Kwa kuwa kuna dalili za wazi kuwa kura za maoni zilizotumia pesa nyingi sana kwa ajili ya zoezi hili hazikuzaa matunda na hakuna yeyote aliyewajibika mpaka sasa, pamoja na makelele mengi kutoka kwa jamii yetu na ya kimataifa kuhusiana na mauaji haya, na kwa kuwa kuna dalili za wazi kuwa wakubwa wanaridhika na yanayoendelea, na kwa kuwa hatuwezi kuendelea kuivumilia aibu ya namna hii kwa taifa basi nashauri moja kati ya hili litumike kumaliza adha hii,
1. Masha aondolewe wizara ya mambo ya ndani na wizara hii apewe Mh John Pombe Magufuli. nina imani hii adha itamalizika mara moja tu hata kama kuna wakubwa wanahusika watashika adabu. Kama hili haliwezekani basi lifanyike hili la pili ambalo ni
2. Kiundwe chombo huru chenye nuvu kutoka kwa Raisi na namwomba Mh Raisi amteue Agustine Lyatonga Mrema Akiongoze chombo hicho. Kuna faida mbili kuu kama atafanya hili. Moja mrema atafanya kazi kama polisi mzoefu na anayependa sifa hivyo atakamilisha kazi yake vizuri kwa taifa na hata kama wahusika ni wanasiasa au wakubwa serikalini, mbele ya Mrema hawatapumua. Mbili kwa kuwa yeye ndiye aliyewahi kutumia mfumo wa kura za maoni na ukafanikiwa basi itakuwa ni kazi ambayo anauzoefu nayo na ataendeleza pale walipoishia wala hakutakuwa tena na gharama nyingine ya kura za maoni. (na pia atapata angalaou kaallowance kakumsaidia kununu dawa jamani! (Joke)
Kama rais angekuwa seriuos ushauri huu ni mzuri sana lakini sijui kama yeye mwenyewe hanufaiki na haya mauaji kwa sababu navyo amini mimi serikali haiwezi kushindwa tatizo kama hili.
Waziri masha nadhani sasa anatuaibisha kwa kushindwa kazi.