Mauaji ya bodaboda Mtwara, Polisi mmeshindwa kazi?

Mauaji ya bodaboda Mtwara, Polisi mmeshindwa kazi?

Joined
Jul 3, 2020
Posts
29
Reaction score
63
Kumekuwepo taarifa ya matukio ya mauaji ya bodaboda mkoa wa Mtwara zaidi ya watano mwaka huu.

Bodaboda hao wanauawa kisha wanaporwa pikipiki zao.

Maiti za bodaboda hizi zimekuwa zikiokotwa maeneo tofauti baada ya kuporwa pikipiki.

Matukio ya mauaji ya bodaboda yamekuwa ya kawaida huku Polisi wakizembea kuyadhibiti. Hali hii inaonesha kwamba polisi kazi imewashinda, hivyo wajitathimini.
 
Ndio hawa hawa ambao imeundwa tume kwaajili ya kuwachunguza kwa kumuaa yule dogo wakagawana dola zake, bado wanaendelea kuua na lile zee Zirro bado linashupaza kichwa tu kuachia ngazi halitaki. Kuna shida nyingi sana kwenye hii nchi believe me.
 
Nalaani sana vitendo vya mauaji na wezi wakikamatwa hamna namba wauawe tu.

Cha kusikitisha pia bodaboda nao wamekuwa wezi sana siku hizi, yaani ukipanda bodaboda ambae hakufahamu na iwe usiku asilimia za kuporwa ni kukudhuru ni kubwa.

Wamegeuka kuwa vibaka, hawa nao wakikamatwa wauawe tu
 
Mimi nawasema vibaya Polisi wanapokosea lakini kwa hili bodaboda wenyewe wanachangia vifo vyao kwa asilimia 75% na kuendelea. Wewe unakodiwa na mtu usiku humjui tena wako wawili uwapeleke kijiji cha mbali, hao Polisi unawajulisha kwamba jamani Mimi nimekodiwa na hawa jamaa mnilinde? Tamaa ya nauli kubwa wanayoahidiwa inawaponza.
 
Polisi kwenye utekaji wa madereva bodaboda hawahusiki kwa 100%. Kutekwa na kuuwawa ni uzembe wao wenyewe. Polisi hapa unawabebesha zifo sio lao.

Ukiwa ni dereva bodaboda na una pikipki mpya jua kabisa inawindwa iibiwe. Ongeza umakini kwa kubeba watu ambao huna mashaka nao.

Usikubali kwenda umbali mrefu nje ya mji.

Kifupi kuwa na tahadhari.
 
Magaidi wanapoua polisi mnakata viuno kwa shangwe,hamuoni hatari iliyoko mbele yenu.

Ugaidi ni vita hatari haitaki unafiki.
 
Hapa Dumila mauaji haya yamekuwa kwa kipindi kirefu saana ila wiki iliyopita yalikuwa yanatokea tena sema Bodaboda kwenye purukushani akafanikiwa kupiga kelele na bahat kulikuwa na watu wanapita hivyo walipokia kelele za msaada wakabidi wawahi.
Kilichofuatia wale wezi wauaji kila mtu akashika njia yake wakimbie mmojawapo kwenda mbele akakutana na mlinzi anayelinda lindo lake naye alisikia kelele za wezi ikabidi amuweke kati na watu kufika pale jamaa ikabd afanywe chakula na wananchi hadi kumuua hapohapo
Ila alikuja kutambulisha ni mwizi anayetokea Morogoro mjini ila naamini wamepata taarifa kuwa waibe ila wakikamatwa ni kifo kama wao wanavyowaua Bodaboda
Mwisho mauaji haya yamekuwa yakitokea sana haswa umeme unapokuwa haupo mida ya usiku kwani umeme Dumila unasumbua saana haswa kipindi hiki hvyo kupelekea uwizi kufanyika saana

TANESCO Rudisheni umeme Dumila hata sasa mmekata

Bodaboda wa Dumila wazidishe umakini watakwisha.Vilevile nashauri wamiliki wa bodaboda wafunge GPS au tracking system kufuatilia pikipiki zao pale zinapoibiwa, waache ushamba.

Dar es Salaam pikipiki nyingi zina vifaa hivi hivyo wizi wa pikipiki umepungua.
 
Back
Top Bottom