Wanabodi,
Taifa bado liko kwenye shock ya nini haswa kilichotokea kwa askari wetu?.
Mauaji haya ya Polisi Wetu ni Ujambazi tuu, ni Ugaidi au Retaliation?. Wakati vyombo vya uchunguzi vikiendelea na kazi yake, Sisi Watanzania kama taifa lazima tujiulize, Nini Kifanyike Kukomesha Hali Hii?,
Kwanza nikiri nimesikitishwa na vifo hivi vya vijana wetu askari polisi kushambuliwa na kuuwawa na majambazi wenye silaha.
Swali ni jee huu ni ujambazi tuu wa kawaida, uvamizi kwa lengo la kuiba silaha, ni ugaidi, ambush au nini haswa?.
Hili kuwaweka polisi wetu kwenye risk na kuwa an easy target, kwa majambazi wanaotumia silaha, niliwahi kulizungumza hapa kwa kirefuhttps://
www.jamiiforums.com/threads/hili-la-polisi-kuruhusiwa-kuwanyanganya-silaha-majambazi-na-kupandishwa-vyeo-limekaaje.1071133/page-5
Kwa tukio kama la jana,jee mnadhani huu sasa ni wakati muafaka wa kuzibadili sheria zetu za jeshi la polisi ili kuwalinda polisi wetu wawe licenced to kill officially na serikali itangaze rasmi kuwa ujambazi wa kutumia silaha adhabu yake ni kifo cha papo kwa papo, no prosecution no kesi, bali ni hukumu ya kifo there and then ili kuwaogofya kabisa majambazi wote wanaotumia silaha wasithubutu?!.
Kama ni ugaidi au retaliation, tufanye nini?.
Natoa pole kwa rais wetu wa JMT, waziri wa Mambo ya Ndani, IGP na familia za askari hao!
RIP Askari Wetu.
Nini Kifanyike? .
Ijumaa Kuu Chungu!.
Paskali