Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mzee Mwanakijiji,
Mkuu hakuna mtu anaye support street justice kuwa ndio njia pekee itumike, isipokuwa tunashauri sheria ya jino kwa jino..Israel na nchi zote za kiarabu, chache za Asia wanatumia sheria hizo na hatuoni watu wakiuana kama unavyodai..
Hizo street justice zipo Tanzania hadi kesho wanakufa vizee na vibaka sioni ukizungumzia hilo kwa mifano ya kisasi isipokuwa inapofikia swala hili...Na ajabu unapinga hoja hii ukitumia maneno ya Pinda (politics) wakati hakuna mtu kati yetu anajali what he said or should have... kwetu imeshapita tunawaachia wanasiasa kina dr. Slaa.
Sasa kama wewe unayo njia zaidi ya kupambana na watu hawa tupe, lakini sio maswala ya rewards...Unachoogopa wewe matokeo ktk usemi wa Pinda hakuna tofauti na hoja yako..kwa tamaa ya fedha biandamu anaweza fanya mengi kinyume cha sheria hiyo hiyo inayowalinda wengine.
Ebu nambie, una tatizo gani na sisi kuunda jeshi litakalo shughulika na hawa watu!.. Na kama serikali haiwezi, tuunde hata Sungusungu, tuliweza miaka ya 70 na bado sheria imesimama..miji midogo vijijini kuna ullinzi wa kila siku usiku kwa zamu toka kila nyumba kupambana na majambazi na wanafanikiwa hatujasikia mauaji ya kisasi, iweje sisi leo hii ktk swala la Albino tufikirie sheria inayowalinda wauaji wakati ndugu zetu wengine wanakufa!...
 
MMM,
Ndiyo maana nikasema kuwa kama nikitokea na kukuta hali kama hiyo, nitafanya hivyo bila kujiuliza mara mbili. Ndiyo maana kuna POLISI ambao inatakiwa wawe wamepata mafunzo ya kudeal na vitu kama hivi. Akitokea ndugu yake anione na yeye animiminie risasi basi hapo ujuwe kwa nini VITA HUANZA DUNIANI.
Nikijua hawa watu wako wapi basi nitakachofanya ni kwenda POLISI na kuriport hili swala na kama POLISI watasuasua na huyo aliyeuwawa na ndugu yangu basi unajua mie na ndugu zangu tutafanya nini. Na atakuwa na bahati mbaya kwani familia letu lilivyo kubwa kwa kweli cha moto atakiona yeye na ndugu zake.

Nimeangalia na kufikia suluhisho moja nalo ni OMBI KWA WAUWA ALBINO:-

-- Tafadhali nendeni na NYUNDO. Mkifika mpigeni nyundo moja kichwani na apoteze fahamu ili asisikie maumivu hayo makali na kuangalia damu inavyotitirika hadi anakata roho. Hiki ni kifo kibaya sana. Kama akipoteza fahamu basi MBEBE kabisa mwili wote ili mtajirike sana....... Na Mungu atakuwa nanyi milele kwa kuuza mwili wake wote, Amen.
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu hakuna mtu anayesema hapa street justice ndio njia pekee isipokuwa sheria ya jino kwa jino..Israel na nchi zote za kiarabu wanatumia sheria hizo na hatuoni watu wakiuana kama unavyodai.

Mzee hapo umesema "sheria" hizo. Wao hizo sheria za kisasi cha namna hiyo wanazo kwenye vitabu vyao na mimi nasema "more power to them". Ndiyo maana nilitoa pendekezo kama tunaona sheria ya visasi ni bora, tusiiache mikononi mwa watu tutunge sheria kama walivyofanya hizo nchi nyingine, tuhakikishe tunatoa kinga kwa watekelezaji wake, na pia tutambue kuwa kinachofanywa ni halali. Ninaposema tutumie sheria sina maana lazima iwe sheria inayokataza wauaji wasiuawe..

HIvyo tunaweza kuweka sheria kabisa kuwa mwizi akatwe mkono, mbakaji ahasiwe, mgoni apigwe mawe, n.k La maana ni kuwa tukubaliane kuwa hiyo ndiyo sheria yetu. Wenzetu wamekubaliana na inaonekana kama ulivyosema inafanya kazi.

