Mauaji ya Kisiasa (Political assassinations) siyo sera bora ya kiutawala

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
21,775
Reaction score
71,893
MAUAJI YA KISIASA (Political Assassinations) ni moja kati ya sera za kiutawala ambazo zimekuwa zikitumika tokea ustaarabu ulivyoanza kutokea duniani. Huwa inatumika kuwazima mara moja maadui wa kisiasa, maadui wa taifa au maadui wa kimaslahi.

Tatizo ni kwamba, tofauti na siku za kale ambapo jamii ziliongozwa kama piramidi, ambapo watu walioshiriki kwenye siasa walikuwa ni wale walioelimika (Educated Elites) na waliotokea familia za kitawala (Aristocrats) tu. Tofauti kabisa ni kipindi hiki, ambapo siasa za nchi zimehalalishwa na kufanywa katika ngazi za kitaasisi (Institutional Levels), ambapo siasa haifanywi na wasomi pekee (Educated Elites) na familia za kitawala (Aristocrats), bali hufanywa katika nyanja zote zinazogusa jamii.

SIASA inafundishwa shuleni na vyuoni, hivyo uhusikwa wa raia unakuwa mkubwa kiwango cha kufanya siasa iaathiri UCHUMI, DINI na UTAMADUNI. Hivyo huwezi kufanya MAUAJI YA KISIASA (Political Assassinations) bila kugusa taasisi nyingi za siasa zinazofanya kazi ndani ya nchi. Katika kufahamu hili, mataifa mengi yaliyoendelea yamefikia kwenye ukweli mchungu kwamba: KAMA SIASA ZINAFANYIKA KWENYE NGAZI ZA KITAASISI, kuua mtu mmoja hakuwezi kubadilisha chochote katika muda mrefu.

Prof Noam Chomsky, kwenye moja ya kazi zake muhimu iitwayo "The Manufactured Consent" anaelezea kwamba katika jamii za ulimwengu wa utandawazi, watu wengi huwa na mawazo sawa kwasababu ya propaganda za kisiasa. Hivyo hata vyama vya siasa wanakuwa na sauti ndani ya jamii kwasababu wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kueneza propaganda za kisiasa ambazo zimefanikiwa kuwaaminisha watu kuhusu matatizo yanayowazunguka.

==============================================================
Mataifa kama UCHINA, mbali na ukatili wao mwingine, huwafanyi MUAJI YA KISIASA (Political Assassinations) kama zamani. Wamefahamu kwamba MAUAJI YA KISIASA ya madhara makubwa sana: Huwafanya watawala wa nchi kushindwa kuyakabila matatizo makubwa ya nchi ya muda mrefu kwa uwazi, ufasaha, weledi na ubunifu.

Matatizo yote ya kisiasa ndani ya nchi hutokana na mawazo (Ideas/Political Thought). Mawazo (Ideas/Political Thought) haya watu hujengewa baada ya kupitia kwenye taasisi fulani, kama Shule, Chuo, Chama Cha Siasa, Umoja wa Wafanyakazi, Vyombo vya Habari, au Taasisi za Kidini. Hivyo unapomuua (Assassinate) mtu kwasababu ya mawazo ya kisiasa, fahamu kwamba huwezi kubadilisha chochote endapo taasisi kama Shule, Chuo, Chama Cha Siasa, Umoja wa Wafanyakazi, Vyombo vya Habari au Taasisi za Kidini hujazifutilia mbali kabisa.

NDIYO MAANA, madikteta wakubwa wote duniani kama Hitler, Mussolini, Mao Zedong, Joseph Stalin na Lenin, walipochukua nchi, hawakufanya MUAJI YA KISIASA (Political Assassinations) peke yake, bali walifanya MAUAJI YA HALAIKI (Mass Murder/Massacre/Genocide), wakishambulia taasisi za muhimu za kisiasa na watu wake waliopata mawazo kutoka kwenye hizo taasisi. Mfano, Lenin aliua mamilioni ya Wakristo na kubomoa maelfu ya makanisa.

