Mauaji ya Polisi wetu ni Ujambazi, Ugaidi au Retaliation? Nini kifanyike kukomesha hali hii?

mbn Isaac Newton ametoa law mda mrefu sana.

"For every action there is equal and opposite reaction"
Hapo umenena

Utawala unapokuwa haueleweki haya hutokea busara ni muhimu sana
 
Hata askari wanaua majambazi lakini hawashtakiwi, sijaona logic yako Paskali
 
Mbona la kutekwa na kuteswa watu hii rai hukuitoa?

Watu wanapotea hii rai hukuitoa,

Tusibase upande mmoja, tuseme hivi, serikali ichunguze vitendo viovu vyote vinavyotokea na kutafuta namna ya kuvikomesha.... Si kwa askari tu, maana hata raia wengine nao ni binadam.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRICA.
 
Acheni uchochezi pigeni kazi! Kazi nikazi ukiuwa kwa upanga utakufa kwa upanga!
Its so sad kwa kweli. Watendaji wasakwe popote pale walipo. May their souls rest in peace.Amen

Kazi ya bashite hiyo, anataka kutengeneza uadui kati ya polisi na raia. Ili aanze kamatakamata ablackmail watu.

Kisifanyike chochote juzi kuna Wabunge wameomba hilo swala lijadiliwe bungeni kuna wanawake jenista mhagama na mwenzie bila hata aibu wanasema ni uchochezi!
Yakasikika makofi ya Wabunge wa ccm waaaa...waaaa....waaaa....
Acha tuendelee hivi hivi
 
Nchi iko salama hao wanaolalamika ni wapiga dili tu,acha maneno ya uchochezi
Huna huruma hata chembe.
Huwaonei huruma wazazi waliofiwa na vijana wao. Askari polisi walio wengi ni vijana wadogo.
RI.P vijana, wapendwa wetu. Nawaombea furaha ya milele.
 
Ndugu. Comments za mzaha zimejaa maumivu mioyoni mwa watu. Ni comments zinazoashiria watu wameanza kukata tamaa kwa sababu ya double standards. Wananchi wamevurugwa.sarcasm ndio namna yao ya kuwasilisha machungu waliyonayo
 
Kuna ujumbe ambao kila baada ya mauaji wauaji wamekuwa wakiuacha, kwamba wanafanya hivyo kupinga manyanyaso ya Polisi na serikali, tusitafute mchawi tujadili huu ujumbe wanaotuachia, vinginevyo mauaji haya hayatakoma na yatasambaa kote
 
Uchochezi tusijadili hili swala, bunge lomekataa!
 
I support your view. 100%
 


Ni kama pale kiongozi wa nchi ambaye mpaka boxer aliyovaa ni kodi zetu anapowakejeli na kuwadhihaki wananchi wanaohitaji faraja inaonekana sawa. Ila akitokea mwananchi akamsema huyo kiongozi tena kwa vtu vyenye mantiki kabisa. Watu wanatikwa povu eti ni utovu wa nidhamu.

Let me recap Newton's third law of motion ''Action and reaction are equal and opposite''

The first law states..An object will remain at rest or in uniform motion in a straight line unless acted upon by an external force.

Hizi law Mbili za mh Newton zina maana kubwa sana kama ukiziangalia kwa jicho la tatu.
 
Tanga,Pwani,Lindi na Mtwara haya maeneo ni yakuangaliwa sana,kuna vijana wako misituni wanapata mafunzo ya kijeshi na kigaidi,siku waki graduate mtaisoma namba vizuri.mbaya zaidi mamlaka husika zinafahamu lakini wameamua kukaa kimya.
 
Mwigulu ni mwoga sana kutumbuliwa lkn naona mtumbuaji akimwangalia kwa jicho la tatu
 
"Nataka ifike mahali raia akimwona polisi ,raia amwogope polisi"(Hii ni sauti ya kichaa mmoja aliwahi kuitoa bila kujua umuhimu wa wananchi katika suala zima la amani ya nchi ).
Huyu kichaa wa wapi tena? Hafai kusikilizwa, hajui kama wananchi wakiwaogopa polisi basi wakiona baya linawanyemelea watanyamaza? Ni jambo jema polisi wetu kuwa rafiki na RAIA wema (ambao ni wengi) kiasi akiona askari tabasamu linakutoka bila kujitambua
 
Mleta mada amekula marahage ya wapi? Uliona wapi duniani kote taifa la kidemokrasia likitoa adhabu ya kifo papo kwa papo bila taratibu za kimahakama? Kama ni kujikomba sasa umevuka mipaka . unataka kuigeuza polisi kuwa mahakama? Unapouliza kuwa ni ujambazi au ugaidi au whatever nani anaweza at this juncture kukujibu wakati tukio limetokea Jana usiku na upelelezi unaendelea??
 
Wako busy kuteka watu. Waache tu, kwanza 80% ya raia wanawachukia polisi. Wakae wajitathmini.
Ndio maana nilikataa kumuoa polisi maana kuna siku ningemtia vitasa tukagawana majengo ya serikali. Yeye hospital mimi cell ya central police.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…