Mauaji ya Kisiasa (Political assassinations) siyo sera bora ya kiutawala


..Nyerere ndiye aliyewashawishi Ccm wakubali vyama vingi, kwasababu walikuwa wamegoma.

..Kwa hiyo, Nyerere alifanya alichoweza. kama ni uharibifu wamefanya warithi wake.
 
Nyerere ametuachia nchi mbovu mno.​
Tusimsingizie Nyerere, yeye aikuwepo kwenye zama zake, ambapo ustaarabu ulikuwa wa hovyo sana, hakukua na utandawazi, ulimwengu mzima ulikuwa kwenye vurugu tupu, Ubaguzi wa rangi, US, SA, Ulaya ndo imetoka vitani, mauwaji ya wayahudi yalikua bado mabichi, ukatiri wa Ujerumani, Japan n.k
Wenzetu wamehama huko, umetolea mfano wa China, hata hapo South Africa tu..SISI tuna viongozi wabinafsi sana, mara elfu bora hata Nyerere, hawa wa sasa hawajali wananchi, ufisadi, watu kupotea, ukamataji usiofuata sheria..na unafiki na uoga wa kuanzia makamanda wa jeshi, polisi n.k
We are doomed, it is a petty.
Mfano ninamalizia kusoma kitabu kuhusu Mossad kikiwa kimeandikwa na x mossad wenyewe...utashangaa mkurugenzi mkuu wa Mossad wanakwambia anaishi kwenye kaa Apartment, simple life, na ni kuhakikisha Jews wako safe...hata kama ni mtu mmoja yuko sijui wapu, watafanya kila mbinu wamuokoe arudi nyumbani...hakuna kuua wananchi, n.k..Sisi huku watuwanatekwa, wanapotea, kuna watu wanakula mishahara, wanatembelea ving'ora wapishwe barabarani but hawasimamii katiba na utawala bora..
SHAME ON CCM, POLICE, TISS & JWTZ....wameshindwa kulinda maisha ya mtanzania mmoja mmoja, wameruhusu mamboya ajabu kutokea..
Ina uma sana na aibu sana.
 
..Nyerere ndiye aliyewashawishi Ccm wakubali vyama vingi, kwasababu walikuwa wamegoma.

..Kwa hiyo, Nyerere alifanya alichoweza. kama ni uharibifu wamefanya warithi wake.
Nyerere alilifahamu fika matatizo ya Tanzania kuanzia KATIBA, MUUNGANO, CCM na UTADAMU WA KUPENDA MAZOEA na siyo sheria. Lakini hakuamua kutumia kiti chake kurekebisha jambo lolote akitegemea siasa za CCM ndiyo zitarekebisha nchi. Kituko ni kwamba alipigia chapuo mfumo wa vyama vingi, lakini alikuwa kinara wa kuhujumu mchakato mzima wa Demokrasia mwaka 1995 yota.

Mzee Nyerere aliingia kaburini na majuto mengi moyoni. Moja ya jambo ambalo alijituia ni KUMPELEKA MKAPA IKULU, lakini pia mawazo yake yalibadilika sana kuhusu MUUNGANO. Aliwachukia wakina Horace Kolimba walivyomwambia ukweli, lakini hata awamu ya MKAPA haijaisha Nyerere alikuwa anataka MKAPA asiendelee kutawala.

ALIFAHAMU KABISA KATIBA NI MBOVU: Kwamba CCM wanapewa nguvu kubwa ya kuvuruga kila kitu nchini, lakini hakufanya chochote. Akifahamu kabisa VYAMA VINGI ni KIINI MACHO kuwahadaa watanganyika. Mwaka 1995 CCM ingekuwa imeshotoka na imebaki historia, ila yeye ndiye aliyetumia UBABA WAKE WA TAIFA KUWAKINGIA KIFUA.

TUTAENDELEA KUMLAUMU MILELE.
​
 


..hoja yangu ni kwamba waliofuata baada ya Mwalimu Nyerere walipaswa kurekebisha makosa na mapungufu katika katiba na mifumo aliyoacha Baba wa Taifa. Sisemi kwamba Mwalimu Nyerere hakufanya makosa.
 

Je, Gen Z ipo tiyari au imejiandaa au kuandalia kwa ajili ya kuchukua nafasi ya hiyo generation uloisema?
 
..Nyerere ndiye aliyewashawishi Ccm wakubali vyama vingi, kwasababu walikuwa wamegoma.

