Mauaji ya Mzee Karume: Acha sasa tuhoji yasiyohojika!

😀 😀 😀

Mbona mbaguzi hapa ni wewe? Mbona wewe unaonesha kuwachukia waarabu?

Hivi unafikiri Nyerere alisema vile kwa sababu ya uarabu Zanzibar? Anajua vyema kuwa lau kama Zanzibar ikipata mamlaka kamili, tutawaacha mbali sana kwa maendeleo. Tena sana, kitu ambacho Nyerere alikichukia sana kuona Zanzibar ikiendelea.

CCM inachukiwa sana kwa sababu ni wanafik na wabaguzi. Walisema mpemba kuingia ikulu ni sawa na mbwa kuingia msikitini, Mungu akawalaani na kuwapa DK. Sheni mpemba ambae ameingia ikulu 😀

CCM waliendesha kampeni na kusema kuwa Maalim Seif anataka kurudisha Usultan Zanzibar, Mungu akawaonesha raia wazanzibar kuwa atakae warudisha sultan zanzibar sio maalim seif bali ni hao hao CCM. Akatuthibitishia siku Ujumbe kutoka Oman ulivokuja Zanzibar, meli za mizigo zote ziliwekwa nje kupisha meli ya mfalme, bandarini hapakuwa na kazi mpaka meli ilipoondoka. Ukisikia Baniani mbaya kiatu chake dawa ndio hichi!

Hao aliowaambia kuwa mwisho wa ukoloni mweusi na wao walikuwa weusi basi kama hujui. Zanzibar imetoka kwa mkoloni beberu mreno, ikaingia Sultan wa Oman, usultan ambao baadae ukawa chini ya beberu muingereza, baada ya kupata uhuru na kufanyika mapinduzi wakuja kama kina Ukwaju na okello wakajifanya wakombozi, kumbe na wao wakawa wakoloni. Sasa wazanzibar hawataki kutawaliwa na mkoloni mweusi, kheri warudi mabeberu na masultan.

Nitajia mkoloni aliehamisha mji mkuu wake kutoka nchi yake na kufanya mji wa sehemu aliyokoloni kuwa ndio mji mkuu wake.

By the way, kwa kisiwa cha Zanzibar, na potential ilokuwepo, watu 1.5m, ina uwezo wa kuwa zaidi ya dubai. Tatizo ni mkoloni mweusi tu.
 

Kwani CCm si Mkoloni?
 
Sasa ndio umefunguka na kujulikana ni mgeni unayeivamia Zanzibar na kuwachukia wenyeji
Oman haikuhamisha Mji wao Mkuu kuwa Zanzibar bali Sultani Sayyid aliugawa Utawala wake sehemu 2 kwa wototo wake na ndio maana Jamsheed hajarudi Oman
acha kutunga weka evidence au link hapa mezani
na mm niwape kisa cha PUNDA HAPANDI MUSCAT
 
Naona anajigonga mwenyewe.... Tangu mwanzo anatwambia kuwa eti wenyeji walimwambia muingereza aje awasaidie kumuondoa Muoman. yaani ata uko UVCCM sifikiri kama wanaweza kuwalisha watu upupu kiasi ichi 😀
sasa Sheikh tunaenda sawa nilichokitaka ni kuweka kumbukumbu kuwa kisiwa hicho wageni wamekuja kukitawala na hawataki kutoka wabakia wajukuu wanadai kwao
Sasa Mzanzibar ni yupi tungeanzia hapo ndipo tungehitimisha kwanini Marehemu Sheikh Abeid Karume kauawa na Mwl Nyerere akasema ningekuwa na uwezo visiwa hivyo ningevisukumia mbali.
https://kwaheri.files.wordpress.com/2010/05/kwaheri-ukoloni-kwaheri-uhuru.pdf
Zanzibar kuna wachache sana waliobaki ambao hawawataki wageni na vurugu zikitokea ndio wa mwanzo kukimbilia Bara na mombasa
Asanteni sana kwa Historia yenu mnayofunguka bila ushahidi wala Link
 
Pole sana mkuu. Chuki, Choyo na Ubaguzi Vinakuumiza. Ni maradhi mazito sana hayo. Sina Chakukusaidia zaidi ya kukuombea
GET WELL SOON rafiki
Mkuu mm niliona km chilubi anaijua sana Historia ya Zanzibar na anakusaidia kuijua kweli
labda ungempa vile vitabu vya akina Farsi na Ghassany vimfungue na kumpa mwanga aujue ukweli na apime mwenyewe
kunaKitabu cha Mzanzibar Mmarekani lkn ni PDF
https://kwaheri.files.wordpress.com/2010/05/kwaheri-ukoloni-kwaheri-uhuru.pdf
 
😀 😀 😀 nani anakufundisha historia?

Sultan Said hakuugawa ufalme wake. wakati akiwa mtawala Zanzibar, alihamisha mji mkuu wa Oman na Zanzibar ndio ikwa mji mkuu wake.... Ufalme wa zanzibar na Oman ulivunjika baada ya kifo chake na watoto wake kuanza kugombania kiti.

Rudi tena Primary usomeshwe hii historia nyepesi, au njoo Zanzibar tukupeleke ukapewe historia mjengoni na wasimamizi.

Hii Picha hapa chini kutoka kwenye ile source yako pendwa.... nashangaa hukuitembelea.



 
sasa Sheikh tunaenda sawa nilichokitaka ni kuweka kumbukumbu kuwa kisiwa hicho wageni wamekuja kukitawala na hawataki kutoka wabakia wajukuu wanadai kwao
Hatuendi sawa mkuu, wewe unajigonga na hsitoria yako ya kutunga na uzushi..... kwani wenyeji kina nani na wakati wao pia wakuja?

