Mauaji ya Polisi wetu ni Ujambazi, Ugaidi au Retaliation? Nini kifanyike kukomesha hali hii?

Mauaji ya Polisi wetu ni Ujambazi, Ugaidi au Retaliation? Nini kifanyike kukomesha hali hii?

Kuna ile alisema majambazi walazwe chini badala ya kusema wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo husika.

Sasa naona majambazi wameamua ku-retaliate..ndo wanawalaza askari chini sasa. Inabidi kwa kweli kiongozi wa nchi apime kauli zake maana........
Asikari use your common sense haya ni maisha tu utaacha watoto wanateseka bure
 
Wachangiaji msifanyie hili suala mzaha Gaidi hana chama wala dini ni mnyama akivaa vesti ya kujilipua huwa hajui ataua nani. Wiki iliyopita huko Misri katika kanisa la Copti mliona jinsi raia wasiokuwa na hatia walivyouliwa.
Tuweke pembeni tofauti zetu na tujadili adui yetu mkubwa Gaidi. Leo tumepoteza vijana wetu saba tunatakiwa tufarijii familia zao sio kutoa comments za mzaha.
 
Kama taifa tusikurupuke, kijiji changu hakina kiongozi hata mmoja wote walisha uwawa na watu hao hao(magaidi) . Nawaita magaidi kwasababu jina jambazi tunajua maana yake. Hawa magaidi hawa chukui mali, wala hawaombi pesa. Wao wanaua tu basi na kuotokomea kusikofahamika.
Kama alivyoshauri mleta uzi vyombo vya usalama vifanyekazi yake kwa umakini zaidi zaidi, top notch upelelezi ili kugundua nini hasa chanzo cha tatizo hili.
R.I.P vijana wetu... Mungu awajaalie furaha ya milele.
RIP , ndugu na marafiki zetu ambao waliuwawa na magaidi hawa.
Ameen.
 
Mheshimiwa paschal mayalla,kuna siku nilileta Uzi humu kuwa kauli za Rais zitahatarisha usalama wa Taifa, maana kutatokea magaidi na majambazi . thread ilifutwa faster,anyway sikulalamika maana ilikuwa ni sensitive issue sana lakini ukweli utabaki kuwa pale pale kuwa kauli za Rais na kumkumbatia Bashite zitaliangamiza Taifa. Utekaji unaofanywa na taasisi muhimu za serikali nazo zinachangia haya yote,kinachofanyika ni visasi dhidi ya serikali.
 
wangekuaja kuwaua hata wanaokinda bunge pale tu labda mwigulu atapata japo kaa akili kidogo.wacha tuuwane tu chama kwanza mengine baadae hii nchi iko salama
 
Inasikitisha na kushangaza sana. Saanane katekwa mwezi wa sita Serikali kimyaaa, Roma na wenzie wametekwa na kuteswa Serikali kimyaaa, uvamizi wa Clouds Serikali kimyaaa, vitisho dhidi ya Wabunge kutishiwa maisha yao Serikali kimyaaaa! Sasa kama Serikali inafumbia macho haya ni jukumu la nani kuhakikisha usalama wa raia na mali zao? Je, Serikali itaendelea na ukimya wake kufuatia haya mauaji ya kutisha dhidi ya polisi?
Nimeshangaa kweli juzi watu wanajadili bungeni kama hao wanaofanyiwa unyama sio binadamu!
Angalia kauli aliyoitoa ally kesi juu ya Roma!
Niliumia kweli ingawa Roma simjui na wala sio ndugu yangu!Sasa walikuwa wanatetea lisijadiliwe kwa faida ya nani!
 
Kweli vifo vya askari wetu ni jambo linalomsikitisha kila raia mpenda amani, lakini kikubwa ninachokiona hapa na hasa hii awamu ya tano ni kiongozi mkuu kutopenda ushirikiano ulikuwa unasaidia kupatikana taarifa kati ya police na raia. Tumeona rais aliyotumia nguvu nyingi kuzuia police jamii wakati hilo liliwekwa kwa ajili ya kupunguza uhalifu kama huo
Nchi hii yetu sote. tushirikiane na tusikilizane kwa mambo yote ya kitaifa. maana uchungu na utamu wa kila jambo tunaonja wote. hakuna adui Bali cc sote ni wamoja
 
Mhe paschal mayalla kuna siku pia niliwahi kuketa thread iliyokuwa inahusu ushawishi wa mkuu wa majeshi ndani ya jeshi ukoje,hii thread ilifutwa haraka sana na nikapigwa na ban juu. Lakini kuna siku kadri muda unavozidi kuendelea tutaelewana tu juu ya usalama wa Taifa hili. Usalama wa Taifa letu ubaharibiwa na viongozi wetu wenyewe kwa matendo na kauli zao. Tutegemee makubwa zaidi ya haya yaliyotokea huko mukuranga japo siombei yatokee. Rais abadili mwenendo wake,watuhumiwa wakubwa kama bashite ni kazma wachukuliwe hatua Kali za kisheria. Tujiandae pia utekaji wa mabasi na malori japo siombei yatokee ila kutokana na hali halisi ilivo nachelea kusema kuwa possibly yatajitokeza.
 