ILI NCHI IENDELEE KWENYE KARNE HII, ni lazima watawala wa kitanzania wafahamu kwamba changamoto za kisiasa zinapokuja ni lazima kuzikabili bila kutafuta njia mbadala. Wakifanya hivyo watajipa nafasi ya wao wenyewe kukua, kukomaa na kuweza kujenga uwezo mkubwa kiutawala kutatua changamoto za kitaifa katika ngazi ya kitaasisi.

Mimi ni moja kati ya watu humu ndani ambao nitaendelea kupinga sera za Mzee Nyerere ambaye ndiye muasisi mkuu wa kutumia SERA YA MAUAJI YA KISIASA (Political Assassinations) katika kutawala nchi. Hakuweza kulijengea taifa la Tanganyika uwezo wa kiutaalamu wa kukaa mezani, kufanya tafiti, kufanya mijadala ya kitaalamu, kukubaliana na mawazo kinzani, na kisha kutafuta suluhu za kisayansi. Huu ndiyo UTAMADUNI aliowajengea CCM + TISS.

Wale wote waliopingana na Mzee Nyerere katika ngazi za kisiasa, aidha walifungwa, walifukuzwa nchi au kuuwawa kinyama. Hakuwa na ujasiri wa kuweza kukaa kwenye meza moja na kuangalia zimwi la mawazo kinzani yaliyomfanya aonekana hana akili au siyo msomi. Hivyo akajificha kwenye kichaka cha kutumia propaganda za mabeberu kuwapa jina maadui zake kisha kuwashughulikia.

LEO HII, ninapoona vijana wa CCM + TISS hawana uwezo wowote ule wa kufanya mijadala ya kisiasa kwa utaalamu, kufanya tafiti za kisomi na kubuni suluhisho, huwa siwashangai hata kidogo. Huo UTAMADUNI watanganyika hatukujengewa tangu nchi ipate uhuru. Hivyo wanapokutana na mawazo makubwa ambayo yamewazidi uwezo, tafasiri yao ni kwamba, hili ni wazo la kibeberu, kihujuma, linalolenga kuvunja amani ya nchi. SULUHISHO NI KUUA TU.

==========================================================
WACHINA
walipolifahamu hili, walitenganisha baina ya changamoto za kisiasa na zile za kiusalama (Pure Security Matters). Ambapo linapokuja suala la kisiasa Chama Cha Kikomunisti Cha Uchina (CCP), kinaamua kutumia akili kutatua tatizo. Hili linawapa watawala uelewa mpana kuhusu tatizo, ujasiri mkubwa wa kukabili matatizo, lakini nchi nzima na taasisi za kisiasa zinajengewa UTAMADUNI wa kuamini kwamba kila kitu kinaweza kutatuliwa kwa mazungumzo na siyo vitisho au kuuana.

================================================================
UKIANZA KUWAFIKIRIA: Abeid Karume, Kassim Hanga, Edward Sokoine, Imran Kombe, Gilman Rutihinda, Stephen Kibona, Horace Kolimba, Daudi Balali, William Mgimwa, Benard Membe, na wengine wengi (Wazuri kwa Wabaya), utafahamu kwamba MAUAJI YA KISIASA (Political Assassinations) hazikubadilisha chochote kile na matatizo yamerudi kwa nguvu zaidi.

Lakini, watawala wangekuwa na hekima, nadhani kuna matatizo mengi tu hapa nchini siyo matatizo kama ambavyo wanasiasa huwa wanayakuza. Mengine yangemalizika kwenye mijadala ya kisiasa ya wazi tu. Hapa ndipo MZUNGU anapomuacha MWAFRIKA. Wamejengwa UTAMADUNI wa kuweza kuhimili tofauti, na kufundishwa kutafuta COMMON GROUND, kupitia tafiti za kisayansi (SCIENTIFIC RESEARCH) na UBUNIFU (INNOVATION).

