cha mkono wa kulia.

Hata hivyo alifariki dunia kutokana na kuvuja damu nyingi.

Kamanda alisema katika tukio hilo, mtu mwingine anayeshikiliwa na Polisi wilayani huyo pamoja na huyo mganga ni Bw. Pancras Binango (58) mkazi wa Kabukaine Kayanza wilayani humo na watu wengine wanne walikimbia
 
....Hongera maharusi Peter & Mariam. Mungu atawajalia ndoa yenu idumu na kufikisha umri wa mika 100. Tulia jazba za wazazi zitatulia na watakuja kugundua makosa yao na watakurudia kama kweli ni wacha mungu...
 
Jamani huyo kijana aliye oa albino nampongeza sana, na kumuombea Mungu amjalie familia yenye furaha ana amani ili liwe fundisho hata kwa jamii inayo wazunguka.

Huyo aliye uliwa inasikitisha sana, Ila jamani watanzania tusipo anagalia tutageuka taifa la washirikina sasa hivi!
 
Kizimbani wakidaiwa kuua albino, kumkata kiganja


Na Theonestina Juma, Bukoba

WATU wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Biharamulo kwa tuhuma za kumuua albino kwa mapanga na kumkata kiganja cha kulia.

Watu hao ambao ni mganga wa kienyeji na baba mkwewe walifikishwa juzi katika Mahakama hiyo, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya hiyo, Bw. Kaliho Mrisho.

Wakisomewa mashitaka na Mwendesha Mashitaka wa Polisi wilayani humo, Bw. Boniphace Mayala, ilidaiwa kuwa watu hao walimkamata albino huyo, Bibi Magdalena Andrea (30), wakati akitoka sokoni na kumkata mapanga.

Watu hao waliofikishwa mahakamani ni Bw. Pancras Binango (58) ambaye ni baba mkwe wa mganga wa kienyeji kutoka Tarime, Bw. Lazack Laiziiyo (38).

Ilidaiwa kuwa Bw. Binango ni mkazi wa kijiji cha Kabukoine Kayanza wilayani Biharamulo.

Mwendesha mashitaka huyo wa Polisi alidai kuwa tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Runazi Rusabya katika kata ya Katoke Septemba 21 mwaka huu, saa 1.30 usiku, wakati mwanamke huyo akitoka sokoni umbali wa meta 10 kutoka nyumbani kwake.

Ilidaiwa kuwa watu hao walikuwa takribani sita na walimkamata albino huyo na kumcharanga mapanga, na hata hivyo hawakuondoka na kiungo chochote baada ya wananchi kujitokeza kumsaidia, kutokana na makelele aliyokuwa akipiga kuomba msaada.

Hata hivyo, watu hao hawakutakiwa kujibu lolote kuhusiana na sataka linalowakabili, kutokana na Mahakama kutokuwa na uwezo wa kuendesha kesi hizo za mauaji.

Kesi hiyo itatajwa Oktoba 2 mwaka huu na watuhumiwa wako rumande kutokana na kesi hiyo kutokuwa na dhamana.

Wakati huo huo, watu wasiojulikana wamemvamia Bibi Mpejwa Mbapura (55) na kumuua kwa mapanga sehemu mbali mbali za mwili nyumbani kwake kwa kile kinachodaiwa kuwa ni imani za kishirikina.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Bw. Arthur Magoti, tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Rusunga kata ya Mkugungusu wilayani Chato Septemba 21 mwaka huu saa 9 alfajiri.

Ilidaiwa kuwa watu hao walifika nyumbani kwake usiku huo na kuvunja mlango na kuingia ndani na kumpiga mapanga hadi kufa.

Katika tukio hilo hakuna mtu anayehusika, ambapo uchunguzi zaidi unaendelea wilayani humo, ili kuwabaini waliohusika.
 
Lakini hili halina tofauti na Wazazi wanaomtenga binti au kijana wao kwa kuolewa/kuoa mke/mume wasiyemtaka kutokana na matakwa yao kwamba binti/kijana wao aowe/aolewe na fulani au na wa dini yake. Haya yapo sana, lakini hayapewi kipaumbele kwenye magazeti yetu kama hili la albino. Pamoja na hayo napinga kabisa mauaji ya albono maana ni unyama wa hali ya kuu kuwaua eti kwa imani za kichawi.
 
