Mauaji ya Kisiasa (Political assassinations) siyo sera bora ya kiutawala

Samahani lakini mkuu Malcom, katika makala zako nyingi zinazogusa maslahi ya tanzania kwenye nyanja za siasa, uchumi na taaluma mara nyingi huwa unamtupia lawama Nyerere. Sawa, inawezekana una sababu zako za msingi kwa nini unamhusisha kila mara mambo yanapokwenda mrama. Lakini naomba kuhoji kama ni lazima iwe hivyo unamvyomfikiria yule mzee. Nyerere ameichukua nchi toka kwa wakoloni 1961 na kaiachia 1985 kama sijakosea, Miaka 24 ya uongozi wake. Takribani miaka 40 baadae tukifeli lawama zinakuja kwako. Kama kweli tuna watu wenye weledi wa kutupeleka mbele miaka 40 ilikuwa mingi sana kubadilisha ideology ya Nyerere isiyofaa na kutupatia taifa tunalolitaka kwa sasa. Sina uelewa mzuri kama wako kwenye siasa za dunia ila tukumbushe misingi ya mataifa yaliyokuwa level zetu miaka ile kama waanzilishi wao walitengeneza misingi iliyowavusha toka kwenye giza au ni watu waliochipukia ndio waliyastawisha hayo mataifa akama china, indonesia, malaysia, korea, japani, n.k. Samahani kwa mwandiko mbovu usiokuwa na aya sababu natumia simu yenye shida kwenye button.

..Nyerere ndiye aliyewashawishi Ccm wakubali vyama vingi, kwasababu walikuwa wamegoma.

..Kwa hiyo, Nyerere alifanya alichoweza. kama ni uharibifu wamefanya warithi wake.
 
Nyerere ametuachia nchi mbovu mno.​
Tusimsingizie Nyerere, yeye aikuwepo kwenye zama zake, ambapo ustaarabu ulikuwa wa hovyo sana, hakukua na utandawazi, ulimwengu mzima ulikuwa kwenye vurugu tupu, Ubaguzi wa rangi, US, SA, Ulaya ndo imetoka vitani, mauwaji ya wayahudi yalikua bado mabichi, ukatiri wa Ujerumani, Japan n.k
Wenzetu wamehama huko, umetolea mfano wa China, hata hapo South Africa tu..SISI tuna viongozi wabinafsi sana, mara elfu bora hata Nyerere, hawa wa sasa hawajali wananchi, ufisadi, watu kupotea, ukamataji usiofuata sheria..na unafiki na uoga wa kuanzia makamanda wa jeshi, polisi n.k
We are doomed, it is a petty.
Mfano ninamalizia kusoma kitabu kuhusu Mossad kikiwa kimeandikwa na x mossad wenyewe...utashangaa mkurugenzi mkuu wa Mossad wanakwambia anaishi kwenye kaa Apartment, simple life, na ni kuhakikisha Jews wako safe...hata kama ni mtu mmoja yuko sijui wapu, watafanya kila mbinu wamuokoe arudi nyumbani...hakuna kuua wananchi, n.k..Sisi huku watuwanatekwa, wanapotea, kuna watu wanakula mishahara, wanatembelea ving'ora wapishwe barabarani but hawasimamii katiba na utawala bora..
SHAME ON CCM, POLICE, TISS & JWTZ....wameshindwa kulinda maisha ya mtanzania mmoja mmoja, wameruhusu mamboya ajabu kutokea..
Ina uma sana na aibu sana.
 
..Nyerere ndiye aliyewashawishi Ccm wakubali vyama vingi, kwasababu walikuwa wamegoma.

..Kwa hiyo, Nyerere alifanya alichoweza. kama ni uharibifu wamefanya warithi wake.
Nyerere alilifahamu fika matatizo ya Tanzania kuanzia KATIBA, MUUNGANO, CCM na UTADAMU WA KUPENDA MAZOEA na siyo sheria. Lakini hakuamua kutumia kiti chake kurekebisha jambo lolote akitegemea siasa za CCM ndiyo zitarekebisha nchi. Kituko ni kwamba alipigia chapuo mfumo wa vyama vingi, lakini alikuwa kinara wa kuhujumu mchakato mzima wa Demokrasia mwaka 1995 yota.