=================================================================
TATIZO LA TANZANIA KWASASA: Ile MIZEE YA COLD-WAR kama Butiku, Warioba, Wassira, Mkuchika, Kikwete, Karume, Lhwavi, Bulembo, Chenge,Lukuvi, Kabudi, Zungu na wengine, pamoja na watoto wao waliopo ndani ya mfumo, hawawezi kutusaidia kwasababu akili zao zimechekaa. Wao wanaitazama dunia katika sura mbili tu. UBEBERU v UJAMAA, kwamba FEDHA NI HARAMU na UMASIKINI NI FAHARI.

FEDHA NI HARAMU kwa Mtanzania wa kawaida, siyo KADA WA CCM na familia yake.
UMASIKINI NI HARAMU kwa KADA WA CCM na familia yake ila kwa mtanzania wa kawaida ni sawa.

===========================================================
NDIYO MAANA, KADA WA CCM akiiba, akipora, akidhulumu au hata akiua taasisi za kiusalama haziwezi kumfanya lolote kwasababu ni mwenzao. MTANZANIA WA KAWAIDA akiwa TAJIRI, ni lazima ameiba au anatumiwa na mabeberu. Kuna imani ndani ya mioyo ya watawala wa Tanzania kwamba, huwezi kuwa tajiri bila kuwa serikalini.

SIJUI KAMA MTANIELEWA, AU NIMEWACHANGANYA.
​
 
Mkuu with all respect hizi hoja ni nzuri, ila ungekuja na namna ya kuzuia au kupambana na utawala dhalimu ingekuwa bora zaidi.

Wakati sisi tuna hubiri kuwa mauaji ni mabaya, wao ndio kwanza wana kwapua mabilioni na kuzidi kushindilia ndugu zetu kwenye makaburi yasiyo julikana.

Na sisi tuna ishia kufanya nini?, kuandika na kuja na misimamo ya Kalamu na keyboard visivyo na tija kwa Sasa.
 
Hii ni hatari sana sana
 
Kusema kwamba Serikali ya Tanzania iache kutegemea kuua wanasiasa ni kuandika makala isiyo na tija ???​
 
Kusema kwamba Serikali ya Tanzania iache kutegemea kuua wanasiasa ni kuandika makala isiyo tija ?​
Kuna maandiko chungu mzima humu yaki Kemea mauaji kila siku, sasa kurudi kwenye mzunguko ule ule si suluhisho.

jamii forum's ime fungiwa, mwenye nayo katishwa, wana harakati wana uliwa halafu sisi tuna endelea kuimba wimbo wa si sawa jamani.

Hapa tuna paswa kupunguza maneno yenye upole kila siku, wana jua kelele zetu hazina impact.
Basi tusi kosee Tena.
 
Kwa hivyo wakimuua yule jamaa haitasaidia?
Sijui kama wamekuelewa.
Jamaa amepata wafuasi au waumini wengi sana.
SUMU ya koboko ikishaingia mwilini na ukachelewa kuchukua hatua, utakata mkono au mguu lakini lazima utakufa. Angekuwa hana madhara sidhani kama wangeenda kutafuta Armenians kusaidia kazi ya kumsaka, lakini pia kurudisha wastaafu kama Othman kule Ikulu. Kipindi hiki wakikosea kidogo tu, ndiyo nitolee hivyo.​
 
Ulichokieleza ni Not more than a Typical Reality ya Kinachoonekana kwa hawa Watawala wetu na ndio maana kuna Muda huwa nasema Hii nchi Ukikaa Ukafikiria kiundani kabisa ni kwamba kama hutaki kuwa Affiliated na Chama tawala Basi Sahau kabisa kuendelea Maishani mwako Labda Usiwe ndani ya Ardhi hii.... Ni Laana.
 
Hii njia anayoitumia huyu mama inamuongezea maadui wengi mpaka basi. Yaani mpaka wale wananchi wanyonge wa vijijini ukiwauliza kuhusu huyu mama, wanamkataa waziwazi kutokana tu na matendo yake ambayo hayaendani na mila na desturi zetu tulizo jiwekea tangu kuundwa kwa hili Taifa.
 
