Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

SERIKALI wilayani Mpanda mkoani Rukwa, imetoa kibali cha kumzika ndani ya nyumba albino John Kapele (42) kutokana na kuhofia kufukuliwa kwa mwili wake na kukatwa viungo. Hatua hiyo imefikiwa kutokana na ombi la familia ya marehemu Kapele aliyefariki dunia kutokana na saratani ya ngozi, kuhofia kuwa iwapo atazikwa kwenye makaburi ya jumuiya, huenda watu wanaotafuta viungo vya albino wakafukua na kukata viungo hivyo.

Akizungumza na gazeti hili, mdogo wa marehemu, Peter Kapele alisema familia iliamua kuiomba Serikali ya Wilaya kutoa kibali cha kufanya maziko ndani ya chumba alimokuwa akilala marehemu, ili kuepuka kufukuliwa na kuibwa maiti huyo.

Peter alisema familia hiyo haitajisikia vizuri iwapo watakuta mwili wa ndugu yao umefukuliwa na kukatwa viungo na kutelekezwa, hivyo katika kukabiliana na suala hilo wameamua maziko yafanyike ndani ya nyumba.

Naye Mkuu wa Wilaya hiyo, Anthony Mzurikwao, alisema wilaya hiyo ilikubali ombi la wanafamilia hao na kutoa kibali na ulinzi ambao ulifanyika kwa kipindi chote cha msiba hadi maziko ili kulinda watu wenye nia mbaya wasijekuvamia msiba huo na kuiba maiti.

Ilielezwa kuwa kutokana na maandalizi ya maziko hayo kuchelewa kuanza, ilipofika saa moja usiku, Mkuu wa Wilaya alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Simon Mayeye, kupeleka jenereta katika nyumba hiyo, ili kupata mwanga kwa kuwa nyumba hiyo haina umeme, ambapo shughuli za kuchimba na kujenga kaburi ndani zilikamilika saa 5.30 usiku.

Baada ya kukamilisha ujenzi wa kaburi hilo, maziko yalifanyika saa 6 usiku na kisha kumimina zege na kukamilisha taratibu zote za maziko saa 7.30 usiku huo na kuendelea na taratibu zingine za msiba.
HabariLeo | Albino afa, azikwa chumbani asiibwe
 
Mchungaji anaswa na viungo vya albino Tuesday, 21 July 2009 16:36 Na Jovin Mihambi, Mwanza

MCHUNGAJI wa Kanisa la Baptist wilayani Magu, Bw. Alfred Komanya (35), anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa na viungo vya albino, aliyeuawa Juni 26 mwaka huu eneo la Ibanda Relini, jijini Mwanza.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Bw. Jamal Rwambow, polisi walifanikiwa kumkamata mchungaji huyo na watu wengine kadhaa wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji albino huyo, Bw. Aron Nongo .

Kamanda Rwambow aliwataja watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa kuwa ni Bw. Chacha Mwita (30) mkazi wa Mahina, Bw. Mathew Mlimi (21), mkazi wa Mahina Nyangulukulu, Bw. Alex Joseph (24) mkulima na mkazi wa Mahina, na Bw. Kishosha Komanya (60), mganga wa jadi mkazi wa Mahina.

Wengine ni Bw. Pascal Mashiku (28) mkazi wa maeneo ya Semba, Buhongwa, Bw. Gervas Komanya (58) ambaye ni mganga wa jadi mkazi wa Nyanguge wilayani Magu na Bw. Paulo Genji (36) mkazi wa Kishiri, Kanindo jijini Mwanza.

Kwa mujibu wa Kamanda Rwambow, baadhi ya watuhumiwa, katika mahojiano yao na Polisi, walikiri kuhusika moja kwa moja na mauaji hayo na kudai kuwa kabla ya kufanya unyama huo, walikwenda kwa waganga wa jadi ili kupewa dawa za kufanya mauaji hayo bila kukamatwa na mkono wa dola.

