Mauaji ya Polisi wetu ni Ujambazi, Ugaidi au Retaliation? Nini kifanyike kukomesha hali hii?

Mauaji ya Polisi wetu ni Ujambazi, Ugaidi au Retaliation? Nini kifanyike kukomesha hali hii?

Wanabodi,
Taifa bado liko kwenye shock ya nini haswa kilichotokea kwa askari wetu?.

Mauaji haya ya Polisi Wetu ni Ujambazi tuu, ni Ugaidi au Retaliation?. Wakati vyombo vya uchunguzi vikiendelea na kazi yake, Sisi Watanzania kama taifa lazima tujiulize, Nini Kifanyike Kukomesha Hali Hii?,

Kwanza nikiri nimesikitishwa na vifo hivi vya vijana wetu askari polisi kushambuliwa na kuuwawa na majambazi wenye silaha.

Swali ni jee huu ni ujambazi tuu wa kawaida, uvamizi kwa lengo la kuiba silaha, ni ugaidi, ambush au nini haswa?.

Hili kuwaweka polisi wetu kwenye risk na kuwa an easy target, kwa majambazi wanaotumia silaha, niliwahi kulizungumza hapa kwa kirefuhttps://www.jamiiforums.com/threads/hili-la-polisi-kuruhusiwa-kuwanyanganya-silaha-majambazi-na-kupandishwa-vyeo-limekaaje.1071133/page-5

Kwa tukio kama la jana,jee mnadhani huu sasa ni wakati muafaka wa kuzibadili sheria zetu za jeshi la polisi ili kuwalinda polisi wetu wawe licenced to kill officially na serikali itangaze rasmi kuwa ujambazi wa kutumia silaha adhabu yake ni kifo cha papo kwa papo, no prosecution no kesi, bali ni hukumu ya kifo there and then ili kuwaogofya kabisa majambazi wote wanaotumia silaha wasithubutu?!.

Kama ni ugaidi au retaliation, tufanye nini?.

Natoa pole kwa rais wetu wa JMT, waziri wa Mambo ya Ndani, IGP na familia za askari hao!

RIP Askari Wetu.
Nini Kifanyike? .
Ijumaa Kuu Chungu!.
Paskali
Hata askari wanaua majambazi lakini hawashtakiwi, sijaona logic yako Paskali
 
Kiukweli nimeumia sana baada ya kupata taarifa hii ya mauaji ya kutisha.Mimi nipo Lindi kwa habari zilizozagaa miongoni mwa polisi aliyeuawa ni ndugu yetu si watumbo moja bali anatokea hapa Lindi. Nimeumia,tumesikitika kwani polisi ni ndugu zetu,watoto wetu ifike wakati serikali ikomeshe haya mauaji imetosha.Ikibidi hata wapelelezi huru kutoka mataifa makubwa waje watupelelezee maana tunaumia jamani ndugu zetu hawaaa.
Mbona la kutekwa na kuteswa watu hii rai hukuitoa?

Watu wanapotea hii rai hukuitoa,

Tusibase upande mmoja, tuseme hivi, serikali ichunguze vitendo viovu vyote vinavyotokea na kutafuta namna ya kuvikomesha.... Si kwa askari tu, maana hata raia wengine nao ni binadam.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRICA.
 
Matukio yanayotokea huko Pwani ni asilimia 100 ugaidi. Kitu cha kushangazaa ni hawa magaidi kuua na kuchukua silaha je wanamipango gani na hiyo silaha. Serikali isichukulie suala hili mzaha ama ujambazi wa kawaida kwani tunatakiwa tujifunze kutoka Nigeria jinsi Boko Haram ilivyoanzishwa. Mkoa wa pwani unapakana na bahari ya hindi na mnavyoelewa kuna tatizo la magaidi Kenya na Somalia je serikali inatathimini vipi watanzania wangapi wamejaribu ama wamejiunga na vikundi hivyo vya kigaidi na kurudi hapa nchini. Leo hii tunaona nchi za ulaya kuna vijana waliokuwa wamejiunga na Islamic State huko Syria wamerudi ulaya na kuanza kufanya ugaidi. Tuangalie suala la uchumi pia sasa hivi sisi na majirani zetu tuko kwenye vita vya kiuchumi katika ujenzi wa bomba la mafuta, reli na utalii majirani zetu wameonekana sio salama na Tanzania imeonekana ni nchi salama kunauwezekano wa hawa majirani zetu wakatumia watu wabaya ili Tanzania isionekane nchi salama,
Serikali ilichukulie hili suala very very serious kabla halijawa out of control.
Acheni uchochezi pigeni kazi! Kazi nikazi ukiuwa kwa upanga utakufa kwa upanga!
Its so sad kwa kweli. Watendaji wasakwe popote pale walipo. May their souls rest in peace.Amen

Kazi ya bashite hiyo, anataka kutengeneza uadui kati ya polisi na raia. Ili aanze kamatakamata ablackmail watu.