Niliwahi kusema kuwa huwezi kuandaa askari then ukashindwa kuwaajili. Je,mitaani kuna askari walio na mafunzo ya kijeshi na hawajaajiriwa?. Hili ni tatizo. Nchi yetu haiko salama kabisa. Wabunge wa ccm hawataki kuzungumzia hali ya usalama nchini. Tutegemee makubwa zaidi ya haya japo siombei
RIP askari wetu.
 
Wachangiaji msifanyie hili suala mzaha Gaidi hana chama wala dini ni mnyama akivaa vesti ya kujilipua huwa hajui ataua nani. Wiki iliyopita huko Misri katika kanisa la Copti mliona jinsi raia wasiokuwa na hatia walivyouliwa.
Tuweke pembeni tofauti zetu na tujadili adui yetu mkubwa Gaidi. Leo tumepoteza vijana wetu saba tunatakiwa tufarijii familia zao sio kutoa comments za mzaha.
Acha unafiki na wewe kwa kujifanya humjui aliyetufikisha hapa .
 
Wanabodi,
Taifa bado liko kwenye shock ya nini haswa kilichotokea kwa askari wetu?.

Mauaji haya ya Polisi Wetu ni Ujambazi tuu, ni Ugaidi au Retaliation?. Wakati vyombo vya uchunguzi vikiendelea na kazi yake, Sisi Watanzania kama taifa lazima tujiulize, Nini Kifanyike Kukomesha Hali Hii?,

Kwanza nikiri nimesikitishwa na vifo hivi vya vijana wetu askari polisi kushambuliwa na kuuwawa na majambazi wenye silaha.

Swali ni jee huu ni ujambazi tuu wa kawaida, uvamizi kwa lengo la kuiba silaha, ni ugaidi, ambush au nini haswa?.

Hili kuwaweka polisi wetu kwenye risk na kuwa an easy target, kwa majambazi wanaotumia silaha, niliwahi kulizungumza hapa kwa kirefuhttps://www.jamiiforums.com/threads/hili-la-polisi-kuruhusiwa-kuwanyanganya-silaha-majambazi-na-kupandishwa-vyeo-limekaaje.1071133/page-5

Kwa tukio kama la jana,jee mnadhani huu sasa ni wakati muafaka wa kuzibadili sheria zetu za jeshi la polisi ili kuwalinda polisi wetu wawe licenced to kill officially na serikali itangaze rasmi kuwa ujambazi wa kutumia silaha adhabu yake ni kifo cha papo kwa papo, no prosecution no kesi, bali ni hukumu ya kifo there and then ili kuwaogofya kabisa majambazi wote wanaotumia silaha wasithubutu?!.

Kama ni ugaidi au retaliation, tufanye nini?.

Natoa pole kwa rais wetu wa JMT, waziri wa Mambo ya Ndani, IGP na familia za askari hao!

RIP Askari Wetu.
Nini Kifanyike? .
Ijumaa Kuu Chungu!.
Paskali
Haya ni.mapungufu kwenye mafunzo na polisi wetu wamezoea kuonea wananchi wasio na silaha, ukiishi kwa upanga utakufa kwa upanga. Polisi wameua raia wengi sana wasio na hatia, wamepiga watu wengi sana wasio na hatia. Nao wamekutana na wenye hasira na hao wavamizi inaweklzekana wanalipiza kisasi fulani huwezi jua
 
Wanabodi,
Taifa bado liko kwenye shock ya nini haswa kilichotokea kwa askari wetu?.

Mauaji haya ya Polisi Wetu ni Ujambazi tuu, ni Ugaidi au Retaliation?. Wakati vyombo vya uchunguzi vikiendelea na kazi yake, Sisi Watanzania kama taifa lazima tujiulize, Nini Kifanyike Kukomesha Hali Hii?,

Kwanza nikiri nimesikitishwa na vifo hivi vya vijana wetu askari polisi kushambuliwa na kuuwawa na majambazi wenye silaha.

Swali ni jee huu ni ujambazi tuu wa kawaida, uvamizi kwa lengo la kuiba silaha, ni ugaidi, ambush au nini haswa?.

Hili kuwaweka polisi wetu kwenye risk na kuwa an easy target, kwa majambazi wanaotumia silaha, niliwahi kulizungumza hapa kwa kirefuhttps://www.jamiiforums.com/threads/hili-la-polisi-kuruhusiwa-kuwanyanganya-silaha-majambazi-na-kupandishwa-vyeo-limekaaje.1071133/page-5

Kwa tukio kama la jana,jee mnadhani huu sasa ni wakati muafaka wa kuzibadili sheria zetu za jeshi la polisi ili kuwalinda polisi wetu wawe licenced to kill officially na serikali itangaze rasmi kuwa ujambazi wa kutumia silaha adhabu yake ni kifo cha papo kwa papo, no prosecution no kesi, bali ni hukumu ya kifo there and then ili kuwaogofya kabisa majambazi wote wanaotumia silaha wasithubutu?!.