Mzee Nyerere aliingia kaburini na majuto mengi moyoni. Moja ya jambo ambalo alijituia ni KUMPELEKA MKAPA IKULU, lakini pia mawazo yake yalibadilika sana kuhusu MUUNGANO. Aliwachukia wakina Horace Kolimba walivyomwambia ukweli, lakini hata awamu ya MKAPA haijaisha Nyerere alikuwa anataka MKAPA asiendelee kutawala.

ALIFAHAMU KABISA KATIBA NI MBOVU: Kwamba CCM wanapewa nguvu kubwa ya kuvuruga kila kitu nchini, lakini hakufanya chochote. Akifahamu kabisa VYAMA VINGI ni KIINI MACHO kuwahadaa watanganyika. Mwaka 1995 CCM ingekuwa imeshotoka na imebaki historia, ila yeye ndiye aliyetumia UBABA WAKE WA TAIFA KUWAKINGIA KIFUA.

TUTAENDELEA KUMLAUMU MILELE.
​
 
..hoja yangu ni kwamba waliofuata baada ya Mwalimu Nyerere walipaswa kurekebisha makosa na mapungufu katika katiba na mifumo aliyoacha Baba wa Taifa. Sisemi kwamba Mwalimu Nyerere hakufanya makosa.
 
Mimi nimekuelewa vizuri sana...

Na kwa hakika hii ndiyo hali halisi ya Bongoland ya sasa...

Ili tujikomboe, ni LAZIMA KIZAZI CHOTE (THE ENTIRE CCM GENERATION) YA KINA NYERERE, BUTIKU,WARIOBA, KIKWETE na WANAOFANANA NAO pamoja na mawazo na ideologies zao ipukutishwe na kupotea kabisa na kuzalisha KIZAZI kipya chenye mawazo mapya ya kisasa..

Yote haya yanayotutokea leo si matatizo katika jina na uhalisia wake kama "MATATIZO" bali haya ni matokeo ya HOFU (FEAR) na MASHAKA tu ya kupoteza ya hawa wazee na kwa sababu ya hofu yao hii, wame influence irrational decisions na kuligharimu taifa na watu wa nchi hii pakubwa...

Je, Gen Z ipo tiyari au imejiandaa au kuandalia kwa ajili ya kuchukua nafasi ya hiyo generation uloisema?
 
..Nyerere ndiye aliyewashawishi Ccm wakubali vyama vingi, kwasababu walikuwa wamegoma.

..Kwa hiyo, Nyerere alifanya alichoweza. kama ni uharibifu wamefanya warithi wake.
Mkuu sidhani kama hayati Nyerere yeye kama yeye binafsi alikubali kuwepo kwa vyama vingi, angetaka iwe hivyo kama alivyoamua uchaguzi wa 1995 basi Tanzania leo ingekuwa chini ya chama kingine kama ilivyokuwa kwa Chiluba Zambia.

Angewachia Kolimba na co wangeenda kuunda chama kikuu cha upinzani ambacho bila shaka yoyote ile kingeitoa CCM madarakani.

Badala yake aliposema kuwa CCM imepoteza dira na mwelekeo aliitwa Chamwino akajieleze na sote twafahamu kilichompata. Kumbuka hiyo ni miaka ya 90s mtu sema CCM imepoteza dira na mwelekeo, aliona mbali huyu mzee.

Kama Chiluba, Horace Kolimba alikuwa na nguvu kubwa ya ushawishi kutokana na historia yake kule JUWATA hivyo angeunganisha chama la akina Kasanga, Tumbo, Chifu Fundikira, Mabere Marando, Auguistine Mrema, kisha mwanasheria mkiuu wa serikali angakuwa Dr Masumbuko Lamwai, nchi ingechimbika.

Na hawa walikuwa ni sehemu tu bado walikuwepo akina Kambona, Bob Makani na wengine wengi ambao kwa kweli walikuwa ni wasomi na kwa namna fulani hayati Nyerere alifahamu walikuwa ni tishio kwake.
 