Kisifanyike chochote juzi kuna Wabunge wameomba hilo swala lijadiliwe bungeni kuna wanawake jenista mhagama na mwenzie bila hata aibu wanasema ni uchochezi!
Yakasikika makofi ya Wabunge wa ccm waaaa...waaaa....waaaa....
Acha tuendelee hivi hivi
 
Nchi iko salama hao wanaolalamika ni wapiga dili tu,acha maneno ya uchochezi
Huna huruma hata chembe.
Huwaonei huruma wazazi waliofiwa na vijana wao. Askari polisi walio wengi ni vijana wadogo.
RI.P vijana, wapendwa wetu. Nawaombea furaha ya milele.
 
Wachangiaji msifanyie hili suala mzaha Gaidi hana chama wala dini ni mnyama akivaa vesti ya kujilipua huwa hajui ataua nani. Wiki iliyopita huko Misri katika kanisa la Copti mliona jinsi raia wasiokuwa na hatia walivyouliwa.
Tuweke pembeni tofauti zetu na tujadili adui yetu mkubwa Gaidi. Leo tumepoteza vijana wetu saba tunatakiwa tufarijii familia zao sio kutoa comments za mzaha.
Ndugu. Comments za mzaha zimejaa maumivu mioyoni mwa watu. Ni comments zinazoashiria watu wameanza kukata tamaa kwa sababu ya double standards. Wananchi wamevurugwa.sarcasm ndio namna yao ya kuwasilisha machungu waliyonayo
 
Kuna ujumbe ambao kila baada ya mauaji wauaji wamekuwa wakiuacha, kwamba wanafanya hivyo kupinga manyanyaso ya Polisi na serikali, tusitafute mchawi tujadili huu ujumbe wanaotuachia, vinginevyo mauaji haya hayatakoma na yatasambaa kote
 
In my point of view this is neither cospiracy nor robbery but it seems to be the FEELING of dehumainsation and oppression thats being conducted by the governing THEATRE...thus, this has the scence of RETALIATION ON THE MOTION and easist target is armed servicemen(women) that exactly giving us "tanzanian" hard time thinking of our "SAFETY" while armed men are dying accassionaly what about we the normads of life? Can we be spared our safety?
I support your view. 100%
 
Mbona la kutekwa na kuteswa watu hii rai hukuitoa?

Watu wanapotea hii rai hukuitoa,

Tusibase upande mmoja, tuseme hivi, serikali ichunguze vitendo viovu vyote vinavyotokea na kutafuta namna ya kuvikomesha.... Si kwa askari tu, maana hata raia wengine nao ni binadam.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRICA.


Ni kama pale kiongozi wa nchi ambaye mpaka boxer aliyovaa ni kodi zetu anapowakejeli na kuwadhihaki wananchi wanaohitaji faraja inaonekana sawa. Ila akitokea mwananchi akamsema huyo kiongozi tena kwa vtu vyenye mantiki kabisa. Watu wanatikwa povu eti ni utovu wa nidhamu.

Let me recap Newton's third law of motion ''Action and reaction are equal and opposite''

The first law states..An object will remain at rest or in uniform motion in a straight line unless acted upon by an external force.

Hizi law Mbili za mh Newton zina maana kubwa sana kama ukiziangalia kwa jicho la tatu.
 
Tanga,Pwani,Lindi na Mtwara haya maeneo ni yakuangaliwa sana,kuna vijana wako misituni wanapata mafunzo ya kijeshi na kigaidi,siku waki graduate mtaisoma namba vizuri.mbaya zaidi mamlaka husika zinafahamu lakini wameamua kukaa kimya.
 
"Nataka ifike mahali raia akimwona polisi ,raia amwogope polisi"(Hii ni sauti ya kichaa mmoja aliwahi kuitoa bila kujua umuhimu wa wananchi katika suala zima la amani ya nchi ).
Huyu kichaa wa wapi tena? Hafai kusikilizwa, hajui kama wananchi wakiwaogopa polisi basi wakiona baya linawanyemelea watanyamaza? Ni jambo jema polisi wetu kuwa rafiki na RAIA wema (ambao ni wengi) kiasi akiona askari tabasamu linakutoka bila kujitambua
 
Mleta mada amekula marahage ya wapi? Uliona wapi duniani kote taifa la kidemokrasia likitoa adhabu ya kifo papo kwa papo bila taratibu za kimahakama? Kama ni kujikomba sasa umevuka mipaka . unataka kuigeuza polisi kuwa mahakama? Unapouliza kuwa ni ujambazi au ugaidi au whatever nani anaweza at this juncture kukujibu wakati tukio limetokea Jana usiku na upelelezi unaendelea??
 
Wako busy kuteka watu. Waache tu, kwanza 80% ya raia wanawachukia polisi. Wakae wajitathmini.
Ndio maana nilikataa kumuoa polisi maana kuna siku ningemtia vitasa tukagawana majengo ya serikali. Yeye hospital mimi cell ya central police.
 
Back
Top Bottom