Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Kwa kuwa kuna dalili za wazi kuwa kura za maoni zilizotumia pesa nyingi sana kwa ajili ya zoezi hili hazikuzaa matunda na hakuna yeyote aliyewajibika mpaka sasa, pamoja na makelele mengi kutoka kwa jamii yetu na ya kimataifa kuhusiana na mauaji haya, na kwa kuwa kuna dalili za wazi kuwa wakubwa wanaridhika na yanayoendelea, na kwa kuwa hatuwezi kuendelea kuivumilia aibu ya namna hii kwa taifa basi nashauri moja kati ya hili litumike kumaliza adha hii,

1. Masha aondolewe wizara ya mambo ya ndani na wizara hii apewe Mh John Pombe Magufuli. nina imani hii adha itamalizika mara moja tu hata kama kuna wakubwa wanahusika watashika adabu. Kama hili haliwezekani basi lifanyike hili la pili ambalo ni

2. Kiundwe chombo huru chenye nuvu kutoka kwa Raisi na namwomba Mh Raisi amteue Agustine Lyatonga Mrema Akiongoze chombo hicho. Kuna faida mbili kuu kama atafanya hili. Moja mrema atafanya kazi kama polisi mzoefu na anayependa sifa hivyo atakamilisha kazi yake vizuri kwa taifa na hata kama wahusika ni wanasiasa au wakubwa serikalini, mbele ya Mrema hawatapumua. Mbili kwa kuwa yeye ndiye aliyewahi kutumia mfumo wa kura za maoni na ukafanikiwa basi itakuwa ni kazi ambayo anauzoefu nayo na ataendeleza pale walipoishia wala hakutakuwa tena na gharama nyingine ya kura za maoni. (na pia atapata angalaou kaallowance kakumsaidia kununu dawa jamani! (Joke)

Kama rais angekuwa seriuos ushauri huu ni mzuri sana lakini sijui kama yeye mwenyewe hanufaiki na haya mauaji kwa sababu navyo amini mimi serikali haiwezi kushindwa tatizo kama hili.

Waziri masha nadhani sasa anatuaibisha kwa kushindwa kazi.
 
Inawezekana amemchukua amlee au kwa nia njema kama vile mtu ukiamua kulea mtoto yatima kwa ridhaa yako mwenyewe. Kama ni tofauti na hivi basi ni HATARI sana!..

Oooh yeah! Pinda ana nia njema ya kumlea yule Albino, ila sasa imepokelewa na hisia tofauti na wananchi wa kawaida, sidhani kama kuna ukweli..lakini kila kitu Tanzania kinawezekana!
 
Hivi masha tangu awe waziri wa mambo ya ndani amefanya nini kwa taifa? Mauaji ya albino yamemshinda, ujambazi umemshinda, n.k.
 
Thank Allah this doesnt happen in Znz or done by Muslims. It's very shame to a country like TZ a well respected and well known country and by this time (21st century) that things like this is happening. A huge number of Police and Army plus what you call "Usalama wa Taifa" is sent to Pemba where there is no killing going on while this shameful thing is going on for years and Nothing has been done. Obviously high ranking people are involve in this practice. If this is the way to become rich then I rather die poor.

Chakarota ......... temea mate chini ndugu yangu mwenzio akinyolewa wewe tia maji kichwa chako.

In green color...... I hope you are not serious! For sure you dont know wahusika eh?
 
Ndio maana nikaseme thank ALLAH Kwani ni yeye tu anapaswa kushukuriwa. and please read my next post after the one you've reffered you will see that I've not accused anybody. Na kwa mpaka hivi sasa tunawajua wengi waliokamatwa na suspects ni kina nani. I hope Govt. one day will be serious in this situation.
 
Sasa jamaa na ndugu zetu hawa wenye matatizo ya ngozi (Albino), ndio hawawezi tena kwenda kuabudu uko kwenye hayo makanisa... Ndio washawakosa...!
 