Badala yake aliposema kuwa CCM imepoteza dira na mwelekeo aliitwa Chamwino akajieleze na sote twafahamu kilichompata. Kumbuka hiyo ni miaka ya 90s mtu sema CCM imepoteza dira na mwelekeo, aliona mbali huyu mzee.
Kuhusu CCM, marehemu Horace Kolimba na Imran Kombe walikuwa mbele ya muda.

Siasa za SUMU, VISU na RISASI inayofanywa na CCM, wanamuiga Mzee Nyerere.

Mzee ndiyo aliasisi hii michezo michafu na kama tukitaka kuliponya taifa ni lazima tutambue kwanza tatizo lilianza wapi, na lini.
​
 
MAUAJI YA KISIASA (Political Assassinations) ni moja kati ya sera za kiutawala ambazo zimekuwa zikitumika tokea ustaarabu ulivyoanza kutokea duniani. Huwa inatumika kuwazima mara moja maadui wa kisiasa, maadui wa taifa au maadui wa kimaslahi.

Tatizo ni kwamba, tofauti na siku za kale ambapo jamii ziliongozwa kama piramidi, ambapo watu walioshiriki kwenye siasa walikuwa ni wale walioelimika (Educated Elites) na waliotokea familia za kitawala (Aristocrats) tu. Tofauti kabisa ni kipindi hiki, ambapo siasa za nchi zimehalalishwa na kufanywa katika ngazi za kitaasisi (Institutional Levels), ambapo siasa haifanywi na wasomi pekee (Educated Elites) na familia za kitawala (Aristocrats), bali hufanywa katika nyanja zote zinazogusa jamii.

SIASA inafundishwa shuleni na vyuoni, hivyo uhusikwa wa raia unakuwa mkubwa kiwango cha kufanya siasa iaathiri UCHUMI, DINI na UTAMADUNI. Hivyo huwezi kufanya MAUAJI YA KISIASA (Political Assassinations) bila kugusa taasisi nyingi za siasa zinazofanya kazi ndani ya nchi. Katika kufahamu hili, mataifa mengi yaliyoendelea yamefikia kwenye ukweli mchungu kwamba: KAMA SIASA ZINAFANYIKA KWENYE NGAZI ZA KITAASISI, kuua mtu mmoja hakuwezi kubadilisha chochote katika muda mrefu.

Prof Noam Chomsky, kwenye moja ya kazi zake muhimu iitwayo "The Manufactured Consent" anaelezea kwamba katika jamii za ulimwengu wa utandawazi, watu wengi huwa na mawazo sawa kwasababu ya propaganda za kisiasa. Hivyo hata vyama vya siasa wanakuwa na sauti ndani ya jamii kwasababu wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kueneza propaganda za kisiasa ambazo zimefanikiwa kuwaaminisha watu kuhusu matatizo yanayowazunguka.

==============================================================
Mataifa kama UCHINA, mbali na ukatili wao mwingine, huwafanyi MUAJI YA KISIASA (Political Assassinations) kama zamani. Wamefahamu kwamba MAUAJI YA KISIASA ya madhara makubwa sana: Huwafanya watawala wa nchi kushindwa kuyakabila matatizo makubwa ya nchi ya muda mrefu kwa uwazi, ufasaha, weledi na ubunifu.

Matatizo yote ya kisiasa ndani ya nchi hutokana na mawazo (Ideas/Political Thought). Mawazo (Ideas/Political Thought) haya watu hujengewa baada ya kupitia kwenye taasisi fulani, kama Shule, Chuo, Chama Cha Siasa, Umoja wa Wafanyakazi, Vyombo vya Habari, au Taasisi za Kidini. Hivyo unapomuua (Assassinate) mtu kwasababu ya mawazo ya kisiasa, fahamu kwamba huwezi kubadilisha chochote endapo taasisi kama Shule, Chuo, Chama Cha Siasa, Umoja wa Wafanyakazi, Vyombo vya Habari au Taasisi za Kidini hujazifutilia mbali kabisa.