Sasa Mzanzibar ni yupi tungeanzia hapo ndipo tungehitimisha kwanini Marehemu Sheikh Abeid Karume kauawa na Mwl Nyerere akasema ningekuwa na uwezo visiwa hivyo ningevisukumia mbali.
Tuvute katiba itwambie Mzanzibar ni yupi.... Na tumuulize nyerere alipo kwanini angevisukumia mbali visiwa ivi....
 
Mbona hicho kitabu sijakisoma chote lakini kuna kipande kifupi tu tayari kinaonesha kuwa Sultan Zanzibar alieka heshima baina ya watu wa makabila tofauti na walikuwa wakiishi na amani na hadi mmishinari kusifia?

Sasa wewe huoni kama hichi kitabu tayari kinaenda kinyume na chuki zako dhidi ya waarabu? 😀 mi nna wasiwasi kuwa huna ulichosoma zaid ya kuhadithiwa upupu...

Unaleta links zinazokugonga mwenyewe... we mtu wa ajabu kweli
 
kwani kukuwekea Link ni kuonesha kuwa nakiunga mkono katika Hoja zangu za kumkataa mwarabu Visiwani au ninakupa Ushuuhuda kuwa wapo Waarabu wanayoyapinga Mapinduzi Matukufu
huyu mwandishi ni AFRABIA jina lililoanzishwa na Ali Mazrui kuonesha kuwa kuna kaTaifa kanataka kukaa katikati ya Afrika na Arabia na kosa kubwa limejitenga kiDini zaidi na chuki kwa mtu mweusi na ndio maana kitabu hicho kinakufaa ujue uongo mnaotuaminisha kuwa ni chuki za kiDini zilileta mapinduzi
Mwandishi huyu na wewe mpo sawa kimlengo wa kutuaminisha kuwa hayo Mapinduzi hayakuletwa na Waislamu ni John Okello Mkristo HIZO NI FITINA KUBWA ZA WAARABU
 
Kuhusu Usultani wa Oman kuja kuuweka Utawala wake katika Visiwa vya Zanzibar bado ilikuwa ni makosa na ndio maana hawa Afrarabia hawarudi tena Oman na ndio nikakuuliza Jamshed mbona haendi kwao? Lakini ujuwe utawala ulikuwepo miaka na miaka huko Omana na biashara zilikuwepo za viungo na Utumwa
Kwa mujibu wa Mwandishi hapa chini anaonesha Zanzibar kwa hao Afrarabia wanaitaka Zaznibar ibakie katika Uarabu Uislam na ikae mbali na Beberu )Mtanganyika)
Chilubi Historia ya Zanzibar ya biashara ya Utumwa ndiyo ninayoijua lkn kuwa mtaarabu huyu mtu hapana ni mpaka leo anajitenga na mengi (Afrabia)
 
Abaaa, Sasa kama nchi ilikuwa inakwenda vizuri na hakuna aliekuwa akionewa, kwanini watu wasipinge mapinduzi? Kwani kupinga mapinduzi ni dhambi? Taifa gani hilo linalotaka kukaa katikati ya afrika? Sudan, Somalia, Egypt, Algeria, Moroko, mbona wote hawa wanaongea kiarabu na wapo afrika? Ubaguzi na chuki zako dhidi ya waarabu na wazanzibar kwa ujumla zitakufanya uweweseke sana.

Mwandishi huyu na wewe mpo sawa kimlengo wa kutuaminisha kuwa hayo Mapinduzi hayakuletwa na Waislamu ni John Okello Mkristo HIZO NI FITINA KUBWA ZA WAARABU
Kwani mapinduzi yameletwa kwa lengo gani? na kwanini tusiamini kuwa lengo la mapinduzi ni kuuondoa uislam ikiwa mifano hai tunaiona saiv? Chuki zenu kwa waislam, chuki zenu kwa wazanzibari, jinsi mlivokuwa brainwashed kwenu nyie muarabu ni adui kuliko beberu wakati mwarabu huyu katawala fukwe tu. Waulize Wacongo mabeberu waliwafanya nini kisha linganisha na walichofanya waarabu. Halafu naomba uniletee picha halisi zenye kuonesha kuwa Waarabu Zanzibar waliwafanya wazanzibari watumwa. Usiniletee michoro ya darasa la sita.\

Unakimbia kivuli chako? Ulichoquote nilikuwa nakujibu UZUSHI wako. Historia nyepesi na za juu ambazo hazina siri ndani yake huijui utaijua yenye undani zaidi. Wacha uongo wewe jamaa, ulisema kuwa eti Sultan Said hakuweka makao makuu yake Zanzibar nimekuletea kipande kimekufanya uwe kipofu 😀 Wacha uzushi na chuki.

Suala la Jamshed kutoenda sio kwamba eti hatakiwi kwao, usitake kunichekesha saiv. Hawa watanzania walioenda kujichimbia ulaya wamefukuzwa makwao? poor judgment!
Chilubi Historia ya Zanzibar ya biashara ya Utumwa ndiyo ninayoijua lkn kuwa mtaarabu huyu mtu hapana ni mpaka leo anajitenga na mengi (Afrabia)
Kwani Biashara ya utumwa alianza muarabu Zanzibar?
 
hapa yatapatikana mengi sana safi sana Members wa JF
 
Nyie mliokuwepo ni bora mkatueleza sisi vijana ambao hata haukuona utawala wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Sidhani kama kuna ukweli wa aliyekuwa Karume kwenye haya maandishi yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…