Hizo street justice zipo tanzania hadi kesho wanakufa vizee na vibaka sioni ukizungumzia hilo isipokuwa inapofikia swala hili..

Nimeshalizungumzia mara kadhaa hata kwenye cheche nimeshaandika, nilisimama kupinga mauaji ya wale "majambazi" kule Moshi, na mara zote sina utata katika suala la kuuana nje ya sheria. Kwangu mimi sijali ni nani anayeuawa alimradi kuwa kama tunataka kumuua iwe ni ndani ya sheria. Kuuana nje ya sheria ni no no.
Na ajabu unapinga ukitumia maneno ya Pinda (politics) wakati hakuna mtu kati yetu anajali what he said or should have...

Mimi najali na nimesema alitakiwa aseme nini. Ninajali alichosema kwa sababu matokeo yake negatively ndiyo haya haya. Na kwa kadiri tunafikiria kisasi kitazuia ndivyo vivyo hivyo wauaji nao watakavyothubutu zaidi kwani wameshapiga hesabu ya gharama.

kwetu imeshapita tunawaachia kina dr. Slaa. Sasa kama wewe unayo njia zaidi ya kupambana na watu hawa tupe, lakini sio maswala ya rewards..

Bila rewards, we are doomed to fail, it is as simple as that. Jaribu njia zote lakini at the end kuweza kukomesha and to change the odds that they may favor Albinos you have to offer more than that the criminals are offering. Hakuna cha jino kwa jino au jicho kwa jicho, kwa sababu as somebody has said.. mkianza jino kwa jino mwisho wote mtajikuta hamna macho!


Unachoogopa wewe matokeo ktk usemi wa Pinda hakuna tofauti na hoja yako..


Tofauti yake ni kama nuru na giza.

Ebu nambie, una tatizo gani na sisi kuunda jeshi litakalo shughulika na hawa watu!..

Sina tatizo lolote, tayari kimeshaundwa kikosi cha namna hiyo na tayari tuna jeshi la Polisi, tuna Magereza, tuna Mgambo, na tuna JWTZ! Sasa kama vyombo hivi vyote vimeshindwa unafikiri kuunda jeshi jingine kutasaidia? Labda tuombe majeshi ya Marekani, na donor community waje kutusaidia. Hili siyo tatizo la kijeshi, hili ni tatizo la kisheria.

Na kama serikali haiwezi, tuunde hata Sungusungu, tulioweza miaka ya 70 na bado sheria imesimama..

Kama serikali haiwezi kulinda raia wake, serikali hiyo inakuwa imepoteza haki yake ya kutawala. Hadi hivi sasa siamini kuwa serikali imeshindwa, ninachooamini kuwa serikali haitaki kufanya kile inachojua inapaswa kufanya! Na kwa kadiri ya kwamba inazidi kuchelewa kufanya kitu hicho, ndivyo vivyo watabakia kukemea, kutoa laana na kupigana mikwara.

miji midogo vijijini kuna ullinzi wa kila siku usiku kwa zamu toka kila nyumba kupambana na majambazi na wanafanikiwa hatujasikia mauaji ya kisasi, iweje sisi leo hii ktk swala la Albino tufikirie sheria inayowalinda wauaji wakati ndugu zetu wengine wanakufa!...

sasa hili la ulinzi nakuunga mkono moja kwa moja, ipo haja ya kuanzisha ulinzi maalum, lakini ulinzi huo kwa gharama gani? You still have to bring a lot of money into this, kwa sababu hadi hivi sasa, hawa wauaji hawajali kama unalinda au hulindwi, wameshafanya mambo haya mchana kweupe, wameshafanya haya ndani ya nyumba ya mtu n.k
 
MMM,
Ndiyo maana nikasema kuwa kama nikitokea na kukuta hali kama hiyo, nitafanya hivyo bila kujiuliza mara mbili. Ndiyo maana kuna POLISI ambao inatakiwa wawe wamepata mafunzo ya kudeal na vitu kama hivi. Akitokea ndugu yake anione na yeye animiminie risasi basi hapo ujuwe kwa nini VITA HUANZA DUNIANI.

that is exactly the point unafikiri kwanini wapalestina wakilipuliwa na mabomu na wao wanajivisha mabomu kuwalipua waisraeli? It is called the cycle of violence..