NDIYO MAANA, madikteta wakubwa wote duniani kama Hitler, Mussolini, Mao Zedong, Joseph Stalin na Lenin, walipochukua nchi, hawakufanya MUAJI YA KISIASA (Political Assassinations) peke yake, bali walifanya MAUAJI YA HALAIKI (Mass Murder/Massacre/Genocide), wakishambulia taasisi za muhimu za kisiasa na watu wake waliopata mawazo kutoka kwenye hizo taasisi. Mfano, Lenin aliua mamilioni ya Wakristo na kubomoa maelfu ya makanisa.

ILI NCHI IENDELEE KWENYE KARNE HII, ni lazima watawala wa kitanzania wafahamu kwamba changamoto za kisiasa zinapokuja ni lazima kuzikabili bila kutafuta njia mbadala. Wakifanya hivyo watajipa nafasi ya wao wenyewe kukua, kukomaa na kuweza kujenga uwezo mkubwa kiutawala kutatua changamoto za kitaifa katika ngazi ya kitaasisi.

Mimi ni moja kati ya watu humu ndani ambao nitaendelea kupinga sera za Mzee Nyerere ambaye ndiye muasisi mkuu wa kutumia SERA YA MAUAJI YA KISIASA (Political Assassinations) katika kutawala nchi. Hakuweza kulijengea taifa la Tanganyika uwezo wa kiutaalamu wa kukaa mezani, kufanya tafiti, kufanya mijadala ya kitaalamu, kukubaliana na mawazo kinzani, na kisha kutafuta suluhu za kisayansi. Huu ndiyo UTAMADUNI aliowajengea CCM + TISS.

Wale wote waliopingana na Mzee Nyerere katika ngazi za kisiasa, aidha walifungwa, walifukuzwa nchi au kuuwawa kinyama. Hakuwa na ujasiri wa kuweza kukaa kwenye meza moja na kuangalia zimwi la mawazo kinzani yaliyomfanya aonekana hana akili au siyo msomi. Hivyo akajificha kwenye kichaka cha kutumia propaganda za mabeberu kuwapa jina maadui zake kisha kuwashughulikia.

LEO HII, ninapoona vijana wa CCM + TISS hawana uwezo wowote ule wa kufanya mijadala ya kisiasa kwa utaalamu, kufanya tafiti za kisomi na kubuni suluhisho, huwa siwashangai hata kidogo. Huo UTAMADUNI watanganyika hatukujengewa tangu nchi ipate uhuru. Hivyo wanapokutana na mawazo makubwa ambayo yamewazidi uwezo, tafasiri yao ni kwamba, hili ni wazo la kibeberu, kihujuma, linalolenga kuvunja amani ya nchi. SULUHISHO NI KUUA TU.

==========================================================
WACHINA
walipolifahamu hili, walitenganisha baina ya changamoto za kisiasa na zile za kiusalama (Pure Security Matters). Ambapo linapokuja suala la kisiasa Chama Cha Kikomunisti Cha Uchina (CCP), kinaamua kutumia akili kutatua tatizo. Hili linawapa watawala uelewa mpana kuhusu tatizo, ujasiri mkubwa wa kukabili matatizo, lakini nchi nzima na taasisi za kisiasa zinajengewa UTAMADUNI wa kuamini kwamba kila kitu kinaweza kutatuliwa kwa mazungumzo na siyo vitisho au kuuana.

================================================================
UKIANZA KUWAFIKIRIA: Abeid Karume, Kassim Hanga, Edward Sokoine, Imran Kombe, Gilman Rutihinda, Stephen Kibona, Horace Kolimba, Daudi Balali, William Mgimwa, Benard Membe, na wengine wengi (Wazuri kwa Wabaya), utafahamu kwamba MAUAJI YA KISIASA (Political Assassinations) hazikubadilisha chochote kile na matatizo yamerudi kwa nguvu zaidi.

Lakini, watawala wangekuwa na hekima, nadhani kuna matatizo mengi tu hapa nchini siyo matatizo kama ambavyo wanasiasa huwa wanayakuza. Mengine yangemalizika kwenye mijadala ya kisiasa ya wazi tu. Hapa ndipo MZUNGU anapomuacha MWAFRIKA. Wamejengwa UTAMADUNI wa kuweza kuhimili tofauti, na kufundishwa kutafuta COMMON GROUND, kupitia tafiti za kisayansi (SCIENTIFIC RESEARCH) na UBUNIFU (INNOVATION).