Bwana mmoja aliwahi kuniambia,ukiona mtu ameanza kuupa ushirikina nguvu katika maisha yake basi ujue huyo ameishiwa mbinu za mapambano.Ingawa sina uhakika kama wimbi hili la kuua albino ni dalili za watanzania kuishiwa mbinu za kupambana na maisha!
 
Hongereni sana maharusi Mungu atawaonyeshea njia hayo matakwa ya wazazi wa bwana harusi ni mapito tu hapa duniani nyie imradi mnapenda basi mengine Mungu atawashushia tu kama anavyo washushia wengine neema.
 
Hivi kwa nini viongozi wote wa sehemu ambako mambo haya yanatendeka wasiwajibishwe? Kuanzia Mjumbe wa nyumba kumi, OCD na kuendelea. Mambo haya yanatia kinyaa!

---mwongozo wa chama hauwaruhusu kuwajibishana! kuanzia ngazi kuu mpaka huko chini kwenye hizo ndogondogo...
 
Mungu awape maisha yenye furaha katika ndoa yenu. Penzi halichagui albino wala asiyekuwa albino. Hao wazazi inabidi waelimishwe ili waache unyanyapaa.
 
....Hongera maharusi Peter & Mariam. Mungu atawajalia ndoa yenu idumu na kufikisha umri wa mika 100. Tulia jazba za wazazi zitatulia na watakuja kugundua makosa yao na watakurudia kama kweli ni wacha mungu...

Hongereni sana Petro and Mariamu. Hivi wazazi ni lini watawapa watoto wao uhuru hasa pale ambao wanaoa au kuolewa na vijana descent?? Mzazi unaweza kumkataza mtoto wako kutooa binti au kijana fulani kama utahakikisha kuwa ana nidhamu mbaya, n.k. Sasa bila aibu at masuala ya ngozi au ualbino unayaingiza katika kukatiza furaha ya mwanao. Unajuaje kama haitatokea mwanafamilia kuzaa albino? Genetically kila kitu ni possible!!!

Basi kuna watu fulani mtoto alizaliwa albino wakwe wakamcharukia binti wa watu kuwa yeye ni malaya amewazalia mtoto wa kizungu. Yaani walimchukia mpaka kesho ila tu mume alijua kuwa si kuwa mke ni mzinzi bali kazaa albino.

Kilichotokea katika watoto wanne wa ile familia yule albino ndiye aliyekuwa bright sana, akaenda kusoma Marekani na kule Chuoni tena reputable Institution alikuwa anaongoza!!!!!! Albino are human beings, same as you , only the skin melanine had made them different.

Have a nice week end.
 
Mkipata njia za kuwasiliana nao mtawasaidia kwa namna yeyote ile hasa kama mnavyojua mama anahitaji vifaa na vitu mbalimbali kufanya maisha yake yawe ya kawaida? au ni kutoa hongera tu?
 
Imeandikwa hivi; mtu atamwacha baba yake na mama yake ataungana na mwenzake nao watakuwa mwili mmoja. Bravo maharusi wetu; hizi ndo harusi ambazo ukiletewa kadi ya kuchangia gharama za sherehe unatakiwa utoe mchango fasta na mchango mnene.

Wazazi wa Bwana harusi tuwasamehe na kuwaombea kwa Mungu awasamehe.

Na pole kwa wote walioguswa na mauaji huko Bukoba
 
Atengwa na wazazi kwa kuoa albino

] “Albino ni mwanadamu kama mwanadamu mwingine na rangi yake imenivutia zaidi kwani hana tofauti na Wazungu," alisema Bw. Msangi ambaye sherehe yake ilikuwa kubwa kuliko kawaida.

Hongera, lakini hii haijatulia kabisaaaaa.
 
MKAZI wa Dodoma mjini, Bw. Peter Msangi, amejikuta katika wakati mgumu baada ya familia yake kumtenga kutokana na kuoa mwanamke albino, Bi. Mariam Simon.