Kamanda Rwambow, alisema Jeshi la Polisi litatoa zawadi ya sh. milioni moja kwa raia wema waliotoa taarifa na baadaye kufanikisha kukamatwa watuhumiwa.
 
Mbona wachungaji tu ndio wanaohusika na hivyo viungo vya albino?.

Je kuna shehe yoyote aliyewahi kukutwa na viungo vya albino huko Tanzania?

Kulikoni WAKRISTU na nini tamko la kanisa hapo
 
Mbona wachungaji tu ndio wanaohusika na hivyo viungo vya albino?.

Je kuna shehe yoyote aliyewahi kukutwa na viungo vya albino huko Tanzania?

Kulikoni WAKRISTU na nini tamko la kanisa hapo

wote hao ni binadamu kila mtu eti sababu mchungaji ndo hana makosa?may be anajifichia humo, mashehe wanajua kucheza karata vyema, wapo advanced sana kwa mambo haya,hawa wachungaji sasa ndo wanajifunza
 
__________________

Nafikiri ingekuwa hehe kabambwa na Viungo vya albino Basi Mada hii ingekuwa patashika. lakin naona akristo imewashika pabaya.

Katika kumbu kumbu zangu huyo ni mchungaji wa pili kukutwa na Nyara hizo hadimu za n viungo vya Albino.

Sasa nini tamko la kanisa kwa mathila haya yanayolitia aibu kama yale ya ushoga?
 
Mbona una jishuku? Kama una fikiri basi ina maana huna uhakika bali una kisia tu. Anyway tunabidi tukemee kwa nguvu zote maovu haya.
 
Nafikiri ingekuwa hehe kabambwa na Viungo vya albino Basi Mada hii ingekuwa patashika. lakin naona akristo imewashika pabaya.

Katika kumbu kumbu zangu huyo ni mchungaji wa pili kukutwa na Nyara hizo hadimu za n viungo vya Albino.

Sasa nini tamko la kanisa kwa mathila haya yanayolitia aibu kama yale ya ushoga?
Now, what is your point?
 
wachungaji hao walio wengi wanakuwa wamefeki tu. ni watu wa kawaida sasa wanaingia kwenye uchungaji ili kuficha maovu. inawezekana wengine ni waislam lakini wanafek tu. hapa haimaanishi kuwa wakristo ndo sana wanaua. kwasababu kwa asili dini ya kikristo si ya uchawi kama kii......, sisi hatufugi majini kama wao, sisi hatutundiki watoto mabegi ya hirizi kama wao, sisi hatuna maroho machafu kutoka kuzimu kama wao. hivyo,naomba hapa msifikiri kuwa waislam ni watakatifu kuliko wakristo. kama umeleta mada hapa kwaajili hiyo, umepotea na utaaibika wewe.
 
alikuwa anaenda kuviuza kwa mwislam. mbona nasikia kuna mnunuaji wa viungu mwarabu huko mwanza wanamgwaya? waislam ndo wanunuaji.
 
Yameripotiwa mauaji ya alibino, kijana wa miaka minne akiwa na bibi yake usiku, kifo kibaya cha kukatwa mikono yote kuanzia mabegani na bibi yake kukatwa panga la kichwa wakati akimpigania mjukuu waku.

Source: BBC swahili news saa kumi na mbili na nusu jioni 23/07/2009

Habari hii imenishtua sana, Je kura za maoni hazikusaidia chochote? Polisi wako wapi Jamaniiiiiiii? Si tunakatwa kodi kubwa sana kwenye mishahara yetu ili walipwe mishahara ya kutulinda sisi na mali zetu? iweje raia wenzetu wanauwawa bila hata tone la huzuni kwa hawa waajiriwa wetu? jamani! Jamani! Jamani! lazima uwajibikaji utokee nchi hii.
 
Last edited by a moderator:

mimi nafikiri iwe illegal kwa shughuli za kiganga za jadi.
 