=================================================================
TATIZO LA TANZANIA KWASASA: Ile MIZEE YA COLD-WAR kama Butiku, Warioba, Wassira, Mkuchika, Kikwete, Karume, Lhwavi, Bulembo, Chenge,Lukuvi, Kabudi, Zungu na wengine, pamoja na watoto wao waliopo ndani ya mfumo, hawawezi kutusaidia kwasababu akili zao zimechekaa. Wao wanaitazama dunia katika sura mbili tu. UBEBERU v UJAMAA, kwamba FEDHA NI HARAMU na UMASIKINI NI FAHARI.

FEDHA NI HARAMU kwa Mtanzania wa kawaida, siyo KADA WA CCM na familia yake.
UMASIKINI NI HARAMU kwa KADA WA CCM na familia yake ila kwa mtanzania wa kawaida ni sawa.

===========================================================
NDIYO MAANA, KADA WA CCM akiiba, akipora, akidhulumu au hata akiua taasisi za kiusalama haziwezi kumfanya lolote kwasababu ni mwenzao. MTANZANIA WA KAWAIDA akiwa TAJIRI, ni lazima ameiba au anatumiwa na mabeberu. Kuna imani ndani ya mioyo ya watawala wa Tanzania kwamba, huwezi kuwa tajiri bila kuwa serikalini.

SIJUI KAMA MTANIELEWA, AU NIMEWACHANGANYA.
​
Baba wa taifa kiatu changu 😂
 
Kuhusu CCM, marehemu Horace Kolimba na Imran Kombe walikuwa mbele ya muda.

Siasa za SUMU, VISU na RISASI inayofanywa na CCM, wanamuiga Mzee Nyerere.

Mzee ndiyo aliasisi hii michezo michafu na kama tukitaka kuliponya taifa ni lazima tutambue kwanza tatizo lilianza wapi, na lini.
​
moja ya swala baya alilotuachia Nyerere ni swala la muungano....hiki ni kiini macho
 
Wiki tatu kabla ya 29 Oktoba 2025.

Lakini WATANGANYIKA hamkuelewa, mkadhani namchukia na kumpondea Mzee Nyerere.

ENIWEI, hamtaki kukubali ukweli mpaka mambo yawakute kwanza na muone damu imemwagika.

CCM haina muda mrefu , ila hata ikitoka kutakuwa na matatizo makubwa mno mpaka nchi ije ikae sawa.
​
 
Umenipa mawazo na mtazamo tofauti kabisa kuhusu huyu mzee japo nilimpatia wasiwasi wa uongozi wake hata kama sikuukuta ni kuhusu hii katiba, kwamba hakuiona kama haifai? Mbona aliwahi kusema kwamba katiba hii ikikutana na dikteta itakuwa hatari?
Kipindi Lissu anambananga Bungeni sikumuelewa Lissu, kumbe jamaa yupo smart sana kichwani kwake.
Huyu mzee hakufaa hata kuadhimishwa siku yake.
Asante sana mkuu MALCOM LUMUMBA .
 
Hakuwa mtu mbaya Mzee Nyerere. Ila sera zake zilikuwa ni mbaya sana na zenye madhara kwa nchi.

Ukimlinganisha BABU NYERERE na watawale wengine, NYERERE NI MTAKATIFU kabisaa.

Tunachokisema ni kile ambacho hata Lissu amekuwa akikisema, kwamba tusilazimishe Mzee Nyerere awe malaika. Makosa aliyoyafanya ni makubwa na mabaya ambayo yanaligharimu hili taifa. Tukimkosoa haimaanishi kwamba hakufanya mazuri, ila ukweli ni kwamba alikosea na akawa mbishi kukubali ukweli huku akiwa anaonea wenzake akidhani anaisaidia nchi kumbe ndiyo anazidi kuvurunda.

Kama sera zake hazikuwa nzuri yeye anakuwaje mzuri wakati kuna waliopata madhara ya kimwili na kihisia? Hata misingi yake sasa inaonekana kutokuwa na maana yoyote?
 
Back
Top Bottom