SUMU ya koboko ikishaingia mwilini na ukachelewa kuchukua hatua, utakata mkono au mguu lakini lazima utakufa. Angekuwa hana madhara sidhani kama wangeenda kutafuta Armenians kusaidia kazi ya kumsaka, lakini pia kurudisha wastaafu kama Othman kule Ikulu. Kipindi hiki wakikosea kidogo tu, ndiyo nitolee hivyo.​
Armenians? unaweza kujazia nyama!
 
MAUAJI YA KISIASA (Political Assassinations) ni moja kati ya sera za kiutawala ambazo zimekuwa zikitumika tokea ustaarabu ulivyoanza kutokea duniani. Huwa inatumika kuwazima mara moja maadui wa kisiasa, maadui wa taifa au maadui wa kimaslahi.

Tatizo ni kwamba, tofauti na siku za kale ambapo jamii ziliongozwa kama piramidi, ambapo watu walioshiriki kwenye siasa walikuwa ni wale walioelimika (Educated Elites) na waliotokea familia za kitawala (Aristocrats) tu. Tofauti kabisa ni kipindi hiki, ambapo siasa za nchi zimehalalishwa na kufanywa katika ngazi za kitaasisi (Institutional Levels), ambapo siasa haifanywi na wasomi pekee (Educated Elites) na familia za kitawala (Aristocrats), bali hufanywa katika nyanja zote zinazogusa jamii.

SIASA inafundishwa shuleni na vyuoni, hivyo uhusikwa wa raia unakuwa mkubwa kiwango cha kufanya siasa iaathiri UCHUMI, DINI na UTAMADUNI. Hivyo huwezi kufanya MAUAJI YA KISIASA (Political Assassinations) bila kugusa taasisi nyingi za siasa zinazofanya kazi ndani ya nchi. Katika kufahamu hili, mataifa mengi yaliyoendelea yamefikia kwenye ukweli mchungu kwamba: KAMA SIASA ZINAFANYIKA KWENYE NGAZI ZA KITAASISI, kuua mtu mmoja hakuwezi kubadilisha chochote katika muda mrefu.

Prof Noam Chomsky, kwenye moja ya kazi zake muhimu iitwayo "The Manufactured Consent" anaelezea kwamba katika jamii za ulimwengu wa utandawazi, watu wengi huwa na mawazo sawa kwasababu ya propaganda za kisiasa. Hivyo hata vyama vya siasa wanakuwa na sauti ndani ya jamii kwasababu wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kueneza propaganda za kisiasa ambazo zimefanikiwa kuwaaminisha watu kuhusu matatizo yanayowazunguka.

==============================================================
Mataifa kama UCHINA, mbali na ukatili wao mwingine, huwafanyi MUAJI YA KISIASA (Political Assassinations) kama zamani. Wamefahamu kwamba MAUAJI YA KISIASA ya madhara makubwa sana: Huwafanya watawala wa nchi kushindwa kuyakabila matatizo makubwa ya nchi ya muda mrefu kwa uwazi, ufasaha, weledi na ubunifu.

Matatizo yote ya kisiasa ndani ya nchi hutokana na mawazo (Ideas/Political Thought). Mawazo (Ideas/Political Thought) haya watu hujengewa baada ya kupitia kwenye taasisi fulani, kama Shule, Chuo, Chama Cha Siasa, Umoja wa Wafanyakazi, Vyombo vya Habari, au Taasisi za Kidini. Hivyo unapomuua (Assassinate) mtu kwasababu ya mawazo ya kisiasa, fahamu kwamba huwezi kubadilisha chochote endapo taasisi kama Shule, Chuo, Chama Cha Siasa, Umoja wa Wafanyakazi, Vyombo vya Habari au Taasisi za Kidini hujazifutilia mbali kabisa.