Thank Allah this doesnt happen in Znz or done by Muslims. It's very shame to a country like TZ a well respected and well known country and by this time (21st century) that things like this is happening. A huge number of Police and Army plus what you call "Usalama wa Taifa" is sent to Pemba where there is no killing going on while this shameful thing is going on for years and Nothing has been done. Obviously high ranking people are involve in this practice. If this is the way to become rich then I rather die poor.
 
... Polisi wako wapi Jamaniiiiiiii? Si tunakatwa kodi kubwa sana kwenye mishahara yetu ili walipwe mishahara ya kutulinda sisi na mali zetu? iweje raia wenzetu wanauwawa bila hata tone la huzuni kwa hawa waajiriwa wetu? jamani! Jamani! Jamani! lazima uwajibikaji utokee nchi hii.

Kwani hujui kuwa polisi wetu wapo kwa ajili ya uchaguzi tu? Tangu lini polisi wakajihusisha na wanyonge wa nji hii. Ndio maana umesikia bungeni kuwa wataajiri polisi zaidi kwa ajili ya uchaguzi wa 2010.

mimi nafikiri iwe illegal kwa shughuli za kiganga za jadi.
Haiwezi kusaidia kwani mafisadi na wapambe wao wanawategemea haohao waganga. Isitoshe wateja wa viungo vya Albino ndio hao wenye fedha chafu na watawala. Sasa watawezaje kukata mkono unao walisha?
 
Kwani hujui kuwa polisi wetu wapo kwa ajili ya uchaguzi tu? Tangu lini polisi wakajihusisha na wanyonge wa nji hii. Ndio maana umesikia bungeni kuwa wataajiri polisi zaidi kwa ajili ya uchaguzi wa 2010.

Haiwezi kusaidia kwani mafisadi na wapambe wao wanawategemea haohao waganga. Isitoshe wateja wa viungo vya Albino ndio hao wenye fedha chafu na watawala. Sasa watawezaje kukata mkono unao walisha?

Kama ni kweli
waganga ndio wanawalisha hao viongozi ni upumbafu tu,sitaki kuamini kama ni hivyo.

Hii miganga ya jadi lazima ipigwe marufuku
 
Kulitokana na vyombo vya habari zaidi ya watu (wauaji) 200 wamekatwa lakini mpaka leo hakuna hata mmoja aliye hukumiwa

Je serikali (mahaka and police) wanafanya nini?

Wenzetu burundi angalau Burundi kidogo wamenza kuwaonyesha rangi wauaji wa nduguzetu albino JE SISI....
 
Kulitokana na vyombo vya habari zaidi ya watu (wauaji) 200 wamekatwa lakini mpaka leo hakuna hata mmoja aliye hukumiwa

Je serikali (mahaka and police) wanafanya nini?

Wenzetu burundi angalau Burundi kidogo wamenza kuwaonyesha rangi wauaji wa nduguzetu albino JE SISI....KUNA SIRIGANI KATIKA SWALA HILI...
 
Mauwaji mengine ya kinyama yanaendelea nchini mwetu na la kutisha zaidi sasa ni watoto wadogo wa ki albino! Kwa mujibu wa bbc 23.7.2009 mtoto wa miaka 4 huko bariadi amekatwa mikono na kufa papo hapo na wauwaji kuondoka na mikono ya mtoto huyo!
Huu ni unyama wa kiwango cha hali ya juu! Jamani serikali yetu iko wapi? Na hii ndio amani tuliyonayo tz? Hawa watu hawana dini? Hawamjui mungu?

Wito wangu kwa serikali yetu:

Albino wote wapewe ulinzi wa polisi mara moja! Kama albino wataendelea kuuliwa basi wote wataisha na walengwa watakaofuatia kuuliwa huenda wakawa watu wenye vipara, vitambi, wafupi, au warefu nk!
 
Back
Top Bottom