Mimi ninakumbuka enzi za halaiki, kulikuwa na di-zeru (Albino) kutoka secondari ya Forodhani, ambaye siku hizi ni mbunge kama sikosei,

Baba yake alikuwa na uwezo sana, kwa hiyo alikuwa aking'aa kama mtishi na vijana kibao walikuwa wakizimia naye sana na kuna waliokuwa waki-mdate pia, na kuna mshikaji aliyeishia kumuoa kabisa, na sikuwahi kusikia noma yoyote, wala sikuwahi kuhisi kuwa kuna tatizo hata siku ya harusi kwa sababu I was there, na nilishwahi kufika kwao kama mara mbili hivi longtime ago

Sasa ninaposikia haya maneno kama ya hii mada, ninakuwa na wasi wasi kwamba huenda hali ya kimaisha ya alikotoka huyo di-zeru inaweza kuwa ni sehemu ya tatizo nini? Kwa sababu how comes hakukuwa na tatizo na yule dada aliyeolewa na mshikaji, au kuna something nina-miss hapa?
 
Hongera Bwn Msangi na Bi Mariam......Mungu awazidishie rehema zake ili mpate kuishi kwa mapenzi yake.........

Mkuu FMES........aisee yaani niliposoma tu hii habari nikaikumbuka sana ile harusi.........hahaha dahh.......nakumbuka pia vijana walivyokuwa wanajigonga kipindi kile
 
lakini,tukienda na mambo ya genetics,hii ndoa no docter could have adviced ifanyike,labda familia ya bwana arusi,inaelewa hii kitu.lazima tukubaliane many years after these two have passed on,ile gene ya albinism will continue.naamini wengi wenu humu if you had been in the shoes of hao wazazi,mngepinga vilevile.Hizi double standards kwa sababu you hiding behind the KEYBOARD is not good
 
Mimi ninakumbuka enzi za halaiki, kulikuwa na di-zeru (Albino) kutoka secondari ya Forodhani, ambaye siku hizi ni mbunge kama sikosei,

Baba yake alikuwa na uwezo sana, kwa hiyo alikuwa aking'aa kama mtishi na vijana kibao walikuwa wakizimia naye sana na kuna waliokuwa waki-mdate pia, na kuna mshikaji aliyeishia kumuoa kabisa, na sikuwahi kusikia noma yoyote, wala sikuwahi kuhisi kuwa kuna tatizo hata siku ya harusi kwa sababu I was there, na nilishwahi kufika kwao kama mara mbili hivi longtime ago

Sasa ninaposikia haya maneno kama ya hii mada, ninakuwa na wasi wasi kwamba huenda hali ya kimaisha ya alikotoka huyo di-zeru inaweza kuwa ni sehemu ya tatizo nini? Kwa sababu how comes hakukuwa na tatizo na yule dada aliyeolewa na mshikaji, au kuna something nina-miss hapa?

Yawezekana huyo albino anatoka sehemu nzuri tu na anag'aa na ndio maana mme anasema kama zungu fulani.

Tatizo hapa yawezekna ni mila potofu ambazo lazima zirekebishwe wengine hapa watasema nazipiga vijembe mila zetu.

FM na mimi nilishaona jamaa kaoa TASHA kutoka SWIZ na ana fedha lakini wazazi wakakataa katakata Lakini jamaa alipotea na zungu lake hajatokea tena Na kwa hili utasema je?
 
FM na mimi nilishaona jamaa kaoa TASHA kutoka SWIZ na ana fedha lakini wazazi wakakataa katakata Lakini jamaa alipotea na zungu lake hajatokea tena Na kwa hili utasema je?

Sina uhakika kama umeielwa point yangu ambayo nimei-present in a question manner, lakini anyways in your case ni jamaa aliyeoa mtishi ndio mwenye pesa,

kwenye case yangu, ni mama albino au kwa lugha yetu ya kizaramo Di-Zeru, ndiye anayetoka kwenye familia ya pesa, wakati kijana aliyemuoa hatoki kwenye pesa, kwa hiyo aliyenufaika hapa ni kijana na familia yake nzima,

Halafu mind you kuwa huyu dada Di-zeru sasa ni mbunge, ndio maana nikauliza kuwa inawezekana kwamba ufukara nao ukawa unachangia haya matatizo ya ma-Di-Zeru? au?
 
Back
Top Bottom