NDIYO MAANA, madikteta wakubwa wote duniani kama Hitler, Mussolini, Mao Zedong, Joseph Stalin na Lenin, walipochukua nchi, hawakufanya MUAJI YA KISIASA (Political Assassinations) peke yake, bali walifanya MAUAJI YA HALAIKI (Mass Murder/Massacre/Genocide), wakishambulia taasisi za muhimu za kisiasa na watu wake waliopata mawazo kutoka kwenye hizo taasisi. Mfano, Lenin aliua mamilioni ya Wakristo na kubomoa maelfu ya makanisa.

==============================================================
ILI NCHI IENDELEE KWENYE KARNE HII, ni lazima watawala wa kitanzania wafahamu kwamba changamoto za kisiasa zinapokuja ni lazima kuzikabili bila kutafuta njia mbadala. Wakifanya hivyo watajipa nafasi ya wao wenyewe kukua, kukomaa na kuweza kujenga uwezo mkubwa kiutawala kutatua changamoto za kitaifa katika ngazi ya kitaasisi.

Mimi ni moja kati ya watu humu ndani ambao nitaendelea kupinga sera za Mzee Nyerere ambaye ndiye muasisi mkuu wa kutumia SERA YA MAUAJI YA KISIASA (Political Assassinations) katika kutawala nchi. Hakuweza kulijengea taifa la Tanganyika uwezo wa kiutaalamu wa kukaa mezani, kufanya tafiti, kufanya mijadala ya kitaalamu, kukubaliana na mawazo kinzani, na kisha kutafuta suluhu za kisayansi. Huu ndiyo UTAMADUNI aliowajengea CCM + TISS.

Wale wote waliopingana na Mzee Nyerere katika ngazi za kisiasa, aidha walifungwa, walifukuzwa nchi au kuuwawa kinyama. Hakuwa na ujasiri wa kuweza kukaa kwenye meza moja na kuangalia zimwi la mawazo kinzani yaliyomfanya aonekana hana akili au siyo msomi. Hivyo akajificha kwenye kichaka cha kutumia propaganda za mabeberu kuwapa jina maadui zake kisha kuwashughulikia.

==============================================================
LEO HII, ninapoona vijana wa CCM + TISS hawana uwezo wowote ule wa kufanya mijadala ya kisiasa kwa utaalamu, kufanya tafiti za kisomi na kubuni suluhisho, huwa siwashangai hata kidogo. Huo UTAMADUNI watanganyika hatukujengewa tangu nchi ipate uhuru. Hivyo wanapokutana na mawazo makubwa ambayo yamewazidi uwezo, tafasiri yao ni kwamba, hili ni wazo la kibeberu, kihujuma, linalolenga kuvunja amani ya nchi. SULUHISHO NI KUUA TU.

==========================================================
WACHINA
walipolifahamu hili, walitenganisha baina ya changamoto za kisiasa na zile za kiusalama (Pure Security Matters). Ambapo linapokuja suala la kisiasa Chama Cha Kikomunisti Cha Uchina (CCP), kinaamua kutumia akili kutatua tatizo. Hili linawapa watawala uelewa mpana kuhusu tatizo, ujasiri mkubwa wa kukabili matatizo, lakini nchi nzima na taasisi za kisiasa zinajengewa UTAMADUNI wa kuamini kwamba kila kitu kinaweza kutatuliwa kwa mazungumzo na siyo vitisho au kuuana.

================================================================
UKIANZA KUWAFIKIRIA: Abeid Karume, Kassim Hanga, Edward Sokoine, Imran Kombe, Gilman Rutihinda, Stephen Kibona, Horace Kolimba, Daudi Balali, William Mgimwa, Benard Membe, na wengine wengi (Wazuri kwa Wabaya), utafahamu kwamba MAUAJI YA KISIASA (Political Assassinations) hazikubadilisha chochote kile na matatizo yamerudi kwa nguvu zaidi.

Lakini, watawala wangekuwa na hekima, nadhani kuna matatizo mengi tu hapa nchini siyo matatizo kama ambavyo wanasiasa huwa wanayakuza. Mengine yangemalizika kwenye mijadala ya kisiasa ya wazi tu. Hapa ndipo MZUNGU anapomuacha MWAFRIKA. Wamejengwa UTAMADUNI wa kuweza kuhimili tofauti, na kufundishwa kutafuta COMMON GROUND, kupitia tafiti za kisayansi (SCIENTIFIC RESEARCH) na UBUNIFU (INNOVATION).