Afungwa Maisha Kwa Kuua na Kuuza Viungo vya Albino Burundi
2601838.jpg

Peter Ash, raia wa Kanada mwenye ulemavu wa ngozi- Albino ambaye anaongoza mapambano dhidi ya mauaji ya albino katika nchi za Afrika Mashariki. Thursday, July 23, 2009 6:53 PM
Mahakama nchini Burundi imemhukumu kifungo cha maisha mwanaume mmoja na wengine wanne kwenda jela miaka 15 baada ya kupatikana na hatia ya kuwaua albino na kuuza vipande vya miili yao kwaajili ya mambo ya kishirikina. Katika kutokomeza mauaji ya albino, mahakama moja nchini Burundi imemhukumu mwanaume mmoja kifungo cha maisha jela na wanaume wengine wanne wamehukumiwa kwenda jela miaka 15 kila mmoja.

Waganga wa kienyeji wanaojishughulisha na biashara ya viungo vya albino nchini humo hudai kuwa viungo vya albino vinaleta bahati nzuri katika maisha, vinasaidia katika mambo ya mambo ya mapenzi na vinaleta utajiri.

Mwanaume mmoja alihukumiwa kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya kupanga na kufanya mauaji ya albino mmoja.

Wanaume wengine watatu walihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela baada ya kupatikana na hatia ya kuandaa mpango wa kuwateka na kuwaua albino wawili.

Kwa kawaida jamii nyingi nchini humo zimekuwa zikiwatenga albino na kuwaona kuwa wanaleta mikosi huku wengine wakiwatuhumu albino kujihusisha na ushirikina.

Nchi ya Burundi ina jumla ya watu milioni nane na ina takribani albino 200 na kati ya hao 11 waliuliwa mwaka jana na viungo vyao kukatwa katwa na kutumika kwenye mambo ya kishirikina. http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2601838&&Cat=2
 
Kwa muda mrefu katika maisha yangu kumekuwa na uvumi kuwa Albino hawafi na hawa zikwi, hapa Tabora leo saa kumi kutakuwa na mazishi ya Albino ambapo mkuu wa mkoa wa Tabora Mh Mwinyimusa atahudhuria, kifo cha albino kimesababishwa na albino huyo kuugua kwa muda mrefu na kifo cha kawaida labda cha ziada ni kuwa mazishi yatafanyika pembeni ya kambi ya jeshi uelekeo wa Airport Tabora!
 
Last edited:
Kwa muda mrefu katika maisha yangu kumekuwa na uvumi kuwa Albino hawafi na hawa zikwi, hapa Tabora leo saa kumi kutakuwa na mazishi ya Albino ambapo mkuu wa mkoa wa Tabora Mh Mwinyimusa atahudhuria, kifo cha albino kimesababishwa na albino huyo kuugua kwa muda mrefu na kifo cha kawaida labda cha ziada ni kuwa mazishi yatafanyika pembeni ya kambi ya jeshi uelekeo wa Airport Tabora!
Kaka sijui dada sasa hii ndio nini?
 
Duu, umeshawapa dili waganga wa kienyeji, watampigia rada huyo....utasikia kaburi la Albino lafukuliwa.....ulinzi utakuwepo?
 
Poleni sana na Mungu amlaze panapostahiki.

Mie sijawahi hata siku moja kusikia na hata kuhudhuria maziko ya mtu mwenye ulemavu wa ngozi Albino.

maziko mema
 
Mazishi yalifanyika chini ya ulinzi mkali, vyombo vya dola vikiwepo, infact urefu wza kaburi na umadhubuti wake ili mtu afikirie kulichimba itamhitaji mchimbajiawe na vyombo maalumu kama vile greda nk na itamchukua mchimbaji si chini ya siku saba pamoja na vifaa hivyo vizito
 
I feel sorry for that..
Sidhani kama hao waganga wanahitaji albino aliye mfu,itakuwa wanavihitaji viungo vya mtu aliye hai,so sidhani kama kuna uwezekano wa kaburi lake kufukuliwa..
 