Nikijua hawa watu wako wapi basi nitakachofanya ni kwenda POLISI na kuriport hili swala na kama POLISI watasuasua na huyo aliyeuwawa na ndugu yangu basi unajua mie na ndugu zangu tutafanya nini.

Ndiyo maana pendekezo langu lazima liwajengee Polisi uwezo wa kushughulikia wanaotoa taarifa za mauaji haya. Hivi unafikiri kwanini hadi sasa Waziri wa Mambo ya Ndani anayetoka kanda ya ziwa hajaenda kule na kukesha vijijini na timu ya Polisi kusimamia au hata kuhamasisha operesheni dhidi ya mauji haya na amebakia kuendeleza malumbano Dar!?

Angalua IGP alikuwa kanda ya ziwa majuzi na huko akatoa ahadi ya kuzawaidia milioni 20 lakini bado jeshi halijajipanga sawasawa kupambana na mauaji haya.

Na atakuwa na bahati mbaya kwani familia letu lilivyo kubwa kwa kweli cha moto atakiona yeye na ndugu zake.

true that..
Nimeangalia na kufikia suluhisho moja nalo ni OMBI KWA WAUWA ALBINO:-

hawa siyo watu wa kuwaomba, ni watu wa kuwashughulikia..



[/quote]-- Tafadhali nendeni na NYUNDO. Mkifika mpigeni nyundo moja kichwani na apoteze fahamu ili asisikie maumivu hayo makali na kuangalia damu inavyotitirika hadi anakata roho. Hiki ni kifo kibaya sana. Kama akipoteza fahamu basi MBEBE kabisa mwili wote ili mtajirike sana....... Na Mungu atakuwa nanyi milele kwa kuuza mwili wake wote, Amen.[/QUOTE]

maombi ya namna hii inabidi yaende kwa shetani!
 
Mzee mwanakijiji,
Bado unachanganya... niliposema sheria ya jino kwa jino ni ktk kutenganisha swala la street justice na ombi letu ktk malipo ya wauaji ili kutenganisha utekelezaji wake tu..
Hakuna haja ya kubadilisha sheria zetu ktk swala ambalo ni la mpito na linaweza shughulikiwa kwa kutumia jeshi maalum au nguvu yetu kulitokomeza..Utatengeneza dawa kwa maradhi yaliyopo lakini kama kumetokea outbreak ya gonjwa la nje inabidi utaratibu wa haraka ufanyike kuhusiana na outbreak hiyo kama vile ilipotokea gonjwa wa SAS..tumeweza kulitokomeza watu tunaendelea na maisha zile karantini zote zimekwisha..hatukusubiri sheria zitungwe kwanza wala kufikiria kwanza uvunjaji wa sheria zilizopo.

Kila unapozungumzia swala la Albino inaonekana kama vile unafikiria kuwa hili ni moja ya tamaduni zetu mbovu hivyo ijengewe sheria kwanza isije kuwa kinyume..It's a one time issue ambayo inahitaji suluhisho la haraka!
Sioni umuhimu wa hivyo, ni sawa na vita ya Kagera kuwmondoa nduli Idd Amin au vita ya ukombozi South kwani sheria andamizi tayari imesha vunjwa na mshiriki wa kwanza..huwezi kutumia korti ukisubiri siku Idd Amin atakubali kuwa Kagera sio sehemu ya Uganda au kaburu akubali kuwa south ni nchi ya mweusi..
Hakuna kisasi kinachoweza kutokea ikiwa tutawasaka wauaji wa Albino, kwani hoja yangu haiwataki ndugu za Albino wawasake wauaji isipokkuwa sisi sote wananchi wenye nia njema.. na nimekuuliza mbona hao vibaka wanauawa na hatuoni visasi vinavyoendelea!..
 
Last edited:
Inatisha sasa! Is this hapening in Tz?

Kwa nini Chief of Armed Forces asitumie mamlaka yake?