=================================================================
TATIZO LA TANZANIA KWASASA: Ile MIZEE YA COLD-WAR kama Butiku, Warioba, Wassira, Mkuchika, Kikwete, Karume, Luhavi, Bulembo, Chenge,Lukuvi, Kabudi, Zungu na wengine, pamoja na watoto wao waliopo ndani ya mfumo, hawawezi kutusaidia kwasababu akili zao zimechekaa. Wao wanaitazama dunia katika sura mbili tu. UBEBERU v UJAMAA, kwamba FEDHA NI HARAMU na UMASIKINI NI FAHARI.

FEDHA NI HARAMU kwa Mtanzania wa kawaida, siyo KADA WA CCM na familia yake.
UMASIKINI NI HARAMU kwa KADA WA CCM na familia yake ila kwa mtanzania wa kawaida ni sawa.

===========================================================
NDIYO MAANA, KADA WA CCM akiiba, akipora, akidhulumu au hata akiua taasisi za kiusalama haziwezi kumfanya lolote kwasababu ni mwenzao. MTANZANIA WA KAWAIDA akiwa TAJIRI, ni lazima ameiba au anatumiwa na mabeberu. Kuna imani ndani ya mioyo ya watawala wa Tanzania kwamba, huwezi kuwa tajiri bila kuwa serikalini.

SIJUI KAMA MTANIELEWA, AU NIMEWACHANGANYA.
​
Tupe muda kwanza...
Maana muda mchache sana..

Lakini Je!
Ni kweli aliyetekwa ni Polepole!??
 
Mimi nimekuelewa vizuri sana...

Na kwa hakika hii ndiyo hali halisi ya Bongoland ya sasa...

Ili tujikomboe, ni LAZIMA KIZAZI CHOTE (THE ENTIRE CCM GENERATION) YA KINA NYERERE, BUTIKU,WARIOBA, KIKWETE na WANAOFANANA NAO pamoja na mawazo na ideologies zao ipukutishwe na kupotea kabisa na kuzalisha KIZAZI kipya chenye mawazo mapya ya kisasa..

Yote haya yanayotutokea leo si matatizo katika jina na uhalisia wake kama "MATATIZO" bali haya ni matokeo ya HOFU (FEAR) na MASHAKA tu ya kupoteza ya hawa wazee na kwa sababu ya hofu yao hii, wame influence irrational decisions na kuligharimu taifa na watu wa nchi hii pakubwa...
 
Samahani lakini mkuu Malcom, katika makala zako nyingi zinazogusa maslahi ya tanzania kwenye nyanja za siasa, uchumi na taaluma mara nyingi huwa unamtupia lawama Nyerere. Sawa, inawezekana una sababu zako za msingi kwa nini unamhusisha kila mara mambo yanapokwenda mrama. Lakini naomba kuhoji kama ni lazima iwe hivyo unamvyomfikiria yule mzee. Nyerere ameichukua nchi toka kwa wakoloni 1961 na kaiachia 1985 kama sijakosea, Miaka 24 ya uongozi wake. Takribani miaka 40 baadae tukifeli lawama zinakuja kwako. Kama kweli tuna watu wenye weledi wa kutupeleka mbele miaka 40 ilikuwa mingi sana kubadilisha ideology ya Nyerere isiyofaa na kutupatia taifa tunalolitaka kwa sasa. Sina uelewa mzuri kama wako kwenye siasa za dunia ila tukumbushe misingi ya mataifa yaliyokuwa level zetu miaka ile kama waanzilishi wao walitengeneza misingi iliyowavusha toka kwenye giza au ni watu waliochipukia ndio waliyastawisha hayo mataifa akama china, indonesia, malaysia, korea, japani, n.k. Samahani kwa mwandiko mbovu usiokuwa na aya sababu natumia simu yenye shida kwenye button.
 
Back
Top Bottom