byongo
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 827
- 1,945
Point namba mbili ya waislam..Nionavyo mimi ni makundi ya maharifu yanakusanya silaha.
Halfu kitu kingine kule yanakotokea haya ni kule kule kwenye pwani isiyokuwa na ulinzii. Ulinzi uimarishwe katika njia chocho za bahari.
Ninaomba JWTZ wafanye operation maalumu katika misitu iliyokatika maeneo hayo. Kunaweza kuwa na kambi maalumu ya uahrifu.
Tatu viongozi wa dini ya kiisilam, wale wanaowaza mema, wakae na wajadili namna ya kukomesha mitazazmo mibovu ya baadhi ya watu walio nao juu ya maisha. Bila shaka wanafahamu haya ni kwa nini yanatokea kwa kuwa eneo yanakotokea haya ni kule kwenye wingi wa wafuasi wao ambao wameshindwa maisha. Wanatakiwa wawape elimu sahihi namna wataboresha maisha yao badala ya kutafuta njia za kiharamia au kutaka kuharibu nchi ili wakose wote. Hii ni roho ya shetani yule mwenye wivu.
Nne jeshi la polisi lirudi katika misingi ya kutenda haki. Waacha uharamia wa kudhulumu na kuonea raia. Polisi waache unyanganyi wa mali na haki za raia ili jamii iwaone kuwa ni sehemu yake na iwape ushirikiano. Polisi wamejitenga na wananchi ki malengo na ndiyo sababu wananchi wako kimya hata wanapoona mipango miovu inatokea. Ninasema hivi kwa sababu, bila shaka hata katika tukio hili kulikuwa na watu karibu. Hao jambazi hakutoka hewani na hakuyeyeyuka baada ya ushetani wake. Watu walimwona akiingia na alikoelelkea wanajua. Jeshi la polisi linahitaji kuhamasisha umoja kati yake na raia ili raia walisaidie kuzuia matukio ya kishetani kama haya.
Tano serikali iache kuwatumia polisi vibaya. Inawajengea chuki dhidi ya wananchi. Wanachi wanaoan polisi ni watesi wao na si wasaidizi n ahivyo kujitenga nao mbali. Viongozi wa ccm na serikali wawekeane mikakati ya kudhibiti matumizi ya jeshi la polisi yasiyo halali. Yanalidhalilisha jeshi letu na kuliweka katika wakati mgumu sana wa kutengwa na umma.
Serikali itambue kwamba hii ni karne nyingine. Budget za serikali ziangalie suala la technolojia ya ulinzi na usalama ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu. Ikiwa tetemeko lilitokea Bukoba na hapakuwa na hata kipimo cha kutambua kabla hatua stahiki zikachukuliwa, na bado serikali ikasema haikuleta tetemeko, niina mashaka na uwepo wa technolojia ya ulizini wa mipaka yetu hasa katika bahari na sehemu zisizokaliwa na watu. Kuliko kutumia nguvu kubwa kudhibiti wapinzani, ninaomba serikali iwekeze kweney technolojia surveillance ndani na nje ya mipaka yetu. Polisi wanaoonyesha uharamia kama kunyang'anya mali za mahabusu kwa nguvu, kutetea uharlfu ndani ya jeshi, kuonea na kusingizia raia, wanatakiwa kuondolewa kwenye kikosi hivi kwa sababu hawa ini hatari kwa jeshi lenyewe. Wanaweza kuuza taarifa hata mipango ya dani ya jeshi kwa maslahi ya 1000,000. Ondoeni maharamia kati ya polisi, sukeni jeshi letu upya, kisha liwezeshwe kwa technolojia inayoona na kutoa taarifa ya matukio hasa katika maeneo yenye wasialam wengi kama huko pwani na mkuranga.
Watanzania ninaomba sana tuendelee kuishauri serikali japo inakataa kushauriwa. Hii la kukataa ushauri wa wanaoongozwa tulichukue kama tatizo linalohitaji tiba kama maradhi lakini hatwezi kujenga taifa pasipo kushauriana na kusikilizana. Ccm ninyi ndio wenye viburi, ninaomba muwe wa kwanza kujirekebisha. Tambueni bila taifa lenye amani ccm haipo.
Viongozi acheni kujenga matabaka miongoni mwa wananchi. Acheni kuwadharau watanzania na kuwabagua, huku mkifanya kebehi za wazi kwa viburi. Migawanyikio mnayoijenga ndiyo inayoondoka mishkikamano na mioyo ya uzalendo . Bila kuwa na umoja na uzalendo, hakuna suluhu rahisi ya matatkzo yanayoinuka.
NINAOMBA NISIITWE MCHOCHEZI MAANA SERIKALI INADHANI IKIWAUNGA WATU VINYWA NDIYO INASHINDA, KUMBE INAJENGA ROHO MBAYA ZA KIKATILI NA MTAWANYIKO UANOANZA KULIGHARIMU TAIFA KWA KASI HII YA AJBU.
Anaetakiwa kuboresha maisha ya wananchi ni serikali na sio mashehe,hao mashehe wenyew wapo hohe hahe watawaambia nn wananchi?
Sio kila sheikh ni kada wa ccm kama Alhadi Mussa Salim.
Sema hivi,serikali ikae chini na wananchi wake,kwanza wajue tatizo lipo wapi na watashirikiana vipi