Awaite Mkuu wa Jeshi, Mkuu wa Police, Jaji Mkuu, PM, Speaker na mawaziri wa fedha, ndani na ulinzi.....atoe mda wa 3 months haya mauaji yaishe!!!!

Laa sivyo hawa wote hanma kazi
 
Last edited:
-- Tafadhali nendeni na NYUNDO. Mkifika mpigeni nyundo moja kichwani na apoteze fahamu ili asisikie maumivu hayo makali na kuangalia damu inavyotitirika hadi anakata roho. Hiki ni kifo kibaya sana. Kama akipoteza fahamu basi MBEBE kabisa mwili wote ili mtajirike sana....... Na Mungu atakuwa nanyi milele kwa kuuza mwili wake wote, Amen.[/QUOTE]

maombi ya namna hii inabidi yaende kwa shetani![/QUOTE]

MMM,
Najua ni OMBI moja baya sana ila kwa mtu niliyepitia JKT/jeshini naona ndiyo njia pekee walau kuwapungunzia hawa jamaa maumivu. Ningelitaka hii kitu isiwepo ila maadamu ipo na Serikali haitaki kushughulikia, nimebaki kuwaombea hao Albino wasife kifo kibaya cha namna hiyo.
Kama yangu mmoja aliyekwenda Msumbiji vitani miaka ya 70, alivyorudi akawa anatuonyesha picha za rafiki yake mpenzi ambaye walikuwa wananunua kila kitu sawa. Huyu jamaa alipigwa risasi tumboni wakiwa msituni na akaanguka. Jamaa kwa kuhofia kuwa atakamatwa na kuteswa, na hawezi kukimbia au kujificha na wenzake lazima wakimbie, basi alimuomba kaka yangu amsaidie kuhama dunia hii. Kaka yangu alikataa na jamaa akamlazimisha kuwa kama kweli yeye ni RAFIKI yake kipenzi, basi lazima afanye hivyo. Mdogo wangu alimuuliza, sasa ulifanyaje?? Jamaa hakujibu.
Sasa kama unasema MAOMBI hayo yaende kwa shetani, you are very right. Kwani Yesu alisema "Ya Kaisari mpeni kaisari na ya Mungu mpeni Mungu". Hivyo hilo ni ombi mahsusi kwa SHETANI, hapo tupo pamoja.
 
Mzee mwanakijiji,
Bado unachanganya... niliposema sheria ya jino kwa jino ni ktk kutenganisha swala la street justice na ombi letu ktk malipo ya wauaji ili kutenganisha utekelezaji wake tu..
Hakuna haja ya kubadilisha sheria zetu ktk swala ambalo ni la mpito na linaweza shughulikiwa kwa kutumia jeshi maalum au nguvu yetu kulitokomeza..Utatengeneza dawa kwa maradhi yaliyopo lakini kama kumetokea outbreak ya gonjwa la nje inabidi utaratibu wa haraka ufanyike kuhusiana na outbreak hiyo kama vile ilipotokea gonjwa wa SAS..tumeweza kulitokomeza watu tunaendelea na maisha zile karantini zote zimekwisha..hatukusubiri sheria zitungwe kwanza wala kufikiria kwanza uvunjaji wa sheria zilizopo.

sasa tulishughulikie kwa sheria au nje ya sheria zilizopo?


Kila unapozungumzia swala la Albino inaonekana kama vile unafikiria kuwa hili ni moja ya tamaduni zetu mbovu hivyo ijengewe sheria kwanza isije kuwa kinyume..It's a one time issue ambayo inahitaji suluhisho la haraka!
Sioni umuhimu wa hivyo, ni sawa na vita ya Kagera kuwmondoa nduli Idd Amin au vita ya ukombozi South kwani sheria andamizo tayari imesha vunjwa na mshiriki wa kwanza..huwezi kutumia korti ukisubiri siku Idd Amin atakubali kuwa Kagera sio sehemu ya Uganda au kaburu akubali kuwa south ni nchi ya mweusi..

Mimi naamini sheria zilizopo na vyombo vilivyopo vinatosha na vinaweza kabisa kushughulikia suala hili.

Hakuna kisasi kinachoweza kutokea ikiwa tutawasaka wauaji wa Albino, kwani hoja yangu haiwataki ndugu za Albino wawasake wauaji isipokkuwa sisi sote wananchi wenye nia njema..

