Mauaji ya Kisiasa (Political assassinations) siyo sera bora ya kiutawala

Kama sera zake hazikuwa nzuri yeye anakuwaje mzuri wakati kuna waliopata madhara ya kimwili na kihisia? Hata misingi yake sasa inaonekana kutokuwa na maana yoyote?
Sera hutekelezwa kisheria na katika ngazi ya kitaasisi.Hivyo kwenye tunaanza na SERA-SHERIA-TAASISI-WANANCHI= MFUMO

Unaweza ukatengeneza sera nzuri lakini utekelezaji wake ukawa mbovu kwasababu za aidha sheria zilizotungwa ni mbaya, taasisi za utakelezaji haziko vizuri, au sera haziendani na mazingira ya jamii husika, au sera hazikubaliki na wananchi. Ndiyo maana sera inaweza ikafanikiwa nchi moja lakini ikafeli vibaya nchi nyingine.

Mfano mzuri sera za kodi(Fiscal Policies) na fedha(Monetary Policies) ambazo tunazitumia kila siku, kuna msimu zinaweza kufanikiwa vizuri na kuna msimu zinaweza zikafeli vibaya kwelikweli.

Jambo la msingi kabisa katika kufanikiwa utekelezwaji wa sera yoyote ile ni USHIRIKISHWAJI NA UTAYARI WA WADAU WAKUBWA ambao ni RAIA WA KAWAIDA. Bila ushirikishwaji wa wananchi na utayari wao, hata sera iwe nzuri kivipi kuna muda utafika itafeli. Mzee Nyerere katika miaka yake zaidi ya 20 madarakani alitengeneza (The Elite Government), ambapo nchi inaongozwa na kikundi cha watu wachache wenye nguvu, ambacho kiliamini kwamba kina uhalali wa kuwaamulia watanganyika na wazanzibari nini sahihi na nini siyo sahihi.

Maamuzi makubwa yanayoathiri nchi mpaka leo yalifanywa na Mzee Nyerere wakati yuko madarakani, bila kuwashirikisha watanganyika na wazanzibari. Tunaendelea kumsema kwasababu ameacha mazimwi makubwa mno yatakayotafuna vizazi vyetu kwa miaka mingi. Hebu zingatia haya:

1. MUUNGANO
Uliratibiwa na kikundi cha watu wachache wakishirikiana na mataifa ya nje. Ukiuliza watanganyika wa wakati huo na wazanzibari kuhusu muungano utafahamu kwamba unasumbua mpaka leo kwasababu haukuwa na baraka za wananchi. Ndiyo maana Tanganyika inafichwa utadhani mimba ya mtawa kwasababu watawala wanafahamu fika siku Tanganyika ikionekana, muungano lazima uvunjike. Kisingizio cha kusema kwamba ilikuwa ni lazima tuungane na Zanzibar kisa usalama, au watanganyika wengi walikuw hawajaelimika hazina mashiko.

2.UJAMAA
Hii sera ilikuwa kubwa na ilitekelezwa katika kila ngazi ya taifa hili. Ukiuliza uhalali wake ulitoka wapi au kama majadiliono ya kitaifa yalifanyika huwezi kupata majibu. Sera kama UJAMAA unavyoipitisha bila idhini ya wananchi, basi hakikisha haifeli na una kila nyenzo ya kuitekeleza. Ila ikifeli lazima tutakubebesha lawama tu. Unavyopitisha AZIMIO LA ARUSHA, uliwashirikisha wananchi???

3. KATIBA YA MWAKA 1977
Watanganyika wengi wanalalamika alichokifanya Kikwete mwaka 2014 kwenye TUME YA WARIOBA ila wanasahau kwamba, jambo kama hilo lilifanywa mwaka 1977 na Mzee Nyerere akiwatumia kina Pius Msekwa kuandika katiba ambayo inatutesa mpaka leo bila kuwashirikisha wananchi. Hapa tukilalama watasema tunamchukia Mzee Nyerere kweli ???

4. KUFUTA VYAMA VINGI
Aliyewashawishi TANU kufuta vyama vingi mwaka 1964 ni nani ? Walifanya hivyo kwa idhini ya nani ?
Halafu vilivyorudishwa mwaka 1992 kwa shinikizo lake, mwaka 1995 akaanza kuwatuma maafisa usalama kina Siyovelwa kuhujumu watu wote wanaompinga Mkapa. Akaanza kuwanyanyasa wapinzani kwa kuwaita "Mbwa" na kusema hawana uwezo wa kuongoza nchi, ilhali mwaka 1992 alilazimisha vyama vingi yeye mwenyewe kinyume na TUME YA NYALALI.

Kina Horace Kolimba, Imran Kombe, Mohamed Babu, Oscar Kambona wote walipata shida kwasababu ya kinyongo ambacho Nyerere alikuwa nacho nao kuhusu kumuweka Mkapa madarakani. Walisema ukweli na yeye hakupenda ukweli, akaamua kuwashughulikia.

5. KUFUTA HAKI ZA BINADAMU KWENYE KATIBA
Hivi mtu mwenye nia njema anaweza akaamka na kufuta haki za binadamu kwenye katiba kwa kisingizio kwamba zinachelewesha maendeleo au ni mambo ya kibeberu ? JPM alichokifanya mwaka 2018-2019, kuzuia watu wasipeleke kesi mahakamani kudai haki za binadamu na kuzuia watu binafsi wasipeleke kesi za haki za binadamu dhidi ya serikali kilianza kufanywa na Mzee Nyerere na Rashidi Kawawa, ambao walisema wazi "Human Rights is a luxury we cannot afford"
=====================================================================================

KINACHONIUMIZA NI HIKI: Mambo yote ambayo Mzee Nyerere hakutaka yafanyike kipindi cha utawala wake, kama kuruhusu Structural Adjustment Programmes (SAP), kuruhusu haki za binadamu kwenye katiba, kuruhusu mali binafsi na kuruhusu siasa za vyama vingi alilazimisha yafanyike chini ya Mzee Mwinyi yeye akiwa MWENYEKITI WA CCM hadi 1988. Halafu ghafla akawa anatoka hadharani anaanza kuwafundisha watawala kuhusu haki za binadamu, umiliki binafsi wa mali na jinsi ya kuendesha siasa za vyama vingi.

Tuna mengi sana ya kusema kuhusu Mzee Nyerere, kuanzia kilichokuwa kinaendelea nchini Uganda, Mauaji ya Rwanda na Raisi Mkapa kunusurika kupata ajali kule kanda ya ziwa akiwa Raisi baada ya kuanza kuzozana kuhusu ubinafsishaji. Sema kwasababu mengine ni mazito tunayaacha kama yalivyo
========================================================================================
​
 
Asante sana, ngoja nitafute muda nikafanye rejea za Tundu Lissu akiwa bungeni kumuhusu.
 
Back
Top Bottom