Kama ni ugaidi au retaliation, tufanye nini?.

Natoa pole kwa rais wetu wa JMT, waziri wa Mambo ya Ndani, IGP na familia za askari hao!

RIP Askari Wetu.
Nini Kifanyike? .
Ijumaa Kuu Chungu!.
Paskali
Mkuu Paskali, tukio hili kwa kweli linaumiza sana. Na linaumiza na kuleta hofu kubwa; kwamba kama askari wetu ambao ndio tunawaamini kuwa wanaweza kutulinda wanapukutishwa kirahisirahisi kiasi hicho, usalama wetu sisi raia uko katika mazingira gani? Ni tukio baya lakini linalotaka tafakuri huru isiyoathiriwa na ubaya wa tukio lenyewe. Kwanza, kuruhusu polisi wawe licenced to kill officially itakuwa ni wazo lililoathiriwa na ubaya wa tukio lakini lisilotatua tatizo la msingi. Kuruhusu polisi kuua hapo hapo ni kuongeza tatizo badala ya kulitatua. Vifo hata vya wasio na hatia vitaongezeka. Na haiwezi kushangaza "majambazi hewa" wakawa wengi kuliko majambazi halisi!

Ni mtazamo wangu kwamba tatizo hili tunaliona sasa-la askari kuuawa kwa namna inavyotokea huko mkoani Pwani, uhusiano baina ya polisi na raia unahusika positively or negatively. Ni bahati mbaya kwamba wakati kuna viongozi wa kisiasa wanaoamini katika kuwepo kwa uhusiano mzuri baina ya askari polisi na raia, bado viongozi wengine kauli na matendo yao ni tangazo kwamba hawataki kabisa polisi wawe na uhusiano mzuri na raia. Hii inakata mtiririko wa polisi kupata taarifa za criminals.

Pili, polisi wasio waadilifu wamekuwa wakishirikiana na raia wasio waadilifu kufanya matukio ya kijinai-wao huwa wanaita "ni kutafuta pesa". Kuna wakati hawa watu hugeukana, na wanapogeukana haya ndio hutokea. Sisemi kwenye tukio hili kuna mazingira haya, bali najaribu kuonyesha mazingira yanayosababisha wakati mwingine kuwepo kwa matukio kama haya.

Tatu, polisi wengi wanachoweka mbele kwenye akili yao ni pesa, yapo matukio ya kuuawa kwao yanayosababishwa na wao kudhani kwamba kila mtu kwao anaweza kuwa "deal". Tukio la askari polisi kuuawa katika kituo cha polisi Stakishari linaingia kweye mfano huu. Baada ya tukio la Stakishari polisi walionekana kushtuka lakini ile hali ya kudhani kila mtu kwao ni "deal" imewarudia tena, unaweza kuona kupitia matukio mbalimbali ya ukamataji "yasiyo rasmi".

Sitaki kuharakisha kuhusisha matukio hayo na ugaidi. Lakini ushauri wangu kwa polisi au serikali yenyewe kwa ujumla, kiwepo kitengo maalum cha kuchunguza mienendo ya askari kuanzia wa vyeo vya juu hadi chini. Kuna mitandao ndani ya polisi ambayo kazi yake ni kupora mali za criminals na mwisho wa siku huibua hasira kwa criminals hao, kushirikiana na criminals kufanya matukio ya kijinai na mwisho wa siku hudhulumiana na baadaye kuwepo matukio ya kulipiza visasi; nakadhalika. Na mwisho, angalau kwa sasa, nashauri viongozi wetu wahubiri uhusiano wa polisi na raia badala ya kuhubiri chuki baina yao!
RIP askari wetu..
 
Wachangiaji msifanyie hili suala mzaha Gaidi hana chama wala dini ni mnyama akivaa vesti ya kujilipua huwa hajui ataua nani. Wiki iliyopita huko Misri katika kanisa la Copti mliona jinsi raia wasiokuwa na hatia walivyouliwa.
Tuweke pembeni tofauti zetu na tujadili adui yetu mkubwa Gaidi. Leo tumepoteza vijana wetu saba tunatakiwa tufarijii familia zao sio kutoa comments za mzaha.

Kama chief comforter wananchi wake wakipatwa na Majanga badala ya kuwafariji anawadhihaki na kuwakejeli unataegemea hao wananchi wafanyeje.

Mkuu hata sisi tuna roho za nyama..tunahisia...tunaumia...usitake nitokwe na machozi bure.
 
Hawa majambazi Tutawanyanganya silaha haraka haraka au tutawateka msijali sana
 
Back
Top Bottom