Hawa wauaji utaanzia wapi kuwasaka, utapata vipi taarifa zao, na wewe unaewasaka utakuwa na nguvu gani ya kuwakamata? Na katika kuwasaka nani anagharimia shughuli hiyo yote ya kutaka wananchi "wenye nia njema" kushiriki kwenye kampeni nzito kama hii?

na nimekuuliza mbona hao vibaka wanauawa na hatuoni visasi vinavyoendelea!..

Unasema kana kwamba ni sawa kuwaua vibaka kwa vile visasi havipo. Point yangu ni kuwa kwa kuruhusu kuuawa vibaka tumefikia mahali tunaua tu alimradi mtu kaitwa kibaka! Sasa kwa vile hakuna visasi, basi wananchi waendelee kuwaua wanaowadhania kuwa ni vibaka?
 
Mzee mwankijiji,
sasa tulishughulikie kwa sheria au nje ya sheria zilizopo?
Mkuu sheria gani tena ikiwa muuaji kisha vunja sheria! ni jinsi gani atapatikana ndio pendekezo langu la kupitisha vita dhidi yao.. kama tulivyoweza kuwasaka Majangili na majambazi sijui kwa sheria gani ndivyo tutatumia sheria kuwasaka hao washenzi!..
Mimi naamini sheria zilizopo na vyombo vilivyopo vinatosha na vinaweza kabisa kushughulikia suala hili.
..
Kama vipi?..unazungumza kama hujui hii ni Tanzania, WATU na MAZINGIRA yetu hayawezi kutii sheria iliyopo..
Toka rais alaani vitendo hivyo, Alboni waandamane Pinda aje na yake ni karibu miezi sita watu wanaendelea kufa..sheria gani unayozungumzia mkuu wangu wakati mimi nazungumzia utekelezaji wa sera hii ya kukomesha mauaji haya...Ni sheria gani inayowapa ruksa jeshi letu kutunguana risasi na majangili huko ktk mbuga zetu!..
Hawa wauaji utaanzia wapi kuwasaka, utapata vipi taarifa zao, na wewe unaewasaka utakuwa na nguvu gani ya kuwakamata? Na katika kuwasaka nani anagharimia shughuli hiyo yote ya kutaka wananchi "wenye nia njema" kushiriki kwenye kampeni nzito kama hii?
Thats exaclty inaifanya operesheni hii iwe unique na kutofuata sheria unazotaka kuziweka.. Ndio maana tunahitaji jeshi maalum kama tunavyowasaka majambazi, majangili au kuingia vitani..au hata kupambana na outbreak ya Kipindupindu sehemu fulani huhitaji kutungia sheria mpya.
Hakuna hata siku moja mapambano ambayo yanaweza kujibiwa na maswali yako kwa urahisi hivyo.. Ni ktk kupambana na ndipo unapo gather info kama hizi lakini kinachotangulia kwanza ni kuwa na dhamira ya kupambana, ukaunsda jeshi au kikundi maalum kwa kazi hiyo kisha hao ndio watashughulika na kutafuta info ulizozitaka. Mkuu kama tungekuwa tukifikiria hivyo basi hata hizo sheri na taasisi kama TAKUKURU hazina sababu ya kuwepo kwani kila issue ya Ufisadi unaweza kuuliza mtaanzia wapi na sijui gharama na kadhalika..
Tumeunda TAKUKURU kabla ya kufikiria kina Lowassa na Karamagi, hawa wamepatikana ndani ya vita yetu dhidi ya Ufisadi na wametokea kina Dr. Slaa, Zitto na wengine wote kutoa taarifa bila rewards..dhamira ya kuwanasa hawa watu ilikuwepo toka mwanzo hata kabla sheria haijajengwa vizuri..
 
Last edited:
Kwa kweli inatisha sana sana kuona binadamu anafanywa hivi. Kwa nini Tanzania tu? Kwa nini siku za karibuni?
 
Kaeni chonjo!...

...karibuni wataanza kusakwa wenye vipara, baada ya viungo vya Albino kutokuwa deal tena!
 