JESHI la Polisi Visiwani Zanzibar limeokota mkono wa mtu mwenye ulemavu wa ngozi (albino) ufukweni mwa bahari ya Hindi katika eneo la Kizingo, mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Bakari Khatib Shaaban amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema jeshi lake limeokota mkono huo mmoja wa albimo majira saa 11.00 juzi jioni.
Amesema jeshi la polisi lilikuwa katika kazi za kawaida walipata taarifa kutoka kwa raia wema ambapo ni wavuvi wa eneo hilo la Kizingi waliokuwa katika shughuli zao za kazi waliona kitu kisicho cha kawaida ndipo walipoiarifu polisi.
Alisema Polisi wamelazimika kuupeleka mkono huo katika hospitali Kuu ya Mnazimmoja, ambako madaktari wanaufanyia uchunguzi zaidi kabla ya kutoa taarifa kamili.
Kamanda Bakari alisema kwamba hadi sasa haijafahamika kama kuna mtu amefanyiwa hujuma Zanzibar au mkono huo umetolewa nje ya Zanzibar kwa kuvutwa na maji kwa kuwa umeonekana katika ufukwe wa bahari.
Kamanda huyo alisema hadi jana hakukuwa na taarifa yoyote ya kutoweka mtu mwenye ulemavu wa ngozi, baada ya Poilisi kufanya uchunguzi katika vituo mbali mbali.
Hata hivyo, alisema kuna uwezekano mkono huo ulifika katika eneo hilo kwa shughuli za uganga kutokana na mazingira uliyokutwa, ambapo ulikuwa umezunguushwa kitambaa cheusi.
“Inawezekana mkono huo umeletwa Zanzibar kwa mambo ya kishirikiana na baadaye wahusika kuutelekeza katika eneo hili”, alisema Kamanda huyo Polisi.
Aliwataka wananchi watoe taarifa Polisi iwapo kutakuwa na watu waliopotea au wenye taarifa kuhusiana na watu wanaohusika na hujuma dhidi ya watu wenye ulemavu wa wa ngozi.
Tukio hilo limelaaniwa na wanachama wa Jumuiya ya Maalbino Zanzibar, ambapo, Mshika Fedha wa Jumuiya hiyo Halima Hassan Seif alisema Polisi lazima ifanye uchungizi mkali, juu ya tukio hilo kwani huenda kukaa na vitendo vya aina hivyo vinaanza kujitokeza visiwani hapa.
“Ni vyema Polisi wafanye uchunguzi wa kina ili jamii ijue iwapo mkono huo uletwa Zanzibar au kuna mtu kahujumiwa hapa hapa Zanzibar”, alisema Halima.
Alisema ili kukabilina na vitendo vya hujuma dhidi ya watu wenye uleamavu wa ngozi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ifanye sensa ili itambue idadi ya maalbino na kuweza kuchukua mikakati ya kuwalinda kwani khofu miongoni mwa albino itaanza mara moja baada ya tukio hilo.
Matukio ya kukatwa viungo watu wenye ulamavu wa ngozi vmeshamiri upande wa Tanzania bara ambapo baadhi ya watuhumiwa wamehukumiwa kifo katika mahakama baada ya kupatika na hatia ya kuwauwa walemavu hao.
SOURCE: ZANZIBAR YETU WEB BLOG.
 
Hv hawa wa bishara hii hawajasikia hukumu ya wenzao ya juzi kunyongwa?
Zao siku zinahesabika, hawawezi kushinda wao kila siku, kuna siku watateleza!
 
Mtoto mdogo Albino amevamiwa akiwa na familia yake na kuuawa kwa kukatwa shingo kisha kukata mguu wake wa kulia na kutoweka nao huko Geita mkoani Mwanza!
Inasikitisha sana!!🙁
 
Back
Top Bottom