..Kwa hiyo, Nyerere alifanya alichoweza. kama ni uharibifu wamefanya warithi wake.
Mkuu sidhani kama hayati Nyerere yeye kama yeye binafsi alikubali kuwepo kwa vyama vingi, angetaka iwe hivyo kama alivyoamua uchaguzi wa 1995 basi Tanzania leo ingekuwa chini ya chama kingine kama ilivyokuwa kwa Chiluba Zambia.

Angewachia Kolimba na co wangeenda kuunda chama kikuu cha upinzani ambacho bila shaka yoyote ile kingeitoa CCM madarakani.

Badala yake aliposema kuwa CCM imepoteza dira na mwelekeo aliitwa Chamwino akajieleze na sote twafahamu kilichompata. Kumbuka hiyo ni miaka ya 90s mtu sema CCM imepoteza dira na mwelekeo, aliona mbali huyu mzee.

Kama Chiluba, Horace Kolimba alikuwa na nguvu kubwa ya ushawishi kutokana na historia yake kule JUWATA hivyo angeunganisha chama la akina Kasanga, Tumbo, Chifu Fundikira, Mabere Marando, Auguistine Mrema, kisha mwanasheria mkiuu wa serikali angakuwa Dr Masumbuko Lamwai, nchi ingechimbika.

Na hawa walikuwa ni sehemu tu bado walikuwepo akina Kambona, Bob Makani na wengine wengi ambao kwa kweli walikuwa ni wasomi na kwa namna fulani hayati Nyerere alifahamu walikuwa ni tishio kwake.
 
Badala yake aliposema kuwa CCM imepoteza dira na mwelekeo aliitwa Chamwino akajieleze na sote twafahamu kilichompata. Kumbuka hiyo ni miaka ya 90s mtu sema CCM imepoteza dira na mwelekeo, aliona mbali huyu mzee.
Kuhusu CCM, marehemu Horace Kolimba na Imran Kombe walikuwa mbele ya muda.

Siasa za SUMU, VISU na RISASI inayofanywa na CCM, wanamuiga Mzee Nyerere.

Mzee ndiyo aliasisi hii michezo michafu na kama tukitaka kuliponya taifa ni lazima tutambue kwanza tatizo lilianza wapi, na lini.
​
 
Baba wa taifa kiatu changu 😂
 
moja ya swala baya alilotuachia Nyerere ni swala la muungano....hiki ni kiini macho
 
Wiki tatu kabla ya 29 Oktoba 2025.

Lakini WATANGANYIKA hamkuelewa, mkadhani namchukia na kumpondea Mzee Nyerere.

ENIWEI, hamtaki kukubali ukweli mpaka mambo yawakute kwanza na muone damu imemwagika.

CCM haina muda mrefu , ila hata ikitoka kutakuwa na matatizo makubwa mno mpaka nchi ije ikae sawa.
​
 
Umenipa mawazo na mtazamo tofauti kabisa kuhusu huyu mzee japo nilimpatia wasiwasi wa uongozi wake hata kama sikuukuta ni kuhusu hii katiba, kwamba hakuiona kama haifai? Mbona aliwahi kusema kwamba katiba hii ikikutana na dikteta itakuwa hatari?
Kipindi Lissu anambananga Bungeni sikumuelewa Lissu, kumbe jamaa yupo smart sana kichwani kwake.
Huyu mzee hakufaa hata kuadhimishwa siku yake.
Asante sana mkuu MALCOM LUMUMBA .
 
Hakuwa mtu mbaya Mzee Nyerere. Ila sera zake zilikuwa ni mbaya sana na zenye madhara kwa nchi.

Ukimlinganisha BABU NYERERE na watawale wengine, NYERERE NI MTAKATIFU kabisaa.

Tunachokisema ni kile ambacho hata Lissu amekuwa akikisema, kwamba tusilazimishe Mzee Nyerere awe malaika. Makosa aliyoyafanya ni makubwa na mabaya ambayo yanaligharimu hili taifa. Tukimkosoa haimaanishi kwamba hakufanya mazuri, ila ukweli ni kwamba alikosea na akawa mbishi kukubali ukweli huku akiwa anaonea wenzake akidhani anaisaidia nchi kumbe ndiyo anazidi kuvurunda.
​
 
Kama sera zake hazikuwa nzuri yeye anakuwaje mzuri wakati kuna waliopata madhara ya kimwili na kihisia? Hata misingi yake sasa inaonekana kutokuwa na maana yoyote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…