Sikonge,
Mkuu unajua hii kitu tunaifanyia mzaha sana kwa sababu wanaokufa wameisha jengewa hukumu subconsciously kuwa cursed ones..Na ndio maana unaona haya maswala ya siasa za sheria itumike..
Nimesema wazi huko ktk mijadala mingine kuwa swala la mauaji ya Albino hayana mjadala wa siasa wala tusiyape nafasi kabisa zaidi ya kuweka sheria kali dhidi ya wauaji..Nchi zote duniani hutangaza vita ktk maswala kama haya na sio kwamba wanavunja sheria kuwinda wauaji.. tumeyafanya kwa Majangili na hata Majambazi...
Ni muhimu ifahamike kwamba tupo vitani hawa jamaa hubeba silaha zao kuwinda ndugu zao Albino...they should be taken as armed and dangerous... hivyo nasi tutaweza tu kupambana na watu kama hawa kwa kubeba silaha vile vile...Iwe liundwe jeshi, taasisi ama kitu chombo chochote kile ambacho kazi yake kubwa itakuwa ku gather info zinazohusiana na hawa washenzi wakubwa..
Sikubaliani tu na swala la kutangaza zawadi au fedha kwani tamaa ya FEDHA ndio chimbuko la mauaji haya..Ukitangaza Utajiri kwa viungo vya albino unatangaza vifo na ukitangaza zawadi kwa wananchi basi hao wauaji wataanza kuua hata ndugu zao kuhakikisha hawaachi shahidi..


Mkandara, nadhani hilo ndio suluhisho sahihi. Toka siku ya kwanza Pinda kutangaza sera ya jino kwa jino binafsi niliiona hiyo ndio muafaka. Of course kama kiongozi na comment za waungwana wakiwemo mwanakijiji, Pinda akamwaga chozi bungeni na kufuta kauli yake. Bahati nzuri pendekezo la Mwanakijiji, (awards) serikari imelitekeleza na ufanisi wake unaonekana ndio hivyo kasi ni kamavile imekuwa catalysed. Kwakuzingatia utawala wa sheria, serikari haina budi kurekebisha sheria hawa watu wauwawe hadharani.
 
It is sad kuona jinsi watu wanavyouwawa simply kwa sababu ni albino. What I can say pamoja na serikali kuwa makini still jamii zetu inabidi kuelimishwa na zaidi kumgeukia MUNGU.
 
Hili kwa kutukana haliwezekani hili Tindi la Bongo kichwa maji matusi ndio chakula yake hili liacheni..Asiyefunzwa na *****...........Think Twice.


SAHIBA.

Kuna aliye na 'matuthi' kumzidi mtume wako Mwamedi a.k.a allah ?
 
Usidandie gari kwa mbele. Kama huna pointi unaweza ukabaki msomaji tu na mambo yakaenda.


Hili lina hasira kweli sina shaka walililawiti kule maombilezoni maana wale wachungaji hatari sana kwa kutangaza neno la bwana kwa vitendo. Think Twice

SAHIBA.
 
....mmmmhhh...........MaxShimba vipi hapo........mafundisho ya wapi haya


The Bible is very clear in re of such things,

The Bible says, Watch out for false prophets. They come to you in sheep's clothing, but inwardly they are ferocious wolves. By their fruit you will recognize them. Do people pick grapes from thorn bushes, or figs from thistles? Likewise every good tree bears good fruit, but a bad tree bears bad fruit. A good tree cannot bear bad fruit, and a bad tree cannot bear good fruit. Every tree that does not bear good fruit is cut down and thrown into the fire. Thus, by their fruit you will recognize them.

Wherefore, if this person was and/or is claimed to be a Pastor, then he is a false and wicked pastor, ad infinitum.

It is shame and sad.

Max Shimba
A Bondservant of Jesus Christ, the Coming King of kings and Lord of lords.
 
Hili lina hasira kweli sina shaka walililawiti kule maombilezoni maana wale wachungaji hatari sana kwa kutangaza neno la bwana kwa vitendo. Think Twice

SAHIBA.


Wacha kutumia lugha chafu. Kama huna hoja, ni bora kukaa kimya.
 
Back
Top Bottom